Posts

Showing posts from August, 2019

BARCELONA YABANWA, YATOA SARE YA 2-2 NA OSASUNA LA LIGA

Image
KINDA wa umri wa miaka 16, winga wa Guinea-Bissau, Anssumane 'Ansu' Fati akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kusawazisha dakika ya 51 akitokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya or Nelson Semedo katika sare ya 2-2 na wenyeji, Osasuna Uwanja wa El Sadar. Mabao yote ya Osasuna yamefungwa na Roberto Torres dakika ya saba na 81 kwa penalti, wakati bao lingine la Barcelona limefungwa na Arthur dakika ya    64. Winga huyo wa Guinea-Bissau, Fati mwenye umri wa miaka 16 na siku 304, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu mdogo kufunga bao kwenye historia ya miaka 90 ya La Liga baada ya Fabrice Olinga aliyeifungia Malaga akiwa na miaka 16 na siku 98 na Iker Muniain aliyekuwa na miaka 16  na siku 289 alipoichezea kwa mara ya kwanza Athletic Bilbao   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

LIVERPOOL YASHINDA MECHI YA 13 MFULULIZO LIGI KUU ENGLAND

Image
Mshambuliaji Sadio Mane akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Liverpool bao la pili dakika ya 37 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Burnley leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England  Uwanja wa Turf Moor huo ukiwa ushindi wa 13 mfululizo kwenye ligi hiyo. Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Chris Wood aliyejifunga dakika ya 33 akijaribu kuokoa krosi ya Trent Alexander-Arnold na Roberto Firmino dakika ya 80   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

DULLAH MBABE ATWAA TAJI LA WBO BAADA YA KUMPIGA MCHINA KWA KO

Image
Na Mwandishi Wetu, QINGDAO   BONDIA Mtanzania, Abdallah Shaaban Pazi ‘Dullah Mbabe’ jana amefanikiwa kutwaa taji la WBO Asia Pacific uzito wa Middle baada ya kumpiga kwa Knockout (KO) raundi ya tatu mwenyeji, Zulipikaer Maimaitiali ukumbi wa TSSG Center mjini Qingdao, China. Dullah Mbabe alilianza pambano kwa kasi na kumpelekea makundi mfululizo Zulipikaer, bondia namba moja China ambaye ndiye aliyekuwa anashikilia mkanda huo, kabla ya kumkalisha chini raundi ya tatu.  Akizungumza baada ya pambano hilo, promota wa Dullah Mbabe, Jay Msangi amesema kwamba kijana wake ameliletea sifa taifa lake, Tanzania kwa ushindi huo. Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ (kushoto) akimuadhibu Zulipikaer Maimaitiali jana China “Ni heshima kubwa, wadau tujitokeze kwa wingi kwenye hafla ya kumpokea bingwa huyu siku ya Jumatatu saa tatu na nusu asubuhi pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere,”alisema Jay Msangi. Kwa ushindi huo, sasa Dullah Mbabe anashikilia mataji mawili makubwa, lingi

AGUERO AFUNGA MAWILI MAN CITY YAICHAPA BRIGHTON 4-0

Image
Sergio Aguero akiifungia Manchester City bao lake la pili dakika ya 55 baada ya kufunga lingine dakika ya 42 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion leo Uwanja wa Etihad kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England. Mabao mengine ya mabingwa hao watetezi yamefungwa na Kevin de Bruyne dakika ya pili na Bernardo Silva dakika ya 79   PICHA ZAIDI GONGA HAPA      

TAMMY ABRAHAM APIGA MBILI LAKINI CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 2-2 DARAJANI

Image
Tammy Abraham akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Chelsea dakika za 19 na 43 kabla ya Sheffield United kusawazisdha kwa mabao ya Callum Robinson dakika ya 46 na Kurt Zouma aliyejifunga dakika ya 89 katika sare ya 2-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge mjini London   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

