Posts

Showing posts from May, 2022

TAIFA STARS KUFUATA NIGER KWA NDEGE YA KUKODI

Image
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakwenda Benin kwa ndege ya kukodi kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Niger Juni 4 Uwanja wa L'AmitiĆ© mjini Cotonou. Taarifa ya TFF imesema kutakuwa na nafasi 50 kwa wapenzi wa soka watakaotaka kwenda kuisapoti Taifa Stars ambao watalazimika kulipiadola za Kimarekani 1,000 – kwa taarifa Zaidi wafike TFF. Baada ya hapo, Taifa Stars itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria Juni 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuwania tiketi ya Ivory Coast 2023. Bahati nzuri kwa Stars, mshambuliaji wa mabingwa wa England, Manchester City, Riyad Mahrez, Said Benrahma na Sofiane Feghouli hawatakuwepo kwa mujibu wa kocha wa Algeria, Djamal Belmadi wote majeruhi. Ikumbukwe Stars pia itaanzia ugenini kwa Somalia kati ya Julai 22 na 24 kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Algeria, kabla ya timu hizo kur

SIMBA SC YAMTUPIA VIRAGO KOCHA PABLO

Image
KLABU ya Simba imeachana na kocha wake, Mspaniola Pablo Franco Martin baada ya makubaliano ya pande zote MBILI na kuelekea mechi zilizobaki kumalizia msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara timu itakuwa chini ya kocha Msaidizi, Suleiman Matola. Pamoja na Pablo aliyejiunga na timu hiyo Novemba mwaka jana, Simba pia imeachana na kocha wa mazoezi ya viungo Daniel De Castro Reyes ambaye pia ni Mspaniola.

DTB YA LIGI KUU NI SINGIDA BIG STARS FC

Image
BAADA ya kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara, timu ya DTB imebadilishwa jina na kuwa Singida Big Stars FC na kituo chake kitakuwa ni Uwanja wa Liti uliopo Singida.

MO DEWJI ASEMA MAFANIKIO SIMBA YALILETWA NA ‘POCHI NENE’

Image
RAIS wa Heshima wa klabu ya Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji amesema bajeti ya uendeshaji ya klabu iliongezeka miaka mitano iliyopita na ndio sababu walifanikiwa kufanya vizuri. “Miaka mitano iliyopita  imekuwa ya mafanikio kwa Simba. Bajeti iliongezeka mara tano, tulishinda makombe mengi ya ndani na tuliweka alama kimataifa kwa kufika robo fainali tatu za michuano ya Afrika,” ameandika Mo Dewji kwenye ukurasa wake wa Instagram. “Najivunia kuweza kusema tupo katika orodha ya vilabu bora 12 Afrika. Hii imekuwa mara ya kwanza Simba kuwa na mwendelezo mzuri katika miaka 86 ya historia yetu. Hakuna kurudi nyuma, tunatakiwa kufanya mabadiliko katika maeneo ambayo tuna madhaifu na kwenda mbele. Mapambano yanaendelea,” amemalizia. Msimu huu mambo yamekuwa tofauti Simba SC, kwani licha ya kutolewa mapema Ligi ya Mabingwa Afrika, pia imekwishavuliwa mataji yote, Ngao ya Jamii, Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) na Ligi Kuu ambako watani wao

WAZIRI WA MICHEZO AWATEMBELEA SERENGETI GIRLS KAMBINI ZANZIBAR

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa na Naibu wake Pauline Gekul pamoja na baadhi ya viongozi wa wizara na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana wametembelea kambi ya timu ya soka ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls baada ya kutembelea kambi yao Zanzibar kujiandaa na mchezo wa mwisho wa marudiano Kufuzu Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini India.

TAIFA STARS MAZOEZINI MKAPA KUJIANDAA KUZIBAA NIGER NA ALGERIA

Image
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania, “Taifa Stars” wakiwa kwenye mazoezi yaliyoanza jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kujandaa na michezo ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 dhidi ya Niger na Algeria itakayochezwa Juni 4 ugenini na Juni 8 nyumbani, Benjamin Mkapa.

TWIGA STARS WANAVYOJIANDAA NA KOMBE LA CHALLENGE KAMBINI BUKOBA

Image
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara, Twiga Stars wakiwa mazoezini Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Kagera kujiandaa na mashindano ya CECAFA Challenge Wanawake yatakayofanyika Uganda mwezi Juni.

KIBWANA NA KIBU WALIPOPEANA POLE BAADA YA KUUMIZANA

Image
BEKI wa Yanga, Kibwana Shomari (kulia) na mshambuliaji wa Simba, Kibu Dennis wakipeana pole baada ya wawili hao kuumia kufuatia kugongana kwenye ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Wote walishindwa kuendelea na mchezo, Yanga ikiibuka na ushindi wa 1-0, bao pekee la Feisal Salum dakika ya 25.

