Posts

Showing posts from February, 2019

YANGA WAIPA MCHONGO STAND UNITED KUIMALIZA SIMBA

Image
KIKOSI cha Simba, Jumapili hii kinashuka uwanjani kupambana na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. Simba itashuka katika mchezo huo, huku ikiwa na kumbukumbu ya kuibu­ka na ushindi wa nguvu hivi karibuni ilipopambana na Lipuli FC huko mkoani Iringa ambako ilishinda mabao 3-1. Hata hivyo, uongozi wa benchi la ufundi la Stand United, umeweka wazi mipango yake iliyojiwekea kwa ajili ya kuhakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ush­indani mkubwa ambapo mbinu hizo zinahusiana na timu ya Yanga ambayo ni mahasimu wakubwa wa Simba. Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilali ameliambia Championi Ijumaa kuwa, wamejipan­ga vilivyo kwa ajili ya mechi hiyo na mbinu watakazotu­mia kupata ushindi katika mechi hiyo hazitakuwa na tofauti sana na zile wali­zozitumia dhidi ya Yanga na wakafanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0. “Tunaiheshimu sana Simba, lakini katika mechi yetu ya Jumapili tutahakiki­s

OKWI AIBUA MSALA SIMBA

Image
KIKOSI cha Simba hivi sasa kipo njiani kuelekea mjini Shinyanga kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United itakayochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini humo keshokutwa Jumapili. Hata hivyo, mshambuliaji wa kutumainiwa wa timu hiyo, Mganda, Emmanuel Okwi ataukosa mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa jambo ambalo limezua hofu kubwa kwa mashabiki wa timu hiyo. Mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Simba ambaye ameomba kutotajwa jina lake, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, Okwi atau­kosa mchezo huo ili aweze kupona vizuri jeraha lake aliloumia chini ya jicho katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC. Okwi alipata jeraha hilo baada ya kugongana na kiungo msham­buliaji wa Azam FC, Mghana Enock Agyei wakati waki­wania mpira na kujikuta akidondoka chini na kupoteza fahamu. “Kwa hiyo, katika mechi yetu hiyo na Stand, Okwi hatakuwepo na hivi sasa yupo Dar es Salaam, kocha alimruhusu aje kupumzika kwani katika mechi dhidi ya Lipuli alicheza lakini alikuw

HUKU NDIKO STAND WALIPOWEKA MAFICHO TAYARI KUWALIZA SIMBA WALIO NJIA KUELEKEA SHINYANGA

Image
Kikosi cha klabu ya Simba kimeondoka mjini Singida asubuhi ya leo kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mechi na Stand United Jumapili hii. Simba wameondoka Singida walipoweka mapumziko ya muda mfupi kisha kuendelea na mazoezi jana kwenye Uwanja wa Namfua. Wakati Simba wakiwa njiani, wapinzani wao Stand United wameweka kambi Bariadi, Simiyu tayari kwa kuandaa dawa maalum ya kuwamaliza Simba. Stand wametamba kuhakikisha wanaimaliza Simba ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 48. Imeelezwa mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu zaidi mkoani humo haswa kutokana na namna Simba ilivyosheheni wachezaji wengi walio na majina makubwa.

KMC WAPANIA KUFUNGA BIASHARA MAPEMA

Image
UONGOZI wa KMC umesema kuwa kesho wataonyesha namna ya ubora wa kikosi chao kilivyo kwa kikosi cha wafanyabiashara kutoka Mara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru. KMC kesho wataikaribisha Biashara United kwenye mchezo wa ligi kuu ikiwa ni mzunguko wa pili. Ofisa Habari wa KMC, Anuwari Binde amesema wanatambua ushindani uliopo kwenye ligi na namna kila timu inavyotafuta matokeo ila wao wataonyesha utofauti. "Kikosi kipo sawa na tupo tayari kwa mapambano, tutaingia uwanjani tukiamini kwamba tunacheza na timu ngumu, ila kikubwa tutakachofanya ni kutumia vema Uwanja wa nyumbani," amesema Binde. KMC imecheza michezo 27 ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 40, ni kinara kwa timu zote ambazo zimepanda daraja msimu huu.

