Posts

Showing posts from April, 2022

ANCELOTTI AIPA REAL MADRID TAJI LA LA LIGA

Image
KOCHA mkongwe Mtaliano, Carlo Ancelotti ameweka rekodi ya kushinda mataji ya ligi zote kubwa Ulaya baada ya jana kuiwezesha Real Madrid kutwaa ubingwa wa La Liga nchini Hispania. Real Madrid imejihakikishia taji la La Liga msimu huu baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Espanyol jana Uwanja Santiago Bernabéu Jijini Madrid, mabao ya Rodrygo dakika ya 33 na 43, Asensio dakika ya 55 na Karim Benzema dakika ya 81, hivyo kufikisha pointi 81 katika mchezo wa 34, ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani. Ancellotti anabeba taji la La Liga baada ya awali kushinda mataji ya Ligi za nyumbani kwao, Italia, England, Ufaransa na Ujerumani hivyo kuwa kocha wa kwanza kubeba mataji ya ligi tano kubwa Ulaya.

MAN CITY YAITANDIKA LEEDS UNITED 4-0 ELLAND ROAD

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Elland Road, Leeds, West Yorkshire. Mabao ya Man City yamefungwa na Rodri dakika ya 13, Nathan Ake dakika ya 54, Gabriel Jesus dakika ya 78 na Fernandinho dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 83 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 34. 

LIVERPOOL YAICHAPA NEWCASTLE 1-0 ST. JAMES' PARK

Image
BAO la kiungo Mgunea, Naby Laye Keïta dakika ya 19 akimalizia pasi ya Mreno, Diogo Jota limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa St. James' Park, Newcastle. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 82, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 34, wakati Newcastle inabaki na pointi zake 43 za mechi 35 nafasi ya 10.

YANGA 0-0 SIMBA (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA NA YANGA HAKUNA MBABE, SARE 0-0 MKAPA

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wametoa sare ya bila mabao na vinara wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa mara nyingine, utamu wa mechi ulikuwa baina ya Wakongo, beki Henock Inonga Baka ‘Varane’ wa Simba na mshambuliaji, Fiston Kalala Mayele wa Yanga namna ambavyo wamepambana leo uwanjani. Kama ilivyokuwa kwenye mechi ya kwanza ya ligi, Inonga alimdhibti vyema Mayele, kinara wa mabao Ligi Kuu ambaye muda wote wa mchezo alipiga shuti moja tu lililogonga nyavu za pembeni, nje kulia kipindi cha pili. Simba pekee waliofanya jaribio la hatari lililolenga lango, Mkongo mwingine, mshambuliaji Chris Kope Mutshimba Mugalu alipounganishia mikononi mwa kipa Djigui Diarra mpira wa adhabu wa beki Shomari Kapombe kipindi cha pili pia. Zaidi ya hapo mechi ilikuwa ya kukamiana na kuonyeshana ubabe baina ya wachezaji wa pande zote mbili na pongezi kwa refa chipukizi, Ramadhani Kayoko kwa kuimudu pamoja na makosa machache ya kibinadam aliyoyafanya.

AZAM FC YALAZIMISHA SARE KWA GEITA, 2-2

Image
WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya 2-2 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu, Geita, Mabao ya Geita Gold yamefungwa na washambuliaji wake nyota, George Mpole dakika ya 26 na Daniel Lyanga dakika ya 82, wakati ya Azam FC yamefungwa na Ismail Aziz Kader dakika ya 35 na Chilo Mkama la kujifunga dakika ya 89. Azam FC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 20, sawa na Namungo waliocheza mechi moja zaidi zikifuatana nafasi ya tatu na ya nne, wakati Geita Gold sasa ina pointi 28 za mechi 21 nafasi ya sita.

