Posts

Showing posts from September, 2023

MASHUJAA YATOA SARE YA 0-0 NA NAMUNGO RUANGWA

Image
TIMU ya Mashujaa ya Kigoma imelazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mashujaa inafikisha pointi nane, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Namungo FC inafikisha pointi mbili nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi nne.

YANGA SC YATINGA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
MABINGWA wa Tanzania, Yanga wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 leo dhidi ya Al Merreikh ya Sudan Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji chipukizi Clement John Mzize dakika ya 66 kwa kichwa akiunganisha krosi ya beki Mkongo, Joyce Lomalisa Mutambala kutoka upande wa kushoto wa Uwanja. Yanga inakwenda hatua ya 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia kuwachapa Al Merreikh 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita mjini Kigali, Rwanda. Mara ya mwisho Yanga kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa mwaka 1998 wakipozitoa Rayon Sport ya Rwanda na Coffee ya Ethiopia katika Raundi mbili za awali. Na msimu huu Yanga wanafika Hatua hiyo baada ya kuzitoa ASAS ya Djibouti na Merreikh.

MAN UNITED WACHAPWA 1-0 NA CRYSTAL PALACE OLD TRAFFORD

Image
WENYEJI, Manchester United wamechapwa 1-0 na wenyeji, Crystal  Palace bao pekee la beki Mdenmark, Joachim Andersen dakika ya 25 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Kwa ushindi huo, Crystal Palace 11 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Manchester United inabaki na pointi zake tisa nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi saba.

KMC YAWAPIGA GEITA GOLD 2-1 PALE PALE NYANKUMBU

Image
TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu mjini Geita. Mabao ya KMC leo yamefungwa na Waziri Junior dakika ya tisa na Juma Shemvuni dakika ya 40, wakati bao pekee la Geita Gold limefungwa na Tariq Seif dakika ya 38. KMC inafikisha pointi saba, Geita Gold inabaki na pointi nne baada ya wote kucheza mechi nne.

ZAYD NA DUBE KUKOSEKANA WIKI TATU AZAM FC

Image
BAADA ya kufanyiwa vipimo vya kina, ni rasmi sasa nyota wawili wa Azam FC, kiungo mzawa Yahya Zayd na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube watakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki tatu kila mmoja. Wachezaji hao walilazimika kufanyiwa mabadiliko ya haraka kipindi cha kwanza, Azam FC ikiichapa Singida Fountain Gate mabao 2-1, kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Dube anasumbuliwa na majeraha ya nyonga, huku Zayd akiwa amechanika kiraba (meniscus) kinachokuwa katikati ya goti, kinacholiimarisha lisikwaruzane. Kiraba hicho pia huwezesha goti kufanya kazi vizuri kwa maana ya kukunja na kukunjua. Wachezaji hao wanaendelea na programu ya kutibu majeraha yao chini ya uangalizi wa Mtaalamu wa tiba za viungo (physiotherapist) wa timu yetu, Joao Rodrigues.

JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE KWA KAGERA SUGAR 1-1 KAMBARAGE

Image
TIMU ya JKT Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Mshambuliaji Daniel Lyanga alianza kuifungia JKT Tanzania kwa penalti dakika ya sita ya muda wa ziada baada ya kutimia dakika 90, kabla ya Gasper Mwaipasi kuisawazishia Kagera Sugar dakika mbili baadaye. Timu zote zinafikisha pointi katika michezo minne, Kagera Sugar nafasi ya nane na JKT Tanzania nafasi ya 10.

COASTAL NA YANGA ZAONYWA, KOCHA WA AZAM APIGWA FAINI

Image
BODI ya Ligi imezionya klabu za za Coastal Unión na Yanga kwa makosa tofauti ya kikanuni, huku Kocha wa Makipa wa Azam FC, Khalifa Aboubakar akitozwa faini kwa utovu wa nidhamu.