REFA AWANYIMA PENALTI MAN UNITED WATOA SARE 1-1 NA SOUTHAMPTON

Image
Mason Greenwood wa Manchester United akiwa chini kwenye boksi baada ya kuangushwa na Pierre-Emile Hojbjerg wa Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England timu hizo zikitoka sare ya 1-1 leo Uwanja wa St. Mary's 1-1. Hata hivyo, refa Mike Dean hakutoa penalti ingawa dakika ya 73 alimtoa kwa kadi nyekundu Kevin Danso wa Southampton kufuatia kumuonyesha kadi ya pili ya njano. Man United walitangulia kwa bao la Daniel James dakika ya 10 kabla ya Jannik Vestergaard kuwasawazishia wenyeji dakika ya 58   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

KABWILI NA ALLY NG’ANZI WAITWA KIKOSI CHA BARA CHINI YA MIAKA 20 KUCHEZA CECAFA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Zuberi Katwila ameita wachezaji 35 katika kikosi cha awali kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U20) itakayofanyika Septemba mwaka huu nchini Uganda.  Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutaja kikosi hicho leo mjini Dar es Salaam, Katwila ambaye pia ni Kocha Mkuu wa klabu ya Mtibwa Sugar alisema kwamba kikosi hicho kitaingia kambini Jumatatu. Aliwataja wachezaji wanaounda kikosi hicho ni makipa; Ramadhani Kabwili wa Yanga SC, Ally Salim wa Simba SC na Abdul Suleiman aliyepandishwa kutoka kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. Kipa wa Yanga SC,  Ramadhani Kabwili  ameitwa kikosi cha U20 kwa ajili ya michuano ya CECAFA   Mabeki ni; Nickson Kibabage (Difaa Hassan El-Jadidi, Morocco), Oscar Maasai (Azam FC), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Dickson Job (Mtibwa Sugar), Gustapha Simon (Yanga SC), Onesmo Mgaya (Mtib

MO DEWJI AWATULIZA WANA SIMBA SC BAADA YA KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA

Image
Na Saada Salim, DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Bodi ya Ukurugenzi ya Simba SC, Mohammed ‘Mo’ Dewji amewataka wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuwa wavumilivu baada ya timu kutolewa mapema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afri  Mabingwa wa Tanzania, Simba SC walitupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na UD Songo ya Msumbiji katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Na baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 mjini Beira wiki mbili zilizopita, maana yake Simba SC ilitolewa kwa sheria ya mabao ya ugenini. Mohammed ‘Mo’ Dewji amewataka wana Simba SC wawe wavumilivu baada ya timu kutolewa mapema Ligi ya Mabingwa     Baada ya kimya cha tangu Jumapili kufuatia kutolewa na UD Songo, Mo Dewji ameibuka leo kuwaomba msamaha wana Simba na kuahidi matokeo mazuri sehemu iliyobaki ya msimu.   “Wanasimba, mnisamehe kwa ukimya. Maumivu ya matokeo yametupata sote. Naomba tukumbushane: Sisi ni SIMBA! Simba lazi

TAIFA STARS WALIVYOANZA KUJIFUA LEO BOKO VETERANI KUJIANDAA NA BURUNDI

Image
Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa Uwanja wa Boko Veterani kwa ajili ya mazoezi kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Burundi wiki ijayo mjini Bujumbura

SAMATTA APANGIWA LIVERPOOL, NAPOLI NA SALZBURG KUNDI E LIGI YA MABINGWA ULAYA

Image
Na Mwandishi Wetu, MONACO NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji imepangwa kundi moja na E Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na mabingwa watetezi, Liverpool ya England, Napoli ya Italia na Salzburg ya Austria. Katika droo ya michuano hiyo iliyofanyika sambamba na tuzo za Mwanasoka Bora Ulaya, Samatta amejikuta akinagushiwa kwenye kundi la mabingwa watetezi, Liverpool na maana yake atakutana tena na Sadio Mane wa Senegal. Mane aliiongoza Senegal kuichapa Tanzania ya Samatta 2-0 kwenye mechi ya Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Juni mwaka huu nchini Misri. Huko walikuwa na Mohamed Salah wa Liverpool, ambaye timu yake, Misri kama Tanzania ilitolewa mapema. Mbwana Samatta amepangwa kundi moja na Liverpool, Napoli na Salzburg Ligi ya Mabingwa Ulaya Simba wa Teranga walifanikiwa kwenda hadi fainali, ambako walikutana tena na wapinzani wao wa Kundi A, Algeria na kuchapwa tena 1-0, bao pekee la Baghdad Bounedjah dakika ya pili tu Uwanja wa Kimat