MAN UNITED SARE 1-1 NA CHELSEA OLD TRAFFORD

Image
WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Chelsea ilitangulia kwa bao la Marcos Alonso dakika ya 60 akimalizia pasi ya Kai Havertz kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Man United dakika ya 62 akimalizia pasi ya Nemanja Matić. Chelsea inafikisha pointi 66 katika mchezo wa 33, ingawa inabaki nafasi ya tatu na Manchester United inatimiza pointi 57 katika mchezo wa 35, japokuwa inasalia nafasi ya sita.

BASHUNGWA MGENI RASMI MECHI YA WATANI, MANARA MWANACHAMA YANGA

Image
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Innocent Bashungwa ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Wakati huo huo, Msemaji wa Yanga, Haji Manara leo amekabidhiwa ya uanachama wa kidijitali ya klabu hiyo.

KAYOKO KUCHEZESHA PAMBANO LA WATANI JUMAMOSI

Image
REFA Ramadhani Kayoko ndiye atakayepuliza kipyenga kwenye mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kayoko atasaidiwa na Frank Kombe, wote wa Dar es Salaam na Mohamed Mkono wa Tanga.

TAARIFA ZASEMA MINO RAIOLA AMEFARIKI DUNIA

Image
WAKALA maarufu wa wanasoka kadhaa wakubwa, Mino Raiola ameripotiwa kufariki dunia. Taarifa rasmi zinasema anapambania maisha yake akiwa amelazwa hospitali hali yake ni mbaya. Lakini vyombo vya Habari nchini vimesema amekwishariki dunia akiwa na umri wa miaka 45. Mino ambaye miongoni mwa wanasoka anaowakilisha ni pamoja na Paul Pogba, Erling Haaland na Romelu Lukaku alipelekwa hospital Januari kwa matibabu ya kawaida.

LIVERPOOL YAICHAPA VILLARREAL 2-0 ANFIELD

Image
WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Villarreal ya Hispania katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield, Liverpool. Bao kwanza la Liverpool beki wa Kimataifa wa Ecuador, Pervis Josué Estupiñán Tenorio alijifunga dakika ya 53 akijaribu kuokoa krosi ya Jordan Henderson.  Na la pili lilifungwa na mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mané dakika mbili tu baadaye akimalizia pasi ya nyota wa Misri, Mohamed Salah na sasa timu hizo zitarudiana  Mei 3 Uwanja wa De la Cerámica mjini Villarreal.

UCHAGUZI WA MATAWI YANGA SC WASOGEZWA MBELE

Image
UCHAGUZI wa viongozi wa Matawi wa klabu ya Yanga umesogezwa mbele hadi mwishoni mwa mwishoni mwa mwezi ujao, imesema taarifa ya klabu leo.

KAPTENI BOCCO AREJEA KUIVAA YANGA JUMAMOSI

Image
NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco amerejea mazoezini kuelekea mechi dhidi ya watani, Yanga Jumamosi baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwezi . Simba watakuwa wageni wa Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya mechi ya kwanza miamba hiyo kutoa sare. Na Bocco, mshambuliaji tegmeo la kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin ameanza mazoezi baada ya kukosekana kikosini kwa muda.

DJUMA SHABANI HATARINI KUWAKOSA SIMBA JUMAMOSI

Image
BEKI hodari na tegemeo wa Yanga SC, Mkongo Djuma Shabani yuko shakani kuiwahi mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya watani wa jadi, Simba Jumamosi Uwanja sa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Shabani aliumia kwenye mechi iliyopita dhidi ya Namungo wiki iliopita mwishoni mwa mchezo na kushindwa kuendelea nafasi yake ikichukuliwa na Dickson Job dakika ya 78, ingawa Yacouba Sogne pia ataendelea kukosekana.