NI MAN UNITED NA NEWCASTLE 16 BORA CARABAO CUP

Image
TIMU ya Manchester United itakutana na Newcastle United katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup Oktoba 30 Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Hayo yatakuwa marudio ya mchezo wa Fainali ya Carabao Cup msimu uliopita, Mashetani Wekundu walipoichapa Newcastle 2-0 Uwanja wa Wembley na kubeba taji hilo. Mechi zote za 16 Bora Carabao Cup zitachezwa Oktoba 30 na Liverpool watawafuata AFC Bournemouth, Arsenal watawafuata West Ham United, wakati Chelsea watawakaribisha Blackburn Rovers. RATIBA HATUA YA 16 BORA CARABAO  Manchester United v Newcastle Chelsea v Blackburn  Bournemouth v Liverpool  Everton v Burnley  West Ham v Arsenal Mansfield Town v Port Valer Exeter City v Middlesbrough  Ipswich Town v Fulham 

LIVERPOOL YATOKA NYUMA NA KUICHAPA LEICESTER CITY 3-1

Image
WENYEJI, Liverpool jana wametoka nyuma na kuichapa Leicester City Mabao 3-1 na kutinga Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup Uwanja wa Anfield. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Cody Gakpo dakika ya 48, Dominik Szoboszlai dakika ya 70 na Diogo Jota dakika ya 89 baada ya Kasey McAteer kuanza kuifungia Leicester City dakika ya tatu ya mchezo huo.

BARAKA MAJOGORO AWA MCHEZAJI BORA WA MECHI AFRIKA KUSINI

Image
BEKI Mtanzania, Bakara Gamba Majogoro jana alipewa tuzo ya Man Of The Match timu yake, Chippa United ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya SuperSport United. Bao pekee la Chippa United lilifungwa na mshambuliaji mkongwe, Mnamibia, Elmo Ukondja Kambindu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini Uwanja wa Nelson Mandela.

NI TANZANIA, KENYA NA UGANDA WENYEJI WA AFCON 2027

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limezipa Tanzania, Kenya na Uganda uenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Pamoja na kuzipa nchi hizo za Afrika Mashariki uenyeji wa AFCON ya 2027, Rais wa CAF, Dk. Patrice Motsepe ameitaja Morocco kuwa mwenyeji wa AFCON ya 2025.

MAN UNITED YAICHAPA CRYSTAL PALACE 3-0 CARABAO CUP

Image
TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Crystal Palace usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Mabao ya Manchester United jana yamefungwa na mshambuliaji kinda wa miaka 19, Muargentina Alejandro Garnacho Ferreyra dakika ya 21, kiungo Mbrazil Carlos Henrique Casemiro dakika ya 27 na mshambuliaji Mfaransa Anthony Jordan Martial dakika ya 55.

TWIGA STARS YAITOA IVORY COAST KWA MATUTA CHAMAZI

Image
TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania imefanikiwa kutinga hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya mwakani nchini Morocco baada ya kuwatoa Ivory Coast kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya jumla ya 2-2. Mchezo wa leo jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam umemalizika kwa Twiga Stars kushinda 2-0, mabao ya Deonisia Minja na Opa Clement hivyo kufanya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia Ivory Coast kushinda 2-0 pia kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa mjini Yamoussoukro. Na kwenye mikwaju ya penalti Twiga Stars wakishinda 4-2 na sasa watakutana na mshindi wa jumla kati ya Djibouti na Togo zinazorudiana leo Saa 12:30 jioni mjini Lome baada ya Togo kushinda 7-0 kwenye mchezo wa kwanza ugenini. Wakati huo huo: Katibu mpya wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewazadia Twiga Stars Sh. Milioni 10 kwa kuitoa Ivory Coast.

SIMBA SC YAWATANDIKA PAN AFRICANS 4-0 BUNJU

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pan Africans katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na Mrundi Saido Ntibanzokiza, Mzambia Moses Phiri, Kibu Dennis na Mcameroon Andre Onana. Simba imeutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yao ya mchezo wao wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili dhidi ya Power Dynamos ya Zambia Jumapili. Simba inahitaji angalau ushindi wa 1-0 au sare isiyozidi 1-1 na Power Dynamos ili kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 2-2 kwenye mechi ya kwanza Jumamosi iliyopita.