VAN DIJK NDIYE MWANASKA BORA ULAYA, AWAANGUSHA MESSI NA RONALDO

JKT TANZANIA 1-3 SIMBA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

SIMBA SC YAANZA VYEMA LIGI KUU, YAWACHAPA JKT TANZANIA 3-0 KAGERE AANZA NA MBILI

Image
Na Saada Salim, DAR ES SALAAM MABINGWA watetezi, Simba SC wameanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddi Kagere alikaribia kufunga hat trick katika mechi ya kwanza baada ya kufunga mabao mawili, huku lingine likifungwa na Miraj Athumani ‘Madenge’ aliyerejeshwa kikosini msimu huu. Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems leo aliwaanzisha wachezaji wapta, Wabrazil Tairone Santos na Gerson Fraga kucheza pamoja safu ya ulinzi kwa mara ya kwanza tangu wasajiliwe Julai na wakafanya vizuri. Kagere aliye katika msimu wake wa pili Msimbazi tangu asajiliwe kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao la kwanza sekunde ya 20 ya dakika ya kwanza akimalizia pasi ya kiungo Hassan Dilunga kabla ya kufunga la pili dakika ya 59 akimalizia pasi ya kiungo mwingine mzawa, Muzamil Yassin. Kagere alikaribia kukamilisha hat trick dakika ya 65 kama si shuti lake kug

MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA TFF, NASSIB AFARIKI DUNIA ATAZIKWA KESHO KISUTU

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM ALIYEWAHI kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ramadhani Nassib amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospital ya Muhimbili mjini Dar es Salaam. Msiba huo umepkewa kwa majonzi makubwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini, akiwemo Rais wa TFF, Wallace Karia ambaye ametuma salamu za pole kwa familia ya marehemu. Kwa mujibu wa taarifa ya familia, mwili wa marehemu utahifadhiliwa kesho baada ya Sala ya ijumaa katika makaburi ya Kisutu baada ya kusaliwa msikiti wa Maamur, Upanga mjini Dar es Salaam. Mungu ampumzishe kwa amani. Amin. Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Ramadhani Nassib (kushoto) amefariki dunia alfajiri ya leo hospital ya Muhimbili

SANCHEZ ATUA MILAN KUKAMILISHA UHAMISHO WA MKOPOPO

Image
Alexis Sanchez akiwapungia mkono mashabiki baada ya kuwasili mjini Milan jana kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya ili kukamilisha uhamisho wake wa mkopo AC Milan baada ya miezi 18 migumu Manchester United ya England   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

JACKPOT KUBWA YA KIHISTORIA YA TANZANIA, SH MILIONI 825 ZAKABIDHIWA KWA WASHINDI WAWILI KUTOKA SPORTPESA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM BAADA ya Jackpot ya SportPesa kuvunjwa kwa mara ya kwanza ikiwa imefikia jumla ya milioni 825,913,640/= na washindi wawili kupatikana,leo hii wamekabidhiwa rasmi mkwanja wao kila mmoja akichomoka na kitita cha milioni 412,956,820/= baada ya kubashiri kwa usahihi mechi kumi na tatu za Jackpot wiki iliyopita. Kingsley Simon Pascal mwenye umri wa miaka 26 akitokea Biharamlo ndiye mshindi  wa kwanza wa Jackpot na mshindi mwingine ni Magabe Matiko Marwa mwenye miaka 31 akitokea wilaya ya Serengeti wote wakigawana kwa usawa kitita hicho cha Jackpot. Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa SportPesa ndugu Tarimba Abbas akizungumza wakati wa kuwakabidhi hundi kwa washindi hao wa kihistoria alisema,” Nafurahia kuwakabidhi  washindi wetu wa shilingi milioni 825,913640/= za Jackpot yetu ambayo ndiyo kubwa zaidi nchini,ni hii ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya betting Tanzania kwa kiasi kama hichi kutolewa kwa washinidi wa michezo ya kubahatisha aliendelea

