Posts

Showing posts from August, 2021

SENZO ATEULIWA MTENDAJI MKUU YANGA SC

Image
UONGOZI wa Yanga leo umemtangaza Senzo Mbatha Mazingiza, raia wa Afrika Kusini kuwa Mtendaji Mkuu wa Muda kufuatia utekelezwaji wa mfumo mpya wa uendeshaji.

SIMBA QUEENS YATOA SARE NA WAGANDA CECAFA

Image
TIMU ya Simba Queens leo imetoka sare ya 0-0 na Lady Doves WFC ya Uganda Uwanja wa Moi Kasarani Jijini Nairobi nchini Kenya katika mchezo wake wa pili wa Kundi A kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake ukanda wa Afrika Mashariki . Kwa matokeo hayo, Queens inafikisha pointi nne kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya PVP FC ya Burundi kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi Uwanja wa Nyayo, Nairobi na watakamilisha mechi za kundi lao Ijumaa kwa kumenyana na FAD FC ya Djibouti. Bingwa atashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri, ambayo itahusisha timu nane, nyingine kutoka kanda nyingine barani zitakazogawanywa katika makundi mawili.

STARS YAIFUATA DRC LUBUMBASHI MECHI ALHAMISI

Image
BEKI wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Shomari Kapombe akiwa kwenye ndege wakati wa safari ya kwenda Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajilli ya mchezo wake wa kwanza wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Alhamisi.

COASTAL UNION YAPATA KOCHA MMAREKANI

Image
 KLABU ya Coastal Union ya Tanga imeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Mmarekani, Melis Medo kuinoa timu hiyo. Medo anachukua nafasi ya Juma Mgunda ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 1988. Taarifa ya Coastal Union imesema kwamba aliyekuwa msaidizi wa Mgunda, Joseph Lazaro ataendelea kuwa Kocha Msaidizi wa Medo. Medo alikuwa Kocha wa Gwambina kuanzia Mei mwaka huu baada ya kufundisha klabu kadhaa nchini Kenya ikiwemo Wazito na Sofapaka.

YANGA SC 1-2 AZAM FC (MECHI YA KIRAFIKI)

Image
 

DUBE AFUNGA AZAM FC YAICHAPA KABWE 1-0 NDOLA

Image
TIMU ya Azam FC jana imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Kabwe Worriers bao pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola nchini Zambia. Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kujipima nguvu kwa Azam FC katika kambi yake ya kujiandaa na msimu mpya Jijini Ndola kufuatia kuchapwa 4-0 na Red Arrows katika mchezo wa kwanza nchini humo Jumatano iliyopita.

YANGA SC WACHAPWA 2-1 NA ZANACO DAR

Image
  WENYEJI, Yanga SC wamechapwa 2-1 na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki kuhitimisha tamasha la kilele cha Wiki ya Mwananchi usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar sa Salaam. Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Makambo alianza kuifungia Yanga dakika ya 30 baada ya kuwachambua mabeki wawili wa Zanaco kufuatia pasi ya kiungo mzawa, Feisal Salum na kufumua shuti lililojaa nyavuni. Winga wa kulia Ackim Mumba akaisawazishia Zanaco dakika ya 60, kabla ya kiungo Kelvin Kapumbu kufunga la ushindi dakika ya 76 na kuzima kabisa shangwe za maelfu ya mashabiki wa Yanga waliofurika Uwanja wa Mkapa leo.

MAN UNITED YAICHAPA WOLVES 1-0 MOLINEUX

Image
WENYEJI, Wolverhampton Wanderers wameshindwa kutumia vizuri Uwanja wa nyumbani, Molineux baada ya kuchapwa 1-0 na Manchester United leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England mjini Wolverhampton. Kwa ushindi huo uliotokana na bao pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa England, Mason Greenwood dakika ya 80, Man United inafikisha pointi saba baada ya mechi tatu.