WAZIRI DK. NDUMBARO ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CAF NA KUZUNGUMZA NA KATIBU MKUU

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro amefanya ziara katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Cairo nchini Misri. Dk. Ndumbaro amefanya ziara hiyo Septemba 25, 2023 ambapo amekutana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Veron Mosengo-Omba na wamejadili masuala mbalimbali ya kuboresha mchezo wa soka nchini. Waziri Dk. Ndumabaro katika ziara hiyo  aliambatana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa, Neema Msitha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia pamoja na watumishi kutoka wizara hiyo na TFF.  Katika hatua nyingine, Waziri Dk. Ndumbaro ameongoza ujumbe wa Tanzania kutembelea Ubalozi Cairo nchini Misri kabla ya siku ya kupiga kura ya kupata nchi mwenyeji wa Mashindano ya Afrika (AFCON 2027) itakayopigwa Septemba 27, 2023 nchini humo. Ndumbaro amesema Tanzania, Kenya na Uganda kupitia Marais wa nchi hizo wako tayari kwa ajili ya mashindano hayo kwa kuwa zina mazingira  m

SERENGETI GIRLS YAICHAPA TENA MOROCCO 2-1 CHAMAZI

Image
TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Morocco U17 katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao yote ya Serengeti Girls yamefungwa na Jamila Rajab baada ya Morocco kutangulia kwa bao la Elanbri Alisha. Huo ulikuwa mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza Serengeti Girls kushinda pia 2-1 mabao yake yakifungwa na Masika Khing na Sabina Alex, huku la Morocco U17 likifungwa na Bentahri Ovafaa.

LIVERPOOL YAICHAPA WEST HAM UNITED 3-1 NA KUKAA NYUMA YA MAN CITY

Image
WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 16, Darwin Nunez dakika ya 60 na Diogo Jota dakika ya 85, wakati bao pekee la West Ham limefungwa na Jarrod Bowen dakika ya 42. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 16 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi sita, wakati West Han United inabaki na pointi zake 10 za mechi sita pia nafasi ya saba.

MBEYA KWANZA YAIFUMUA MBEYA CITY 4-0 MTWARA

Image
TIMU ya Mbeya Kwanza jana imepanda kileleni mwa Ligi ya NBC Championship baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Mechi nyingine za Ligi ya NBC Championship jana Cosmopolitan ililazimishwa sare ya bila kufungana na TMA Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Ruvu Shooting ikachapwa 3-0 na Ken Gold Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Ikumbukwe juzi Stand United iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba FC ya Mwanza Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, huku Mbuni FC ya Arusha ikiwazima wenyeji, Pan African kwa kuwachapa 1-0 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Msimamo wa Ligi ya NBC Championship sasa ni Mbeya Kwanza, Ken Gold na Mbuni FC zote zipo juu kila timu ikiwa na pointi saba baada ya wote kucheza mechi tatu.  Ligi hiyo inaendelea leo kwa mechi nyingine tatu kukamilisha mzunguko wa tatu; Green Warriors na Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru, Transit Camp na FGA Talents Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na Biashara United dhidi

BRUNO FERNANDES AING’ARISHA MAN UNITED

Image
BAO pekee la Bruno Fernandes dakika ya 45 limeipa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Burnley 1-0 Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley. Ni ushindi ambao unaifanya Manchester United ifikishe pointi tisa katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya nane, wakati Burnley inabaki na pointi yake moja ikiendelea kushika mkia baada ya kucheza mechi tano.

HAALAND AFUNGA MAN CITY YAICHAPA NOTTINGHAM FOREST 2-0

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mabao ya Manchester City yamefungwa na Phil Foden dakika ya saba na Erling Haaland dakika ya 14 katika mchezo huo timu ya kocha Mspaniola, Pep Guardiola ilimaliza pungufu kufuatia Rodri kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 46 kwa kumpiga Morgan Gibbs-White wa Nottingham Forest. Manchester City inafikisha pointi 18 kileleni, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake saba baada ya wote kucheza mechi sita.

SERENGETI GIRLS YAWACHAPA MOROCCO 2-1 CHAMAZI

Image
TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Morocco katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Masika Khing na Sabina Alex, wakati la Morocco limefungwa na Bentahri Ovafaa na timu hizo zitarudiana Jumatatu hapo hapo Azam Complex.

