HAALAND AFUNGA MAN CITY YAILAZA CRYSTAL PALACE 1-0


BAO pekee la Erling Haaland dakika ya 78 kwa penalti limeipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumamosi Uwanja wa Venue Selhurst Park Jijini London.
Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 61 katika mchezo wa 27, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Arsenal ambao pia wana mechi moja mkononi.
Kwa upande wao Crystal Palace wanabaki na pointi zao 27 za mechi sasa nafasi ya 12.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA