Posts

Showing posts from March, 2022

LIGI KUU YAREJEA LEO, UHONDO WOTE AZAM TV

Image
BAADA ya mapumziko ya wiki moja na ushei kupisha kalenda y mechi za kimataifa, Ligi Kuu ya Tanzania Bara inarejea leo kwa mchezo mmoja, Polisi Tanzania wakiwakaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, ambayo itaonyeshwa LIVE na Azam Sports 1 HD kuanzia Saa 10:00 jioni.

SIMBA NA GENDAMARIE KUCHEZWA SAA 4:00 USIKU

Image
MCHEZO baina ya wenyeji, Simba SC na US Gendamarie ya Niger utachezwa muda mmoja na mchezo mwingine wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, RSB Berkane na ASEC Mimosas Jumapili. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeamua mechi zote zianze Saa 4:00 usiku ili kuondoa uwezekano wa upangwaji matokeo iwapo michezo hiyo itachezwa muda tofauti. Wakati Simba watakuwa wenyeji wa US Gendamarie Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ASEC watakuwa wageni wa Berkane Uwanja wa Manispaa ya Berkane nchini Morocco, Saa 4:00 usiku. ASEC ndio inaongoza Kundi D kwa pointi zake tisa, ikifuatiwa na Berkane na Simba zenye pointi saba kila moja, wakati Gendamarie ina pointi tano, maana yake timu zote zinaweza kumaliza nafasi mbili za juu na kwenda Robo Fainali.

AISHA MASAKA ALIVYOYAANZA MAISHA YA ULAYA

Image
MSHAMBULIAJI chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Aisha Khamis Masaka ‘Aisha Magoal’ (18), akiwa mazoezini na timu yake mpya, BK Hacken Jijini Gothenburg, Sweden baada ya kutambulishwa kufuatia kujiunga nayo akitokea Yanga Princess ya nyumbani, Dar es Salaam.

UNGA MAHSUS WA BOFLO UNAPATIKANA ZANZIBAR PEKEE

Image
Tumia unga wetu mahsus kwa ajili ya Boflo kuandaa mikate bora ya Boflo. Unapatikana Zanzibar pekee.  Use our special Boflo flour to prepare the best Boflo breads. Available in Zanzibar Only. @zanzibarmilling @officialbakhresagroup

YANGA YAICHAPA MAFUNZO 3-2 CHAMAZI

Image
VIGOGO, Yanga SC wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na Mapinduzi Balama dakika ya 19, Heritier Makambo dakika ya 52 na Fiston Kalala Mayele kwa penalti dakika ya 71, wakati ya Mafunzo yamefungwa na Ahmed Maulid dakika ya tisa na Abdulhakim dakika ya 55.

HUHITAJI LAINI MPYA KUJIUNGA NA AZAM PESA

Image
Manake hapo kwanza nicheke! 😆 Huhitaji laini mpya kujiunga na AzamPesa! Vimba kwa kutumia namba yako ya Tigo, Airtel au Zantel.  Jisajili leo kupitia wakala wa AzamPesa karibu yako ufurahie Huduma za Kifalme kwa Bei za Kizawa. @officialbakhresagroup @azampesa #AzamPesa #HudumazaKifalme #BeizaKizawa

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA JUMA PONDAMALI (II)

Image
 

MASATU KATIKA KUNDI LA WACHEZAI WA YANGA

Image
BEKI wa Simba SC, George Magere Masatu katika kundi la wachezaji wa Yanga wakati wa mazoezi ya kupasha misuli moto kabla ya mchezo baina ya watani wa jadi mwaka 1993 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

TANZANIA 1-1 SUDAN (MECHI YA KIRAFIKI)

Image
 

BRUNO APIGA MBILI, URENO YAFUZU KOMBE LA DUNIA

Image
MABAO ya mshambuliaji wa Manchester United, Bruno Fernandes dakika ya 32 na 65 jana yaliipa Ureno ushindi wa 2-0 dhidi ya Macedonia Kaskazini katika mchezo wa mwisho wa mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia Uwanja wa Do Dragão Jijini Porto.  Macedonia Kaskazini iliyoitoa Italia katika mechi ya kwanza ya mchujo, ilishindwa kufurukuta mbele ya Ureno iliyoongozwa na gwiji wake, mshambuliaji wa Manchester United.