TWIGA STARS YACHAPWA 2-0 NA IVORY COAST KUFUZU WAFCON

Image
TIMU ya Taifa ya wanawake Twiga Stars jana imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Ivory Coast  Uwanja wa Yamoussoukro  katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) mwakani nchini Morocco. Timu hizo zitarudiana Septemba 26 Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Djibouti na Togo katika hatua ya mwisho ya mchujo mwezi ujao.

STAND UNITED WAICHAPA PAMBA 1-0, PAN AFRICAN YAPIGWA UHURU

Image
WENYEJI, Stand United wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba FC ya Mwanza, bao pekee la Emmanuel Mtambuka dakika ya 55 katika mchezo wa Ligi ya NBC Championship leo Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Mechi nyingine ya NBC Championship leo Mbuni FC ya Arusha imewazima wenyeji, Pan African kwa kuwachapa 1-0 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mbuni FC wanapanda kileleni wakifikisha pointi saba, Pamba FC inashukia nafasi ya tatu ikibaki na pointi sita, Stand United pointi nne nafasi ya nane na Pan Africans nafasi ya 11 pointi tatu baada ya wote kucheza mechi tatu.   

MAWAZIRI WA MICHEZO AFRIKA MASHARIKI WAJADILI UENYEJI AFCON 2027

Image
MAWAZIRI wanaoshughulikia michezo katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda wamekutana kujadili maombi yao ya pamoja ya kuwa wenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027 kabla ya kwenda kuwasilisha maombi hayo ambayo yatapigiwa kura Septemba 27, 2023 Jijini Cairo Misri. Kikao hicho kimefanyika leo Septemba 22, 2023 Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania ambapo Kenya imewakilishwa na Bw. Peter Kiplagat Tum ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo nchini na Uganda imewakilishwa na Bw. Tashobya Ambrose ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo la nchi hiyo. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema nchi hizo zina nafasi kubwa na uwezo mkubwa wa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa kuwa zina Jiografia inayofanana na miundombinu ya michezo inayokidhi mashindano hayo pamoja na Serikali zote tatu kuwa tayari kukarabati miondombinu itakayotumiwa kwenye michez

WAZIRI NDUMBARO AJIUZULU KAMATI YA RUFANI YA LESENI ZA KLABU TFF

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dk. Damas Ndumbaro amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

LIVERPOOL YATOKA NYUMA KUSHINDA 3-1 UGENINI EUROPA LEAGUE

Image
TIMU ya Liverpool imetoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, LASK usiku wa jana katika mchezo wa Kundi E UEFA Europa League Uwanja wa Raiffeisen Arena mjini Linz nchini Austria. Florian Flecker alianza kuifungia LASK dakika ya 14, kabla ya Liverpool kuzinduka na mabao ya Darwin Nunez dakika ya 56, Luis Diaz dakika ya 63 na Mohamed Salah dakika ya 88. Mechi nyingine ya Kundi E jana, wenyeji Union Saint-Gilloise walilazimishwa sare ya 1-1 na Toulouse ya Ufaransa Uwanja wa Lotto Park mjini Brussel, Ubelgiji.

WIZARA ZA MICHEZO TANZANIA, KENYA NA UGANDA ZAJADILI MAANDALIZI AFCON 2027

Image
TIMU ya Wataalamu wakiongozwa na Makatibu Wakuu wa michezo kutoka Tanzania, Kenya na Uganda ambazo kwa pamoja zinaomba kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kupitia maombi ya EA Pamoja Bid imekutana kujadili maandalizi. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho kilichofanyika Septemba 21, 2023 jijini Dar es Salaam kufuatia barua Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambalo limeainisha na kuitaja Septemba 27, 2023 ndiyo siku ya kupiga kura Cairo, Misri kuamua ni nchi gani itapewa dhamana ya kuandaa michuano hiyo 2027. “Tuliona ni muhimu kama nchi zetu ambazo tunaomba kwa pamoja tukutane tupange mikakati ya namna ya kupata ushindi, leo tulikuwa na Makatibu Wakuu wa Michezo kutoka Tanzania, Kenya na Uganda na kujadili kwa kina ili tufanikiwe na ni kikao cha kujipanga kwa ajili ya Mawaziri ambao watakutana hapa kesho Septemba 22, 2023 kwa ajili ya kupanga mikakati hiyo” amesema Kat