VIDEO- FULANA YA ZAHERA YAIBUA MSALA, USHIRIKINA WATAJWA, MWENYE AIBUKA NA KUKANUSHA

Image
Kocha ya Yanga Mwinyi Zahera amekanusha uvumi kuwa anatumia ndumba kushinda mechi kutokana na aina yake ya Tisheti yake kuwa ya aina moja hasa pale anapokua katika benchi la ufundi pale timu yake inapocheza.

RUVU SHOOTING NDIYO TIMU INAYOFUATILIWA ZAIDI KWA SASA TANZANIA BARA

Image
Hauwezi amini lakini ndiyo maneno ya Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire, ameibuka na kusema kuwa timu yake ndiyo inayofuatiliwa zaidi kwa sasa. Bwire ambaye ni msemaji asiyeishiwa na maneno, ameeleza namna ya soka ambalo Ruvu Shooting inacheza inasababisha timu yake kufuatiliwa kuliko kawaida. Amefunguka kuwa Ruvu inacheza soka la kisasa ambalo timu nyingine zinashindwa kuhimili aina ya mchezo huo wa soka na kuifanya timu izidi kuwa na wadau wengi. "Hakuna timu ambayo inafuatiliwa zaidi kama Ruvu Shooting kwa sasa, tuko vizuri na tunapiga soka la kisasa kabisa na ndiyo maana tunazungumziwa kila iitwapo leo" alisema.

KIFAA KIMOJA CHONGEZWA YANGA

Image
Baada ya kutoonekana dimbani kwa mechi kadhaa, kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko, amejumuishwa katika wachezaji watakaocheza dhidi ya Alliance FC. Kamusoko ambaye alikuwa majeruhi amejiunga na wachezaji wenzake kuelekea mechi ya kesho na Alliance ambayo itapigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Kurejea kwa Kamusoko inaweza kuwa chachu ya nafasi ya kiungo kwa Yanga kuongeza makali haswa katika upikaji wa mipira kuelekea eneo la ushambuliaji. Wakati huo Yanga imeendelea na mazoezi jana na leo itafanya ya mwisho kabla ya kukipiga na Alliance. Kuelekea mechi hiyo, Yanga mpaka sasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 61 dhidi ya Azam yenye 50 na Simba ikiwa na 48.

DUH KUMBE BADO BAO 3 ZA SIMBA ZINAISHI LIPULI, HASIRA ZAO SASA WANAZIPELEKA HUKU

Image
KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa wachezaji wake bado wana maumivu ya kupoteza mbele ya Simba na wameahidi kumaliza hasira zao kwa Kagera Sugar kwani mchezo ulikuwa mkononi mwao makosa yao yaliwaponza. Akizungungumza na Saleh Jembe, Matola amesema mapema tu alimaliza mchezo kutokana na mbinu kali alizowapa wachezaji wake ila bahati haikuwa upande wake hali iliyomfanya apoteze mchezo wake aliopania kupindua meza kibabe kabla ya mechi. "Unajua mpira una matokeo ya kushangaza, tuliwazidi mbinu kipindi cha kwanza ila makosa madogo tuliyofanya tukapoteza kwa kufungwa, hamna namna hesabu zetu ni kwa mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar. "Wachezaji waliumia na wana hasira za kupoteza hivyo imani yangu ni kuendelea kutoa dozi kwa wapinzani wetu ila hawa Simba, we acha tu sio poa kubeba poini tatu nyumbani acha tu," amesema Matola. Simba inakuwa timu ya kwanza kuvunja uteja dhidi ya Lipuli kwani tangu Lipuli ipande daraja msimu wa mwaka 2017/18 walikutana mara tatu

MAKAMBO APOTEZWA VIBAYA

Image
SAHAU kabisa kuhusiana na Emmanuel Okwi, John Bocco na huyu Mzambia anayeitwa Claytous Chama. Wala usihangaike na Amissi Tambwe, Ibrahim Ajibu au Mrisho Ngassa. Shoo ya Simba na Yanga sasa imehamia kwa watu wawili tu ambao wametumwa Dar es Salaam tena mitaa ya Kariakoo kutafuta noti. Huku Yanga yupo mtu mtaalam wa kuwajaza, ukizubaa tu kwenye boksi tayari utamkuta kule pembeni akiwajaza na mikono yake. Anaitwa Heritier Makambo. Huku Simba kuna mzee kijicho Meddie Kagere a.k.a MK14. Wote wamefunga idadi ya mabao 12. Sasa sikia balaa la Makambo. Tathmini ya mabao ya Makambo inaonyesha kuwa jamaa ni bora kwenye kuzifumania nyavu kutokana na uwezo wa kutumia mguu adimu wa kushoto kitu ambacho kimekuwa adimu kwa washambuliaji wengi.  Guu hilo limemtofautisha na Kagere ambaye ndiye straika mwiba kwa Simba. Ubora wa Makambo umeonekana kutokana na kuwa na matumizi makubwa ya mguu wa kushoto katika ufungaji wa mabao matano kati ya 12 aliyonayo. Straika huyo ametumia mguu wake wa kushoto k