QATAR 2022 NI CAMEROON, SENEGAL, GHANA, MOROCCO NA TUNISIA

Image
MABALOZI wa Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini Qatar ni Cameroon, Ghana, Morocco, Senegal na Tunisia. Cameroon imefuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya nane baada ya ushindi wa 2-1 ndani ya dakika 120 dhidi ya wenyeji, Algeria usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida.  Mshambuliaji wa Bayern Munich ya Ujerumani, Erick Choupo-Moting alianza kuifungia Cameroon dakika ya 22, hilo likiwa sawa na bao la kusawazisha baada ya Algeria kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Younde bao pekee la mshambuliaji wa Sporting Lisbon ya Ureno Islam Slimani dakika ya 40. Mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza baada ya kutimua dakika 90 Cameroon ikiongoza 1-0 na mshambuliaji wa RKC Waalwijk ya Uholanzi, Ahmed Touba akaisawazishia Algeria dakika ya 118 likiwa sawa na bao la ushindi kwao kwa matokeo ya jumla. Lakini wakati refa Bakary Papa Gassama wa Gambia anajiandaa kupuliza kipyenga cha kuhitimisha mchezo huku mashabiki wa nyumbani

STARS YATOA SARE 1-1 NA SUDAN DAR

Image
TANZANIA imelazimishwa sare ya 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Sudan ilitangulia kwa bao la Sadiq Totto mapema tu dakika ya pili, kabla ya Simon Msuva kuisawazishia Taifa Stars dakika ya 67.

AZAM FC YAICHAPA DTB 1-0 KIRAFIKI CHAMAZI

Image
BAO pekee la beki Edward Charles Manyama dakika ya 79, limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya DTB katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

KONGAMANO LA MICHEZO MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA

Image
WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeandaa kongamano la Michezo kuazimisha mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan madarakani.

YANGA KUKATA UTEPE ROBO FAINALI ASFC

Image
VIGOGO, Yanga SC ndio watakata utepe katika Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kumenyana na Geita Gold Aprili 10, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

YANGA YAMPONGEZA KIONGOZI WAKE KWA UTEUZI

Image
KLABU ya Yanga imempongeza Mwanasheria wake, Wakili Simon Patrick kwa kuteuliwa kwake kuwa mmoja wa Mawakili Wasaidizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

WANAFUNZI UDOM WATEMBELEA AZAM COMPLEX

Image
WANAFUNZI na wakiambatana na Serikali yao ya wanafunzi, wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), leo wametembelea makao makuu ya klabu ya Azam FC, Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu klabu hiyo yenye uwekezaji mkubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati.

BERKANE WATOZWA FAINI MILIONI 250 FUJO DHIDI YA SIMBA

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeitoza faini klabu ya RS ​​Berkane ya Morocco faini ya jumla ya dola za Kimarekani 108,000, zaidi ya Sh. 250 za Tanzania  kwa kufanya vurugu kwenye mechi zote mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya Simba. Katika mechi hizo za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika, nchini Morocco mashabiki wa Berkane waliwatupia vitu wachezaji wa Simba Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Februari 27, mwaka huu  wenyeji wakishinda 2-0 na kwa kosa hilo wametozwa faini ya dola 8,000. Na kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wenyeji Simba wakiibuka na ushindi wa 1-0 Machi 13, Makamu wa Rais wa Berkane, Majjid Madrane alivamia uwanjani na kuwaongoza wachezaji wake kuwafanyia fujo marefa. Kwa kosa hilo, Kamati ya Nidhamu ya CAF kwanza imemfungia Madrane kujihusisha na shughuli zozote za soka zinazotambauliwa na bodi hiyo ya kandanda barani kwa mwaka mmoja pamoja na kumpiga faini ya dola za Kimarekani 100,000.
Image
TIMU ya Azam FC itakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya DTB Jumanne Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.  Kwa Azam, mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC Aprili 6, mwaka huu hapo hapo Azam Complex. Na kwa DTB mechi hiyo ni ya kujipanga kwa michezo yake ijayo ya ligi ya kuwania kupanda Ligi Kuu, ijulikanayo kama Championship. Ikumbukwe Yanga wao watakuwa na mechi ya kujipima pia Jumatano hapo hapo Chamazi dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.

MAYELE AKIMPA MAARIFA YA KIUSHAMBULIAJI CHIPUKIZI WA YANGA

Image
KINARA wa mabao Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele akimpa maarifa ya kiushambuliaji na ufungaji mshambuliaji chipukizi wa timu hiyo, Yussuf Athumani katika mazoezi ya timu hiyo kambini kwao, Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

SIMBA SC WAINGIA KAMBINI KUJIANDAA KUIVAA USGN

Image
KIKOSI cha Simba kimeingia kambini leo kujiandaa mechi yake ya mwisho ya Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendamarie ya Niger Aprili 3, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Simba inahitaji ushindi lazima katika mchezo huo ili kujikatia tiketi ya kwenda Robo Fainali.