WAZIRI NDUMBARO AIAGIZA MIKOA KUJIANDAA VYEMA MASHINDANO YA SAMIA TAIFA CUP

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro ameiagiza Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya Samia Taifa Cup ambayo yatafanyika mwishoni mwa mwaka huu. Ndumbaro ametoa maagizo hayo Septemba 21, 2023 Zanzibar wakati akikabidhi  vifaa vya michezo kwa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya maandalizi ya  mashindano hayo ambayo yatahusisha michezo mbalimbali. "Mwaka huu mashindano yatajumuisha pia Zanzibar na kutakua na Mashindano ya Muziki wa Kizazi Kipya. Lengo la mashindano haya ni kuendelea kuenzi Muungano wetu na  kuhakikisha jamii inajishughulisha na michezo, Sanaa  na Utamaduni kwakua ni Sekta ambazo zinaibua vipaji na kutoa fursa ya ajira" amesema Mhe. Ndumbaro. Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita amesema  vifaa hivyo vitagawiwa katika mikoa yote ya Zanzibar na mashindano yataanzia katika ngazi ya Shehia mpaka Mkoa

AZAM FC YAICHAPA SINGIDA FOUNTAIN GATE 2-1 CHAMAZI

Image
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki Msenegal, Cheikh Sidibé dakika ya 10 na kiungo mzawa, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 90 ushei, wakati la Singida Fountain Gate limefungwa na kiungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya Marouf Tchakei dakika ya 57. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi tisa sawa na Yanga na Simba, inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa wastani wa mabao, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi mbili baada ya wote kucheza mechi tatu.

BAKEKE APIGA HAT-TRICK SIMBA YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 UHURU

Image
MSHAMBULIAJI Mkongo, Jean Othos Baleke amefunga mabao yote Simba ikiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Unión ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Baleke ambaye yupo katika msimu wake wa pili Simba baada ya kusajiliwa dirisha dogo, Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amefunga mabao hayo dakika za saba, 11 na 40 kwa penalti baada ya kiungo wa Kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kuchezewa rafu kwenye boksi. Coastal Union ilimaliza pungufu baada ya mshambuliaji wake, Haji Ugando kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 19 kufuatia kumchezea rafu beki wa Simba, Mkongo Henock Inonga Baka ‘Varane’ aliyeshindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na Kennedy Juma dakika ya 24. Simba SC inafikisha pointi tisa na kuungana na watani wao, Yanga ambao wanaendelea kuongoza Ligi kwa wastani wa mabao, wakati Coastal Unión inabaki na pointi moja baada ya wote kucheza mechi t

YANGA SC 1-0 NAMUNGO FC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

MAN UNITED YACHAPWA 4-3 NA BAYERN MUNICH UJERUMANI

Image
TIMU ya Manchester United imeanza vibaya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 4-3 na wenyeji, Bayern Munich katika mchezo wa Kundi A usiku wa Jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Múnich nchini Ujerumani. Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Leroy Sané dakika ya 28, Serge Gnabry dakika ya 32, Harry Kane kwa penalti dakika ya 53 na Mathys Henri Tel dakika ya 90 na ushei. Kwa upande wao, Manchester United mabao yao yamefungwa na Rasmus Højlund dakika ya 49 na Carlos Henrique Casemiro dakika ya 88 na 90. Mchezo mwingine wa Kundi A, wenyeji Galatasaray walitoka sare ya 2-2 na FC Copenhagen Uwanja wa Rams Global mjini İstanbul nchini Uturuki.

YANGA YAIZIMA NAMUNGO FC DAKIKA ZA MWISHONI, 1-0 CHAMAZI

Image
BAO la dakika ya 88 la kiungo Mzanzibari, Mudathir Yahya Abbas limeipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mudathir alifunga bao hilo kwa kupenyeza mguu katikati ya mlinzi Derrick Mukombozi na kipa wa Namungo FC, Deogratius Munishi ‘Dida’ kuunganishia nyavuni krosi ya winga Mkongo, Jesus Moloko. Mfungaji na mtoa pasi ya bao waliinuliwa kwa pamoja kutokea benchi dakika ya 67 kuchukua nafasi ya mshambuliaji mzawa, Clement Mzize na kiungo Muivory Coast, Pacome Zouazoua. Ushindi huo mwembamba unaifanya Yanga ifikishe pointi tisa na kurejea kileleni ikiizidi pointi mbili Mashujaa FC baada ya wote kucheza mechi tatu, wakati Namungo FC iliyocheza mechi tatu pia inabaki na pointi moja.

