DUH KUMBE BADO BAO 3 ZA SIMBA ZINAISHI LIPULI, HASIRA ZAO SASA WANAZIPELEKA HUKU


KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa wachezaji wake bado wana maumivu ya kupoteza mbele ya Simba na wameahidi kumaliza hasira zao kwa Kagera Sugar kwani mchezo ulikuwa mkononi mwao makosa yao yaliwaponza.

Akizungungumza na Saleh Jembe, Matola amesema mapema tu alimaliza mchezo kutokana na mbinu kali alizowapa wachezaji wake ila bahati haikuwa upande wake hali iliyomfanya apoteze mchezo wake aliopania kupindua meza kibabe kabla ya mechi.

"Unajua mpira una matokeo ya kushangaza, tuliwazidi mbinu kipindi cha kwanza ila makosa madogo tuliyofanya tukapoteza kwa kufungwa, hamna namna hesabu zetu ni kwa mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar.

"Wachezaji waliumia na wana hasira za kupoteza hivyo imani yangu ni kuendelea kutoa dozi kwa wapinzani wetu ila hawa Simba, we acha tu sio poa kubeba poini tatu nyumbani acha tu," amesema Matola.

Simba inakuwa timu ya kwanza kuvunja uteja dhidi ya Lipuli kwani tangu Lipuli ipande daraja msimu wa mwaka 2017/18 walikutana mara tatu na waliishia kugawana sare kwenye michezo hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA