Posts

Showing posts from January, 2022

FURAHIA SAFARI ZAKO KWA KUSAFIRI NA AZAM MARINE

Image
Furahia safari yako kwa kusafiri na Azam Marine kati ya Dar Es Salaam na Zanzibar kila siku. Karibu kwa usafiri salama huku ukipata huduma bora. Enjoy your journey by traveling with Azam Marine between Dar Es Salaam and Zanzibar everyday. Welcome for a safer journey while getting the best services.

BEKI MZANZIBARI, SEBBO AONGEZA MIAKA MIWILI AZAM FC

Image
BEKI Mzanzibari, Abdallah Kheri 'Sebbo' ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuchezea Azam FC. Sebbo amesaini mkataba huo leo mbele ya Mtendaji Mkuu wa klabu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na sasa ataendelea kupiga kazi timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Bakhresa na familia yake hadi mwaka 2024. Aidha, Azam pia imeingia mkataba wa miaka mitatu na Omar Abdikarim Nasser, kuwa Kocha Msaidizi mpya, chini ya Msomali mwenzake, Abdihamid Moallin. Nasser amewahi kufanya kazi katika nchi mbalimbali, mara ya mwisho 2019, akiitumikia moja ya vigogo vya nchini Qatar, Al Sadd, akiwa kama mchambuzi wa mechi (analyst) wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 (U-23), kabla ya kufanya majukumu kama hayo akiwa Al Duhail ya huko pia. Al Sadd ni moja ya timu kubwa nchini humo, iliyokuwa ikinolewa na gwiji wa zamani wa Hispania, Xavi Hernandez, kabla kurejea Barcelona, akiwa kama Kocha Mkuu. Omary, mzaliwa wa Somalia aliyekulia England na kuchukua uraia wa huko, pia alikuwa Kocha Msaidi

NANI KUCHEZA NA NANI 16 BORA ASFC

Image
MECHI za Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) zitachezwa mwishoni mwa Februari zikihusisha timu 13 za Ligi Kuu, moja ya Championship ambayo ni Pamba na mbili za Daraja la Kwanza, ambazo ni Baga Friends na Mbuni FC.

MAN UNITED YAMSIMAMISHA MASON GREENWOOD

Image
KLABU ya Manchester United imetangaza kumsimamisha kwa muda mshambuliaji wake, Mason Greenwood ambaye anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga mpenzi wake, Harriet Robson. Harriet aliposti katika ukurasa wake wa Instagram clip ya sauti na video za mwili wake zinazoonyesha namna alivyopigwa na mchezaji huyo wa Man U na Polisi imethibitisha kumshikilia Greenwoon. “Mason Greenwood hatarejea kwenye mazoezi au kucheza mechi hadi ikapotangazwa. Tunafahamu picha na tuhuma zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii. Hatutatoa maoni yoyote zaidi hadi ukweli utakapothibitishwa. Manchester United haikubaliani na vurugu za aina yoyote,” " Imesema taarifa ya Man U.

MISRI NA SENEGAL ZAKAMILISHA NUSU FAINALI AFCON

Image
TIMU ya taifa ya Senegal imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Equatorial Guinea usiku huu Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, Cameroon. Mabao ya Simba wa Teranga yamefungwa na Famara Diedhiou dakika ya 28, akimalizia pasi ya Sadio Mane, Cheikhou Kouyate dakika ya 68 na Ismaila Sarr dakika ya 79, wakati la Equatorial Guinea limefungwa na Jannick Buyla dakika ya 57. Awali ya hapo, Misri ilitangulia Nusu Fainali kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Morocco hapo hapo Ahmadou Ahidjo katika mchezo uliodumu kwa dakika 120. Sofiane Boufal alianza kuifungia Morocco kwa penalti dakika ya sita na Mohamed Salah akaisawazishia Misri dakika ya 53, kabla ya nyota huyo wa Liverpool kumsetia Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan ‘Trezeguet’ kufunga la ushindi dakika ya 100. Sasa Misri itakutana na wenyeji, Cameroon Alhamisi baada ya Senegal kumenyana na Burkina Faso katika Nusu Fainali ya kwanza Jumatano.