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Image
MUONEKANO wa 'Backpage' gazeti la CHAMPIONI Ijumaa leo tarehe 1 Marchi 2019

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Image
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele gazeti la CHAMPIONI Ijumaa, leo Marchi 01/2019

HILI LA KUSEMA KILA MMOJA ASHINDE MECHI ZA NYUMBANI NI TATIZO LINALOUA SOKA 'MDOGOMDOGO'

Image
MAUMIVU yanazidi kuwa makubwa kadri siku zinavyozidi kwenda hasa kwa timu ambazo zipo chini kwenye ligi kuu pamoja na uwezo wao kiuchumi kushindwa kuwa bora. Kwa zile ambazo zina matumaini ya kuendelea na safari kwa imani ni chache kwa sasa kutokana na kila mmoja kutumia nafasi aliyonayo kuona anapata matokeo uwanjani hata kwa njia ambazo sio halali. Timu nyingi kwa mzunguko huu wa pili zinazidi kuonewa na vigogo wa ligi ambao wanatafuta mafanikio yasiyo halali hasa kwa kuja na tabia ambayo imeanza kuleta matokeo ambayo ni ya ajabu na huwezi kusema kuna haki. Kwa sasa kumekuwa na mtindo kwenye ligi kwamba kila timu inashinda mchezo wa nyumbani tena kwa mipango na maelekezo kutoka kwa viongozi jambo ambalo naona halipo sawa hasa kwenye soka letu. Nasema haipo sawa kutokana na ukweli kwamba kutengeneza matokeo kabla ya mchezo hili jambo halikubaliki mamlaka husika kwa sasa namaanisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa kuwa macho muda wote kuona haya mambo hayatokei tena.

MECHI ZA SIMBA UGENINI KATIKA LIGI KUU BARA ZILIZOSALIA HIZI HAPA

Image
Hizi hapa mechi za ugenini kwa Simba katika Ligi Kuu Tanzania Bara Machi 3 Vs Stand United- Kambarage, Shinyanga Aprili 6 Vs KMC – Taifa, Dar Aprili 15 Vs Coastal Union-Mkwakwani, Tanga   Aprili 19 Vs Kagera Sugar- Kaitaba, Bukoba Aprili 22 Vs Alliance- CCM Kirumba, Mwanza Aprili 25 Vs Biashara- Karume, Musoma Aprili 30 Vs Prisons- Sokoine, Mbeya Mei 22 Vs Singida Utd- Namfua, Singida Mei 3 Vs Mbeya City – Sokoine, Mbeya Mei 26 Mtibwa Sugar- Jamhuri, Morogoro

ISHU YA ZAHERA KUTIMKIA AZAM FC KUBEBA MIKOBA YA PLUIJM IPO NAMNA HII

Image
UONGOZI wa Azam FC, unatambua ubora wa kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera na namna anavyoibeba timu yake hali iliyofanya watoe tamko lao namna wanavyopasua kichwa kumpata mbeba mikoba wa Hans Pluijm na Juma Mwambusi pamoja na tetesi za kumpa shavu kocha huyo. Ofisa Habari wa Azam FC, Jafary Maganga amesema mchakato wa kumtafuta kocha unaendelea na katika makocha walioomba ajira kukinoa kikosi hicho hakuna jina la Zahera wa Yanga. "Wengi wameomba ajira ya kukinoa kikosi cha Azam kwa sasa, ila katika orodha ya majina hayo hakuna jina la kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, hivyo mashabiki wa Yanga wasiwe na presha. "Tunatambua kazi anayoitenda Zahera ndani ya Yanga, anatimiza majukumu yake kwa kiwango kinachowafanya mashabiki wawe na furaha ila uongozi wa Azam FC haujakaa na kuzungumza naye mpaka sasa, suala la kocha ni gumu linahitaji muda wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa kwa sasa bodi bado inajadili," amesema Maganga. Matokeo mabovu kwenye ligi yametajwa sababu ya

