Posts

Showing posts from February, 2023

MAN CITY YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND

Image
TIMU ya Manchester City imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bristol City jana Uwanja wa Ashton Gate Jijini Bristol. Mabao ya Manchester City yalifungwa na Phil Foden mawili, dakika ya saba na 74 na Kevin De Bruyne la tatu dakika ya 81.

WAJUMBE WAPYA WA BODI YA SIMBA SC UPANDE WA MWEKEZAJI

Image
RAIS wa heshima wa Simba SC, Mohamed ‘Mo’ Dewji ameteua Wajumbe wapya wanne wa Bodi chini ya Mwenyekiti, Salum Abdallah Muhene 'Try Again'. Hao ni Dk. Raphael Chageni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi. Hatua hiyo inafuatia kufanyika uchaguzi mkuu uliomrejesha madarakani Mwenyekiti Murtaza Mangungu na Wajumbe Dk. Seif Ramadhan Muba, Asha Baraka, CPA Issa Masoud Iddi, Rodney Chiduo na Seleman Haroub.

MO DEWJI AMTEUA TENA TRY AGAIN KUONGOZA BODI SIMBA

Image
RAIS wa heshima wa Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji amemteua Salum Abdallah Muhene 'Try Again' kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya klabu kwa awamu nyingine. Hatua hiyo inafuatia kufanyika uchaguzi mkuu uliomrejesha madarakani Mwenyekiti Murtaza Mangungu na Wajumbe aliyemshinda Dk. Seif Ramadhan Muba, Asha Baraka , CPA Issa Masoud Iddi, Rodney Chiduo na Seleman Haroub.

BETIKA KUWALETA DAR KWA NDEGE MASHABIKI KUONA SIMBA NA YANGA

Image
Promosheni ni MTOKO WA KIBINGWA (katika promosheni hii betika inawapa fursa watumiaji wake kuja jijini Dsm kwa usafiri wa ndege kwenda na kurudi kutoka mkoa wowote Tanzania kuja  kuutazama mtanange wa simba dhidi ya yanga pale uwanja wa Benjamin mkapa siku ya tarehe 16 katika siti za VIP A, watasindikizwa na ving’ora na ulinzi mkali kwenda uwanjani, vile vile  betika watagharamia malazi na chakula katika hoteli ya nyota 5.) , huu ni msimu wa 5 na kauli mbiu ya msimu huu wa 5 ni HAINA MBAMBAMBA. Katika msimu huu Betika inahitaji jumla ya mabingwa 100 2. Mpaka sasa mabingwa kutoka mikoani waliojishindia ticket za ndege kuja kwenye mtoko wa kibingwa ni…………………… 3. Washindi wanapatikana kupitia droo za kila wiki na kila wiki betika wanatangaza washindi Zaidi ya 10. 4. Tarehe za Draw za wiki hii ni tarehe 27,1,3. 5. Jinsi ya kushiriki kwenye droo beti mikeka 5  kila siku na hakikisha kila mkeka unabeti kwa dau la kwanzia 500 na kuendelea. Unaweza ukabeti kwenye website yetu ya www.bet

SINGIDA BIG STARS YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 LITI

Image
MABAO ya Rodrigo Fegu dakika ya 11 na Meddie Kagere dakika ya 37 yameipa Singida Big Stars ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 47, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 29 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 24.

BAKHRESA GROUP, AZAM MEDIA NI SUPER BRANDS

Image
KAMPUNI ya Azam Media pamoja na Kampuni mama ya Bakhresa Group zimeng’ara kwenye tuzo za Super Brands (Chaguo la Afrika Mashariki) kwa mwaka 2022 – 2024. Tuzo hizo zimekabidhiwa kwa kampuni hizo na waandaji wa tuzo hizo katika ofisi za Azam Media zilizopo, Tabata, Dar es Salaam. Kwa upande wa Azam Media na Bakhresa Group tuzo hizo zilipokelewa na Afisa Uhusiano wa Bakhresa Group, Rehema Salim na Mhariri wa Dawati la Habari na Matukio wa Azam media, Ben Mwang’onda. Jumla ya kampuni nane zimepokea tuzo hiyo na kukabidhiwa kwao na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrand, Jawad Jaffer.