ORLANDO PIRATES 0-0 (PENALTI 4-3) SIMBA SC (KOMBE LA SHIRIKISHO)

Image
 

MAN CITY YAICHAPA REAL MADRID 4-3 ETIHAD

Image
WENYEJI, Manchester City jana wamepata ushindi wa 4-3 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad, Jijini Manchester. Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ya pili, Gabriel Jesus dakika ya 11, Phil Foden dakika ya 53 na Bernardo Silva dakika ya 74. Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 33 akimalizia pasi ya Mfaransa mwenzake, beki Ferland Mendy dakika ya 33 na la penalti ya Panenka dakika ya 82 na lingine Vinícius Júnior dakika ya 55. Timu hizo zitarudiana Mei 4 Uwanja wa Santiago Bernabeu Jijini Madrid.

BAKHRESA GROUP INAWATAKIA MAAZIMISHO MEMA YA SIKU YA MUUNGANO

Image
Tunawatakia Watanzania wote Maadhimisho mema ya siku ya Muungano. We wish all Tanzanian's Happy Celebrations of The Union Day. @officialbakhresagroup

SIMBA WAREJEA, HASIRA ZOTE KWA MTANI YANGA JUMAMOSI

Image
KIKOSI cha Simba kimerejea Dar es Salaam leo baada ya jana kutolewa na wenyeji, Orlando Pirates katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa penalti 4-3 Jijini Johannesburg, Afrika Kusini kufuatia sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani. Moja kwa moja Simba inaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

YUSSUF BAKHRESA NA BEKI MGHANA WA LEICESTER CITY...

Image
MKURUGENZU wa Azam FC, Yussuf Bakhresa akiwa na beki Mghana wa Leicester City, Daniel Amartey katika ziara yake ya England.

MUITE HAJI OLE SUNDAY MANARA WA YANGA

Image
MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Sunday Manara leo ameibuka kwenye mkutano na Waandishi wa Habari akiwa kavaa vazi la Kimasai na kusema kuanzia sasa ataitwa Haji Ole Sunday Manara.

KIINGILIO YANGA NA SIMBA SH 5,000 JUMAMOSI DAR

Image
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa watani wa jadi, Yanga na Simba Jumamosi Uwanja sa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ni Sh. 5,000 kwa mzunguko wa chini. Taarifa ya wenyeji wa mchezo, Yanga imesema kwamba viingilio vingine ni Sh. 30,000 VIP A, Sh. 20 000 VIP B. 15,000 VIP C na 10,000 kwa kwa viti vya rangi ya Chungwa (Orange).

YANGA SC 2-1 NAMUNGO FC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC YAFA KIUME, YATOLEWA KWA MATUTA SAUZI

Image
KWA mara nyingine tena, safari ya Simba katika michuano ya Afrika imeishia kwenye Robo Fainali baada ya kutolewa na Orlando Pirates katika Kombe la Shirikisho leo kwa penalti 4-3. Orlando Pirates walimaliza dakika 90 wakishinda 1-0 Uwanja wa Orlando Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, bao la Peprah Kwame dakika ya 60 kwa kichwa, hivyo kufanya sare ya jumla ya 1-1 baada ya Simba kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya Robo Fainali wiki iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwenye mikwaju ya penalti Jonás Mkude na Hennock Inonga Baka walikosa upande tea Simba, huku Shomari Kapombe, Meddie Kagere na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wakifunga. Waliofunga penalti za Orlando Piratas ni Deon Hotto, Hellings ‘Gabadinho’ Mhango, Tshegofatso Mabasa na kipa Richard Ofori , huku ya Kabelo Dlamini ikiokolewa na kipa Aishi Manula.

YANGA PRINCESS YAFUTA UTEJA KWA SIMBA QUEENS

Image
TIMU ya Yanga Princess imeweka historia baada ya kuibuka na ushindi kwa mara ya kwanza dhidi ya mahasimu, Simba Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Bao pekee la Yanga Princess katika mchezo wa leo limefungwa na Clara Luvanga dakika ya 45 na kwa ushindi huo, Watoto we Malkia wa Jangwani wanafikisha pointi 35, ingawa wanabaki nafasi ya tatu, nyuma ya Fountain Gate Princess wenye pointi 38 na mabingwa watetezi, Simba Queens wenye pointi 42 baada ya wote kucheza mechi 15.

