Posts

Showing posts from June, 2019

MADAGASCAR YAIPIGA NIGERIA 2-0 NA KUFUZU 16 AFCON, UGANDA NAYO YAPETA

Image
MADAGASCAR imeshitua baada ya kuichapa Nigeria 2-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 Jumapili Uwanja wa Alexandria nchini Misri. Ushindi huo umetokana na mabao ya nyota wake, kiungo wa Paris ya Ligue 2 Ufaransa, Lalaina Nomenjanahary dakika ya 13 na mshambuliaji wa Ohod ya Saudi Arabia, Charles Carolus Andriamatsinoro dakika ya 53. Kwa matokeo hayo, Madagascar imemaliza kileleni mwa Kundi B ikifikisha pointi saba kufuatia kushinda mechi mbili sare moja, ikifuatiwa na Nigeria iliyomaliza na pointi sita na zote zinasonga hatua ya 16 Bora. Kiungo wa Madagascar, Lalaina Nomenjanahary akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza Guinea pamoja na kuifunga Burundi 2-0, mabao ya mshambuliaji wa Auxerre ya ya Ligue 2 Ufaransa, Mohamed Lamine Yattara dakika za 25 na 52 Uwanja wa Al Salam mjini Cairo, lakini imemaliza nafasi ya tatu kwa pointi zake nne. Burundi imeshika mkia baada ya kufungwa mechi zote tatu. Nayo Uganda imefanikiwa kwend

WINGA MACHACHARI WA TP MAZEMBE, DEO KANDA MUKOKO ATUA SIMBA SC KWA MKOPO

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM WINGA wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Deo Gracia Kanda Mukoko anatarajiwa kujiunga na klabu ya Simba ya Dar es Salaam kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya Lubumbashi. Taarifa ya TP Mazembe leo imesema kwamba Kanda amekuja Tanzania kukamilisha mipango ya kujiunga na mabingwa wa Tanzania kwa mkopo wa msimu mmoja. Hakukuwa na ufafanuzi zaidi juu ya mpango huo, lakini taarifa zisizo rasmi zinasema Simba SC wanapewa Kanda kwa mkopo baada ya kukubali kumuachia kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu iliyemsajili tena kutoka kwa mahasimu, Yanga. Deo Kanda Mukoko anatarajiwa kujiunga na Simba kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya Lubumbashi Inadaiwa Simba SC wamerejeshewa fedha zao walizompa Ajibu na kupewa Kanda kwa mkopo baada ya mazungumzo ya kiungwana yaliyozaa makubaliano hayo.  Kanda alitua kwa mara ya kwanza Mazembe mwaka 2009 na alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoshiriki klabu bingwa ya dunia ya FIFA mwaka 2010, kabla ya kuhamia

SINGIDA UNTED YAANZA KAZI, YASAJILI MSHAMBULIAJI WA GHANA NA BEKI MZANZIBARI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KUFUATIA kufunguliwa rasmi leo kwa dirisha la usajili la Ligi Kuu ya Tanzania Bara, klabu ya Singida United imetaja wachezaji wawili wapya iliyoanza nao katika kujenga kikosi cha msimu mpya. Hao ni beki wa kushoto, Muharami Salum ‘Marcelo’ kutoka klabu ya Malindi ya Zanzibar na mshambuliaji Herman Frimpong  kutoka Ghana. “Marcelo aliyetikisa Ligi Kuu visiwani Zanzibar na hasa wakati wa Mapinduzi Cup, amejiunga nasi kwa kandarasi ya miaka mitatu. Herman Frimpong ni Ingizo Jipya katika kuimarisha safu ya Ushambuliaji. Huyu ni Raia wa Ghana ambaye amshawasili nchini tayari kwa kuanza pre-season,”imesema taarifa ya Singida United leo. Mshambuliaji Herman Frimpong amesaini mkataba wa kujiunga na Singida United kutoka Ghana. Taarifa hiyo inakuja muda mfupi baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufungua dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2019/2020. Taarifa ya Afisa Habari na Mawasili