MASHABIKI WANNE WA NAMUNGO WAFARIKI AJALINI WAKIIFUATA YANGA

Image
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa salamu za pole kufuatia vifo vya mashabiki wanne wa Namungo FC na wengine 16 kujeruhiwa kwenyeajali iliyotokea eneo la Miteja karibu na Somanga mkoani Lindi wakiwa safarini kutoka Ruangwa kuja Dar es Salaam kushuhudia mchezo dhidi ya Yanga leo.  

BARCELONA YAITANDIKA ROYAL ANTWERP 5-0 HISPANIA

Image
WENYEJI, FC Barcelona wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Royal Antwerp ya Ubelgiji katika mchezo wa kwanza wa Kundi H Uwanja wa Olímpic Lluís Companys Jijini Barcelona nchini Hispania. Mabao ya Barcelona yamefungwa na João Félix dakika ya 11 na 66, Robert Lewandowski dakika ya 19, Jelle Bataille aliyejifunga dakika ya 22 na Gavi dakika ya 54. Mechi nyingine ya Kundi H jana, FC Porto ya Ureno iliwachapa wenyeji, FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine mabao 3-1 Uwanja wa Volksparkstadion Jijini Hamburg, Ujerumani.

NOVATUS DISMAS ACHEZA MWANZO MWISHO LIGI YA MABINGWA ULAYA

Image
KIUNGO wa Kimataifa wa Tanzania, Novatus Dismas Miroshi usiku wa jana amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, FC Shakhtar Donetsk y Ukraine ikichapwa mabao 3-1 na FC Porto ya Ureno katika mchezo wa kwanza wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Volksparkstadion Jijini Hamburg, Ujerumani. Mabao ya FC Porto yamefungwa na washambuliaji wake Mbrazil,  Wenderson Galeno mawili dakika ya nane na 15 na Muiran Mehdi Taremi dakika ya 29. Bao pekee la FC Shakhtar Donetsk inayolazimika kuchezea mechi zake za nyumbani Ujerumani kutokana na machafuko yanayoendelea nchini kwao kufuatia uvamizi wa majeshi ya Urusi limefungwa na mshambuliaji wake Mvenezueala, Kevin Kelsy dakika ya 13. Miroshi anakuwa Mtanzania wa tatu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Athumani Machuppa na Mbwana Samatta na mchezaji wa tatu kwa ujumla kutoka nchi hii kucheza michuano ya Ulaya baada ya Kassim Manara kucheza iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi.

TWIGA STARS YAIFUATA IVORY COAST MECHI YA KUFUZU WAFCON

Image
KIKOSI cha timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars kimeondoka leo kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) dhidi ya wenyeji Ijumaa. PICHA: KIKOSI CHA TWIGA STARS KILIVYOONDOKA LEO DAR

ABDALLAH KHERI WA AZAM FC AFANYIWA UPASUAJI WA GOTI AFRIKA KUSINI

Image
BEKI wa kati wa Azam FC, Abdallah Kheri 'Sebo', atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kulia. Sebo ameumiza gegedu 'cartilage' ya maungio ya goti lake la mguu wa kulia, ambayo imelika na pia ameumiza mifupa midogo midogo kutokana na mlalo wa goti lake la kulia na tege alilokuwa nalo. Beki huyo kisiki, amefanyiwa upasuaji huo leo Jumatatu asubuhi, kwenye Hospitali ya Vincent Palloti, jijini Cape Town, Afrika Kusini. Abdallah Kheri ‘Sebo’ aliumia kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons, Azam FC ikishinda mabao 3-1 na kushindwa kuendelea wakati wa mapumziko nafasi yake ikichukuliwa na Nathan Chilambo. Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyeambatana na beki huyo, amesema kuwa Sebo atarejea kwenye soka la ushindani baada ya miezi mitatu ya matibabu ya majeraha yake kumalizika. "Sebo amefanyiwa upasuaji wa kisasa unaoitwa arthroscopic, ambao wametoa mifupa midogo mid