ALIKIBA NA MKEWE WAPATA MTOTO WA KIUME

Image
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva na mkurugenzi wa Rockstar, Alikiba amethibitisha kupata mtoto wa kiume baada ya mke wake, Amina kujifungua. Kupitia ukurasa wa Snapchat msanii huyo amepost picha zikionesha sura na miguu ya mtoto. ikidaiwa mke wake Amina amejifunua jana. Baada ya muda kidogo msanii huyo ali-post clip fupi ya video ikiwaonyesha watoto wakituma salamu kwa msanii huyo wakimwambi “Hongera kwa kupata mtoto wa kiume na mlinde mtoto kwa ajili yetu.” Alikiba na mke wake wanasherekea ujio wa mtoto wao huyo ikiwa ni miezi michache tangu kufunga kwa ndoa yao mwaka jana na mke wake amina kutoka nchini kenya.

SPOTI HAUSI: SERIKALI YAIPA UGUMU SIMBA KULIPA KISASI - VIDEO

Image

SERIKALI YAMWAGA AJIRA MPYA ZA WALIMU 4,549

Image
SERIKALI imetangaza nafasi za ajira 4,549 za walimu wa shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kupunguza uhaba wa walimu ulipo nchini. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,amesema Serikali inajua kuwa kuna changamoto nyingi katika sekta ya elimu nchini hasa uhaba wa walimu hivyo itaajiri walimu ili kupunguza uhaba uliopo. Hata hivyo Jafo amesema kuwa ajira hizo mpya kwa waombaji zinapaswa kuombwa kwa njia ya mtandao na mwisho wa kupokea maombi utakuwa Machi 15, mwaka huu. ”Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli inaendelea kuongeza idadi ya watumishi katika sekta ya umma kwa kutoa nafasi mbalimbali za ajira kwa vijana wa kitanzania katika sekta ya Elimu” amesema Jafo. Waziri Jafo amesema kuwa Ofisi ya Rais Tamisemi inawatangazia walimu wenye sifa hizo kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao (Online Teacher Employment Application System-OTEA

MJADALA HOT: MSANII KUBISHANA NA WAZIRI NI SAHIHI?

Image
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, jana aliliamuru Jeshi la Polisi na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumkamata Msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini a.k.a Dudu Baya kutokana na kauli zake. Waziri Mwakyembe alifikia hatua hiyo baada ya Dudu Baya kumsema vibaya marehemu Ruge Mutahaba. Mara baada ya waziri kutoa amri hiyo, Dudu Baya aliibuka tena na kumwambia waziri asisumbue polisi, wasipeleke magari kumkamata bora wakakamate majambazi, badala yake awaambie polisi atakwenda mwenyewe iwe Kituo cha Polisi Oysterbay, Mabatini, Salender Bridge au Central. Je, msanii kubishana na waziri kama hivyo ni sawa? Jadili; tafadhali usitukane.

SIMBA NA YANGA KUANZIA DAR

Image
YANGA na Simba zitaanzia nyumbani kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Wanawake utakaoanza Machi 9. Simba wataikaribisha Tanzanite kutoka Arusha huku Yanga wakianza na Alliance Girls kutoka Mwanza. Kwa upande wa Yanga wao wamefanya usajili wa wachezaji tisa katika dirisha la usajili lililofungwa Februari 25, tofauti na Simba ambao wameongeza mchezaji mmoja tu. Everyine Oppa ambaye anacheza katika nafasi ya ushambuliaji. Katika msimamo wa michuano hiyo Simba Queens inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 22,Yanga wao ni wa saba wakiwa na pointi 13.

