Posts

Showing posts from April, 2020

TUKIWAPA THAMANI WACHEZAJI WETU, WATAFANYA MAKUBWA

Image
Na Ibrah Mkemia, DAR ES SALAAM NIANZE kwa kuliombea na kulitakia afya njema  Taifa langu la Tanzania,  Taifa ambalo lina watu wakarimu na wenye busara, amani, na upendo. Tukiwa bado tunaendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa hatari wa corona, yapo mambo mengi ambayo kama wanamichezo wapenda burudani ya mpira wa miguu tunapaswa kujadili kwa kina ili kuweza kupata mawazo chanya kama sio muarubaini kabisa. Kipindi hiki ambapo kuna mengi magumu tunayapiti lakni kwa uwezo wa Mungu naimani yatapita na Taifa litaendelea kubaki kama Taifa lenye malengo, matumaini ya kufika katika uchumi wa kati wa viwanda. Kama kaulimbiu ya Mheshimiwa Rais kwamba Tanzania iwe nchi ya viwanda. Na kiwanda kimoja wapo kipo kwenye michezo nacho ni mpira wa miguu (kandanda). Maswali mengi ya watanzania, wapenda michezo yamekuwa yakiuliza ni kwanini tumekuwa na hatua za mtoto mdogo katika kuyatafuta mafanikio na sio hatua za mtu mzima hususani katika swala la michezo. Hili limekuwa gonjwa sugu ambal

SOKA YA TANZANIA BADO NI RIDHAA, SI YA KULIPWA KAMA TUNAVYOAMINI

Image
Na Ally Msigwa, IRINGA Kwa Tanzania, Soka ni Ajira kama Ajira zingine  Huku Tukiamini Ni Sahihi, Tunaamini Soka ni Professionalism kwa Aspect ya Mikataba na Renumeration clauses ila Je,  misingi ya ajira inafuatwa kisheria?Je, Viongozi na wachezaji wako kiprofessional in a Grassroot Descipline Level and operation?  Kosa kubwa kwetu kufanya Soka letu ni Professional football, Wakati hata level ya semi Professional bado.. Ni rahisi soka la Tanzania hapa lilipo kushuka na kuporomoka kuliko kupanda mbele.. Hatujatatua misingi , hatujaanda nguzo za kuwa pro hatujaandaa mentality na mindset kuelekea Pro Tulichofanya, tumelipamba hili soka kwa nakshi nyingi zinazo attract professionalism na competitiveness katika ngazi ya mavuno zaidi. Tanzania tumefanikiwa kuendesha soka kwa mikataba na kutoheshimu mikataba yenyewe kwa yale ambao pande mbili wamekubaliana. Najua tunafahamu kesi nyingi sana juu ya mikataba kwa baadhi ya Vilabu kutofuata taratibu pia hili linatokea kwa wachezaji pia, Na m

HARUNA HAKIZIMANA NIYONZIMA SASA MUME WA WAKE WAWILI, AOA NA BINTI WA KITANZANIA BAGAMOYO

Image
Kiungo Mnyarwanda wa Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima akiwa na mke wake wa pili, Mtanzania baada ya kufunga ndoa hivi karibuni Bagamoyo mkoani Pwani Beki Juma Abdul (kushoto) ni mchezaji mwenzake pekee aliyehudhuria ndoa hiyo ya siri. Mke mkubwa wa Haruna, Naillah Uwineza ni Mnyarwanda mwenzake.