NI COASTAL NA YANGA FAINALI ASFC, AZAM YAFA KWA MATUTA

Image
TIMU ya Coastal Union ya Tanga imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalti 6-5 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Sasa Coastal, mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwaka 1988 watakutana na Yanga katika Fainali Julai 2, mwaka huu hapo hapo Sheikh Amri Abeid. Waliofunga penalti za Coastal ni Muhsin Makame, Amani Kyata, Paschal Kitenge, Abdul Suleiman, Willy Kisingi na Mbaraka Hamza, wakati Miraj Hassan alipiga juu ya lango. Kwa upande wa Azam waliofunga ni Rodgers Kola, Bruce Kangwa, Never Tigrere, Aggrey Morris na Idris Mbombo, wakati ya Lusajo Mwaikenda iliokolewa na kipa Mohamed Hussein huku Charles Zulu akipiga juu. Ikumbukwe jana Yanga iliwatoa mabingwa watetezi, Simba kwa kuwachapa 1-0, bao la Feisal Salum Abdallah dakika ya 25 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

NI REAL MADRID MABINGWA ULAYA

Image
TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kutwaa taji la UEFA Champions League  kwa mara ya 14 ya rekodi baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Liverpool, bao pekee la VinĆ­cius JĆŗnior dakika ya 59 usiku wa jana Uwanja wa Stade de France, Saint-Denis nchini Ufaransa.

MO DEWJI ATAKA SIMBA ISUKWE UPYA IREJESHE MAKALI

Image
RAIS wa heshima wa Simba SC, Mohamed 'Mo' Dewji amesema timu inahitaji kusukwa upya ili kurejesha makali. Kauli hiyo inafuatiwa timu kutemeshwa Kombe la shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kutolewa katika Nusu Fainali. Mo Dewji ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram mara tu baada ya pambano dhidi ya watani, Yanga jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Simba ikichapwa 1-0 bao la kiungo Mzanzibar, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' dakika ya 25 "Hogereni watani! Huu umekuwa msimu mbaya zaidi kwa Simba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Bodi inahitaji kufanya maamuzi magumu juu ya njia ya kusonga mbele. Tunahitaji kurekebisha timu kwa mkakati wa kurudi kwenye matokeo mazuri. Tulikosa ari na kiu ya kushinda mataji mwaka huu,"amesema Mo. Tayari Simba imekwishapoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, kutokana kuachwa mbali na watani wao hao, Yanga. Ikumbukwe mapema mwanzo wa m

YANGA SC 1-0 SIMBA SC (NUSU FAINALI ASFC)

Image
 

FEI TOTO AIPELEKA YANGA FAINALI ASFC, SIMBA YALALA 1-0

Image
VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu, Simba SC jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 25 akimalizia pasi ya kiungo Mganda, Khalid Aucho. Sasa Yanga itakutana na mshindi kati ya Azam FC na Coastal Union zitakazomenyana kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha katika Fainali Julai 2 huko huko Arusha.

KIKOSI CHA YANGA SC KINACHOANZA LEO DHIDI YA SIMBA

Image
 

KUKOSI CHA SIMBA KINACHOANZA LEO DHIDI YA MTANI

Image
 

SIMBA NA YANGA ZATOZWA FAINI KWA MAKOSA TOFAUTI KIRUMBA

Image
KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini kwa makosa tofauti kwenye mechi zao kadhaa zilizopita za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zikiewemo za Jumapili na Jumatatu Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

MAKOCHA, MANAHODHA SIMBA NA YANGA WAELEZA MIPANGO

Image
KOCHA Mkuu wa kikosi cha Yanga, Nassredine Nabi, amesema kesho hawata waachia simba nafasi ya kutinga fainali kwani msimu huu malengo yao ni ubingwa wa Kombe la Shirukisho la Azam ( ASFC) . Yanga wanashuka katika dimba la CCM Kirumba saa Tisa Alasiri, kuvaana na mabingwa watetezi wakombe hilo Wekundu wa Msimbazi Simba SC. Watani wajadi hao kwa msimu huu walikutana mara ya mwisho Mei 30 katika mchezo wa Ligi Kuu nakushindwa kuonuonyeshana umwamba kwakumaliza mchezo huo kwa suluhu kwenye Uwanja wa Mkapa. Akizungumza na Bin  Zubery  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Gold Crest Mkoani Mwanza, Kocha Nabi alisema kesho hawata bweteka katika kulipambania nafasi ya kutinga fainali ya ASFC. Alisema mchezo huo nitofauti kabisa namchezo wa ligi hivyo wataingia kwa tahadhari na malengo yao yakiwa nikuwafunga wapinzani wao. "Tutaingia Kwa tahadhari maana mchezo huu nitofauti nawaligi kwahiyo nia namalengo yetu nikupata ushindi mechi hii ndio funguo ya kwenda fainali lazima tupa

