Posts

Showing posts from June, 2023

NI MTIBWA NA GEITA GOLD FAINALI LIGI YA VIJANA U20

Image
TIMU za Mtibwa Sugar na Geita Gold zimefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya kuzitoa Azam FC na Kagera Sugar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Katika Nusu Fainali ya kwanza Geita Gold imeichapa Kagera Sugar 2-0, mabao ya Saluja Mhoja na Frank Maganga na Nusu Fainali ya pili Mtibwa Sugar ikailaza Azam FC 2-1. Mabao yote ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Athumani Makambo huku la Azam FC likifungwa na David Chiwalanga. Fainali itapigwa Jumapili hapo hapo a Chamazi ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu katí ya Kagera Sugar na Azam FC.

DIRISHA LA USAJILI LIGI KUU KUFUNGULIWA JUMAMOSI HADI AGOSTI 31

Image
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema dirisha la usajili kwa timu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, Daraja la Kwanza na Ligi Kuu ya Wanawake linatarajiwa kufunguliwa Jumamosi ya Julai 1 hadi Agosti 31.

LISAJO ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI AZAM FC

Image
BEKI mahiri kiraka, Lusajo Mwaikenda ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuendelea kuichezea Azam FC hadi mwaka 2025.

TWIGA STARS YASONGA MBELE BILA JASHO KUFUZU OLIMPIKI 2024

Image
TIMU ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, “Twiga Stars” imefuzu kucheza Raundi ya Pili ya kufuzu Michezo ya Olimpiki 2024 Paris  baada ya Kongo kujiondoa. Sasa Twiga Stars iliyo chini ya kocha Bakari Nyundo Shime itacheza na Botswana katika Raundi ya Pili ya kuwania tiketi ya Paris 2024 mwezi Oktoba ikianzia nyumbani. 

ABDALLAH KHERI AONGEZA MKATABA AZAM FC HADI 2026

Image
BEKI wa katí, anayeweza kucheza pembeni pia, Mzanzibari Abdallah Kheri ‘Sebo’ ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Azam FC hadi mwaka 2026.

YANGA SC YAACHANA NA KIPA ERICK JOHOLA

Image
KLABU ya Yanga imeachana na kipa wake nne, Erick Johola baada ya misimu miwili tangu awasili Jangwani akitokea Aigle Noir ya Burundi. Erick Johola anakuwa mchezaji wa sita kuachwa Yanga baada ya beki, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, kiungo Mzanzibari Feisal Salum aliyeuzwa Azam FC, mawinga Mghana, Bernard Morrison, Mkongo Tuisila Kisinda na mzawa, Dickson Ambundo. Yanga pia imeachana na Kocha wake Mkuu, Mtunisia Nasredeen Nabi na Kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov na kuajiri Kocha mpya, Muarngentina Miquel Angel Gamondi.

AZAM. MTIBWA KAGERA NA GEITA GOLD ZATINGA NUSU FAINALI LIGI YA U20

Image
TIMU za Azam FC, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Geita Gold zimefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Vijana U20 baada ya ushindi kwenye mechi zao za leo za Robo Fainali Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Azam FC imewatupa nje Tanzania Prisons kuwa kuwachapa 3-1, mabao yao yakifungwa na Asharfu Kibeku, George Chande na Abdulkarim Kiswanya, la wapinzani wao likifungwa na Iddy Kichindo. Mtibwa Sugar imewatoa Coastal Unión kwa kuwachapa 2-0, mabao ya Athumani Makambo na Said Makambo, wakati Kagera Sugar imetupa nje Dodoma Jiji kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Said Said na Kassim Fakhi huku. Geita Gold ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufungua milango ya Nusu Fainali baada ya kuizaba Mbeya City 2-1. Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Nicodemus Ntarema na Shijja Abdallah, huku la Mbeya City likifungwa na Baraka Mwilubunju. Nusu Fainali zitapigwa Ijumaa hapo hapo Azam Complex, Geita Gold na Azam FC na Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.

YANGA YATOZWA FAINI KWA MASHABIKI KUSHAMBULIA STEWARDS SOKOINE

Image
KLABU ya Yanga imetozwa faini ya Sh. Milioni 1 baada ya mashabiki wake kuwarushia chupa walinzi wa Uwanja wa Sokoine wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City.

AZAM FC YASAJILI MCHEZAJI KUTOKA RAJA CASABLANCA

Image
KLABU ya Azam FC imemtambulisha kiungo wa Kimataifa wa Gambia,  Gibril Sillah kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao baada ya kufikia makubaliano na klabu yake, Raja Club Athletic ya Morocco. “Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano na klabu ya Raja AC ya kumnunua kiungo wao mshambuliaji Gybrill Sillah,” imesema taarifa ya Azam. Nyota huyo wa Gambia, anatarajiwa kutua nchini muda wowote kuanzia sasa kumalizia taratibu za mwisho za usajili. Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu ya Morocco, Sillah alifanikiwa kufunga jumla ya mabao saba na kutoa pasi za mwisho nne, wakati akiwa kwa mkopo JS Soualem. Huyo anakuwa mchezaji mpya wa pili tu Azam FC baada ya kiungo mwingine, Feisal Salum Abdallah kutoka Yanga SC.

MALICKOU NDOYE AONGEZA MKATABA AZAM FC HADI 2025

Image
BEKI wa kati, Msenegal Malickou Ndoye amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea na kazi Azam FC hadi mwaka 2025. Ndoye aliyetua Azam FC msimu uliopita akitokea Teungueth  ya kwao, Rufisque msimu ujao ata ataungana na kocha wake wa zamani, Youssouph Dabo.

TANZANIA YAANZA VIBAYA MICHEZO YA AFRIKA SOKA LA UFUKWENI

Image
TIMU ya taifa ya Soka la Ufukweni, imeanza vibaya Michezo ya Afrika baada ya kufungwa na Morocco 6-4 katika mchezo wa Kundi la Kwanza Ufukweni wa Hammamet nchini Tunisia.

BARAZA LA MICHEZO UINGEREZA LAVUTIWA NA MAENDELEO YA MICHEZO NCHINI

Image
KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Uingereza Bi. Katherine Grainger ambapo amesema wamevutiwa na maendeleo ya michezo nchini. Kikao hicho cha Viongozi hao kimefanyika Juni 27, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo wamejadili namna Tanzania na Uingereza kuimarisha ushirikiano katika michezo ambao ni wa kihistoria. Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejikita katika maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika mafunzo ya michezo ambayo yametekelezwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita tangu 2012 wakati Uingereza ilipokuwa inaandaa mashindano ya Olympic ambapo walifundisha walimu wa michezo na kuhimiza watu kushiriki katika michezo. Matokeo baada ya himizo hilo, michezo ya marathoni iliongezeka Tanzania kutoka mashindano mawili mpaka 126 ambayo yapo hadi sasa, michezo ya jogging na kuongezeka kwa idadi ya makocha ambao sasa wanafundisha ligi mbalimbali nchini. Kwa upan

DANIEL AMOAH ASAINI MKATABA MPYA AZAM FC HADI 2025

Image
BEKI wa kati Mghana, Daniel Amoah amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuchezea Azam FC hadi mwaka 2025.

TANZANIA PRISONS YAACHANA NA SHAABAN KISIGA MALONE

Image
KLABU ya Tanzania Prisons imeachana na wachezaji wake watatu, ambao ni Ramadhani Ntabi, Michael Masinda na Shaaban Kisiga ‘Malone’ aliyewahi kuwika Simba SC na SC Villa ya Uganda.

MKURUGENZI WA UFUNDI TFF KATIKA MAFUNZO YA UKOCHA UINGEREZA

Image
MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Oscar Mirambo  akiwa kwenye kozi ya juu ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), UEFA Pro Diploma inayoendelea Uingereza.