KWA WENGINE BARAKOA NI YA KUFUNIKA PUA NA KINYWA, KWA MOURINHO YA KUSHIKA MKONONI TU

Image
Kocha Mreno wa Tottenham Hotspur ya England, Jose Mourinho akitembea huku ameshika barakoa mkononi kipindi hiki klabu yake imesitisha mazoezi kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19

MACHO YA WAPENDA KANDANDA HUPENDA KUTAZAMA SOKA SAFI

Image
Na Ibrah Mkemia, DAR ES SALAAM MOJA ya vitu ambavyo watanzania wengi wameshindwa, ni kufanya utalii hasa ule wa ndani ya nchi. Tanzania ni nchi ambayo imejaaliwa vivutio vingi kama wanyama, milima, misitu, na n.k. lakini imekuwa ngumu kwa watanzania kufanya hivyo. Ila kupitia wizara ya maliasiri na utalii wamejaribu kuongeza chachu ya watanzania kupenda kufanya utalii wa ndani kwa kuanzisha kampeni nyingi kuhusu utalii kama kupanda milima, n.k Nikapata muamko wa mimi kuanzisha safari kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi, Kilimanjaro kwa kupitia usafiri wa reli kwa maana ya garimoshi (treni). Kiukweli nilifarijika kuona uzuri wa nchi yetu, ukubwa wa maeneo ya wazi yenye miti mirefu na mifupi iliyopambwa na rangi nzuri ya kijani moyoni nikasema "Nakupenda Tanzania". Nikiwa kwenye viti ambacho ni maalumu kwa watu wawili,  vyenye kutazamana kwa jumla ya idadi ya watu wanne. Nilipata bahati ya kukaa na watu wa makomo hivi,  japo walikuwa sio wazee sana ila walikuwa na umri mkub

PAPY KABAMBA TSHISHIMBI ADHIHIRISHA MAPENZI YAKE KWA TANZANIA BAADA YA KUVAA JEZI YA TAIFA STARS

Image
Kiungo Papy Kabamba Tshishimbi (kushoto), raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amevaa jezi ya timu ya taifa ya Tanzania tayari kwa mazoezi binafsi, kipindi hiki klabu yake, Yanga imesitisha mazoezi kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19 Jezi namba tano Taifa Stars huvaliwa na mchezaji mwenzake wa Yanga SC, Kelvin Yondan

MLINDA MLANGO BENO KAKOLANYA ANAPOMAANISHA ANACHOKISEMA KUHUSU MAISHA YAKE SIMBA SC

Image
Kipa wa pili wa Simba SC, Beno David Kakolanya akiwa ametulia nyumbani kwake, Mwanjelwa mkoani Mbeya kipindi hiki klabu yake imesitisha mazoezi kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa COVID19. Kakolanya amekaririwa akisema anafurahia maisha Simba SC kutokana na namna anavyopewa ushirikiano na viongozi wa klabu hiyo 

MIRAJ ATHUMANI MADENGE 'SHEVA' ANAVYOFANYA MAZOEZI UFUKWENI KUJIWEKA FITI AREJESHE MAKALI MSIMBAZI

Image
Mshambuliaji wa Simba SC, Miraj Athumani Madenge 'Sheva' akifanya mazoezi ya kukimbia ufukweni kujiweka fiti kipindi hiki klabu yake imesitisha mazoezi kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa COVID19 

IBRAHIM AJIBU MIGOMBA ANAVYOKAMUA KWA BIDII GYM KUJIWEKA FITI AREJESHE HESHIMA SIMBA SC

Image
Kiungo wa Simba SC, Ibrahim Ajibu Migomba akifanya mazoezi gym kujiweka fiti kipindi hiki klabu yake imesitisha mazoezi kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa COVID19 

MKALI WA MABAO LIGI KUU YA TANZANIA, MEDDIE KAGERE ANAENDELA VIZURI KABISA NYUMBANI KWAO, KIGALI

Image
Mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere anayechezea Simba SC ya Dar es Salaam akiwa nyumbani kwake, Kigali kipindi hiki klabu yake imesitisha mazoezi kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa COVID19 

MSHAMBULIAJI WA AZAM FC BARAKA YUSSUF NI MMOJA WA WANASOKA WANAOZINGATIA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

Image
Mshambuliaji wa Azam FC, Mbaraka Yussuf akiwa amevaa barakoa kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa COVID19, ambao umesababisha michezo yote duniani kusimamishwa 