TFF YAFUNGUA RASMI DIRISHA LA USAJILI KWA KLABU ZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) imetangaza kufunguliwa kwa Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu,Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2019/2020. Taarifa ya Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo leo imesema kwamba dirisha litafungwa Julai 31, mwaka huu na hakutakua na muda wa ziada baada ya zoezi hilo kufungwa. Taarifa hiyo imesema kwamba ssajili wa mashindano ya CAF kwa Klabu za Simba, Yanga SC, Azam FC na KMC wenyewe utafungwa Julai 10, mwaka huu. Baada ya kipindi hicho cha usajili klabu zitakuwa na siku tisa za kusajili kwa kulipa faini ya dola za Kimarekani 250 kuanzia Julai 11 hadi Julai 20, mwaka huu. Taarifa imesema kutakuwa na kipindi cha pili cha usajili wa CAF kitakachokua na siku 10 kuanzia Julai 21 hadi Julai 31, 2019 kipindi ambacho watalipa dola 500 na mchezaji ataanza kutumika kuanzia raundi ya pili. Simba na Yanga SC wanawakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC na

AMUNIKE AJIPA MATUMAINI YA KUPATA MATOKEO MAZURI DHIDI YA ALGERIA KESHO

Image
Na Mwandishi Wetu, CAIRO KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Taifa, Mnigeria Emmanuel Amuneke anaamini timu yake ina nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa mwisho wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 dhidi ya Algeria kuanzia Saa 4:00 usiku wa kesho Uwanja wa Al- Salam mjini Cairo, Misri. Akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa leo, Amuneke amesema kuwa licha ya Algeria kuwa na kikosi kizuri, lakini bado ana matumaini makubwa na vijana wake kuwa watafanya vizuri katika mchezo huo wa mwisho wa kundi C. “Tumecheza na Algeria mara kadhaa, nakumbuka mchezo wa Dar es Salaam tuliocheza tukafungwa 2-0 na baadaye tukaja kucheza nao tukatoka nao 2-2, nakumbuka pia walikuja wakatufunga bao 7-0, lakini hiyo yote ni historia,”alisema na kuongeza: Emmanuel Amuneke anaamini Taifa Stars itafanya vizuri dhidi ya Algeria kesho mjini Cairo “Kwa sasa hivi tunachokitazama ni namna gani tutaweza kusawazisha makosa yetu yaliyotokea katika michezo miwili iliyopit

SIASA NA ITIKADI ZAKE VISIRUHUSIWE SANA KUINGILIA MICHEZO

Image
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itaingia kwenye mchezo wa mwisho wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 dhidi ya Algeria kesho kukamilisha ratiba na kusaka heshima. Hiyo ni baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Kenya katika mchezo wake wa pili wa Kundi C Alhamisi wiki hii Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo. Baada ya kufungwa 2-0 na Senegal kwenye mchezo wa kwanza Juni 23, sasa Taifa Stars itaingia kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria Julai 1 kukamilisha ratiba na kusaka heshima, wakati Kenya itahitaji ushindi mbele ya Senegal kuangalia uwezekano wa kusonga mbele kufuatia kupoteza mechi ya kwanza. Alhamisi ya Juni 27, kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Simon Happygod Msuva alianza kuifungia Taifa Stars bao zuri na la mapema dakika ya sita tu ya mchezo. Lakini mshambuliaji wa Kashiwa Reysol ya Japan aliyewahi kuchezea Girona ya Hispania kwa mkopo, Michael Ogada Olunga aliisawazishia Harambee Stars kwa tik tak dakika ya 39 akitumia makosa

TAIFA STARS WAKIPASHA UFUKWE WA COPACABANA KATIKA KAMBI YA BRAZIL 2007

Image
Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya Kocha Mbrazil, Marcio Maximo wakiwa mazoezini kwenye ufukwe wa Copacabana mjini Rio de Janeiro nchini Brazil mwaka 2007 kwenye kambi ya kujiandaa na mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2008 zilizofanyika nchini Ghana. Hata hivyo, timu hiyo haikufuzu.

NDIKUMANA ALIVYOANZA KAZI RASMI AZAM FC JANA CHAMAZI

Image
Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Mrundi Suleiman Ndikumana akiwa mazoezini jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika mwezi ujao mjini Kigali, Rwanda Suleiman Ndikumana akiwa na mchezaji mwenzake kutoka Burundi, Emmanuel Mvuyekure  Suleiman Ndikumana akiwa mazoezini jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi 

ALEXIS SANCHEZ AIPELEKA CHILE NUSU FAINALI COPA AMERICA

Image
Alexis Sanchez akiifungia penalti ya mwisho Chile ikiibuka na ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 katika mchezo wa Robo Fainali ya Copa America usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Arena Corinthians mjini Sao Paulo, Brazil na sasa itamenyana na Peru Julai 4 katika Nusu Fainali   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SUAREZ AKOSA PENALTI URUGUAY YATUPWA NJE COPA AMERICA