SIMBA SC YAFUTA GUNDU KWA DAR CITY, YAICHAPA 6-0

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Dar City usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na wageni watupu, mshambuliaji Mnyarwanda mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere mawili dakika ya tano na 13, viungo Wazambia, Clatous Chama dakika ya 18 na Rally Bwalya dakika ya 22, beki Muivory Coast, Pascal Wawa dakika ya 48 na mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu dakika ya 80. Mechi nyingine za 32 Bora leo, Mtibwa Sugar imewatoa wenyeji, African Sports kwa penalti 4-2 baada y sare ya 0-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na Kagera Sugar imewachapa wenyeji, African Lyon 4-0, Meshack Abraham akipiga hat trick, lingine akifunga Abeid Athumani.

YANGA SC 1-0 MBAO FC (KOMBE LA TFF)

Image
 

CAMEROON NA BURKINA ZATINGA NUSU FAINALI AFCON

Image
WENYEJI, Cameroon wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Gambia jana Uwanja Douala. Mabao ya Cameroon jana yalifungwa na mshambuliaji wa Lyon ya Ufaransa, Karl Brillant Toko Ekambi yote mawili dakika ya 50 na 57 na sasa watakutana na Brukinha Faso, ambayo imeitoa Tunisia kwa kuichapa 1-0, bao pekee la Dango Ouattara dakika ya 45 na ushei Uwanja wa Roumde Adjia, Jijini Garoua. 

MAYELE AIPELEKA YANGA 16 BORA KOMBE LA TFF

Image
VIGOGO. Yanga SC wamefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza jioni ya leo. Bao pekee la Yanga leo limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Mkongo Fiston Kalala Mayele dakika ya 54 kwa kichwa akimalizia krosi maridadi ya kiungo  mzawa, Farid Mussa Malik kutoka kulia.

SHABANI NA MAREFA YANGA NA POLISI WAFUNGIWA

Image
BEKI Mkongo wa Yanga SC, Djuma Shabani amefungiwa mechi tatu za kutozwa faini ya Sh. Milioni 1 kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu baina ya timu hizo. Taarifa ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imesema kwamba pamoja naye, refa Hance Mabena na wasaidizi wake, Paschal Joseph na Jackson Samuel wote wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kadhaa wa Ligi Kuu kwa mechi tatu hadi tano kwa kutochukua hatua dhidi ya tukio hilo.

KOCHA WA SIMBA AFUNGIWA NA FAINI MILIONI 2

Image
KOCHA Mspaniola wa Simba SC, Pablo Franco Martin ametozwa faini ya Sh. Milioni 2 jumla kwa makosa mawili yanayofanana na kufungiwa mechi tatu kwa kupiga chupa chini kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar. Taarifa ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imesema kwamba Pablo ametozwa faini ya Sh. Milioni 1 kila mchezo dhidi ya Mtibwa na dhidi ya Kagera Sugar kwa kukataa kufanyiwa mahojiano na Waandishi wa Habari baada ya mechi hizo za ugenini.

HERSI AONYWA, MASHABIKI WAIPONZA COASTAL

Image
KIONGOZI wa klabu ya Yanga, Hersi Said amepewa onyo kali kwa kosa la kuingia uwanjani kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Taarifa ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imesema kwamba nayo Coastal imetozwa faini ya Sh. Milioni 1 baada ya mashabiki wake kumtupia chupa mchezaji wa Yanga wakati akishangilia.

SIMBA NA YANGA ZATOZWA FAINI KWA MAKOSA TOFAUTI

Image
KLABU za Simba na Yanga zote zometozwa faini kwa makosa kadhaa kwenye michezo yake ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwezi huu, Taarifa ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imesema.

