MSHAMBULIAJI Mfaransa, Kylian Mbappé Lottin jana alifunga bao lake la 29 katika msimu wa La Liga , Real Madrid ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Sevilla Uwanja wa Ramón Sánchez Pizjuán Jijini Sevilla. Mbappe alie katika msimu wake wa kwanza baada ya kuwasili kutoka Paris Saint-Germain alifunga bao hilo dakika ya 75 akimalizia pasi ya kiungo mkongwe Mcroatia, Luka Modrić – kabla ya kiungo wa Kimataifa wa England, Jude Bellingham kufunga bao la pili dakika ya 87 akimalizia pasi yamshambuliaji Gonzalo GarcÃa. Mbappe anaendelea kuongoza kwa mabao yake 29, kati ya hayo saba amefunga kwa penalty akifuatiwa na mshambuliaji mkongwe wa Kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski mwenye mabao 25. Kwa ujumla Mbappe amekwishafunga mabao 40 katika mechi 54 za msimu wake huu wa kwanza Hispania baada ya kujiunga na Los Blancos – idadi ambayo inapitwa na Ronaldo Lima pekee aliyefunga mabao 47 akiwa Barcelona msimu wa 1996/1997. Mbappe amefunga kwenye michuano mikubwa, mbali na mabao 29 ya La Lig...
Samahani mimi niliunganishwa azam pesa ya uwakala mda kidogo umepita saivi nikijaribu kuingia inagoma sijui tatizo ni nini..?
ReplyDelete