Posts

Showing posts from November, 2021

AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0

Image
BAO pekee la mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 52 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya sita, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake mbili baada ya timu zote kucheza mechi saba na kuendelea kushika mkia.

YANGA SC YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-0

Image
VINARA Yanga SC wametanua uongozi wao hadi pointi tano dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 18 na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 26 akimalizia pasi ya kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto'. Yanga SC inafikisha pointi 19 baada ya mechi saba na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya watani wao wa jadi, Simba SC ambao wana mechi moja mkononi na kesho watawakaribisha Geita Gold Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mbeya Kwanza wanabaki na pointi zao saba za mechi saba katika nafasi ya 11. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Biashara United wamelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. Mshambuliaji Adam Adam aliwatanguliza wageni, Polisi dakika ya 46, kabla ya Nassib Mpapi dakika ya 61

SIMBA NA JKT, YANGA NA IHEFU, AZAM NA WARRIORS ASFC

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wataanza na JKT Tanzania katika Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), wakati watani wao, Yanga waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Ihefu SC ya Mbeya. Timu nyingine maarufu ya Ligi Kuu, Azam FC kama Simba na Yanga nao watacheza na timu ya Championship katika Raundi ya Kwanza, ambayo ni Green Warriors ya Dar es Salaam.

MESSI AWEKA REKODI BALLON D’OR YA SABA

Image
MUARGENTINA Lionel Messi ameweka historia baada ya kushinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya saba usiku wa Jumatatu ukumbi wa Theatre Du Chatelet  Jijini Paris, Ufaransa. Messi amebeba tena tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 38 akiwa na Barcelona msimu uliopita kabla ya kuhamia Paris St Germain kama mchezaji huru kufuatia kumaliza mkataba. Muargentina huyo amemshinda mshambuliaji wa kimataifa wa Poland na klabu ya Bayern Munich, Roberto Lewandowski na nyota wa Chelsea, Jorginho alioingia nao fainali. Mpinzani wake wa muda mrefu kwenye kinyang’nyiro hicho, Mreno Cristiano Ronaldo ameshika nafasi ya sita na hakuhudhuria tafrija hiyo. Messi pia anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya Ballon d’Or katika miongo mitatu tofauti. Katika tuzo hiyo ambayo hutokana na kura za waandishi wa habari za soka 180 duniani kote, mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema ameshika nafasi ya nne, Mfaransa mwenzake, kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante wa tano mbele ya Ronaldo. Mshambuliaji wa

DODOMA JIJI YALAZIMISHWA SARE NA COASTAL

Image
WENYJI, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa Jumapili Uwanja wa Jamhiri Jijini Dodoma. Kwa sare hiyo, Dodoma Jiji wanafikisha pointi 12 na kurejea nafasi ya tatu, wakati Coastal Union inatimiza pointi nane na kusogea nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi saba.

SIMBA SC 3-0 RED ARROWS (KOMBE LA SHIRIKISHO)

Image
 

MAN UNITED YAIKOSAKOSA CHELSEA, 1-1

Image
VINARA, Chelsea wamepunguzwa kasi baada ya sare ya 1-1 na Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London leo. Jadon Sancho alianza kuifungia Manchester United dakika ya 50 hilo likiwa bao lake la pili wiki hii, kabla ya Jorginho kuisawazishia The Blues kwa penalti dakika ya 69 kufuatia Aaron Wan-Bissaka kumchezea rafu Thiago Silva. Chelsea inafikisha pointi 30 baada ya sare hiyo na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi mbili zaidi ya Manchester City, wakati Man United inafikisha pointi 18 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kucheza mechi 13.

MAN CITY YAICHAPA WEST HAM 2-1

Image
WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad. Mabao ya Manchester City yamefungwa na Ilkay Gundogan dakika ya 33 na Fernandinho dakika ya 90, wakati la West Ham limefungwa na mtokea benchi, Manuel Lanzini dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 29 na kurejea nafasi ya pili, sasa ikizidiwa pointi mbili na vinara, Chelsea wakati West Ham inabaki na pointi zake 23 katika nafasi ya nne baada ya timu zote kucheza mechi 13.