SIMBA NA AZAM ZOTE LONYA LONYA LIGI YA VIJANA U20

Image
TIMU za Simba na Yanga zimekamilisha mechi zao za makundi bila ushindi katika Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, michuano inayoendelea Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Yanga imetoa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Kundi B bao la wana Jangwani likifungwa na Fred Dennis huku la Maafande likifungwa na Jackson Hizza. Nayo Simba imechapwa 2-0 na Azam FC mabao ya Daudi Said na Cyprian Kachwele katika mchezo wa Kundi D, huku mechi za leo Dodoma Jiji wakishinda 4-2 dhidi ya Tanzania Prisons Kundi B na Kagera Sugar wakiichapa Ihefu SC 4-0 Kundi D. Azam FC iliyokusanya pointi zote tisa imekwenda Robo Fainali  pamoja na Kagera Sugar iliyomaliza na pointi nne Kundi D, huku Dodoma Jiji ikiongoza Kundi B kwa pointi zake saba mbele ya Tanzania Prisons pointi sita na zote zimekwenda Robo Fainali. Timu nyingine zilizokwenda Robó Fainali ni mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar na Mbeya City kutoka Kundi A na Geita Gold na Coastal Unión kutoka Kundi C. Robo F

TANZANIA PRISONS YAACHANA NA ISMAIL MGUNDA

Image
KLABU ya Tanzania Prisons ya Mbeya imetangaza kuachana na Ismail Mgunda huyo akiwa mchezaji wa pili ndani ya siku mbili baada ya Oscar Paul.

BODI YAANZA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI KUU

Image
BODI ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) imesema maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara yamekwishaanza na matarajio ni kuwa msimu Bora zaidi.

SINGIDA STARS YAMUONGEZEA MKATABA AZIZ ANDAMBWILE HADI 2026

Image
KLABU ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ imemuongezea mkataba kiungo wake Aziz Andambwile hadi mwaka 2026. Aziz Andambwile anakuwa mchezaji wa tatu kuongeza mkataba kutoka kikosi cha msimu uliopita baada ya Mbrazil Bruno Gomez hadi mwaka 2025 na Yusuph Kagoma hadi mwaka 2025. Aidha, Singida Big Stars imeachana na kiungo wake Muargentina, Miquel Escobar baada ya msimu mmoja wa kuwa na timu hiyo.

MTIBWA GEITA GOLD ZATINGA ROBO FAINALI LIGI YA U20

Image
MABINGWA watetezi, Mtibwa Sugar wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Vijana U20 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Said Mkopi na Samuel Mbigiri, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Samson Joseph. Mechi nyingine ya Kundi A jana Mbeya City iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Namungo FC, wakati mechi za Kundi KMC iliichapa Singida Big Stars 3-0 na Geita Gold ikailaza Coastal Unión 1-0. Kwa matokeo hayo Mbeya City inaungana na Mtibwa Sugar kutoka Kundi A kwenda Robo Fainali, wakati kutoka Kundi C Geita Gold wamefuzu kama vinara kwa pointi zao tisa wakifuatiwa na Coastal Union waliomaliza na pointi sita.

SINGIDA FOUNTAIN GATE YAMTIA PINGU KAGOMA HADI 2026

Image
KLABU ya Singida Fountain Gate imemuongezea mkataba wake kiungo Yusuph Kagoma ambao utamuweka kwenye timu hiyo hadi mwaka 2026.

OSCAR PAUL MCHEZAJI WA KWANZA KUACHWA TANZANIA PRISONS

Image
KLABU ya Tanzania Prisons imeachana na kiungo wake Oscar Paul akiwa mchezaji wa kwanza kutemwa kuelekea msimu ujao. “Tunamshukuru Oscar Paul kwa mudawake wote aliyoutumia katika timu yetu. Uongozi unamtakia kila la kheri katika maisha yake mengine nje ya Tanzania Prisons SC,” imesema taarifa ya Prisons.

SIMBA NA YANGA ZALA VICHAPO AZAM YASHINDA LIGI YA U20

Image
VIGOGO, Simba na Yanga wameendelea kuboronga katika Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya wote kufungwa katika mechi za leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Yanga SC imechapwa 3-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Kundi B mabao ya washindi yakifungwa na Emanuel Mbogo, Kelvin Sengati na Iddy Kichindo huku bao pekee la ‘Makinda ya Jangwani’ likifungwa na Ladius Lucas. Mechi nyingine ya Kundi B timu za Dodoma Jiji na Polisi Tanzania zimetoka sare ya 2-2. Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Edward Maliganya na John Nyamba na ya Polisi Tanzania yamefungwa na  Crespo Haule na Baraka Mwambe aliyejifunga. Nayo Simba imechapwa 1-0 na Ihefu SC bao pekee la Ben Ng’wani, wakati Azam FC imeshinda 1-0 dhidi ya Kagera Sugar bao pekee la Cyprian Kachwele katika mechi za Kundi D. Mechi za kwanza Yanga ilichapwa 1-0 na Dodoma Jiji, wakati Simba ilitoka sare ya 0-0 na Kagera Sugar na Azam FC iliichapa Ihefu 1-0 na Prisons iliichapa Polisi Tanzania 4-2.

