Posts

Showing posts from May, 2021

CAS YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA MORRISON DHIDI YA KESI YA YANGA SC, ITAANZA KUSIKILIZWA JUNI 2

Image
  MAHAKAMA ya Usuluhishi wa Kimataifa ya Michezo (CAS) imetupilia mbali pingamizi la winga Mghana, Bernard Morrison kutaka kesi iliyofunguliwa na Yanga dhidi yake itupwe. Sasa CAS imeamua shauri hilo ambalo Yanga inadai Morrison amesaini kwa wapinzani, Simba akiwa na mkataba na wana Jangwani hao lililofunguliwa Septemba mwaka jana itaanza kusikilizwa Juni 2, mwaka huu.

SIMBA SC KUONDOKA KESHO KWA NDEGE KWENDA MWANZA KUMENYANA NA RUVU SHOOTING MECHI YA LIGI KUU ALHAMISI

Image
 MABINGWA watetezi, Simba SC wanatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kesho asubuhi kwa ndege kwenda Mwanza Alhamisi watacheza mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kufuatia wenyeji, Ruvu Shooting kuamua hivyo, tofauti na kawaida yao mechi zao dhidi ya Simba na Yanga kuchezea Dar es Salaam badala ya Mlandizi mkoani Pwani, ambao Uwanja wao wa Mabatini haukidhi vigezo vya mechi za mashabiki wengi.

FREDDY FELIX MINZIRO ATEULIWA KOCHA BORA WA LIGI DARAJA LA KWANZA BAADA YA KUIPA GEITA GOLD UBINGWA

Image
  KOCHA mzoefu, Freddy Felix Kataraiya Minziro ameteuliwa Kocha Bora wa msimu wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya kuiwezesha timu yake, Geita Gold kutwaa ubingwa wa ligi hiyo. Geita Gold ilitawazwa kuwa bingwa wa ligi hiyo jana baada ya jana kuifunga Mbeya Kwanza 1-0 katika fainali ya Ligi Daraja la Kwanza Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Pamoja na Minziro kuwa kocha Bora, wachezaji wa Geita Gold, Geoffrey Julius amekuwa Mchezaji Bora na John Mwanda amekuwa Kipa Bora.

YANGA SC YAACHANA NA KIUNGO MUANGOLA CARLOS CARLINHOS ALIYEKUWA ANAANDAMWA NA MAJERUHI MFULULIZO

Image
  KLABU ya Yanga imemuacha kiungo Muangola, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo, maarufu kama Carlinhos kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya karibu msimu mzima wa kuwa Jangwani.  Carlinhos hakuwa na msimu mzuri Jangwani tangu asajiliwe Julai mwaka jana kutokana kuandamwa na majeruhi.

GEITA GOLD NDIYO MABINGWA WA LIGI DARAJA LA KWANZA BAADA YA KUICHAPA MBEYA KWANZA 1-0 LEO UWANJA WA UHURU

Image
 TIMU ya Geita Gold imetwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika Fainali leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 120 baada ya 90 kumalizika bila timu hizo kufungana, bao pekee la Geita Gold inayofundishwa na kocha mzoefu, Freddy Felix Isaya Kataraiya Minziro 'Majeshi' limefungwa na Omary Ramadhan dakika ya 111. Ikumbukwe Mbeya Kwanza na Geita Gold zote zimepanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao baada ya kuongoza makundi yao, A na B.

PAMBA SC NA TRANSIT CAMP ZAPANGIWA WAPINZANI VITA YA KUWANIA KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO

Image
MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Muungano, Pamba FC ya Mwanza itamenyana na timu itakayomaliza nafasi ya 13 kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu kuwania kupanda ligi hiyo msimu ujao. Katika droo iliyochezeshwa leo Dar es Salaam, Transit Camp itamenyana na timu itakayomaliza nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu msimu huu. Mechi za kwanza zitachezwa Julai 21 na timu za Daraja la Kwanza zote zitaanzia nyumbani kabla ya kusafiri kuzifuata timu za Ligi Kuu kwa mechi za marudiano Julai 24. Mbeya Kwanza na Geita Gold zimepanda moja kwa moja baada ya kuongoza makundi A na B, wakati Transit Camp na Pamba zinapitia kwenye mchujo, maarufu kama Play-Offs kuwania kupanda.