NAMUNGO FC YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 RUANGWA

Image
WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Relliant Lusajo dakika ya 21 na Parterne Counou dakika ya 47, wakati la Geita Gold limefungwa na Elias Maguri dakika ya 64. Kwa ushindi huo Namungo FC inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya saba, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 34 nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 24.

LIVERPOOL NA CRYSTAL PALACE HAKUNA MBABE

Image
WENYEJI, Crystal Palace wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Selhurst Park Jijini London, Uingereza. Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 36 katika mchezo wa 23 nafasi ya saba na Crystal Palace inafikisha pointi 27 za mechi 24 nafasi ya 12.

MWANA FA NAIBU MPYA WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amemteua mwanamuziki na Mbunge wa jimbo la Muheza mkoani Tanga kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, akichukua nafasi ya Pauline Philipo Gekul aliyehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.

MAN CITY YAIFUMUA BOURNEMOUTH 4-1 VITALITY

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vitality Jijini Bournemouth, Dorset. Mabao ya Manchester City yamefungwa na Julian Alvarez dakika ya 15, Erling Haaland dakika ya 29, Phil Foden dakika ya 45 na  Christopher Mepham aliyejifunga dakika ya 51, wakati la Bournemouth limefungwa na Jefferson Lerma . Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 55 katika mchezo wa 25, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Arsenal ambayo pia ina mechi moja mkononi. Kwa upande wao, Bournemouth wanabaki na pointi zao 21 za mechi 24 nafasi ya 19.

ARSENAL YAICHAPA LEICESTER CITY 1-0 KING POWER

Image
BAO pekee la  Gabriel Martinelli dakika ya 46 limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa King Power Jijini Leicester, Leicestershire. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 57 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Leicester inabaki na pointi zake 24 za mechi 24 nafasi ya 14.

COASTAL UNION YAICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0 MKWAKWANI

Image
BAO pekee la kiungo Gustapha Simon dakika ya 49 limeipa Coastal Union dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Kwa ushindi huo, Coastal Union wanafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya 11, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 22 nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi 24.

IHEFU SC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI

Image
TIMU ya Ihefu SC imepata ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mabao ya Ihefu SC leo yamefungwa na washambuliaji wa kigeni, Nelson Okwa dakika ya 40 na Mburkinabe, Yacouba Sogne dakika ya 45, wakati bao pekee la Dodoma Jiji limefumgwa na mzawa, Muhsin Makame dakika ya 62. Kwa ushindi huo, Ihefu SC inafikisha pointi 30 na kusogea nafasi ya saba, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 24 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 24.

KAGERA SUGAR YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 MOROGORO

Image
BAO pekee la mshambuliaji Mganda, Hamisi Kizza ‘Diego’ dakika ya 90 limetosha kuipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya sita, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 17 ikiendelea kushika mkia baada ya wote kucheza mechi 24.

MAN UNITED NA BETIS, ARSENAL NA SPORTING 16 BORA EUROPA LEAGUE

Image
TIMU ya Manchester United itakutana na Real Betis ya Hispania katika Hatua ya 16 Bora ya UEFA Europa League, wakati Arsenal itamenyana na Sporting Lisbon ya Ureno. RATIBA KAMILI 16 BORA EUROPA LEAGU Union Berlin vs Union Saint-Gilloise  Sevilla vs Fenerbahce  Juventus vs Freiburg Bayer Leverkusen vs Ferencvaros  Sporting Lisbon vs Arsenal  Manchester United vs Real Betis  Roma vs Real Sociedad  Shakhtar Donetsk vs Feyenoord  Mechi kwanza zitachezwa Alhamisi ya Machi 9, wakati za marudiano zitafuatia Machi16, mwaka huu.