MAMELODI YATOLEWA, AHLY YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

Image
VIGOGO, Mamelodi Sundowns wametupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Atlético Petróleos ya Angola katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2, kufuatia kuchapwa 2-1 kwenye mechi ya kwanzq Jijini Luanda wiki iliyopita. Mabingwa watetezi, Al Ahly wao wametinga Nusu Fainali baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Raja Club Athletic jana Uwanja wa Mfalme Mohamed wa 5 Jijini Casablanca na wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia kushinda 2-1 Cairo wiki iliyopita.

YONDAN NA NABI WAFUNGIWA, REFA YANGA NA GEITA KIKAANGONI TFF

Image
BEKI wa Geita Gold, Kelvin Yondan amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh. Milioni 1 kwa kosa la kumchezea rafu ya makusudi mshambuliaji wa Yanga, Mkongo Fiston Kalala Mayele kwenye mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

BAYERN MUNICH WAWEKA REKODI MPYA YA MATAJI ULAYA

Image
VIGOGO, Bayern Munich wamefanikiwa kutwaa taji la 10 mfululizo la Bundesliga baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya mahasimu, Borussia Dortmund jana. Ushindi huo ulitokana na mabao ya Serge Gnabry, Robert Lewandowski na Jamal Musiala unaifanya Bayern itawe ubingwa kwa tofauti ya pointi 12 na Dortmund wanaofuatia na huo ni ushindi wa nane mfululizo dhidi ya Dortmund kwenye ligi ambao hawajashinda mechi yoyote Munich tangu mwaka 2014. Na taji hilo la 10 mfululizo kwa Bayern ni rekodi katika ligi kubwa tano Ulaya, wakifuatiwa Juventus iliyowahi kubeba mataji tisa mfululizo ya Serie A kuanzia msimu wa 2012- hadi 2020.

MESSI AIPA TAJI LA KWANZA PSG

Image
NYOTA Muargentina, Lionel Messi ameiwezesha Paris Saint-Germain kutwaa taji la 10 la rekodi ya Ligue 1, Ufatransa kwa kufunga kwenye sare ya 1-1 na Lens jana Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris. Hilo likiwa taji lake la kwanza anashinda klabu hiyo baada ya kujiunga nayo msimu huu akitokea Barcelona ambako alishinda mataji 10 ya La Liga na manne ya Champions Leagues – na amebakiza mkataba wa mwaka mmoja PSG.

TYSON FURY ASTAAFU BAADA YA KUMCHAPA WHITE KO RAUNDI YA SITA

Image
BONDIA Tyson Luke Fury 'Gipsy King' ametangaza rasmi kustaafu ndondi baada ya kutetea tena taji lake la WBC uzito wa juu kwa kumpiga Muingereza mwenzake, Dillian Whyte mbele ya mashabiki 94,000 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Wembley Jijini London. Fury alimmaliza White kwa Knockout (KO) raundi ya sita na ikibidi awekewe kifaa cha kumsaidia kupumua baada ya kichapo hicho. Fury anastaafu baada ya kushinda mapambano  Anakuwa bondia wa pili tu wa uzito wa juu baada ya Mmarakani, marehemu Rocco Francis Marchegiano 'Rocky Marciano' kustaafu bila kupoteza pambano. Marciano aliyepigana ngumi za kulipwa kuanzia mwaka 1947 hadi 1955, alishikilia ubingwa wa dunia kuanzia mwaka 1952 hadi 1956 kabla ya mbabe huyo aliyekuwa anapigana style ya Orthodox kama Fury kufariki dunia Agosti 31, mwaka 1969 akiwa ana umri wa miaka 45 huko Newton, Iowa, Marekani. Alipigana jumla ya mapambano 49 akishinda yote, 43 kati ya hayo kwa KO, wakati Fury ameshinda mapambano 32, kati ya hayo, 23

DODOMA JIJI YAZINDUKA, YAICHAPA MBEYA CITY 2-1

Image
 

YANGA YAICHAPA NAMUNGO 2-1 , MAYELE ATETEMA TENA

Image
VIGOGO, wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 17 na kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 39, wakati la Namungo limefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 33. Yanga inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 20 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 13 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi, wakati Namungo inabaki na pointi zake 29 za mechi 21 sasa nafasi ya tatu.