CHELSEA YAKATALIWA BAO IKITOA DROO NA BOURNEMOUTH

Image
BEKI Levi Colwill akishangilia baada ya kuifungia bao Chelsea dhidi ya wenyeji, AFC Bournemouth kabla ya kuambiwa alikuwa ameotea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliomalizika kwa sare ya bila kufungana Jumapili Uwanja wa Vitality mjini Bournemouth, Dorse. Matokeo hayo yanaifanya Chelsea ifikishe pointi tano nafasi ya 14, wakati Bournemouth imefikisha pointi tatu nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi tano.

ARSENAL YAICHAPA EVERTON 1-0 PALE PALE GOODISON PARK

Image
TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Goodison Park Jijini Liverpool. Bao pekee la Arsenal leo limefungwa na mshambuliaji wake Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 69 akimalizia kazi nzuri ya Bukayo Saka na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 13, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa wastani wa mabao na Liverpool na Tottenham Hotspur baada ya wote kucheza mechi tano. Kwa upande wao Everton baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi yao moja waliyovuna kwenye sare na Sheffield United ugenini kufuatia kufungwa mechi nyingine tatu dhidi ya Aston Villa 4-0, Wolverhampton Wanderers 1-0 na Fulham 1-0.

KAGERA SUGAR YAWACHAPA GEITA GOLD 1-0 KAITABA

Image
TIMU ya Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na Disan Galiwango dakika ya 90 na ushei huo ukiwa ushindi wa kwanza kwao baada ya kufungwa mechi mbili za awali, wakati Geita imepoteza mechi ya kwanza ikitoka kushinda moja na kutoa sare moja awali.

COASTAL UNION YASAINI MKATABA YA UDHAMINI NA MAKAMPUNI MAWILI

Image
KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu ametoa wito kwa makampuni mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kujitokeza kudhadhili vilabu vya soka na michezo mbalimbali nchini ili ziwe na ushindani  katika medani za kitaifa na kimataifa. Katibu Mkuu, Yakubu ametoa wito huo jijini Tanga akiwa Mgeni Rasmi wakati timu ya Coastal Union ilipokuwa ikisaini mkataba na kampuni ya Elsewedy Electric Cable East Africa Ltd ambayo itaifadhili timu hiyo kwa msimu wa 2023/2024 pamoja na kuzindua jezi itakayotumika kwa msimu huu. "Mpira sasa unahitaji vitu vitatu, ufundi kwa maana ya utaalam wa michezo kwa wachezaji na viongozi, vipaji vya wachezaji vinavyokuzwa na kulelewa na kuwaandaa kuwa wachezaji bora ambao watumiwa na vilabu, timu ya taifa na hata soka la kulipwa nje ya nchi pamoja na fedha ambazo ndiyo chachu ya soka na michezo mingine kwa kuzingatia michezo ni ajira" amesema Katibu Mkuu, Yakubu. Amewataka uongozi wa timu ya Coastal Union kutumia fedha zitakazot

MANCHESTER CITY WAICHAPA WEST HAM 3-1 LONDON

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wametoka nyuma na kuwachapa wenyeji, West Ham United mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London. West Ham ilitangulia na bao la dakika ya 36 la James Ward-Prowse, kabla ya Manchester City kuzinduka na mabao ya J. Doku dakika ya 46, Bernardo Silva dakika ya 76 na Erling Haaland dakika ya 86. Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya  Tottenham Hotspur na  Liverpool, wakati West Ham inabaki na pointi zake 10 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi tano.

MAN UNITED YABUTULIWA 3-1 NA BRIGHTON PALE PALE OLD TRAFFORD

Image
WENYEJI, Manchester United wametandikwa mabao 3-1 na Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford, Manchester. Mabao ya Brighton & Hove Albion yamefungwa na  Danny Welbeck dakika ya 20, Pascal Groß dakika ya 53 na  João Pedro dakika ya 72, wakati bao pekee la Manchester United limefungwa na Hannibal Mejbri dakika ya 73. Kwa ushindi huo, Brighton & Hove Albion wanafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya nne, wakati Manchester United wanabaki na pointi zao sita nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi tano.