SHABIKI WA SIMBA ASHINDA SH MILIONI 168 PERFECT 12

Image
MKAZI  wa mkoa wa Kagera, Baraka Lugwisha Shoki amejishindia kitita cha Sh 168,972, 500 baada ya kubashiri kiusahihi mechi 12 za mchezo wa   Perfect 12   unaondeshwa na kampuni   ya M-Bet Tanzania . Shoki    ambaye ni shabiki wa Simba, Geita Gold FC na Chelsea alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa yeye kushinda kiasi kikubwa cha fedha hicho kutokana na ugumu wa kubashiri kwa baadhi ya timu zilizokuwa zinacheza.  Alisema kuwa mechi iliyompa wakati mgumu ni kati ya Dodoma Jiji FC na Namungo FC iliyochezwa uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Dodoma Jiji FC kushinda.   Alifafanua kuwa kabla ya mechi hiyo, Namungo FC ilikuwa na matokeo mazuri na Dodoma Jiji FC ilikuwa na matokeo mabaya na ilifanya mabadiliko ya benchi lake la ufundi. Msemaji wa kampuni ya M-Bet Tanzania David Malley (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa droo ya Perect 12 Baraka Lugwisha Shoki ambaye aliweza kubashiriki kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za ligi mbalimbali duniani na kufanikiwa kushinda Sh168, 972,500.

TAIFA STARS KUANZA NA SOMALIA KUFUZU CHAN YA MWAKANI

Image
TANZANIA itaanzia ugenini kwa Somalia katika kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Algeria. Mechi hiyo itachezwa kati ya Julai 22 na 24, kabla ya timu hizo kurudiana Tanzania kati ya Julai 29 na 31 katika mkoa utakaotajwa baadaye na mshindi wa jumla atasonga mbele kwenye mechi za mchujo zitakazofikia tamati Septemba 2, mwaka huu. Fainali za CHAN ilikuwa zifanyike Julai 10 hadi Agosti 1, mwaka huu lakini Shirikisho la Soka (CAF) likasogeza hadi mwakani kutokana na kuahirishwa kwa fainali za zilizopita kusogezwa mbele sababu ya Janga la maambukizi ya virusi vya corona. Ikumbukwe mwezi ujao, Taifa Stars itakuwa na mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).   Taifa Stars itakuwa mgeni wa Niger katika mchezo wa kwanza wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Juni 4 Uwanja wa L'AmitiĆ© mjini Cotonou. Baada ya Taifa Stars itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili wa Kundi F dhidi ya Algeria Juni 8 Uwan

PRISONS NA GEITA GOLD ZAGAWANA POINTI SOKOINE

Image
WENYEJI, Tanzania Prisons wamegawana pointi na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya Leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Jeremiah Juma alianza kuifungia Tanzania Prisons dakika ya 38, kabla ya Danby Lyanga kuisawazishia Geita Gold dakika ya 50. Kwa matokeo hayo, Prisons inafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya 14, wakati Geita Gold pamoja na kufikisha pointi 36 inabaki nafasi ya tano baada ya wore kucheza mechi 26.

CHESA SUPA JACKPOT YA BILIONI 1 KWA SH 1000

KAMPUNI  ya   Michezo na   Burudani   SportPesa   leo   im ezindua   rasmi  Jackpot  mpya   inayoitwa  Supa Jackpot   kama   moja   ya   huduma yao   nyingine   kwa   wachezaji  wake. Akizungumza   ofisini   kwake ,  Oysterbay ,   Mwenyekiti wa   Bodi   ya   Wakurugenzi   Tarimba  Abbas  alisema   leo ni  siku  nyingine   ambayo   kampuni   ya   Sportpesa inatambulisha   huduma   hiyo . ‘’ Najua   bado   watu   wanashauku   na  Jackpot  yetu ambayo   imeliwa  siku  si   nyingi   zilizopita ,   kwa muktadha   huo   baada   ya   kuona   wachezaji   wetu wameanza   kuzoea   viwango   vikubwa   basi   tumeonelea tuwaletee   bidhaa   ambayo   inaendana   na   matamanio yao . Kwa  hivyo   tunazindua   rasmi   leo  Jackpot  hii ambayo   itaanzia   bilioni   moja   na   itaenda   kwa   jina  la SUPA JACKPOT ’’. Akiendelea   Tarimba   anasema  Supa Jackpot  itakuwa   na jumla   ya   timu  17  na  pia  kiwango  cha  pesa   ambacho mchezaji   atatakiwa   kuweka   ni   Tsh   1 000  ili   aweze kuc