Posts

MTIBWA SUGAR 1-3 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

DURAN APIGA MBILI ASTON VILLA YATOA SARE 3-3 NA LIVERPOOL

Image
WENYEJI, Aston Villa usiku wa jana wametoa sare ya kufungana mabao 3-3 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham. Mabao ya Aston Villa yalifungwa na kiungo Mbelgiji, Youri Marion Tielemans dakika ya 12 na mshambuliaji Mcolombia, Jhon Jader Duran mawili dakika ya 85 na 88. Mabao ya Liverpool yalifungwa na kipa Muargentina, Emiliano Martínez aliyejifunga dakika ya pili, winga Mholanzi Cody Mathes Gakpo dakika ya 23 na beki Muingerea mwenye asili ya Ghana, Jarell Amorin Quansah dakika ya 48. Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 79, ingawa inabaki nafasi ya tatu, wakati Aston Villa inafikisha pointi 78 nayo inabaki nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 37.

YANGA SC MABINGWA TENA LIGI KUU YA NBC TZ BARA

Image
RASMI, Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo na mara ya 30 jumla baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mtibwa Sugar walitangulia kwa bao la Charles Ilamfya dakika ya 32, kabla ya Yanga kutoka nyuma kwa mabao ya Mzambia Kennedy Musonda dakka ya 62, Nasry Kyombo aliyejifunga dakika ya 66 na Clement Mzize dakika ya 81. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 71 katika mchezo wa 27 ambazo hakuna timu nyingine katika Ligi Kuu inayoweza kuzifikisha, hivyo kujihakikishia taji la ubingwa msimu huu, 2023-2024. Hali inazidi kuwa mbaya kwa Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo ikibaki na pointi zake 20 za mechi 27 mkiani kabisa mwa Ligi Kuu. Sehemu pekee ya Mtibwa Sugar kujinusuru kutoshuka Daraja ni kwenye mchujo, Play-Offs kama itashinda mechi zake zote tatu zilizobaki dhidi ya Namungo nyumbani na Ihefu na Mashujaa ugenini na kumaliza nafasi ya 14 au ya 13. Na hiy

TABORA UNITED YAICHAPA MASHUJAA 1-0 UWANJA WA MWINYI

Image
BAO pekee la Eric Okutu dakika ya 70 jana liliipa Tabora United ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Kwa ushindi huo, Tabora United inafikisha pointi 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14, wakizidiwa wastani wa mabao na Mashujaa FC baada ya wote kucheza mechi 27. Wapo mbele ya Geita Gold yenye pointi 24 nafasi ya 15 na Mtibwa Sugar pointi 20 nafasi ya mwisho, ya 16 baada ya wote kucheza mechi 26. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu zitashuka daraja na mbili nyingine, ya 13 na 14 zitamenyana baina yao nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kusalia Ligi Kuu.

NICOLAS JACKSON AIPIGIA LA USHINDI CHELSEA YAICHAPA NOTTINGHAM 3-2

Image
  TIMU ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire. Mabao ya Chelsea yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Ukraine, Mykhailo Mudryk (23) dakika ya nane, washambuliaji Muingereza mwenye asili ya Jamaica, Raheem Shaquille Sterling (29) dakika ya 80 na Msenegal mzaliwa wa Gambia, Nicolas Jackson dakika ya 82. Kwa upande wao  Nottingham Forest mabao yao yamefungwa na beki Muivory Coast, mzaliwa wa Ufaransa, Willy-Arnaud Zobo Boly (33) dakika ya 16 na winga mwenye asili ya Ghana, Callum James Hudson-Odoi (23) dakika ya 74. Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya saba, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake 29 za mechi 37 nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.

MAN CITY YAITANDIKA FULHAM 4-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND

Image
MABINGWA watetezu, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London. Mabao ya Man City yamefungwa na beki Mcroatia, Josko Gvardiol (22) mawili dakika ya 13 na 71, huku mengine yakifungwa na kiungo Muingereza, Philip Walter Foden (23) dakika ya 71 na mshambuliaji Muargentina, Julian Alvarez (24) kwa penalti dakika ya 90'+6. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 85 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England ikiizidi pointi mbili Arsenal baada ya wote kucheza mechi 36, wakati Fulham inabaki na pointi zake 44 za mechi 37 nafasi ya 14.