YANGA SC 0-1 RUVU SHOOTING (LIGI KUU YA TANZANIA BARA)

Image

KMC 0-1 AZAM FC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

YANGA SC YAANZA VIBAYA LIGI KUU, YACHAPWA BAO 1-0 NA RUVU SHOOTING LEO UHURU

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya Ruvu Shooting imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwaangusha vigogo, Yanga SC kwa kuwachapa 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Bao pekee la ushindi la Ruvu Shooting leo limefungwa na Saadat Mohammed dakika ya 20 aliyefanikiwa kuwazidi mbio mabeki wa Yanga kufuatia pasi ndefu ya mshambuliaji mwenza, Said Dilunga. Na bao hilo lilikuja baada ya Yanga kuanza vizuri mchezo na kupoteza nafasi nzuri ya kupata bao dakika ya kwanza tu kufuatia nyota wake, Mnamibia Sadney Urikhob kuunganishia juu ya lango krosi ya mshambuliaji mwenzake mpya, Mganda Juma Balinya. Lakini Yanga SC iliendele kupeleka mipira mbele kwenye eneo la Ruvu Shooting kusaka bao la kusawazisha, tatizo hawakuwa na maarifa ya kuipenya ngome ya wapinzani.  Nafasi nyingine nzuri na ya mwisho walitengeneza Yanga ilikuwa ni dakika ya 70 wakati mpira uliounganishwa kwa Nahodha na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokras

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA DOUGLAS MUHANI, MCHEZAJI WA ZAMANI WA COASTAL UNION

Image

SIMBA SC KUTOLEWA MAPEMA LIGI YA MABINGWA KUNA JAMBO LA KUJIFUNZA

Image
Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM Imekuwa ni jambo la kushangaza huku wengi wakiwa hawaamini kilichotokea Kwani katika hali ya kawaida wadau wengi waliamini Simba ni lazima ipite hatua hii ya kwanza wakilinganisha na mafanikio ya msimu uliopita. Yapo mengi sana yatasemwa kama ilivyo ada ila kwa upande wangu nimeona mambo yafuatayo na mengine nilishaandika katika makala zangu za siku za nyuma! 1. Usajili uliofanywa Niliwahi kuandika nikishangaa na kuhoji kwanini klabu ya Simba inasajili wachezaji wengi zaidi ya 10 wakati tayari gari lilikuwa limewaka na kuhitaji kutia gia ya mwendo kasi..Kwani msimu uliopita walikuwa na kikosi bora ambacho kilikuwa na maelewano makubwa na kuwa na kasoro ndogondogo tu na pengine kuhitaji marekebisho madogo sana ili kuongeza uimara wao lakini cha ajabu ni sawa na kulizima gari ambalo tayari lilisha waka na kuanza kulisukuma tena. Simba SC ya msimu uliopita ilikuwa na mapungufu yasiyozidi manne kwa maana beki wa kati mzoefu,kiungo mkabaji,winga mmoj

AZAM FC YAANZA VYEMA LIGI KUU TANZANIA BARA, YAICHAPA KMC 1-0 LEO UWANJA WA UHURU

Image
Na Saada Salim, DAR ES SALAAM TIMU ya Azam FC imeuanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo. Pongezi kwa mshambuliaji mpya, Iddi Suleiman ‘Nado’ aliyesajiliwa kutoka Mbeya City aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 14 tu ya mchezo akimalizia pasi ya beki Mganda, Nicolas Wadada kutoka upande wa kulia. Azam FC inayofundishwa na kocha wa KMC msimu uliopita, Mrundi Etienne Ndayiragijje ingeweza kuvuna mabao zaidi kama ingetumia vyema nafasi zake ilizotengeneza.  Iddi Suleiman ‘Nado’ameifunga bao pekee Azam FC ikiilaza KMC 1-0 leo Uwanja wa Uhuru   KMC ya kocha Mganda, Jackson Mayanja nayo haikuwa doro kabisa, kwani kupitia washambuliaji wake, Vitalis Mayanga, George Sangija na Hassan Kabunda ililitia majaribu lango la Azam FC mara kadhaa, lakini leo kipa Mghana, Razack Abalora alikuwa makini. Refa Isihaka Mwalile alimuonya kwa kadi ya njano kipa wa Azam FC, Razack Abalola dakika ya 85 kwa ko