MDUDU HUYU ANATIBUA SOKA LETU, SERENGETI BOYS MSIJISAHAU

Image
KIPINDI cha lala salama ni kipindi hatari kuliko vipindi vyote tunavyopitia hasa kwenye ligi zetu ambazo zinasimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na matapeli wengi kujitokeza kuongoza upatikanaji wa matokeo. Kwa sasa ni muda ambao huamua nani atabeba ubingwa wa ligi kwa upande wa Ligi Kuu Bara na ni nani atakayeshuka daraja baada ya mzunguko wote kukamilika haya mambo kama yakichukuliwa kiwepesi lazima uumie kwani huwa yanaleta usumbufu. Ipo wazi kwamba hakuna timu ambayo imepanda daraja na ina mpango wa kushuka daraja kwa sasa kila mmoja anapambana ili abaki ligi kuu sasa hapo ndio unaona kasheshe linaanzia hapo. Kama matokeo ambayo yanapatikana uwanjani yangekuwa hayana ukakasi hapo tungesema tumefika sehemu nzuri ila kiukweli hali ni mbaya mzunguko huu wa lala salama kila mmoja anazungumza vile anavyotaka ama namna ambavyo anaona mwenendo wa ligi unakwenda. Pia hata kwa wale wa Ligi Daraja la Kwanza nao wamekuwa wakipata shida timu zao kupata matokeo chanya

VIDEO: KIKWETE ATOA NENO LAKE ZITO JUU YA MAREHEMU MSIBA WA RUGE MUTAHABA

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili msibani nyumbani kwa Baba mzazi wa Aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba, aliyefariki dunia juzi Februari 26, 2019, akiwa nchini Afrika Kusini alipokuwa akipata matibabu.

KIBARUA KINGINE KIGUMU KWA AZAM FC HIKI HAPA

Image
BAADA ya kocha aliyeachiwa mikoba na Hans Pluijm pamoja na Juma Mwambusi, Idd Cheche wa Azam FC kutinga hatua ya nane bora ya kombe la Shirikisho mtihani wake wa kwanza Ligi Kuu Bara ni kesho. Azam itakaribishwa na African Lyon kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Uhuru ikiwa ni mara ya kwanza kuongoza jahazi bila uwepo wa Pluij  kwenye benchi. Cheche amesema kuwa anawatambua vizuri wachezaji wake na anajua namna ya kuwatumia hivyo hana mashaka katika kazi yake. "Nawatambua wachezaji wangu kutokana na uzoefu nilionao hapa kwenye kikosi sina mashaka naamini kila kitu kitakuwa sawa," amesema Cheche. Kwa mujibu wa mratibu wa Azam FC, Philip Alando kuhusu mchakato wa makocha amesema zaidi ya maocha 10 wameomba kazi kwa kutuma CV zao kwenye email hivyo watazipitia ili kujua nani atabeba mikoba ya Pluijm.

USHINDI WA KWANZA 2019 WAWAPA JEURI MTIBWA SUGAR,HIKI HAPA WAMESEMA

Image
BAADA ya Mtibwa wa Sugar kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union, uongozi wa Mtibwa Sugar umesema wamezinduka upya mwaka huu. Mtibwa haikuwa na matokeo chanya katika michezo yake ya mwanzo, ilianza mwaka kwa kupoteza mbele ya Prisons (1-0), Mbeya City (1-0), Lipuli (1-0) ikalazimisha suluhu na JKT (0-0) Ndanda (0-0) ikalazimisha sare na African lyon  (1-1) kabla ya kupoteza kwa  Biashara United (2-1) Mwadui (1-0) na  KMC (1-0). Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobas Kifaru amesema mfululizo wa matokeo mabaya ulikuwa unawapasua kichwa hali iliyowafanya wakae na wachezaji, hivyo kwa sasa wanaona mwanga. "Hatukuwa na matokeo chanya kwenye michezo yetu iliyopita hivyo wa sasa naona kuna kitu kipya kinakuja kizuri kwa ajili ya mashabiki wetu na wadau wa soka. "Upinzani ni mkubwa nasi tunajitahidi kuongeza juhudi, lengo letu kubwa kwa sasa ni kuona tunarejea kwenye nafasi za juu huo ndio mpango wetu mkubwa," amesema Kifaru. Mtibwa Sugar inashika nafasi 12 kwen