YANGA SC NA GSM KWA PAMOJA WAIPONGEZA AZAM MEDIA LIMITED KWA KUINGIA MKATABA WA BILIONI 225.6 KUONYESHA LIGI KUU

Image
  KLABU ya Yanga imeipongeza Azam Media Limited kwa kusaini mkataba mpya mnono na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wa Haki za Matangazo ya Televisheni ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Pamoja na Yanga, wafadhili na wadhamini wao, GSM kupitia Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Gharib Mohamed nao wameipongeza Azam Media kwa kitendo hicho. Wiki hii Azam Media Limited imesaini mkataba mpya na TFF wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu kwa miaka 10 zaidi kuanzia msimu ujao wenye thamani ya Sh. Bilioni 225.6.

NAMUNGO FC 1-3 SIMBA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
 

CHELSEA BINGWA ULAYA, YAIPIGA MAN CITY 1-0 URENO

Image
TIMU ya Chelsea imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester City usiku huu Uwanja wa Do Dragão Jijini Porto, Ureno. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 42 akimalizia pasi ya kiungo mwingine wa kimataifa wa England, Mason Mount. Hilo linakuwa taji la pili tu la Ligi ya Mabingwa kwa The Blues baada ya lile walilolitwaa msimu wa 2011–2012 wakiwafunga wenyeji, Bayern Munich katika fainali Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 chini ya kocha wa muda, Mtaliano Roberto Di Matteo. Ushindi huu ni mwendelezo wa ubabe wa kocha Mjerumani, Thomas Tuchel kwa kocha Mspaniola wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Pep Guardiola baada ya kuifunga pia Man City 1-0 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA Aprili 17 na 2-1 kwenye ligi Mei 8.

PAMBA YABISHA HODI LIGI KUU BAADA YA KUITANDIKA KEN GOLD 4-1 LEO UWANJA NYAMAGANA JIJINI MWANZA

Image
 MABINGWA wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pamba SC wamefanikiwa kufuzu hatua ya kuwania kupanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Ken Gold leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Pamba wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 kufuatia kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza. Nayo Transit Camp ya Dar es Salaam imefanikiwa kuwatoa mabingwa wengine wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 1-1 kila timu ikishinda 1-0 nyumbani, mechi ya marudiano ikichezwa leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Sasa Pamba na Transit Camp iliyowahi kucheza Ligi Kuu pia zitamenyana na timu zitakazoshika nafasi ya 13 na 14 Ligi Kuu msimu huu kuwania kupanda. Droo ya mechi hizo itafanyika kesho Dar es Salaam na timu hizo zitacheza mechi mbili nyumbani na ugenini na washindi wa jumla watapanda, au kubaki Ligi Kuu.

BOCCO, MUGALU NA MORRISON WAFUNGA SIMBA SC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA NAMUNGO FC 3-1 RUANGWA

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wametoka nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Namungo ilitangulia kwa bao la Mrundi, Nzigamasabo Steve dakika ya 22, kabla ya Simba kuzinduka kipindi cha pili kwa mabao ya washambuliaji, Mkongo Chris Kope Mutshimba Mugalu dakika ya 79, John Raphael Bocco dakika ya 84 na kiungo Mghana, Bernard Morrison dakika ya 88. Simba SC inafikisha pointi 64 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya mahasimu wao, Yanga SC ambao pia wamecheza mechi tatu zaidi. Namungo FC inabaki na pointi zake 40 za mechi 29 sasa katika nafasi ya nane, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Tanzania Prisons wanaoshika nafasi ya saba, mbele ya Dodoma Jiji FC yenye pointi 39 za mechi 29 pia.

TANZANIA YAKAMILISHA MECHI ZAKE KWA KUCHAPWA 4-2 NA MISRI FAINALI ZA SOKA LA UFUKWENI NCHINI SENEGAL

Image
 TANZANIA imeambulia kipigo cha mabao 4-2 mbele ya Misri katika mchezo wa kuwania nafasi ya tano kwenye Fainali za Afrika za soka la Ufukweni katika ufukwe wa Sally Beach, pembezoni mwa Bahari ya Atlantic Jijini Dakar, Senegal. Tanzania imekamilisha mechi zake za michuano hiyo bila kushinda hata moja kufuatia kufungwa 4-3 na Uganda na 3-1 na wenyeji, Senegal katika Kundi A. Fainali ya michuano hiyo inafanyika leo baina ya Senegal na Msumbiji, ambayo itatanguliwa na mechi ha kusaka mshindi wa tatu baina ya Morocco na Uganda.

