Posts

Showing posts from August, 2020

PAPY KABAMBA TSHISHIMBI AJIUGA NA AS VITA CLUB BAADA YA KUMALIZA MKATABA WAKE YANGA SC

Image
ALIYEKUWA kiungo wa Yanga SC, Papy Kabamba Tshishimbi leo amejiunga na AS Vita ya kwao, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasa ya Kongo (DRC) kufuatia kumaliza mkataba wake tmu ya Jangwani

YANGA SC YALAANI VIKALI KITENDO CHA MASHABIKI WAKE KUMFANYIA FUJO SHABIKI WA SIMBA SC

Image
KLABU ya Yanga SC ya Dar es Salaam imelaani vikali kitendo cha mashabiki wake, kumfanya fujo mchezaji wa timu pnzan, Smba SC.

POLISI TANZANIA YAWASAJILI YAHYA MBEGU KUTOKA MWADU FC NA DEUS 'SHARO' WA ALLIANCE FC

Image
Beki wa kushoto, Yahaya Mbegu akikabidhiwa jezi ya Polisi Tanzania baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu hiyo aktokea Mwadui FC ya Shinyanga  Kiungo mshambuliaji Deusdedit Cossmas 'Sharo' (kulia) amesiani mkataba wa miaka miwili kujiunga na Polisi Tanzania kutoka Alliance FC ya Mwanza

YACOUBA SOGNE AKABIDHIWA JEZI NAMBA 10 BAADA YA KUKAMILISHA UHAMISHO WAKE YANGA SC

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Sogne akiwa ameshka jezi namba 10 baada ya kukabidhiwa leo kufuatia kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Yanga SC Asante Kotoko ya Ghana  

HAMAD HILIKA ASAJILIWA MTIBWA SUGAR NA KUFUNGA MABAO MAWILI KATIKA USHINDI WA 6-2 LEO GAIRO

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KLABU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Ibrahim Hamad Ahmada 'Hilika' kutoka Zimamoto ya Zanzibar. Hilika anacheza nafasi ya ushambuliaji, mfungaji bora mara mbili ligi kuu Zanzibar msimu 2019/2020 na 2016/2017, Pia amewahi kuibuka mfungaji bora katika kombe la Mapinduzi Cup. Hilika almaarufu striker wa nchi amesaini mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi cha wana tam tam. Mtibwa Sugar imemsajili mshambuliaji Ibrahim Hamad 'Hilika' kutoka Zimamoto ya Zanzibar  Hilika pia ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha Zanzibar Heroes, Huu ni usajili wetu wa nane na mwisho kuelekea msimu wa 2020/2021. Wengine wapya Mtibwa Sugar ni  Abubakar Ame Omar   AbalKassim Khamis, Baraka Gamba Majogoro, George Makanga, Geofrey Luseke na Hassan Kessy Ramadhan. Wakati huo huo: Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 6-2 dhidi Kombaini ya Gairo katika mchezo kirafiki Uwanja wa CCM Gairo.  Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Boban Z

LUIS MIQUISSONE APIGA HAT TRICK SIMBA SC YAITANDIKA ARUSHA FC 6-0 MECHI YA KIRAFIK SHEIKH AMRI ABED

Image
Kiungo wa Simba SC, Luis Miquissone raia wa Msumbiji (kulia) akishangilia bada ya kuifungia timu yake hiyo mabao matatu dakika za 64, 76 na 88 katika ushindi wa 6-0 dhido ya Arusha FC kwenye mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Aruaha. Mabao mengine ya Simba yamefungwa na mshambuliaij Meddie Kagere mawili dakika ya tano na 34 na Mzambia, Larry Bwalya dakika ya 24                  

MSHAMBULAJI MPYA, YACOUBA SOGNE AWASILI KUTOKA KWAO, BURKINA FASSO KUKAMILISHA KIKOSI KIPYA CHA YANGA SC

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Sogne akiwapungia mkono huku amebeba bendera mashabiki wa Yanga SC baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiunga na klabu yake hiyo mpya, akitokea Asante Kotoko ya Ghana  Yacouba Sogne (kulia)  akiwa   na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM, wadhamini wa Yanga SC leo JNIA 