GEITA GOLD YAILAMBA KMC 2-0 NYANKUMBU

Image
WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Mabao ya Geita Gold ya kocha Freddy Felix Minziro yamefungwa na Amos Charles dakika ya 48 na George Mpole dakika ya 75 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 27 katika mchezo wa 20 na kupanda nafasi ya tano, ikizidiwa pointi moja na Azam FC ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi. KMC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 24 za mechi 21 ikishukia nafasi ya tisa.

JESUS APIGA NNE, MAN CITY YAITANDIKA WATFORD 5-1

Image
WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Pongezi kwa Gabriel Jesus aliyefunga mabao manne peke yake dakika za nne, 23, la penalti dakika ya 49 na 53, wakati lingine limefungwa na Rodri dakika ya 34, huku bao pekee la Watford likifungwa na Hassane Kamara dakika ya 28. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 80 katika mchezo wa 33 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi. Watford baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 22 za mechi 33 nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20.

ARSENAL YAICHAPA MAN UNITED 3-1 EMIRATES

Image
WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Nuno Tavares dakika ya tatu, Bukayo Saka dakika ya 32 kwa penalti na Granit Xhaka dakika ya 70, wakati la Man United limefungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 34 huku Bruno Fernandes akikosa penalti dakika ya 57. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 60 katika mchezo wa 33 na kujiweka sawa nafasi ya nne, ikiizidi pointi sita Man United ambayo imecheza mechi moja zaidi na inabaki nafasi ya sita.

MBEYA KWANZA YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 SONGEA

WENYEJI, wahamiaji Mbeya Kwanza wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma. Mabao ya Mbeya Kwanza leo yamefungwa na Hamisi Kanduru dakika ya 26 na Willy Edgar dakika ya 90 na kwa ushindi huo inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 21, ingawa inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16, ikizidiwa pointi moja na ndugu zao, Tanzania Prisons ya Mbeya nayo, ambayo pia ina mechi moja mkononi. Coastal Union baada ya kipigo cha leo inabaki na pointi zake 21 za mechi 21 na kushukia nafasi ya 14. Mbali ya timu mbili kushuka moja kwa moja mwishoni mwa msimu, mbili zitakwenda kucheza na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.

FEI TOTO NA AUCHO FITI KABISA KUIVAA NAMUNGO KESHO

Image
KIUNGO Mzanzibari wa Yanga SC, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ aliyekosekana tangu mwezi uliopita yuko fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Pamoja na Fei Toto, kiungo Mganda Khalid Aucho aliyekosekana pia tangu mwezi uliopita na winga Mkongo, Chico Ushindi nao wako tayari kwa mchezo wa kesho. Lakini kwa mujibu wa Kocha Msaidizi, Cedric Kaze kesho Yanga itawakosa kiungo Mrundi mwenzake, Saido Ntibanzokiza na majeruhi wa muda mrefu, mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne ataendelea kukosekana.

SIMBA SC WALIVYOTUA SAUZI KUIVAA ORLANDO PIRATES JUMAPILI

Image
WACHEZAJI wa Simba SC baada ya kuwasili Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini leo kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Orlando Pirates Jumapili.

MBUNI YAPANDA LIGI YA CHAMPIONSHIP MWANZA

Image
TIMU ya Mbuni FC ya Arusha imefanikiwa kupanda Ligi ya Championship kutoka First League baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 katika mchezo wa Nusu Fainali leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.