DTB YAENDELEZA UBABE CHAMPIONSHIP

Image
TIMU ya DTB imeendeleza ubabe katika mbio za kuwania kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara kupitia michuano ya Championship baada ya ushindi wa 2-1 jana dhidi ya Transit Camp Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mabao ya DTB yalifungwa na Johnson Clement na Mghana Nicholas Gyan  la Transit Camp lilifungwa na Kalegea Wazanga. Katika mchezo huo, timu zote zilimaliza, DTB wakimpoteza mshambuliaji wao Mrundi, Amissi Tambwe na Transit wakiwapoteza Wazanga na Omar Shaaban waliotolewa kwa kadi nyekundu. Kwa matokeo hayo, DTB inafikisha pointi 52 na kuendelea kuongoza Championship kwa pointi tano zaidi ya zote, Ihefu SC ya Mbeya na Kitayosce ya Tabora baada ya timu zote kucheza mechi 22.

KIDUKU ATWAA UBINGWA WA AFRIKA

Image
BONDIA Mtanzania, Twaha Kassim Rubaha ‘Twaha Kiduku’ jana amefanikiwa kutwaa taji la ubingwa wa Afrika wa UBO uzito wa Super Middle baada ya ushindi wa pointi dhidi ya Mkongo Alexandre Kabangu Tshiamuandaukumbi wa Tanzanite Hall mjini Morogoro. Kiduku anafikisha mapambano 19 ya kushinda, akiwa amepoteza, moja droo na manane ya kupigwa, saba akiwa amepigwa nje ya nchi – moja tu alichapwa na mwamba anaitwa Idd Pialari Desemba 25, mwaka 2016 PTA Saba Saba, Dar es Salaam, ambalo lilikuwa pambano lake la tisa la ngumi za kulipwa.

MUDA WA KUVIMBA NA AZAM PESA

Image
Ni muda wa kuvimba na @AzamPesa, huduma mpya ya kifedha nchini Tanzania. Weka, tuma, pokea na toa pesa, fanya malipo ya bidhaa & bili.  Wahi kujisajili kwa wakala wetu ukiwa na vitu vitatu tu; 1. Simu📱 2. NIDA 💳 3. Dole gumba 👍🏾 @azampesa @azampesa @azampesa #AzamPesa #HudumazaKifalme #BeizaKizawa

MAMBO YANAVYOZIDI KUNOGA KITUO CHA TFF KIGAMBONI

Image
ZOEZI la utandikaji nyasi bandia kwenye uwanja wa Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam linaendelea vizuri kama inavyoonekana pichani.

WAARABU WANNE WATANGULIZA MGUU MMOJA MMOJA QATAR 2022

Image
TIMU za Kaskazini mwa Afrika zimepata matokeo mazuri dhidi ya timu za ukanda wa Jangwa la Sahara katika mechi za kwanza za raundi ya mwisho kufuzu Kombe la  Dunia baadaye mwaka huu nchini Qatar. Uwanja wa Kimataifa Cairo Jijini Cairo, wenyeji Misri wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Senegal, bao la kujifunga la beki wa Nancy ya Ufaransa, Saliou Ciss dakika ya nne. Uwanja wa Douala Jijini Douala, wenyeji, Cameroon wamechapwa 1-0 na Algeria, bao pekee la mshambuliaji wa Sporting Lisbon ye Ureno, Islam Slimani dakika ya 40, Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako, wenyeji, Mali wamechapwa 1-0 na Tunisia, bao la kujifunga la beki wa Standard Liège ya Ubelgiji, Moussa Sissako dakika ya 36. Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa, wenyeji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wamelazimishwa sare ya 1-1 na Morocco.  Mshambuliaji sa Brentford ya England,  Yoane Wissa alianza kuifungia DRC dakika ya 12, kabla ya mshambuliaji wa Gent ya Ubelgiji, Tarik Tissoudali kuisawazishia Mo

WANAFUNZI FEZA BOYS WATEMBELEA AZAM FC LEO

Image
WANAFUNZI wa shule ya Feza Boys leo wametembelea viunga vya Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu klabu hiyo pendwa.

KUZIONA SIMBA NA GENDAMARIE BUKU TATU TU

Image
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba was SC na US Gendamarie ya Niger Aprili 3, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ni Sh 3,000.