Image
Mshambuliaji Luis Suarez akipiga penalti ambayo alikosa, timu yake, Uruguay ikifungwa kwa penalti 5-4 na Peru kufuatia sare ya 0-0 katika mchezo wa Robo Fainali ya Copa America usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Arena Fonte Nova mjini Salvador, Bahia   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

CAMEROON YAJIWEKA NJIA PANDA KUFUZU 16 BORA AFCON, LEO NI MISRI NA UGANDA

Image
MABINGWA watetezi, Cameroon wamelazimishwa sare ya 0-0 na Ghana katika mchezo mkali wa Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 usiku wa jana Uwanja wa Ismailia.   Matokeo hayo japo yanaifanya Cameroon iendelee kuongoza kundi hilo kwa pointi zake nne baada ya kucheza mechi mbili, lakini hayaihakikishii nafasi ya kwenda 16 Bora. Kwani baada ya mchezo kati ya Benin na Guinea-Bissau kumalizika kwa sare ya 0-0 pia, kila timu katika kundio hilo ina nafasi ya kwenda hatua ya 16 Bora kama itashinda mechi yake ya mwisho. Mkongwe wa Ghana, Asamoah Gyan akijaribu kumtoka kiungo wa Cameroon, Michael Ngadeu-Ngadjui jana   Ghana inafuatia ikiwa na pointi mbili sawa na Benin, wakati hata Guinea-Bissau yenye pointi moja ikishinda mechi yake ya mwisho inaweza kusonga mbele kama wapinzani watapoteza. Cameroon nayo itahitaji japo sare kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Benin Julai 2 ili kujihakikishia tiketi ya hatua ya mtoano.   Mchezo mwingine wa Kundi E jana jioni baina ya Mau

ARGENTINA KUMENYANA NA BRAZIL NUSU FAINALI COPA AMERICA BAADA YA KUITOA VENEZUELA

Image
Lionel Messi akimpongeza Lautaro Martinez baada ya kuifungia bao la kwanza Argentina dakika ya 10 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Venezuela kwenye mchezo wa Robo Fainali michuano ya Copa America usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Jornalista Mario Filho, Maracana mjini Rio de Janeiro, Brazil. Bao la pili lilifungwa na Giovani Lo Celso dakika ya 74 na sasa Argentina itamenyana na Brazil katika Nusu Fainali Julai 3   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

BAFANA BAFANA YAFUFUA MATUMAINI YA KUSONGA MBELE AFCON 2019

Image
BAO pekee la nyota wa Amiens SC ya Ufaransa, Bongani Zungu dakika ya 68 lilitosha kuipa Afrika Kusini ushindi wa 1-0 dhidi ya Namibia katika mchezo wa Kundi Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Al Salam mjini Cairo. Kwa ushindi huo, Bafana Bafana inajipatia pointi tatu za kwanza baada ya kufungwa 1-0 Ivory Coast  kwenye mchezo wa kwanza kuelekea mchezo wake wa mwisho dhidi ya Morocco keshokutwa. Morocco sasa ndiyo inaongoza kundi D baada ya jana kuifunga Ivory Coast 1-0, bao pekee la nyota wa Leganes ya Hispania, Youssef En-Nesyri dakika ya 23 Uwanja wa Al Salam mjini Cairo, hivyo kufikisha pointi sita, wakati Namibia ambayo haina pointi inashika mkia.  Bongani Zungu amefufua matumaini ya Bafana Bafana kwenda hatua ya 16 Bora Mchezo mwingine wa jana ulikuwa wa Kundi E uliomalizika kwa sare ya 1-1 Uwanja wa New Suez, Mali wakitangulkia kwa bao la Diadie Samassekou dakika ya 60 kabla ya Wahbi Khazri kuisawazishia Tunisia dakika ya 70. Mali sasa inaongoza Kundi E kwa poi