M-BET YAMWAGA MAMILIONI KWA WASHINDI WAWILI, YAIOMBEA HERI SIMBA

Image
KAMPUNI ya mchezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania imewazawadia washindi wawili kila mmoja Sh175.3 millioni baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12. Washindi hao ni Mesharam Bakunda na Abdallah Segatwa ambao walizawadiwa fedha zao jana katika halfa fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya M-BET Tanzania jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-BET Tanzania Allen Mushi alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kubadili maisha ya mashabiki hao wa soka ambao wote ni wafuasi wa klabu ya Arsenal. Mushi alisema kuwa washindi hao wawili wanaungana na wengine wengi katika nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kujaribu bahati zao kwa kubashiri na kampuni yao. “Mbali ya kubadili maisha ya washindi wetu kupitia kubashiri michezo, pia tunajisikia fahari kuchangia  asilimia 20 ya kodi ya ushindi ambayo inaigia moja kwa moja serikalini . Sisi ni walipa kodi wazuri wa serikali na tunachangia maendeleo,” alisema Mu

MAN UNITED YAICHAPA BARCELONA 2-1 EUROPA LEAGUE

Image
  WENYEJI, Manchester United wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora michuano ya UEFA Europa League baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Barcelona usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Lakini haukuwa ushindi mwepesi kwao, kwani Mashetani Wekundu walilazimika kutoka nyuma baada ya Robert Lewandowski kuitanguliza Barca kwa bao la penalti dakika ya 18 kufuatia Bruno Fernandes kumchezea rafu Alejandro Balde kwenye boksi ambayo ilibidi refa Mfaransa, Clement Turpin apate msaada wa VAR kufanya maamuzi. Lakini Manchester United ikazinduka kwa mabao ya Wabrazil wawili, kiungo Fred dakika ya 47 na Antony dakika ya 73 na kukata tiketi ya Hatua ya 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 4-3 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mechi ya kwanza Barcelona.

YANGA SC YAWAFUATA REAL JIJINI BAMAKO MECHI JUMAPILI USIKU

Image
KIKOSI cha Yanga kimeondoka leo nchini kwenda Bamako nchini Mali kwa ajili ya mchezo wake wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Réal Bamako Jumapili kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako. Mechi nyingine ya kundi hilo Jumapili; TP Mazembe watakuwa wenyeji wa Monastir ya Tunisia kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, DRC.

MAN CITY YATOA SARE NA LEIPZIG 1-1 UJERUMANI

Image
WENYEJI, RB Leipzig jana wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na Manchester City katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Leipzig nchini Ujerumani. Manchester City walitangulia kwa bao la dakika ya 27 la nyota Mualgeria, Riyad Mahrez kabla ya J. Gvardiol kuisawazishia Leipzig dakika ya 70. Timu hizo zitarudiana Machi 14 Uwanja wa Etihad na mshindi wa jumla atakwenda Robo Fainali.

KMC 0-1 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

KLABU 13 KUSHIRIKI MASHINDANO YA TALISS- IST KUOGELEA

Image
KLABU 13 zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST yaliyopangwa kufanyika Februari 25 na 26 kwenye Bwawa la Kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki. Meneja wa klabu ya Taliss-IST, Hadija Shebe amezitaja klabu hizo kuwa Dar es Salaam Swim Club (DSC), Bluefin, Morogoro Piranhas, Mwanza Swim Club, Wahoo Zanzibar, FK Blue Marlins na klabu kutoka Uganda  Flash Swim Club. Klabu nyingine ni Braeburn Arusha, Premiere Swim Club (Dar es Salaam), Mwanza Swim Club, Lake Swim Club, Taliss-IST na HPT. Muogeleaji Lina Goyayi akichapa maji katika mashindano yaliyopita Hadija alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na waogeleaji wanafanya mazoezi ili kushindania zawadi mbalimbali siku hiyo. Alisema kuwa waogeleaji zaidi ya 200 wanatarajia kushiriki katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na International School of Tanganyika (IST), Bwana Sukari, Pepsi, Jubilee Insurance, Dehli Darbaar, Wrap and Roll, F and L Juices na  Burgers 53. K