MINZIRO AANZA KWA KUCHECHEMEA SINGIDA UNITED, WACHEZAJI WATOA YA MOYONI

Image
KOCHA Msaidizi wa Singida United, Fred Minziro, jana kwenye Uwanja wa Sokoine ameanza kukaa benchi kwa kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0. Miziro ameongezwa kwenye benchi la ufundi baada ya kocha  mkuu, Dragan Popadic kusimamishwa kuongoza timu kwa michezo mitatu kwa kosa la kumzonga mwamuzi kwenye mchezo wao dhidi ya Ndanda. Minziro aliipandisha Singida United Ligi Kuu kabla ya kupigwa chini amerejeshwa na uongozi ili kuendeleza gurudumu la kuinoa timu hiyo. Nahodha wa Singida United, Nizar Khalfan amesema hawezi kutoa maoni kwa mwalimu wao mpya kwa kuwa bado hajakaa na timu muda mrefu. "Tumejituma kutafuta matoko ila tumekwama, uwepo wa mwalimu wetu bado siwezi kuzungumzia kwani hatujakaa naye muda mrefu. "Mtindo uliopo kwa sasa ni kubebana nyumbani, nadhani kuna kampeni ya kila timu ishinde nyumbani, hicho ndiyo kilituponza ila tutaendelea kupambana," amesema Khalfan.

KABLA YA KUWAVAA KMC, BIASHARA UNITED HALI NI TETE, KUWAKOSA WACHEZAJI TISA

Image
KOCHA Mkuu wa timu ya Biashara United, Amri Said amesema kwa sasa timu yake ipo kwenye hali mbaya kiuchumi hali inayofanya wajiendeshe kwa kuungaunga. Said amesema kukosekana kwa mdhamini mkuu kunaathiri ubora wa ligi kwani wachezaji wamekuwa katika mazingira magumu huku kikosi chake cha kwanza kikiwa na wachezaji watatu pekee ambao ni wazima. Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema atawatumia wachezaji wa kikosi cha pili kutokana na wachezaji 9 wa kikosi cha kwanza kusumbuliwa na malaria na wengine kusumbuliwa na majeraha. "Tunapitia kwenye kipindi kigumu kwa sasa kwani ligi ni ngumu na kila timu inatafuta matokeo, kikosi changu kipo sawa ila nitawakosa wachezaji wangu muhimu 9 kwenye mchezo wangu dhidi ya KMC. "Nimewavuta vijana wa timu b kwa ajili ya kutafuta matokeo, uchumi kwetu ni mgumu na mambo ni mengi kwetu, hivyo wadau watupe sapoti katika hili maana hakuna namna tunajikongoja kwa sasa," amesema Said. Biashara United itamenyana na KMC uwanja wa Uhuru J

ALLIANCE :TUTAWAFUNDISHA YANGA NAMNA SOKA LINAVYOCHEZWA

Image
UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa utatumia uwanja wa nyumbani wa CCM Kirumba kuwapeleka darasani wachezaji wa Yanga ili kupata pointi tatu. Alliance wataikaribisha Yanga ambao ni vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza michezo 25 huku wao wakiwa nafasi ya 7 na wakiwa wamekusanya pointi 36 baada ya kucheza michezo 28. Kocha mkuu wa Alliance, Malale Hamsini  amesema wanatambua ushindani uliopo na namna kikosi cha Yanga kilivyo bora ila kazi yao ni moja tu kubeba pointi. "Tayari kwa sasa vijana wameshajibu na mfumo umeanza kueleweka na ndo maana unaona tunapata matokeo chanya, tunaiheshimu Yanga kutokana na uzoefu wao lakini tumejipanga kubeba pointi tatu nyumbani. "Tutawafundisha namna mpira unavyochezwa uwanjani kwa kuwa hiki ni chuo ambacho kinafundisha mpira, wachezaji wangu wengi bado hawana uzoefu ila wale ambao wapo nao wanaendeleza jahazi kwa kasi," amesema Hamsini. 

YANGA WASILI MWANZA KIBABE KUCHUKUA POINTI 3 ZA ALLIANCE NA SI KINGINE

Image
Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Mwanza leo tayari kwa kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Alliance FC. Yanga itacheza na Alliance Machi 2 ambayo itakuwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kuelekea mechi hiyo, Kocha Mwinyi Zahera amesema ligi ina ushindani na wapo tayari kupambana kwa ajili ya kusaka alama tatu. Ikumbukwe Yanga ipo kileleni kwa alama 61 nyuma ya Azam iliyo na 50 na Simba ikiwa na 48. Mechi hiyo inaenda kupigwa huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mechi yake iliyopita dhidi ya Mbao FC