YANGA SC YAVAMIA KAMBI ZA AFCON MISRI NA KUSAJILI KIPA WA KENYA NA BEKI WA TAIFA STARS

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KLABU ya Yanga SC imesajili wachezaji wawili wapya, kipa Mkenya Farouk Shikalo na beki Mtanzania, Ally Mtoni ‘Sonso’ ambao wapo na timu zao za taifa kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019 zinazoendelea nchini Misri.  Picha zimevuja wachezaji hao wawili wakiwa na kiongozi wa Yanga SC wanasaini mikataba leo mjini Cairo siku moja tu baada ya timu zao kukutana katika mchezo wa Kundi C jana. Shikalo, kipa wa Bandari ya Mombasa na Sonso beki wa Lipuli FC ya Iringa wote walikuwa benchi kama wachezaji wa akiba timu zao zikimenyana katika mchezo wa Kundi C AFCON 2019, Kenya wakiibuka na ushindi wa 3-2. Yanga SC ilivutiwa na Shikalo baada ya kumuona kwenye michuano ya SportPesa Super Cup akiwa na Bandari, wakati Sonso ilikumbana naye katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Kipa Mkenya, Farouk Shikalo (kulia) akisaini mkataba wa kujiunga na Yanga SC kwenye kambi ya Harambee Stars mjini Cairo    Beki Ally Mtoni ‘Sonso’ akisaini mkataba wa kujiun

YANGA SC KUANIKA KIKOSI KIPYA JULAI 27 TAIFA KWA MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM YANGA SC itacheza mechi ya kwanza ya msimu Julai 27 mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam dhidi ya wapinzani kutoka nje ya nchi. Hayo yamesemwa mchana wa leo na Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Mshindo Msolla katika mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani mjini Dar es Salaam.  “Tarehe 27/07 tutakuwa na matukio matatu, moja ni kutambulisha jezi, pili kutambulisha wachezaji wapya na tatu ni tutakuwa na mchezo kimataifa wa kirafiki,”amesema Dk. Msolla, kocha wa zamani wa Taifa Stars.  Aidha, Dk. Msolla amesema kwamba usajili walioufanya ni mzuri kwa sababu umezingatia vigezo vya kitaalamu kimpira.  Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Mshindo Msolla (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu  “Tumesajili kulingana na matakwa ya mwalimu, hata huko alipo lazima atakuwa ana furaha, maana wachezaji wote wa nje na ndani aliokuwa akiwahitaji tumewapata, pia siku tatu zilizopita mwalim

AZAM FC YAMSAJILI MKONGWE WA BURUNDI, NDIKUMANA ALIYEWAHI KUCHEZA SIMBA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Burundi, Suleiman Ndikumana, kwa mkataba wa mwaka mmoja. Nyota huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam pia, amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', mmoja wa maofisa wa timu hiyo, Abubakar Mapwisa na wakala wa mchezaji huyo, Milner James. Ndikumana aliyekuwa akichezea Al Adalah ya Saudi Arabia, ni mmoja wa washambuliaji wazoefu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na ametua Azam FC baada ya kupendekezwa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' (kulia), akimkabidhi jezi ya klabu hiyo mshambuliaji mpya, Suleiman Ndikumana   Hii ni timu ya pili kuwahi kucheza nchini Tanzania, nyingine ikiwa ni Simba aliyochezea 2006, pia akiwa na uzoefu barani Ulaya, akipita Molde ya Norway na FK Tirana ya Albania. Huo ni usajili wa tatu

LIVERPOOL YASAJILI BEKI KINDA WA MIAKA 17 KWA PAUNI MILIONI 4.4

Image
Beki kinda wa umri wa miaka 17,  Sepp van der Berg akiwa ameshika jezi ya  Liverpool baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka PEC Zwolle akisaini mkataba wa muda mrefu kwa dau la Pauni Milioni 4.4  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SIMBA SC YASAJILI MCHEZAJI MWINGINE KUTOKA KLABU YA LIGI DARAJA LA NNE BRAZIL

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SIMBA SC imesajili mchezaji mwingine kutoka Brazil, ambaye ni beki Tairone Santos da Silva mwenye umri wa miaka 30 aliyesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara. Tairone Santos da Silva anajiunga na Simba SC akitokea klabu ya Atletico Cearense FC inayocheza Ligi Daraja la Nne nchini Brazil, maarufu kama Serie D. “Kazi ya kuimarisha kikosi cha Mabingwa wa nchi inaendelea kama kawaida, beki Tairone Santos da Silva (30) amesaini mkataba wa miaka miwili kuchezea Msimbazi. @tairone89 amejiunga na klabu yetu akitokea ya Atlético Cearense FC ya nchini kwao Brazil,”imesema taarifa ya Simba SC leo. Tairone Santos da Silva anakuwa Mbrazil wa tatu kusajiliwa Simba SC baada ya beki Gerson Fraga Vieira kutoka klabu ya ATK ya Ligi Kuu ya India na mshambuliaji Wilker Henrique da Silva kutoka Bragantino ya Ligi Daraja la Nne pia nchini Brazil. Na kwa ujumla Silva anakuwa mchezaji mpya wa sita kusajiliwa Simba SC baada ya kipa Beno