MTIBWA SUGAR YASAJILI WENGINE WAWILI JUMA NYANGI NA ABUBAKAR AME NA KUFIKISHA SABA WAPYA JUMLA

Image
KLABU ya Mtibwa Sugar imemsajili kiungo wa kati Juma Nyangi Ganabali kutoka Alliance FC ya Mwanza iliyoshuka daraja kwa mkataba wa miaka miwili.  Mtibwa Sugar imemsajili beki, Abubakar Ame Omar kutoka Malindi FC ya Zanzibar ambaye pia yumo kwenye kikosi cha timu ya visiwani humo, Zanzibar Heroes akiwa anamudu kucheza nafasi za beki wa kati, kiungo wa chini na beki wa kulia. Pichani kutoka kushoto ni Mohamed Jabr (Mwenyekiti Malindi), Swabr Abubakar (Ofisa wa sheria na utawala Mtibwa Sc), Abubakar Ame, Mohamed Masoud (Katibu Malindi) na Hussein Ahmada (meneja wa mchezaji) Sasa Mtibwa Sugar imesajili wachezaji wapya saba, wengine AbalKassim Khamis, Baraka Gamba Majogoro, George Makanga, Geofrey Luseke na Hassan Kessy Ramadhan.

YANGA SC 2-0 AIGE NOIR (MECHI YA KIRAFIKI MKAPA)

Image

SIMBA SC 2-0 NAMUNGO FC (NGAO YA JAMII ARUSHA)

Image

AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA TANZANIA PRISONS LEO CHAMAZI

Image
Mshambuliaji wa Azam FC, Richard Ella D'jodi akitafuta maarifa ya kumtoka beki wa Tanzania Prisons katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka 1-1, Prisons wakitangulia kwa bao la Jeremiah Juma kabla ya Mzambia Obrey Chirwa kuisawazishia Azam FC 

YANGA SC YAWACHAPA AIGLE NOIR 2-0 MKAPA KWENYE KILELE CHA WIKI YA MWANANCHI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM VIGOGO wa soka Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Burundi, Aigle Noir katika mchezo wa kirafiki usiku wa leo Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi. Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais mstaafu wa awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete – Aigle Noir iliwaruhusu Yanga kupata mabao baada ya kiungo wake, Mghana Koffi Kouassi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29 kufuatia kuonyeshwa kadi ya njano ya pili na refa Martin Saanya wa Morogoro.  Baada ya hapo Yanga SC wakapata bao la kwanza dakika ya 39 likifungwa na winga wake mpya, Tuisila Kisinda aliyemchambua kipa Mtanzania wa Aigle Noir, Erick Johola kufuatia pasi nzuri ya Feisal Salum ‘Fei Toto’.   Mshambulaji mpya, Mghana Michael Sarpong akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 59 kwa kichwa kikali kutoka umbali wa mita sita kufuatia krosi maridhawa ya Ditram Nchimbi. Na ikashuhudiwa kipindi

MORRISON ASETI LA KWANZA, APIGA LA PILI SIMBA YAICHAPA NAMUNGO 2-0 NA KUTWAA NGAO YA JAMII YA SITA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA wa mataji yote nchini, Simba SC wamefanikiwa kutwaa na Ngao ya Jamii baaa ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Namungo FC jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Nyota wa mchezo wa leo amekuwa ni mchezaji mpya, winga Mghana Bernard Morrison aliyeseti bao la kwanza kipindi cha kwanza na kufunga la pili kipindi cha pili. Nahodha John Raphael Bocco aliifungia Simba SC bao la kwanza kwa penalti dakika ya saba baada ya Morrison kuangushwa kwenye boksi – kabla ya winga huyo Mghana kufunga la pili dakika ya 60 akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama. Na huo unakuwa ushindi wa sita wa Ngao ya Jamii kwa Simba SC tangu ianzishwe mwaka 2001, na kuwa timu iliyobeba taji hilo mara nyingi zaidi, ikifuatiwa na watani wa jadi, Yanga SC waliotwaa mara tano.  Simba SC imebeba Ngao ya Jamii katika miaka ya 2011 ikiifunga Yanga 2-0, 2012 ikiifunga Azam FC 3-2, mwaka 2017 ikiwafunga Yanga kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0, 2018 ikiwafunga Mt