CHELSEA PUNGUFU YATOA SARE 1-1 NA LIVERPOOL

Image
WENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield. Chelsea ilimaliza pungufu leo baada ya Reece James kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 na ushei kwa kuunawa mpira kwenye boksi na kusababisha penalti ambayo Mohamed Salah aliifungia Liverpool. James aliikutwa na majanga hayo baada ya kuisaidia Chelsea kupata bao la kuongoza dakika ya 22 kwa kazi yake nzuri kumaliziwa na mfungaji Kai Havertz na sare hiyo inafanya timu zote zifikishe pointi saba baada ya mechi tatu za mwanzo.

TORRES APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA ARSENAL 5-0

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wameendeleza 'mauaji' baada ya kuichapa Arsenal 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad, Manchester huo ukiwa ushindi wa pili katika mechi tatu, kufuatia kuchapwa 1-0 na Tottenham Hotspur na kushinda 5-0 dhidi ya Norwich City.  Katika mchezo huo ambao Arsenal ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Granit Xhaka kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35 kwa kumchezea rafu Joao Cancelo, mabao ya Man City yamefungwa na Ilkay Gundogan dakika ya saba, Ferran Torres dakika ya 12 na 84, Gabriel Jesus dakika ya 43 na Rodri dakika ya 53.

SIMBA QUEENS YASHINDA 4-1 MICHUANO YA CECAFA

Image
TIMU ya Simba Queens imeanza vyema mechi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake ukanda wa Afrika Mashariki baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya PVP FC ya Burundi katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi, Kenya. Mabao ya Simba Queens yamefungwa na beki Mzimbabwe, Danai Bhobho dakika ya 10, winga Mkongo Flavine Mawete Musolo dakika ya 32 na 81 na mshambuliaji mzawa, Aisha Juma Mnunka dakika ya 84. Simba Queens itateremka tena dimbani Jumanne kumenyana na Lady Doves WFC ya Uganda, kabla ya kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na FAD FC ya Djibouti Ijumaa. Bingwa atashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri, ambayo itahusisha timu nane, nyingine kutoka kanda nyingine barani zitakazogawanywa katika makundi mawili.

KOFFI OLOMIDE AWASILI KUWATUMBUIZA WANA YANGA KESHO DAR

Image
  MWANAMUZIKI nguli barani Afrika, Koffi Olomide amewasili leo Dar es Salaam kutoka kwao, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tayari kutumbuiza kwenye tamasha la klabu ya Yanga lijulikanalo kama kilele cha Wiki ya Mwananchi kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini. Pamoja na Koffi, kwenye tamasha hilo pia watakuwepo wasanii wengine mbalimbali wa nyumbani, akiwemo Nandy, Wanaume Family TMK na Chegge. Tamasha hilo ni maalum kwa Yanga kuzindua rasmi msimu mpya kwa kutangaza kikosi chake pamoja na jezi itakazotumia nyumbani na ugenini msimu ujao. Kutakuwa na mechi za vikosi vya Yanga kuanzia vya vijana, wanawake na maveterani kabla ya utambulisho wa kikosi cha msimu mpya kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco ya Zambia Saa 1:00 usiku.

SIMBA WAKAMILISHA KAMBI YA SIKU 17 MOROCCO

Image
 MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamekamilisha kambi yao ya siku 17 nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya na wataondoka kesho kurejea Dar es Salaam. Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba awamu ya pili ya mazoezi ya kujiandaa msimu itaanza baada ya kurejea kwa wachezaji wa klabu hiyo waliopo kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia mapema mwezi ujao. Simba iliyowasili Morocco Agosti 11, katika kambi hiyo ya wiki mbili na ushei Jijini Rabat ilipata pia na mechi mbili za kirafiki na zote ilitoa sare 1-1 na Khourigba na 2-2 na Rabat. Dhidi ya Khourigba, kiungo Papa Ousmane Sakho alianza kuifungia Simba dakika ya 37, kabla ya Mseegal mwenzake, mshambuliaji Adama Diom kuwasawazishia wenyeji dakika ya 61. Na dhidi ya FAR Rabat, mabao ya Simba yalifungwa na viungo Hassan Dilunga dakika ya 54 na Sakho dakika ya 81 baada ya FAR Rabat kutangulia kwa mabao ya Chabani dakika ya 14 na Abba dakika ya 26.