BRUNO GÓMEZ AONGEZA MKATABA SINGIDA BIG STARS HADI 2025

Image
KIUNGO Mbrazil, Bruno Barroso Gómez ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea na kazi Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ hadi mwaka 2025.

MASHUJAA WAIPIGA TENA MBEYA CITY PALE PALE SOKOINE NA KUPANDA LIGI KUU

Image
TIMU ya Mashujaa ya Kigoma imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa marudiano wa Mchujo wa kuwania kucheza ligi hiyo msimu ujao uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Bao pekee la Mashujaa leo limefungwa na John Budeba dakika ya 87 na kwa kwa matokeo hayo wanapanda kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kushinda 3-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma wiki iliyopita. Mashujaa walifikia hatua hii baada ya kuwatoa Pamba FC ya Mwanza waliokuwa nao Championship, wakati Mbeya City iliangukia hapo baada ya kutolewa na KMC waliokuwa nao Ligi Kuu katika mechi za mchujo wa kwanza. Hii inamaanisha msimu ujao kutakuwa na wageni watatu kutoka Championship, mbali na Mshujaa nyingine ni mabingwa JKT Tanzania na washindi wa pili, KITAYOSCE ya Tabora, wakati timu tatu zimeshuka kutoka Ligi Kuu, pamoja na Mbeya City ni Ruvu Shooting na Polisi Tanzania.

YANGA FAIDA TUPU 2022-2023 KUJENGA UWANJA WA KISASA JANGWANI

Image
KLABU ya Yanga msimu wa 2022-2023 imeingiza jumla ya Sh. Bilioni 17.8 kutokana na mapato mbalimbali, ikiwemo udhamini wao kutoka makampuni ya SportPesa, Azam Media Limited, Haier, GSM Group, Jembe Energy, CRDB Bank, Unicef, Smile na Robbialac. Hayo yamesemwa na Rais wa Yanga, Mhandishi Hersi Ally Said katika Mkutano Mkuu wa mwaka klabu uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Hersi amesema katika fedha hizo, matumzi ya klabu yamemuwa Bilioni 17.3, maana yake Faida ambayo wamevuna kutokana na wadhamini ni Sh. Milioni 500. Aidha, Rais Hersi amesema msimu wa 2022-2023 klabu pia imevuna kiasi cha Bilioni 3.5 kutokana na zawadi za ushiriki wao kwenye mashindano mbalimbali na kwamba kwa msimu ujao Bajeti yao ya matumizi itakuwa zaidi ya Sh. Bilioni 20. Pamoja na kutwaa Ngao ya Jamii, ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Yanga ilishika na

KOCHA MPYA WA YANGA NI MUARGENTINA MIQUEL ANGEL GAMONDI

Image
KLABU ya Yanga imemtambulisha Muargentina, Miguel Ángel Gamondi (59) kuwa kocha wake mpya akirithi mikoba ya Mtunisia, Nasredeen Mohamed Nabi aliyeondoka. Kocha huyo ametambulishwa mchana huu katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Gamondi, ambaye ni mzaliwa huyo wa mji wa Olavarría, alianza kama mchezaji katika klabu ya nyumbani kwao, Ferrocarril Sud na alipostaafu mwaka 1987 akahamia kwenye ukocha. Alianza kufundisha klabu za kwao Ferrocarril Sud, Racing, El Fortín, San Martín de Tucumán na Racing Club de Avellaneda kabla ya kuja barani Afrika. Mwaka 2000 alikuwa Msaidizi wa Muargentina mwenzake,  Oscar Fulloné katika klabu ya Al-Ahly ya Libya kabla ya kuhamia naye timu ya taifa ya Burkina Faso Desemba mwaka 2001. Akawa pia Kocha Msaidizi wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Wydad Casablanca ya Morocco, Espérance na Étoile du Sahel za Tunisia kabla ya kuwa Msaidizi wa  Muargentina mwenzake mwingine, Ánge