BETIKA YAZINDUA KAMPENI YA SODO 4 CLIMATE

Image
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri Tanzania Betika kampeni ya Sodo 4 Climate,  katika kampeni hii betika wanahamasisha utunzaji wa mazingira  kupitia mchezo wa sodo. Kauli mbiu ya kampeni hii ni “Shabikia soka sio  uharibifu wa mazingira”. Meneja mkuu wa betika Bw.Tumaini Maligana katika uzinduzi huo alisema kwamba “ Lengo ni kupambana kupunguza mabadiliko ya tabia za nchi kwa ujumla, kupitia utunzaji wa mazingira basi tutahakikisha hali ya hewa nzuri, afya bora na pia maendeleo katika jamii yetu”.   Katika sodo 4 climate itachezeka ligi katika soka la ufukweni pale uwanja wa coco beach ambapo Betika wamealika jumla ya timu 8 zitakazoshiriki na ligi hii itaenda kwa muda wa takribani wiki saba. Ligi hii itahusisha team zifuatazo, Betika staff fc, Coco beach FC, RC FC , Tulia trust foundation FC, Espanyol fc, Bodaboda msasani fc, Ipp media. Katika ligi hii pia kila team watakua na team za wanawake na wanaume ambazo kila jumamosi kutakua na mechi moja ya wanawake na mechi moja

SIMBA SC 1-1 AZAM FC (LIGI KU TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO KUPATA SARE NA AZAM FC 1-1

Image
WENYEJI, Simba SC wameambulia sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Azam FC walitanguli na bao la dakika ya kwanza tu la mshambuliaji wake wa Kimataifa wa Zimbabwe. Prince Dube Mpumelelo, kabla ya beki Mzanzibari Abdallah Kheri ‘Sebo’ kujifunga dakika ya 90 na ushei kuipa bao la kusawazisha Simba. Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 54 na kuendelea kushika nafasi ya pili ikiizidi pointi 10 Azam FC baada ya wote kucheza mechi 23, wakiwa nyuma ya Mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 59 za mechi 22.

YANGA SC 3-0 TP MAZEMBE (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)

Image
 

SIMBA SC 0-3 RAJA CASABLANCA (LIGI YA MABINGWA AFRIKA)

Image
 

BETIKA YASAKA WATU 100 KUSHUHUDIA SIMBA NA YANGA APRILI 16

Image
MTOKO wa kibingwa msimu wa 5 bado unaendelea na katika msimu huu betika tunahitaji idadi ya mabingwa 100 kuja kushuhudia mtanange wa Simba dhidi ya Yanga pale Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 16.  Katika wiki ya kwanza ya promotion hii tulikua na droo 3 , na droo hizo tumepata jumla ya mabingwa 5 mabingwa hao ni Mariamu kutokea Chamazi, Fahame kutokea Simiyu, Clement kutokea Songea , Steven kutokea kagera na Joshua Charles kutokea Mkuranga kwahyo imebaki idadi ya mabingwa 95 ambao tunawahitaji, Mabingwa hawa wanaotokea mkoani watapata ticket za ndege kwenda na kurudi na watalala kwenye hoteli ya nyota 5 wakiwa jijini dar es salaam.  Kushiriki kwenye droo beti mikeka 5 kila siku na kwa kila mkeka weka dau la kwanzia 500 ya kuendelea moja kwa moja utaingia kwenye mtoko wa kibingwa, unaweza ukabeti katika ligi zozote duniani kama la liga, ligi ya uingereza , ujerumani , ligi ya ufaransa, ligi ya italia na pia mechi za ligi ya NBC. Tutakua na droo siku za tarehe 20,22,24. na katika wik

MANCHESTER UNITED YAICHAPA LEICESTER CITY 3-0 OLD TRAFFORD

Image
WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Mabao ya Manchester United yamefungwa na mshambuliaji aliye katika kiwango kizuri mno, Marcus Rashford mawili dakika ya 25 na 56 na Jadon Sancho dakika ya 61. Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 49, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Leicester City inabaki na pointi zake 24 za mechi 23 nafasi ya 14.