BEKI HODARI WA KULIA, HASSAN RAMADHANI KESSY AREJEA KLABU YA MTIBWA SUGAR KUTOKA NKANA FC YA ZAMBIA

Image
BEKI wa kulia, Hassan Ramadhan Kessy akiwa na nakala za mkataba wa kujiunga tena na Mtibwa Sugar ya Morogoro kutoka Nkana FC ya Zambia. Kessy aliibukia Mtibwa Sugar kabla ya kwenda kuchezea watani wa jadi, Simba na Yanga SC za Dar es Salaam 

CARLOS CARLINHOS NA NYOTA WENGINE YANGA SC KWENYE MAZOEZI LEO MKAPA MBELE YA KOCHA MPYA

Image
Kiungo wa Yanga SC, Muangola Carlos Carlinhos akipiga mpira kwenye mazoezi ya timu yake leo Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi kesho kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Mshambulaji mpya wa Yanga SC, Mghana Michael Sarpong akipiga mpira mazoezini leo   Kiungo mpya wa Yanga SC, Mkongo Tonombe Mukoko akipiga mpira mazoezini leo   Mshambulaji mpya wa Yanga SC, Waziri Junior akipiga mpira mazoezini leo   Kocha mpya wa Yanga SC, Mserbia Zlatko Krmpotic (kulia) akiwa na Mweyekiti wa klabu, Dk Mshindo Msolla mazoezini leo  

RALLY BWALYA NA MAFUNDI WENGINE MAZOEZINI SIMBA SC LEO IKIJIANDAA KUIVAA NAMUNGO FC KESHO ARUSHA

Image
Kiungo mpya wa Simba SC, Mzambia Rally Bwalya akifanya vitu vyake kwenye mazoezi ya timu hiyo leo kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii kesho dhidi ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Beki Shomari Kapombe akipasua na mpira kwenye mazoezi ya leo ya Simba   Charles Ilamfya akiwakokota wachezaji wenzake mazoezini leo Arusha  Beki Kennedy Wilson akimiliki mpira katikati ya viungo Clatous Chama (kushoto) na Jonas Mude kushoto  Nahodha na mshambuliaji John Bocco akiudhibiti mpira leo mazoezini

TWAHA KIDUKU ALIVYOMSHINDA DULLAH MBABE KWA POINTI

Image

ARSENAL WAICHAPA LIVERPOOL KWA MATUTA NA KUBEBA NGAO YA JAMII ENGLAND

Image
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia na Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Liverpool jioni ya leo Uwanja wa Wembley Jijini London. Arsenal ilitangulia kwa bao la Nahodha wake, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 12 kabla Takumi Minamino kuisawazishia Liverpool dakika ya 73. Waliofunga penalti za Arsenal ni Reiss Nelson, Ainsley Maitland-Niles, Cedric Soares, David Luiz na Aubameyang na za Liverpool walifunga Mohamed Salah, Fabinho,  Minamino na Curtis Jones,wakati Rhian Brewster alikosa   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI LIGI KUU, NOVATUS DISSMAS AONGEZA MKATABA AZAM FC HADI 2023

Image
Mchezaji Bora Chipukizi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita, Novatus Dissmas akiwa na Biashara United alipokuwa anacheza kwa mkopo ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuwa mali ya Azam FC hadi mwaka 2023 

GEITA GOLD YAMCHUKUA KOCHA FREDDY FELIX MINZIRO AWASAIDIE KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO

Image
KLABU ya Geita Gold FC leo imemtangaza rasmi Freddy Felix Minziro (kushoto) kuwa Kocha wake mpya atakayeiongoza timu hiyo katika jaribio lingine tena la kupanda Ligi Kuu ya Tanzana Bara msimu ujao kwa mkataba wa mwaka mmoja