NAHODHA MSAIDIZI 'YANGA AFRIKA' JUMA ABDUL JAFFAR MNYAMANI AKIJIFUA BARABARANI KUILINDA PUMZI YAKE

Image
Nahodha Msaidizi wa Yanga SC, Juma Abdul Jaffar Mnyamani akifanya mazoezi binafasi kujiweka fiti kipindi klabu yake imesitisha mazoezi ya vikosi vyake kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa COVID19 

KELELE ZA MPIGA KELELE AMBAYE HAONEKANI KATIKA SOKA LETU

Image
Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM BAADA ya kufungua macho yangu na kuianza asubuhi yangu ya jumatatu hii, hakika ilikuwa asubuhi yenye staili ya kipekee kabisa. Niliwaza mambo mengi huku nikitafakari kile kinachoendelea Duniani kote juu ya hili janga la Corona,sikuishia hapo nikawaza kwa namna tunavyoendelea kukosa burudani za soka kila wikiendi na zile za kati ya wiki,ila mwisho wa siku nikajifariji kwakuwa afya ni zaidi ya chochote. Ilinibidi kuamka na kuachana na shuka lililokuwa likiniingiza kwenye limbi zito la mawazo. Turudi kwenye mada yetu, kwenye hoja yetu  sidhani kama kuna mtu anaweza kupinga hili pale tunapo wazungumzia wadogo zetu kina Baraka Majogoro, Zawadi Mauya, Yassin Mustapha, Yussuf Mhilu, Marcel Kaheza, Jaffar Kibaya, Hassan Kibailo na wengineo, msimu huu walikuwa kwenye kiwango bora kabisa. Hakika wamezisaidia sana timu zao,hakika walistahili kuvaa jezi za timu zao na kuwa sehemu ya vikosi vya kwanza vya timu zao,wamepambana mno na kwenye hilo hakuna ubish

KUNA TATIZO ZAIDI YA IDADI YA WACHEZAJI WA KIGENI LIGI KUU

Image
Na Ibrah Mkemia, DAR ES SALAAM WAKATI dunia ikipambana na ugonjwa hatari wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya covid_19 (corona) ambao umeonekana ni tishio, na kuua watu wengi katika baadhi ya nchi. Hali hii imesababisha shughuli nyingi sana kusimama. Ikiwemo soka na hata shughuli za kiuchumi.  Baada ya janga hili kutokea, kumeibuka mijadala mingi kuhusu michezo. Hasa katika kandanda hapa naamanisha mpira wa miguu. Ipo mijadala kuusu umalizaji wa ligi katika nchi husika, kupanda na kushuka daraja. Lakini mjadala ambao umenifanya nishike kalamu nyeusi na niweze kuandika ni kuhusu mjadala amabo umetokea katika mjengo ambao wawakilishi wa majimbo (wabunge) hukutana na kujadili mambo yanayoihusu nchi yetu Tanzania. Mshambuliaji Mzimbabwe wa Azam FC, Donald Ngoma akimiliki mpiraa mbele ya beki Mganda wa Lipuli FC, Joseph Owino katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara Mjadala kuhusu wachezaji wa kigeni. Huu ni hoja ambayo imetolewa na waziri mwenye dhamana ya michezo. "

ISSA ATHUMANI NA MDOGO WAKE, KASONGO SIMBA NA YANGA 1993

Image
Wanasoka ndugu, beki Kasongo Athumani Mgaya wa Simba SC (kushoto) akiwania mpira dhidi ya kaka yake, Issa Athumani Mgaya wa Yanga SC (sasa marehemu) katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (sasa Ligi Kuu) baina ya watani hao wa jadi Machi 27, mwaka 1993 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-1, mabao yake yote yakifungwa Said Mwamba 'Kizota' (sasa marehemhu) dakika ya 47 na 57 mara zote akimalizia pasi za Zamoyoni Mogella, wakati bao pekee la Simba SC lilifungwa na Edward Chumila (marehemu pia) dakika ya 75 