WAZIRI WA MICHEZO DK. PINDI CHANA AITA WAWEKEZAJI KWENYE NETIBOLI

Image
WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewakaribisha wadau na wapenda michezo wa sekta binafsi wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika shughuli za michezo hususani mchezo wa Netiboli. Mhe. Chana amesema hayo Juni 23, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mashindano ya Klabu Bingwa ya Netiboli katika viwanja vya Netiboli, Benjamini Mkapa. “Nitoe wito kwa wadau wengine zikiwemo taasisi mbalimbali za ndani na nje kuwekeza katika michezo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kimichezo Pamoja na kugharamia shughuli za michezo hususani michezo ya wanawake pamoja na watu wenye ulemavu” amesema Mhe. Chana Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Dkt. Devota Marwa amesema kuwa wataendelea kuratibu programu mbalimbali za maendeleo ya mchezo huo. Mashindano hayo yamelenga kuchochea ushindani na kupata timu bora ya taifa. PICHA: WAZIRI DK PINDI CHANA AKIFUNGUA KLABU BINGWA NETIBOLI

MTIBWA SUGAR YAENDELEZA UBABE LIGI YA VIJANA U20

Image
MABINGWA watetezi, Mtibwa Sugar wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Athumani Makambo mawili na Ezekiel Zenobi moja na huo ukiwa ushindi wa pili mfululizo baada ya kuichapa Mbeya City 5-0 kwenye mchezo wa kwanza. Mechi nyingine ya Kundi A leo Mbeya City imeshinda 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting, wakati mechi za Kundi C Geita Gold wameiltandika Singida Big Stars 3-1 na Coastal Unión imeilaza KMC 1-0.

HISTORIA YA SHAIBU NINJA YAFIKIA TAMATI YANGA SC

Image
KLABU ya Yanga imetangaza kuchana na beki wake wa katí, Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’, huyo akiwa mchezaji wa tano kuondoka baada ya msimu mzuri wa mafanikio. “Tunamshukuru Abdallah Shaibu (Ninja) kwa mchango wake katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya Young Africans SC,” imesema taarifa Yanga jioni hii. Ninja alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2017 akitokea ya kwao, Zanzíbar kabla ya kuuzwa MFK Vyškov ya Jamhuri ya Czech, mwaka 2019 ambayo ilimpeleka kwa mkopo LA Galaxy II ya Marekani alikocheza hadi mwaka 2020 akarejea Jangwani. Msimu uliopita Ninja alipelekwa kwa mkopo Dodoma Jiji, kabla ya kurejeshwa dirisha dogo lakini hakuweza kumshawishi Kocha Mtunisia, Nasredeen Nabi. Abdallah Shaibu ‘Ninja’ anakuwa mchezaji wa tano kuondoka Yanga baada ya kiungo Mzanzibari Feisal Salum aliyeuzwa Azam FC, mawinga Mghana, Bernard Morrison, Mkongo Tuisila Kisinda na mzawa, Dickson Ambundo. Tayari Yanga imeachana na Kocha wa

BEKI CHIPUKIZI NATHANIEL CHILAMBO AONGEZA MKATABA AZAM FC HADI 2025

Image
BEKI mahiri wa kulia, Nathaniel Chilambo amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Azam FC hadi mwaka 2025.

MAYELE YUPO MAPUMZIKONI ZANZÍBAR ANAKULA BATA HOTEL VERDE

Image
MCHEZAJI Bora na Mfungaji Bora mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Fiston Kalala Mayele  wa Yanga SC yupo mapumzukoni visiwani Zanzíbar na familia yake na amefikia katika hoteli ya Verde inayomilikiwa na Bilionea Alhamisi Sheikh Said Salim Bakhresa.