DUDUBAYA AKAMATWA NA POLISI

Image
KAMANDA wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema msanii, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Oyster Bay jijini Dar es Salaam kwa mahojiano kutokana na tuhuma za kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba. Jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe alilielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua ‘Dudu Baya’ kwa kumdhihaki Ruge ambaye alifariki jana nchini Afrika Kusini. Lakini baadaye kupitia akaunti yake ya Instagram, Dudu Baya alimjibu waziri huyo na kusema asisumbuke kuwaagiza polisi wamsake kwani watapoteza mafuta bure, badala yake wamuelekeze ni kituo gani cha polisi akaripoti.

MANARA VIKALI TENA DISMAS TEN INSTA, KISA NDEMLA 'AMEKOSA KIKI'

Image
Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amemvaa tena Msemaji wa Yanga, Dismas Ten kuhusiana na picha ya kiungo wa Simba, Said Ndemla aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram. Ten aliweka picha hiyo ambayo Ndemla alikuwa amevaa jezi yenye rangi ya njano na kuandika "Rangi ya njano kwenye bendera yetu tukufu ya Tanzania ina maana ya kutukumbusha juu ya utajiri wa madini tuliyonayo... Mambo mengi, muda mchache.. Tusubiri joto lipungue". Kutokana na POSTI hiyo, Manara naye alimjibu namna hii "Baada ya kukosa kiki kuhusu Uchawi na Madawa Vyumbani,yule yule anaependa kuzua kaja na Porojo nyingine!! "Guys Hayupo mchezaji kwa sasa anaeweza kuhama Simba akaenda klabu ambayo hawajui Shibe yao ya kesho!! Puuzeni Takataka zinazoandikwa kimafumbo, Ndemla ni sehemu ya klabu bingwa ya nchi"

LUKAKU, WILSON, JOVIC: TETESI KUBWA NA KALI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO ALHAMIS

Image
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 25, anapania kujiunga na Juventus endapo atalazimishwa kuondoka Manchester United. (Sun) QPR huenda wakahamia uwanja wao mpya wenye uwezo wa kuhimili mashabiki 45,000 kama sehemu ya mradi wa maendeleo uliyogharimu euro milioni 425. (Mail) Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anataka kutumia euro milioni 40 kumjumuisha mshambuliaji wa Bournemouth na England Callum Wilson, 27 katika kikosi chake. (Sun) Manchester City wanamfuatilia mshambuliaji wa Benfica na Serbia Luka Jovic, ambaye anaichezea Eintracht Frankfurt kwa mkopo. (Mail) Chelsea ni miongoni mwa vilabu vya ligi ya Primia vinavyomtafuta kiungo wa kati wa Croatia na Maritimo Josip Vukovic, 26. (Talksport) Arsenal imemuita nyumbani kipa wake Emiliano Martinez ambaye amekuwa akichezea Reading kwa mkopo. Emiliano anatarajiwa kuwa mlinda lango wa pili kwasababu hawana uwezo wa kumnunua kipa mwingine kuchukua nafasi ya Petr Cech anayeelekea kustaafu. (Sun) Meneja wa Leeds United David Hoc

BEKI SIMBA APEWA HESHIMA YA KIPEKEE

Image
KATIKA kuonyesha kuwa uwezo wake umekubalika ndani ya kikosi cha Simba, mashabiki wa timu hiyo, juzi walimpa heshima ya pekee beki wao, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast. Mashabiki hao walifanya hivyo wakati kikosi cha Simba kilipokuwa kikiingia uwanjani tayari kuikabili Lipuli kwenye Uwanja wa Samora, Iringa. Championi lilishuhudia tukio hilo ambapo wakati wachezaji wa Simba walipoanza kushuka kwenye basi lao, mashabiki walionekana kuwa kwenye hali ya kawaida, lakini ilipofika zamu ya Wawa, wale wote waliokaa jukwaa kuu waliinuka na kuanza kumshangilia kwa kumpigia makofi. Hali hiyo ilichukua muda kidogo jambo ambalo lilidhihirisha wazi Wawa ni kipenzi cha mashabiki wa Simba. Wakati mashabiki hao wakiibuka na shangwe hilo baada ya kumuona Wawa, hali ilizidi baada ya Meddie Kagere naye kushuka kwenye basi.