POLISI TANZANIA YAICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0 MOSHI

Image
BAO pekee la Kelvin Kongwe Sabato dakika ya 81 limeipa Polisi Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Kwa ushindi huo, Polisi Tanzania inafikisha pointi 19 na kusogea ya 15, ikizidiwa pointi tatu na Tanzania Prisons baada ya wote kucheza mechi 22.

KAGERA SUGAR YAICHAPA NAMUNGO FC 1-0 KAITABA

Image
BAO pekee la chipukizi Erick Mwijage dakika ya 79 limeipa  Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar ya kocha Mecky Mexime inafikisha pointi 29 na kusogea nafasi ya sita ikiizidi tu wastani wa mabao Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 23.

COASTAL UNION YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 MKWAKWANI

Image
BAO pekee la Vincent Abubakar dakika ya 11 limewapa wenyeji, Coastal Union ushindi wa 1-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 22 na kusogea nafasi ya 13, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 24 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 23.

ARSENAL YATOKA NYUMA MARA MBILI KUSHINDA 4-2

Image
TIMU ya Arsenal imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 4-2 dhidi ya wenyeji, Aston Villa leo Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham. Haukuwa mshindi mwepesi kwa Washika Bunduki hao, kwani mara mbili walilazimika kutoka nyuma kabla ya kupata mabao mawili ya ushindi dakika za majeruhi. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka dakika ya 16, Oleksandr Zinchenko dakika ya 61, Emiliano Martínez aliyejifunga dakika ya tatu ya nyongeza baada ya kutimia 90 za kawaida na  Gabriel Martinelli dakika ya nane ya muda wa nyongeza. Kwa upande wao Aston Villa walioanza vizuri mchezo wa leo kabla ya kupoteza mwishoni, mabao yao yamefungwa na Ollie Watkins dakika ya tano na Philippe Coutinho dakika ya 31. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 54 na kurejea kileleni ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 23, wakati Aston Villa inabaki na pointi zake 28 za mechi 23 nafasi ya 11.

NYOTA WA GHANA, CHRISTIAN ATSU AFARIKI DUNIA UTURUKI

Image
MWILI wa mwanasoka wa Ghana Christian Atsu umepatikana chini ya jengo alilokuwa akiishi kusini mwa Uturuki baada ya tetemeko kubwa la ardhi wiki iliyopita. Wakala wa winga huyo wa zamani wa Chelsea amenukuliwa na Reuters akielezea kifo cha nyota huyo wa Ghana ambaye alikuwa anachezea Hatayspor ya Ligi Kuu ya Uturuki. "Mwili wa Atsu ulipatikana chini ya vifusi," Murat Uzunmehmet aliwaambia waandishi wa habari huko Hatay, ambapo mwili wa mwanasoka huyo ulipatikana. "Kwa sasa, vitu zaidi bado vinatolewa. Simu yake pia ilipatikana."  Atsu alikuwa amepanga kusafiri Kusini mwa Uturuki saa chache kabla ya tetemeko hilo kutokea, lakini alisema Ijumaa Mghana huyo aliamua kusalia na klabu hiyo baada ya kufunga bao la ushindi katika mechi ya Februari 5 ya ligi ya Uturuki (Super Lig). Atsu aliwahi kuichezea Newcastle United pia. Mungu ampumzishe kwa amani. Amin. WASIFU WA MAREHEMU CHRISTIAN ATSU Jina Kamili Christian Atsu Twasam [1] Tarehe ya Kuzaliwa 10 Ja