WACHEZAJI 40 WAITWA KIKOSI CHA AWALI CHA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars Bakari Nyundo Shime ametaja kikosi cha wachezaji 40 watakaoingia kambini kujiandaa na mashindano mbalimbali. Kikosi hicho kitakachoingia kambini rasmi Agosti 30 hadi Septemba 21mwaka huu kinaundwa na Najat Abas (JKT), Tausi Abdallah (Mlandizi), Zubeda Mgunda (Simba), Stumai Abdallah (JKT) na Wema Richard (Mlandizi). Wengine ni Enekia Kasonga (Alliance), Vailet Thadeo (Simba), Fatuma Issa (Evergreen), Vailet Singano (Simba), Happy Hezron (JKT), Janeth Christopher (Mlandizi), Eva Wailes (Ruvuma) na Amina Ally (Simba). Wamo pia Diana Lucas (Ruvuma), Asha Hamza (Kigoma), Pheromena Daniel (Mlandizi), Opa Clement (Simba), Herieth Shija (Mash Academy), Donisia Minja (JKT), Joyce Fredy (Tanzanite) na Janeth Shija (Simba). Wengine ni Masha Omari (Panama), Ester Mabanza (Alliance), Anastazia Nyandago (Panama), Rahabu Joshua (Alliance), Dotto Tossy (Simba), Neema Charles (Panama), Lucia Mrema (Pana

HONGERA YANGA SC KWA KUITOA ROLLERS, LAKINI ILI KUITOA ZESCO...

Image
Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM KUNA msanii mmoja wa Bongo Fleva ile ya zamani kidogo wakati nipo kwenye ujana wangu hasa aliimba nyimbo iliyokwenda kwa jina la siku nzuri ni kijana wa Tanga kama sikosei anaitwa Danny Msimamo katika mashairi yake yenye kibwagizo kisemacho "siku nzuri inavyokwenda wewe mwenyewe utaipenda ×2." na mashairi mengi yaliyotulia ndani yake daaah ilipendeza sana,ndivyo ambavyo mashabiki wa Yanga SC siku ya Jumamosi baada ya ushindi wa ugenini dhidi ya Township Rollers walivyokuwa na furaha na kuona kila kitu kinakwenda sawa na hapo ndipo unapoweza kupata raha katika mchezo wa soka na kufanya uwe ni mchezo unaoshika hisia za watu wengi kutokana na matokeo mbalimbali kuna wakati kwenye soka  1+1  sio lazima jibu liwe 2 kwani jibu linaweza kuwa 3,4 au 5 ndio raha ya mchezo wa soka. Yanga wanakila sababu ya kufurahi na kutamba kutokana na presha waliyokuwa nayo baada ya matokeo ya 1-1 wakiwa nyumbani huku wakiwa na mwanzo usio mzuri sana na pengine w

GRIEZMANN APIGA MBILI BARCELONA YAICHAPA REAL 5-2 LA LIGA

Image
Mshambuliaji mpya, Antoine Griezmann akishangilia baada ya kufunga mabao mawili dakika ya 41 na 50, Barcelona ikiibuka na ushindi wa 5-2 dhidi ya Real Betis kwenye mchezo wa La Liga jana Uwanja wa Camp Nou. Mabao mengine ya Barca yalifungwa na Carles Perez dakika ya 56, Jordi Alba dakika ya 60 na Arturo Vidal dakika ya 77, wakati ya Betis yamefungwa na Nabil Fekir dakika ya 15 na Loren Moron dakika ya 59   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

KOVALEV AMDUNDA ANTHONY YARDE KWA KO RAUNDI YA 11 URUSI

Image
Anthony Yarde akiwa chini baada ya kuangushwa na Sergey Kovalev raundi ya 11 katika pambano la ubingwa wa dunia usiku wa jana ukumbi wa Traktor Sport Palace, Chelyabinsk nchini Urusi. Kovalev alishinda kwa Knockout (KO) raundi ya 11 na kufanikiwa kutetea taji lake la WBO uzito wa Light Heavy   PICHA ZAIDI GONGA HAPA