SIMBA SC YAACHANA NA GARDIEL MICHAEL BAADA YA MIAKA MINNE

Image
KLABU ya Simba imetangaza kuachana na beki wa kushoto, Gardiel Michael Mbaga baada ya miaka minne ya kupiga kazi Msimbazi tangu Julai 2019 aliposajiliwa kutoka kwa watani, Yanga. “Uongozi wa klabu unapenda kuwajulisha kuwa hatutaendelea kuwa na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael baada ya mkataba wake kufikia tamati,” imesema taarifa ya Simba mchana huu. Gardiel Michael anakuwa mchezaji wa saba kuachwa Simba baada ya kipa Beno Kakolanya, beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, na viungo Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Wanigeria, Nelson Okwa, Víctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah. Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.

NAMUNGO FC YAMTAMBULISHA ERASTO NYONI SIKU MOJA TU BAADA YA KUTEMWA SIMBA

Image
KLABU ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi imemtambulisha kiungo mkongwe anayeweza kucheza nafasi zote za ulinzi pembeni na katikati, Erasto Edward Nyoni kuwa mchezaji wake kwanza mpya kuelekea msimu ujao. Namungo FC inamtambulisha Erasto siku moja tu baada ya klabu ya Simba kutangaza kuachana naye kufuatia kudumu Msimbazi tangu mwaka 2017 akitokea Azam FC.

YANGA YAPIGWA NA DODOMA JIJI SIMBA YADROO AZAM YASHINDA

Image
VIGOGO, Simba na Yanga wameanza kwa kusuasua Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 katika mechi zao za leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Wakati Simba imelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar katika mchezo wa Kundi D, Yanga imechapwa 1-0 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Kundi B. Mechi nyingine za leo, Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu katika mchezo wa Kundi D, wakati Tanzania Prisons imeitandika Polisi Tanzania 4-2 katika mchezo wa Kundi B mechi zote zikichezwa hapo hapo Chamazi Alhamisi.

JAMES AKAMINKO AONGEZA MKATABA AZAM FC HADI MWAKA 2026

Image
KIUNGO Mghana, James Akaminko ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea na kazi Azam FC hadi mwaka 2026. Taarifa ya Azam FC jioni hii imesema; “Kiungo chuma, James Akaminko, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya klabu yetu. Hivyo, bado yupo yupo sana kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026,”. Akaminko alijiunga na Azam FC Julai mwaka jana akitokea Great Olympic ya kwao, baada ya awali kuchezea Pure Joy Stars, Tema Youth, Medeama na Ashanti Gold za kwao pia na US Tataouine ya Tunisia.

SIMBA SC YAMTEMA JONÁS MKUDE BAADA YA MIAKA 13 KAZINI

Image
KLABU ya Simba SC imeachana na kiungo wake mkongwe na kipenzi cha mashabiki, Jonás Gerard Mkude aliyedumu kikosini kwa miaka 13 tangu apandishwe kutoka timu ya vijana. “Uongozi wa klabu unatoa shukrani za dhati kwa mchango mkubwa aliotoa kwenye timu yetu kiungo mkabaji, Jonas Mkude katika muda wote wa miaka 13 aliyodumu nasi,” imesema taarifa ya Simba jioni hii na kuongeza. “Tunamtakia kila la kheri kwenye changamoto mpya ya maisha ya soka nje ya Simba,”. Jonás Mkude anakuwa mchezaji wa saba kuachwa Simba baada ya kipa Beno Kakolanya, beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, na viungo Erasto Nyoni, Wanigeria, Nelson Okwa, Víctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah. Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.

COASTAL UNION YAACHANA WACHEZAJI SABA WAGENI WATANO

Image
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imetangaza kuachana na wachezaji saba baada ya kumalizika msimu wakijakilishia kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara katika siku ya mwisho kabisa. Walioachwa ni kipa Mcomoro, Mahamoud Mroivili, mabeki Mganda Joseph Zziwa, Mrundi, Emery Nimubona, kiungo Mbenin Djibril Naim Olatoundji na wazawa, kiungo Yussuf Jamal Kisongo na mshambuliaji Yussuf Athumani.