SIMBA YAITANDIKA RED ARROWS 3-0

Image
SIMBA SC imejiweka katika nafasi nzuri ya kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, nyota wa mchezo alikuwa ni kiungo Mghana, Bernard Morrison aliyefunga mabao mawili na kuseti moja. Mchezaji huyo wa zamani wa wapinzani wa jadi, Yanga alifunga bao la kwanza dakika ya 17 na la tatu dakika ya 78, wakati la pili 'alimtafunia' mshambuliaji Mnyarwanda mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere aliyefunga dakika ya 20. Timu hizo zitarudiana Desemba 5 Jijini Lusaka na mshindi wa jumla atakwenda hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.

REFA ALIYEWAPA YANGA PENALTI ACHUKULIWA HATUA

Image
REFA Abel William aliyewapa Yanga penalti ya uraia iliyowapatia bao la kusawazisha wako toa sare ya 1-1 na Namungo FC wiki iliyopita Lindi amechukuliwa hatua. Taarifa ya Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imesema kwamba refa huyo amepelekwa Kamati ya Waamuzi akajadiliwe kwa makosa aliyoyafanya.

ARSENAL YAICHAPA NEWCASTLE UNITED 2-0

WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka dakika ya 56 na Gabriel Martinelli dakika ya 66 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya tano, wakati Newcastle United inabaki na pointi zake sita na kuendelea kushika mkia.

LIVERPOOL YAICHAPA SOUTHAMPTON 4-0

WENYEJI Liverpool wameibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield leo. Mabao ya Liverpool leo yamefungwa na mshambuliaji Mreno, Diogo Jota mawili dakika ya pili na 32, kiungo Mspaniola, Thiago Alcântara dakika ya 37 na beki Mholanzi, Virgil van Dijk dakika ya 52. Kwa ushindi huo, kikosi cha kinafikisha pointi 28 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya pili, kikizidiwa pointi moja na vinara, Chelsea ambao pia wana mechi moja mkononi. Southampton inabaki na pointi zake 14 za mechi 13 nafasi ya 14. 

PRISONS YAIPIGA NAMUNGO 3-1, MCC NA KMC 2-2

Image
WENYEJI, Tanzania Prisons wamepata ushindi wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Namungo FC mabao 3-1 jioni ya leo Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. Mabao yote ya Tanzania Prisons leo yamefungwa na mshambuliaji Jeremiah Juma dakika ya nne, 11 na 26, wakati bao pekee la Namungo FC limefungwa na mshambuliaji Mrundi, Bigirimana Blaise dakika ya 68. Kwa ushindi huo, Prisons inafikisha pointi nane na kujiinua hadi nafasi ya nane, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake sita katika nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 13. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji Mbeya City wamelazimishwa sare ya 2-2 na KMC Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Paul Nonga dakika ya nane na Richardson Ng'ondya dakika ya 67 na ya KMC yamefungwa na Matheo Anthonyu dakika ya 13 na Mohamed Samatta dakika ya 86.   Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya tatu, wakati KMC inafikisha pointi sita na

RUVU SHOOTING YAICHAPA KAGERA 2-1

Image
WENYEJI, Ruvu Shooting wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Mabao ya Ruvu yamefungwa na Zuberi Dabi dakika ya 30 na Rashid Juma dakika ya 84, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Ally Nassor dakika ya 84. Kwa matokeo hayo, Ruvu inafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya sita, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake nane katika nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi saba.