MAREFA WA KIKE WA TANZANIA KUCHEZESHA KOMBE LA DUNIA

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limewateua marefa wa kike wa Tanzania, Florentina Zabron, Janeth Balama, Helen Mduma na Tatu Malogo kuchezesha mechi ya kufuzu Kombe la Dunia kwa Wasichana U17 baina ya Djibouti na Burundi kati yaMachi 4 na 6 Jijini Bujumbura.

REFA KOMBA APEWA MAJUKUMU MENGINE NA CAF

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika limemteua refa wa Tanzania, Frank Komba katika orodha ya Waamuzi watakaochezesha mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Raja Club Athletic na Amazulu ya Afrika Kusini. Mechi hiyo itafanyika Februari 12, mwaka huu Uwanja Wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco na Kombe atakwenda huko baada ya kumaliza majukumu yake ya sasa kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Cameroon kwa sasa. Aidha, CAF pia imemteua Meneja Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto kuwa Mratibu wa mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa baina ya wenyeji, Mamelodi Sundowns na Al Hilal ya Sudan Februari 11 nchini Afrika Kusini. Naye Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo ameteuliwa na CAF kuwa Ofisa Habari wa mchezo wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho kati ya wenyeji, Simba SC na ASEC Mimosas ya Ivory Cost utakaochezwa Februari 13 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaa

MILIKI NYUMBA YA NDOTO YAKO FUMBA

Image
Unaweza kumiliki nyumba ya ndoto zako Zanzibar. Karibu Fumba Uptown Living, Zanzibar. You can own your dream house in Zanzibar. Welcome to Fumba Uptown Living, Zanzibar.

DODOMA JIJI, POLISI ZASONGA MBELE KOMBE LA TFF

Image
TIMU ya Dodoma Jiji FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Sumbawanga United usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na Khamis Mcha mawili, moja kwa penalti dakika ya tisa na lingine dakika ya 22, wakati mengine yamefungwa na Seif Abdallah Karihe dakika ya 30 na Anuary Jabir dakika ya 80. Mechi nyingine za 32 Bora michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Polisi Tanzania imeitoa Ndanda FC kwa kuichapa 3-1, wakati Bagamoyo Friends imeitoa Catamine kwa kuichapa 2-1.

YANGA WAKIIFANYIA MAZOEZI MBAO FC LEO KIRUMBA

Image
KIUNGO mpya Mkongo wa Yanga, Chico Ushindi akifanya mazeozi leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kujiandaa na mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Mbao FC. Kiungo mpya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ akifanya mazeozi leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao FC Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Wachezaji wa Yanga wakifanya mazeozi leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao FC Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

SIMBA SC WAREJEA KUPOZA MACHUNGU KWA DAR CITY

Image
MSHAMBULIAJI Mkongo wa Simba SC, Chris Kope Mutshimba Mugalu aliteremka kwenye ndege baada ya ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kutoka Bukoba ambako jana walifungwa 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba. Simba SC itateremka tena dimbani Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salam kumenyana na Dar City katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC). Ikumbukwe Simba haijapata ushindi katika mechi tatu zilizopita kufuatia kufungwa 1-0 mara mbili, nyingine na Mbeya City na sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar, zote ugenini.

HAPPY BIRTHDAY MHE RAIS SAMIA

Image
Tunamtakia Heri ya Kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿�� We wish a Happy Birthday to Her Excellency Samia Suluhu Hassan, The President of The United Republic of Tanzania 🇹🇿