CRISTIANO RONALDO ANAVYOJIFUA 'KINYAMA' KUHAKIKISHA ANAENDELEA KUWA FITI KUPITA MAELEZO

Image
Mshambuliaji Mreno wa Juventus ya Italia, Cristiano Ronaldo akifanya mazoezi binafsi kipindi hiki timu zao zimesitisha mazoezi kwa sababu ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19

KIUNGO MKENYA WA SIMBA SC, FRANCIS KAHATA NYAMBURA AKIJFANYA MAZOEZI BINAFSI KWAO NAIROBI NA BARAKOA YAKE

Image
Kiungo Mkenya wa Simba SC ya Dar es Salaam, Francs Kahata Nyambura akifanya mazoezi peke yake kwao na barakoa Jijini Nairobi kipindi hiki timu yake imesitisha mazoezi kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19

KIPA MKONGWE JUMA KASEJA ANAVYOJIFUA PEKE YAKE KUHAKIKISHA ANAKUWA FITI ZAIDI NA KUENDELEA KUFANYA VIZURI KATIKA SOKA

Image
Kipa mkongwe nchini, Juma Kaseja anayechezea KMC ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam akiruka juu kudaka mpira wakati wa mazoezi yake binafsi kipindi hiki timu yake imesitisha mazoezi kwa sababu ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19

MSHAMBULIAJI WA MTIBWA SUGAR, STAHMIL MBONDE ANAVYOZINGATIA TAHADHARI KUJINGA NA MAAMBUKIZI YA COVID 19

Image
Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Stahmil Mbonde akiwa amevaa barakoa sare yeye pamoja na wanawe nyumbani kujinga maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19

WASHAMBULIAJI WAWILI NDUGU, DANIEL NA MDOGO WAKE AYOUB LYANGA WAKIFANYA MAZOEZI YA PAMOJA NYUMBANI KUJIWEKA FITI

Image
Wachezaji wawili ndugu, washambuliaji Daniel Lyanga wa JKT Tanzania (kulia) na mdogo wake, Ayoub Lyanga wa Coastal Union wakifanya mazoezi ya pamoja kujiweka fiti kipindi hiki timu zao zimesitisha mazoezi kwa sababu ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19

MRISHO NGASSA ALIPOCHANGAMKIA OFA YA VIFAA VYA MICHEZO KWENYE DUKA MDHAMINI WA YANGA SC LEO

Image
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa (kulia) akiwa na Afisa wa Idara ya Habari ya Yanga SC, Antonio Nugaz leo kwenye duka la nguo la mfadhili wa klabu yao, GSM liiitwalo Anta liliopo Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupewa vifaa vya michezo vya kufanyia mazoezi nyumbani kipindi hiki mazoezi ya pamoja yamesitishwa kwa sababu ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19  Kundi lingine la wachezaji wa Yanga baada ya kupatiwa vifaa vyao juzi

MNAJUA KWAMBA KIPRE TCHETCHE ALIYEKUWA AZAM NA KPAH SHERMAN WA YANGA SASA WANACHEZA TIMU MOJA MALAYSIA?

Image
Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Muivory Coast, Kipre Herman Tchetche (kulia) akiwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman pamoja na wachezaji wenzao wa Kedah FC ya Ligi Kuu ya Malaysia kipindi hiki klabu yao imesitisha mazoezi kwa sababu ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19   

KIUNGO WA SIMBA SC, SAID HAMISI NDEMLA ALIPOMSINDIKIZA BEKI WA YANGA SC, ALLY MTONI 'SONSO' KUOA DAR

Image
Beki wa Yanga SC, Ally Abdulkarim Mtoni 'Sonso' akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa jana Mbagala Jijini Dar es Salaam.  Ally Mtoni 'Sonso' alisindkizwa na rafiki yake, kiungo wa Simba SC, Said Hamisi Ndemla (kulia) kwenda kuoa jana