RAIS WA TFF, KARIA AFUNGA KOZI YA GRASSROOTS DAR

Image
RAIS Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia leo amefunga Kozi ya siku tano ya FIFA ya Grassroots iliyokua inafanyika Makao Makuu ya TFF, Uwanja wa Karume, Ilala, Kozi Jijini Dar es Salaam ambayo ilishirikisha makocha 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

CRISTIANO RONALDO KUREJEA MAN UNITED

Image
NYOTA Mreno, Cristiano Ronaldo atarejea Manchester United kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Juventus ya Italia. Manchester United imethibitisha kurejea kwa mchezaji huyo kwa ada ya Pauni MIlioni 21.4 ambayo Juventus waliitaka kutoka kwa mahasimu, Manchester City na Ronaldo atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 480,000 kwa wiki. Ronaldo mwenye umri wa miaka 36, awali alijiunga na United mwaka 2003 akitokea Sporting CP ya kwao, Ureno na akahudumu hadi mwaka 2009 alipotimkia Real Madrid ambako alicheza kwa mafanikio makubwa hadi mwaka 2018 alipohamia Juventus.

CAS YASOGEZA HADI SEPTEMBA 21 KESI YA MORRISON NA YANGA

Image
  MAHAKAMA ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) imesogeza mbele kesi ya klabu ya Yanga dhidi ya wings Mghana, Bernard Morrison hadi Septemba 21, mwaka huu. Kwa mujibu wa barua ya CAS kwenda Yanga wanaowakilishwa na Mawakili Alex Mgongolwa na Simon Patrick na kwa Morrison kupitia kwa klabu yake, Simba kesi hiyo itaendelea Septemba 21. Yanga wanamlalamikia Morrison kusaini mkataba na Simba akiwa bado ana mkataba na klabu hiyo ya Jangwani. Wakati kesi hiyo ikisikilizwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilithibitika Morrison alikuwa ana mkataba na Yanga wakati amassing Simba lakini ilibainika ulikuwa una mapungufu.

SAKHO AFUNGA TENA SIMBA SC YATOA SARE 1-1 MOROCCO

Image
 MABINGWA wa Tanzania, Simba SC leo wametoa sare ya 1-1 na wenyeji, Khourigba katika mchezo wa kirafiki mjini Rabat nchini Morocco. Kiungo Papa Ousmane Sakho alianza kuifungia Simba dakika ya 37, kabla ya Mseegal mwenzake, mshambuliaji Adama Diom kuisawizishia Khourigba dakika ya 61. Huo unakuwa mchezo wa pili katika kambi ya Simba ya kujiandaa na msimu mpya mjini humo kufuatia sare nyingine, 2-2 na FAR Rabat wiki iliyopita. Mabao ya Simba siku hiyo yalifungwa na viungo Hassan Dilunga dakika ya 54 na Sakho dakika ya 81 baada ya FAR Rabat kutangulia kwa mabao ya Chabani dakika ya 14 na Abba dakika ya 26. Simba SC imeweka kambi Rabat kwa wiki ya pili sasa ikijiandaa na msimu mpya, lengo lao kuendeleza mafanikio yao yaliyodumu kwa misimu minne iliyopita.