KAGERA SUGAR 1-0 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

MISRI YATINGA ROBO FAINALI AFCON, IVORY COAST NA MALI NJE

Image
MABINGWA wa kihistoria, Misri wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa  penalti 5-4 dhidi ya Ivory Coast kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 Uwanja wa Douala nchini Cameroon. Waliofunga penalti za Misri ni Ahmed Mostafa Mohamed Sayed ‘Zizo’, Amr El Soleya, Omar Kamal, Mohamed Abdelmonem na Mohamed Salah. Upande wa Ivory Coast waliofunga ni Nicolas Pépé, Ibrahim Sangaré, Gnaly Cornet na Wilfried Zaha, wakati mkwaju wa Eric Bailly ulipanguliwa na kipa Mohamed Abou Gabal aliyeingia dakika ya 88 kufuatia Mohamed El Shenawy kuumia. Mechi ya mwisho ya Hatua ya 16 Bora, Equatorial Guinea pia ilitinga Robo Fainali kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 6-5 baada ya sare ya bila kufungana na Mali Uwanja wa Limbe. Robo Fainali zitaanza Jumamosi, wenyeji Cameroon wakimenyana na Gambia, Burkina Faso na Tunisia, Jumapili Misri na Morocco Na Senegal dhidi ya Equatorial Guinea, wakati Nusu Fainali zitafuatia Februari 2 na 3 na Fainali ni Februari

MSIMAMO WA LIGI KUU BAADA YA KILA TIMU KUCHEZA MECHI 13

Image
MSIMAMO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ulivyo sasa baada ya mechi 13 za awali za msimu.

KIIZA ATOKEA BENCHI KUIUA SIMBA KAITABA

Image
MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ ametokea benchi kuifungia bao pekee Kagera Sugar ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera. Kiiza aliingia dakika 56 kuchukua nafasi ya Ally Ramadhani na akafunga bao hilo dakika ya 70 akimalizia pasi nzuri ya Ally Nassor ‘Ufudu’, kabla ya Mganda huyo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano. Kagera Sugar inafikisha pointi 17 na kupanda hadi nafasi ya nane, wakati Simba inabaki na pointi zake 25 katika nafasi ya pili, ikizidiwa pointi 10 na vinara, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi 13 za msimu.

MOROCCO NA SENEGAL ZATINGA ROBO FAINALI AFCON

Image
MOROCCO imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Malawi katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika usiku huu Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé nchini Cameroon. Malawi ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Hellings Frank ‘ Gabadinho’ Mhango dakika ya saba, kabla ya mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri kuisawazishia Morocco dakika ya 45 na ushei na beki wa Paris-Saint Germain, Achraf Hakimi Mouh kufunga la ushindi dakika ya 70 kuwapeleka Robo Fainali Simba wa Atlasi. Katika mchezo uliotangulia, Senegal ilikwenda Robo Fainali pia baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya  Cape Verde, mabao ya washambuliaji, Sadio Mané wa Liverpool dakika ya 63 na Cheikh Ahmadou Bamba Mbacke Dieng wa Marseille dakika ya 90 na ushei Uwanja wa Bafoussam. Cape Verde ilicheza pungufu kwa muda mrefu, kufuatia wachezaji wake wawili kutolewa kwa kadi nyekundu,kiungo Patrick Andrade dakika ya 21 na kipa Josimar José Évora Dias  ‘Vóz

SITA WAFARIKI WAKIGOMBEA KUINGIA UWANJANI CAMEROOB

Image
WATU wasiopungua sita wamefariki na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea nje ya Uwanja wa Olembe Jijini Yaounde wakigombea kuingia kutazama mechi baina ya wenyeji wa Fainali za AFCON, Cameroon dhidi ya Comoro jana – Serikali ya nchi hiyo imethibitisha na kusema kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka. Maafisa wa hospitali ya Messassi wamesema wamepokea kiasi cha watu 40 waliojeruhiwa, ambao walikimbizwa hospitalini hapo na Polisi na wasamaria wema – na chanzo cha vurugu hizo imeelezwa ni walinzi ‘Stewards’ kufunga mageti kuzuia watu zaidi kuingia uwanjani – na baada ya tafrani hiyo ilishuhudiwa viatu, kofia na mawigi vikizagaa chini. Katika mechi hiyo ya Hatua ya 16 Bora, Cameroon ilishinda 2-1 na kwenda Robo Fainali.  Pamoja na hayo, Hatua ya 16 Bora ya AFCON inaendelea leo kwa mechi mbili, washindi wa pili wa 2019 Senegal wakimenyana na Cape Verde Saa 1:00 usiku na Morocco dhidi ya Malawi Saa 4:00 usiku. Kocha wa Morocco, Vahid Halilhodzic amesema kambi yak