HISTORIA YA BENO KAKOLANYA SIMBA SC YAFUNGWA RASMI

Image
HATIMAYE klabu imeachana na mlinda mlango Beno David Kakolanya baada ya miaka minne ya kuwa naye tangu awasili kutoka kwa mahasimu, Yanga SC. “Hatutaendelea kuwa na mlinda mlango, Beno Kakolanya baada ya mkataba wake kumalizika,”imesema taarifa ya Simba SC mchana wa leo. Kakolanya anakuwa mchezaji wa tano kuachwa Simba baada ya beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, na viungo Wanigeria, Nelson Okwa, Víctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah. Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.

YANGA YAACHANA NA TOTO TUNDU BERNARD MORRISON

Image
KLABU ya Yanga imetangaza kuachana na winga Mghana, Bernard Morrison baada ya msimu mmoja tangu arejee kutoka kwa mahasimu, Simba SC. “Tunamshukuru Morrison kwa mchango wake katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya Young Africans SC,”imesema taarifa ya Yanga usiku huu. Morrison alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza katika dirisha dogo mwaka 2020 akitokea DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mwishoni mwa msimu akahamia kwa mahasimu, Simba ambako alicheza hadi Julai mwaka jana aliporejea Jangwani. Bernard Morrison anakuwa mchezaji wa nne kuondoka baada ya kiungo Mzanzibari Feisal Salum aliyeuzwa Azam FC, mawinga wengine, Mkongo Tuisila Kisinda na mzawa, Dickson Ambundo. Tayari Yanga imeachana na Kocha wake Mkuu, Mtunisia Nasredeen Nabi na Kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov.

SIMBA SC YAMUACHA NELSON OKWA ILIYEMTOA RIVERS UNITED

Image
KLABU ya Simba imeachana na kiungo mshambuliaji Mnigeria, Nelson Esor-Bulunwo Okwa baada ya msimu mmoja tangu asajiliwe kutoka Rivers United ya kwao. Pamoja na kusajiliwa mwanzoni mwa msimu, lakini Okwa alipelekwa kwa mkopo Ihefu SC ya Mbeya ambako alimalizia msimu. Anakuwa mchezaji wa nne kuonyeshwa mlango wa kutokea Simba baada ya beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, kiungo Mnigeria Víctor Akpan na winga Mghana, Augustine Okrah. Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.

SOSPETER BAJANA ASAINI MKATABA MPYA AZAM FC HADI 2026

Image
NAHODHA wa Azam FC, Sospete Bajana amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea na kazi Chamazi hadi mwaka 2026.

YANGA SC YAACHANA NA WINGA WAKE DICKSON AMBUNDO

Image
KLABU ya Yanga imeachana na winga Dickson Ambundo baada ya misimu miwili ya kuwa na timu hiyo tangu akizungumza nayo kutoka Dodoma Jiji FC. Dickson Ambundo anakuwa mchezaji wa tatu kuondoka Yanga kutoka kikosi cha msimu uliopita baada ya kiungo Mzanzibari Feisal Salum aliyeuzwa Azam FC na winga mwingine, Mkongo Tuisila Kisinda. “Tunamshukuru Ambundo kwa mchango wake katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya Young Africans SC,”imesema taarifa ya Yanga jioni hii. Tayari Yanga imeachana na Kocha wake Mkuu, Mtunisia Nasredeen Nabi na Kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov.

SOPU APIGA HAT TRICK TEAM SAMATTA YAICHAPA TEAM KIBA 4-2

Image
KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Abdul Suleiman Sopu amefunga mabao matatu kuipa Timu ya marafiki wa Mbwana Samatta ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Marafiki wa mwanamuziki Ally Kiba leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo wa Hisani kwenye Tamasha la Sama Kiba, linalojulikana pia kama Nifuate Sopu amefunga mabao yake dakika za 45,63 na 71, wakati la lingine limefungwa na Nahodha wa Simba, John Bocco dakika ya 21. Mabao ya Team Kiba yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ayoub Lyanga dakika ya 69 na mwanamuziki Omary Ally Mwanga ‘Mario’ dakika ya 90 na ushei. Samatta, mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji amekuwa akishirikiana na mwanamuziki Ally Kiba kufanya tamasha hilo la hisani kwa Hisani kwa miaka mitano sasa.