SAMATTA AIFUNGIA ANTWERP YATOA SARE UJERUMANI

Image
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ameifungia bao la pili timu yake, Royal Antwerp ikitoa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya wenyeji, Eintracht Frankfurt katika mchezo wa Kundi D UEFA Europa League Uwanja wa Deutsche Bank Park Jijini Frankfurt, Ujerumani. Samatta alifunga dakika ya 88 baada ya kiungo Mbelgiji, Radja Nainggolan kufunga la kwanza dakika ya 33, wakati mabao ya Eintracht Frankfurt yalifungwa na Daichi Kamada dakika ya 12 na Gonçalo Paciência dakika ya 90. Kwa sare hiyo, Antwerp inafikisha pointi mbili na kuendelea kushika mkia, wakati Eintracht Frankfurt inafikisha pointi 11 na kuendelea kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Olympiakos ya Ugiriki yenye pointi tisa na Fenerbahce ya Uturuki yenye pointi tano.

MSUVA AWAIBUKIA YANGA MAZOEZINI KIGAMBONI

Image
  MSHAMBULIAJI wa Wydad Athletic ya Morocco, Simon Happygod Msuva jana ametembelea mazoezi ya timu yake ya zamani, Yanga SC eneo la Avic Town, Somangira, Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Msuva alipata fursa ya kuzungumza na makocha, viongozi na wachezaji wenzake kwa furaha.

AGGREY MORRIS ASOMEA UKOCHA KOZI YA CAF

Image
BEKI aliyesimamishwa Azam FC kwa utovu wa Nidhamu, Aggrey Morris Ambrose ni miongoni mwa washiriki wa Koziya Ukocha ya CAF Diploma C inayoendelea Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Ilala Jijini Dar es Salaam. Pamoja na Aggrey Morris, lakini wapo mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Shauri Iddi Mussa na mchambuzi wa Azam Tv, Ally Kamwe.

SIMBA SC NA RED ARROWS SH 5,000 TU

Image
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC na Red Arrows ya Zambia ni Sh.5000. Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba viingilio vingine katika mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni ni Sh.20,000 kwa VIP B na C na 40,000 kwa VIP A.

MAN CITY YAICHAPA PSG 2-1 ETIHAD

Image
WENYEJI, Manchester City wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad. Kylian Mbappe alianza kuifungia Paris Saint-Germain dakika ya 50, kabla ya Man City kuzinduka kwa mabao ya Raheem Sterling dakika ya 63 na Gabriel Jesus dakika ya 76 na kwa matokeo hayo zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora. Manchester City inaongoza Kundi kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na PSG nane, RB Leipzig nne sawa na Club Brugge.

LIVERPOOL YAENDELEZA USHINDI 100% ULAYA

Image
WENYEJI, Liverpool jana wameedeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa Porto mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Anfield. Mabao ya Liverpool jana yamefungwa na Thiago Alcantara dakika ya 52 na Mohamed Salah dakika ya 70 na ushindi huo ni mwendelezo wa rekodi nzuri ya kushinda mechi zake zote.  Liverpool sasa inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza kundi hilo ikifuatiwa kwa mbali na Porto pointi tano, AC Milan nne sawa na Atletico Madrid baada ya wote kucheza mechi tano.

REAL MADRID YASHINDA 3-0 UGENINI

Image
MABAO ya David Alaba dakika ya 30, Tony Kroos dakika ya 45 na ushei na Karim Benzema dakika ya 55 jana yameipa Real Madrid ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Sheriff Tiraspol katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Bolshaya Sportivnaya Arena Jijini Tiraspol. Real Madrid ambayo imeshafuzu 16 Bora, inafikisha pointi 12 na kuendelea kuongoza kundi mbele ya Inter Milan yenye pointi 10, Sheriff sita na Shakhtar Donetsk moja.

BAYERN YASHINDA, BARCA DROO

Image
TIMU ya Bayern Munich imeendeleza ubabe baada ya kuwachapa wenyeji, Dynamo Kiev 2-1 katika mchezo wa Kundi E Uwanja wa NSK Olimpiki Jijiji Kiev nchini Ukraine. Mabao ya Bayern Munich usiku wa jana yalifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 14 na Kingsley Coman dakika ya 42, wakati la Dinamo Kiev lilifungwa na Denys Harmash dakika ya 70. Mechi nyingine ya kundi hilo, FT Barcelona chini ya kocha mpya, Xavi ililazimishwa sare ya 0-0 na Benfica Uwanja wa Camp Nou. Bayern Munich ambayo tayari imeshafuzu Hatua ya 16 Bora inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Barcelona yenye pointi saba, Benfica tano na Dinamo Kiev moja. Barcelona italazimika kushinda mechi ya mwisho dhidi ya Bayern Munich Desemba 8 Ujerumani ili kwenda Hatua ya 16 Bora au kuwaombea mabaya Benfica wafungwe na Dinamo Kiev kwenye mechi ya mwisho Ureno.

CHELSEA YAIBAMIZA JUVENTUS 4-0

Image
MABINGWA watetezi, Chelsea wameibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Juventus katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijiji London. Mabao ya The Blues yalifungwa na Trevoh Chalobah dakika ya 25, Reece James dakika ya 55, Callum Hudson-Odoi dakika ya 58 na Timo Werner dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 12 na kupanda kileleni ikiizidi wastani wa mabao tu Juventus baada ya wote kucheza mechi tano na zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora mbele ya Zenit yenye pointi nne na Malmo pointi moja.

MAN UNITED YATINGA 16 BORA ULAYA

Image
TIMU ya Manchester United imeanza vyema maisha bila kocha Ole Gunnar Solskjaer baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Villarreal katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Cerámica, Villarreal. Mabao ya Man United chini ya kocha mpya na wa muda, Michael Carrick baada ya kufukuzwa Solskjaer yamefungwa Cristiano Ronaldo dakika ya 78 na Jadon Sancho dakika ya 90 hilo likiwa bao lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu. Kwa ushindi huo, United inafikisha pointi 10 na kupanda kileleni ikiizidi pointi tatu Villarreal baada ya wote kucheza mechi tano, hivyo kuingia Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

GSM WADHAMINI WAPYA LIGI KUU

Image
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani (Kulia) na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Group, Mhandisi Hersi Said (kushoto) wakionyesha mfano wa Hundi ya mkataba uliosainiwa leo wa Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.1 kwa miaka miwili.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA HUSSEIN BALLO

Image

YANGA SC YAKUBALI YAISHE KWA MORRISON

Image
KLABU ya Yanga imekubaliana na maamuzi ya Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kutupilia mbali kesi yao dhidi ya winga Mghana, Bernard Morrison. “Matokeo ya kesi hii hayatoirudisha nyuma klabu ya Yanga katika kupambania haki zake pale itakapoona inafaa kufanya hivyo,”imesema taarifa ya Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla. Mapema leo taarifa ya CAS ilisema kwamba mkataba wa awali wa Yanga na Morrison ulimalizika Julai 14, mwaka 2020 na wa pili ambao Mghana huyo anaukana alisharejesha fedha za klabu hiyo dola za Kimarekani 30,000 hivyo hakuna kesi baina yao.

YANGA YAIZAWADIA JEZI FAMILIA YA MWALIMU NYERERE

Image
MWENYEKITI wa Yanga SC, Dk. Mshindo Msolla leo amewakabidhi jezi za timu hiyo, mke wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere pamoja na mwanawe, Madaraka Nyerere nyumbani kwao Msasani, Jijini Dar es Salaam.

MORRISON AWAGARAGAZA YANGA CAS

Image
MAHAKAMA ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) imetupilia mbali kesi ya klabu ya Yanga dhidi ya winga Mghana, Bernard Morrison hadi. Taarifa ya CAS imesema kwamba mkataba wa awali wa Yanga na Morrison ulimalizika Julai 14, mwaka 2020 na wa pili ambao Mghana huyo anaukana alisharejesha fedha za klabu hiyo dola za Kimarekani 30,000 hivyo hakuna kesi baina yao.

TANZANIA YAMALIZA YA PILI COSAFA

Image
TANZANIA jana imemaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya Soka la Ufukweni baada ya kufungwa 3-1 na Msumbiji katika Fainali ufukwe wa South Beach Arena Jijini Durban. Ushindi huo ni mwendelezo wa ubabe wa Msumbiji kwa Tanzania, kwani mechi ya Kundi B walishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4. Mechi nyingine Tanzania iliyo chini ya kocha Boniphace Pawasa ilishinda 3-1 dhidi ya Comoro Kundi A kabla ya kuifunga Angola 5-2 kwenye Nusu Fainali.