AZAM FC WAMZAWADIA JEZI MPYA BOSI KAMPUNI YA BAKHRESA

Image
MENEJA Mauzo na Masoko wa Azam FC, Tunga Ally, leo amemtembelea Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bakhresa Food Products, Salim Aziz na kumkabidhi zawadi ya jezi za msimu mpya za klabu hiyo. Baada ya kumpatia zawadi hiyo, Salim Aziz, alielezea furaha yake huku akifurahishwa zaidi kwa ubunifu na ubora wa jezi zetu. Katika hatua nyingine Salim Aziz, alitumia nafasi hiyo kuitakia kila la kheri Azam FC ili ifanye vizuri kitaifa na kimataifa kwenye msimu mpya unaotarajiwa kuanza Novemba 29 mwaka huu.

MIQUISSONE ATAMBULISHWA RASMI MCHEZAJI MPYA AL AHLY

Image
  RASMI klabu ya Al Ahly ya Misri imemtambulisha kiungo mshambuliaji wa kimafaifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kuwa mchezaji wake mpya kutoka Simba SC ya Tanzania.  GONGA HAPA KUTAZAMA VIDEO

SIMBA KUWEKA KAMBI MAREKANI MWAKANI

Image
  MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Gulam Dewji amesema kwamba timu hiyo itakwenda Marekani mwakani kuweka kambi kwa mwaliko ya klabu ya D.C. United ya Washington D.C. Mo Dewji amesema mwaliko huo ameupata baada ya kukutana na mmoja wa wamiliki wa D.C. United, Jason Levien anayemiliki kwa pamoja na Erick Thohir tangu mwaka 2012 walipoinunua. "Ilikua ni furaha kukutana na Jason Levien, ambae ni mmiliki wa klabu ya mpira wa miguu ya DC United ambayo ina thamani ya dola za kimarekani millioni 700," amesema Mo Dewji na kuongeza; "Nina furaha kutangaza  ushirikiano mpya kati ya klabu za DC United na Simba. Ifikapo mwaka 2022, klabu ya Simba itasafiri kwenda Marekani kwa ajili ya mazoezi na maandalizi ya msimu mpya, na pia itashiriki katika mashindano ya kimataifa yatakayoandaliwa na klabu ya DC United, ambayo yatahusisha timu za ligi ya MLS na vilabu kutoka Amerika ya Kusini,".

BAYERN MUNICH WASHINDA 12-0 KOMBE LA UJERUMANI

Image
MABINGWA wa Ujerumani, Bayern Munich usiku wa Jumatano wameionea timu ya daraja la Tano nchini humo, Bremer SV baada ya kuichapa mabao 12-0 katika mchezo wa Raundi ya Kwanza Kombe la Ujerumani Uwanja wa Wohninvest Weser mjini Bremen. Katika mchezo huo ambao kocha Julian Nagelsmann aliwapumzisha nyota wake tegemeo kabisa, Robert Lewandowski, Leon Goretzka na Manuel Neuer mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Eric Maxim Choupo Moting manne, Jamal Musiala mawili, Malik Tillman, Leroy Sane, Jan-Luca Warm aliyejifunga, Michael Cuisance, Bouna Sarr na Corentin Tolisso kila mmoja moja. Ushindi mkubwa zaidi kihistoria kwa Bayern Munich ni 23-0 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu dhidi ya FC Rottach Egern mwaka 2019.  Vigogo hao wa Ujerumani waliichapa timu hiyo hiyo mabao 20-2 mwaka uliotangulia.

AUBAMEYANG APIGA HAT TRICK, ARSENAL YAUA 6-0

Image
TIMU ya Arsenal usiku wa Jumatano imekonga nyoyo za mashabiki wake baada ya ushindi wa 6-0 dhidi ya wenyeji, West Bromwich Albion kwenye mchezo wa Raundi ya Pili ya Kombe la Ligi England Uwanja wa The Hawthorns. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Pierre-Emerick Aubameyang matatu dakika ya 17, 45 na 62, Nicolasa Pépé dakika ya 45, Bukayo Saka dakika ya 50 na Alexandre Lacazette dakika ya 69.