BRAZIL YATINGA NUSU FAINALI COPA AMERICA BAADA YA KUITOA PARAGUAY KWA MATUTA

Image
Nyota wa Manchester City, Gabriel Jesus akishangilia baada ya kuifungia penalti ya mwisho na ya ushindi Brazil ikiilaza kwa penalti 4-3 Paraguay katika mchezo wa Robo Fainali ya Copa America usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Arena do Gremio mjini Porto Alegre, Rio Grande do Sul na kutinga Nusu Fainali. Penalti nyingine za Brazil zilifungwa na Willian, Marquinhos na Philippe Coutinho, wakati Roberto Firmino alikosa na kwa upande wa Paraguay iliyomaliza pungufu baada ya Fabián Balbuena kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 58 penalti zao zilifungwa na Miguel Almiron, Bruno Valdez na Juan Rodrigo Rojas wakati Gustavo Gómez na Derlis González walikosa   PICHA ZAIDI GONGA HAPA   

KENYA 3-2 TANZANIA (AFCON 2019)

Image

TAIFA STARS YAGONGWA 3-2 NA HARAMBEE STARS NA KUTUPWA NJE MICHUANO YA AFCON

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuchapwa 3-2 na Kenya katika mchezo wa Kundi C usiku huu Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo. Baada ya kufungwa 2-0 na Senegal kwenye mchezo wa kwanza, sasa Taifa Stars itaingia kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria Julai 1 kukamilisha ratiba na kusaka heshima, wakati Kenya itahitaji ushindi mbele ya Senegal kuangalia uwezekano wa kusonga mbele kufuatia kupoteza mechi ya kwanza. Katika mchezo wa leo uliokuwa mkali na wa kusisimua, kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Simon Happygod Msuva alianza kuifungia Taifa Stars bao zuri na la mapema dakika ya sita tu ya mchezo. Kipa wa Tanzania, Aishi Manula akiokoa moja ya hatari kwenye mchezo huo  Manahodha; Mbwana Samatta wa Tanzania (wa pili kulia) na Victor Wanyama wa Kenya (wa pili kushoto) kabla ya mchezo huo Lakini mshambuliaji wa Kashiwa Reysol ya Japan aliyewahi kuchezea Girona ya Hispania kwa mkopo, Michae

ALGERIA YATANGULIA 16 BORA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA BAADA YA KUIPIGA SENEGAL 1-0

Image
BAO pekee Mohamed Youcef Belaili limetosha kuipa ushindi wa 1-0 Algeria dhidi ya Senegal katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 leo Uwanja wa Juni 30 mjini Cairo, Misri. Mshambuliaji huyo wa Esperance ya kwao, alifunga bao hilo dakika ya 49 akimalizia kazi nzuri ya kiungo wa Galatasaray ya Uturuki, Sofiane Feghouli. Matokeo hayo yanaihakikishia tiketi ya hatua ya 16 Bora Algeria wakifikisha pointi sita kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Kenya kwenye mchezo wa kwanza wa kunzi hilo. Sasa Senegal watakuwa na wajibu wa kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Kenya ili kwenda hatua ya mtoano. Mchezo mwingine wa kundi hilo unafuatia Saa 5:00 usiku kati ya Kenya na Tanzania, wapinzani wa Afrika Mashariki wanaozungumza lugha moja, Kiswahili na majirani kweli. Mapema jioni ulitangulia mchezo wa Kundi B na bao pekee la kiungo wa Sporting Charleroi ya Ubelgiji, Marco Ilaimaharitra dakika ya 76 likatosha kuipa Madagascar ushindi wa 1-0 dhidi  Burundi Uwanja

SHOMARI KAPOMBE AONGEZA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI KUBAKI SIMBA SC

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM BEKI wa kulia kimataifa wa Tanzania, Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu ya Simba SC.  Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba Kapombe ambaye hajacheza mpira tangu Novemba mwaka jana alipoumia ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi baada ya kusaini mkataba huo. “Beki bora wa kulia nchini Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ambao utamwezesha kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Mabingwa. Shomari kwa sasa yupo fiti kucheza na atakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitaenda nje ya nchi kujiandaa na msimu mpya,” imesema taarifa ya Simba leo. Shomari Kapombe amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu ya Simba SC Kapombe anaingia kwenye orodha ya wachezaji wengine waliokuwemo kwenye kikosi cha msimu uliopita cha Simba kusaini mkataba mpya. Wengine ni kipa Aishi Manula, mabeki Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Nahodha Msaidizi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala, viungo