MAN CITY YAICHAPA EVERTON 3-0

Image
WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad. Mabao ya Man City leo yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya 44, Rodri dakika ya 55 na Bernardo Silva dakika ya 86 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi  26, wakizidiwa tatu na vinara, Chelsea baada ya wote kucheza mechi 12.

KMC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU

Image
TIMU ya KMC imepata ushindi wa kwanza wa msimu baada ya kuichapa Azam FC 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mabao ya KMC leo yamefungwa na Matheo Anthony Simon dakika ya 13 na Hassan Salum Kabunda dakika ya 90, huku la Azam FC likifungwa na Mzambia, Charles Zullu dakika ya 43. Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi tano na kupanda kwa nafasi mbili kutoka mkiani katika ligi ya timu ya timu 16.

SOLSKJAER AFUKUKUZWA MAN UNITED

Image
KLABU ya Manchester United imemfukuza kocha wake, Ole Gunnar Solskjaer kifuatia kipigo cha 4-1 ugenini mbele ya Watford jana. Taarifa ya klabu imesema kwamba Micheal Carrick ataiongoza timu kwa muda hadi atakapotangazwa kocha mpya. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo, Solskjaer amekuwa kazini takribani miaka mitatu mitatu Manchester United na dalili za kufukuzwa zilianza baada ya kufungwa na Liverpool na Manchester City. Na kufukuzwa kwake kunafuatia kikao cha dharula kilochoitishwa jana baada ya kipigo kisichotarajiwa cha Watford.

NAMUNGO FC 1-1 YANGA SC (LIGI KUU)

Image
 

MESSI AFUNGA BAO LA KWANZA UFARANSA

Image
MSHAMBULIAJI Lionel Messi jana amefunga bao lake la kwanza Ligue 1, Ufaransa akiiwezesha Paris Saint-Germain kuichapa 3-1 Nantes Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris. Messi alifunga bao la tatu dakika ya 87 akimalizia pasi ya Kylian Mbappe aliyefunga pia bao la kwanza dakika ya pili tu, wakati bao la pili Dennis Appiah alijifunga dakika ya 81. Bao pekee la Nantes lilifungwa na Randal Kolo Muani dakika ya 76 katika mchezo huo ambao PSG ilimaliza pungufu baada ya Keylor Navas kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 65.

LIVERPOOL YAITANDIKA ARSENAL 4-0

Image
WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumamosi Uwanja wa Anfield. Mabao ya Wekundu wa Anfield yamefungwa na Sadio Mane dakika ya 39, Diogo Jota dakika ya 52, Mohamed Salah dakika ya 73 na Takumi Minamino dakika ya 77. Liverpool imefikisha pointi 25 baada ya ushindi huo na kurejea nafasi ya pili ilizidiwa pointi nne na vinara, Chelsea baada ya wote kucheza mechi 12, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 20 za mechi 12 pia nafasi ya  tano.

WATFORD YAICHAPA MAN UNITED 4-1

Image
WENYEJI, Watford wameiadhibu Manchester United kwa kipigo cha 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vicarage Road, Watford. Mabao ya Watford yamefungwa na Josh King dakika ya 28, Ismailia Sarr dakika ya 48, Joao Pedro dakika ya 90 na ushei na dakika tatu baadye Emmanuel Dennis akafunga la nne, wakati mtokea benchi Donny van de Beek ndiye mfungaji wa bao pekee la United dakika ya 50. Kipigo hicho cha tano cha msimu kinaifanya Manchester United iliyomaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Harry Maguire kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 69 ibaki na pointi zake 17 baada ya mechi saba katika nafasi ya saba. Kwa upande wao, Watford ya kocha Claudio Ranieri inatimiza pointi 13 baada ya kucheza mechi 13 katika nafasi ya 16.