MWAKINYO AMPIGA MUANGOLA KWA KO NA KUTWAA TAJI LA WBC

Image
BONDIA Mtanzania Hassan Mwakinyo ametwaa taji la WBC Afrika uzito wa Super Welter baada ya kumpiga kwa Knockout (KO) raundi ya tisa Muangola Antonio Mayala usiku wa Ijumaa ukumbi wa Next Door Arena, Masaki Jijini Dar es Salaam. Mtanzania mwingine,  Ibrahim Mgendera 'Ibra Class' amemshinda kwa pointi Sibusiso Zingange wa Afrika Kusini katika pambano lisilo la ubingwa uzito wa Super Feather raundi nane. Lakini haukuwa usiku nzuri kwa Mtanzania mwingine, Shaaban Jongo maarufu kama Jongo Jongo aliyepigwa kwa KO raundi ya pili na Mnigeria, Olanrewaju Durodora katika pambano la kuwania taji a WBC Afrika uzito Cruiser.

AL AHLY YATWAA SUPER CUP BAADA YA KUICHAPA BERKANE 2-0 QATAR

Image
 TIMU ya Al Ahly ya Misri imefanikiwa kutwaa taji la Super Cup ya Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya RSB Berkane  Uwanja wa Jassim Bin Hamad, au Al-Sadd Jijini Doha nchini Qatar. Mabao ya Ahly yamefungwa na Mohamed Sherif dakika ya 57 akimalizia pasi ya Hussein El Shahat na Salah Mohsen dakika ya 82 akimalizia pasi ya Taher Mohamed. Mechi ya Super Cup hukutanisha bingwa wa Ligi ya Mabingwa ambaye kwa sasa ni Al Ahly na bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, ambaye ni Berkane.

DILUNGA WA SIMBA SC AENGULIWA KIKOSI CHA TAIFA STARS NAFASI YAKE APEWA MUDATHIR YAHYA WA AZAM FC

Image
KIUNGO wa Simba SC, Hassan Dilunga ameenguliwa kwenye kikosi kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichotajwa leo na kocha Mdenmark, Kim Poulsen na nafasi yake amepewa nyota wa Azam FC, Mudathir Yahya. Sasa Mudathir ataungana na wenzake watakaoingia kambini Juni 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi. Sasa kikosi hicho kinabaki na wachezaji saba wa klabu bingwa ya nchi, Simba SC, na wanne kutoka kila timu, Yanga SC na Azam FC zinazofuatia kwa ubora katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Wengine wanne wanacheza nje ya nchi, wawili hapa hapa Afrika na wawili Ulaya, wakati waliosalia wanatoka klabu mbalimbali za hapa nchini. timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoingia kambini Juni 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi. Katika kikosi hicho kuna wachezaji wanane kutoka klabu bingwa ya nchi, Simba SC, na wanne kutoka kila timu, Yanga SC na Azam FC zinazofuatia kwa ubora katika Ligi Kuu ya Tanzani

KIM POULSEN AITA 27 TAIFA STARS, WANANE WANATOKA SIMBA SC...AZAM NA YANGA ZATOA WANNE KILA TIMU

Image
 KOCHA Mdenmark, Kim Paulsen ametaja kikosi cha wachezaji 27 cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoingia kambini Juni 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi. Katika kikosi hicho kuna wachezaji wanane kutoka klabu bingwa ya nchi, Simba SC, na wanne kutoka kila timu, Yanga SC na Azam FC zinazofuatia kwa ubora katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Wengine wanne wanacheza nje ya nchi, wawili hapa hapa Afrika na wawili Ulaya, wakati waliosalia wanatoka klabu mbalimbali za hapa nchini.

KAMATI YA UTENDAJI YAKUTANA LEO DAR NA KUAMUA UCHAGUZI MKUU WA TFF UFANYIKE AGOSTI 7, MWAKA HUU

Image
 UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utafanyika Agosti 7, mwaka huu, imeelezwa. Hayo yamesemwa na Rais wa TFF, Wallace Karia katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari kufuatia kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo kilichofanyika leo ambacho ni cha kawaida cha kikatiba kuzungumzia ajenda za maendeleo ya soka. "Tumepitisha tarehe ya mkutano Mkuu wa TFF kwamba itakuwa ni tarehe 7 Agosti na tarehe hiyo tutampelekea pia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi kumuambia kwamba ni tarehe ambazo tumezipanga kwa mkutano wetu, kwa hiyo na yeye ataendelea kwa taratibu zake, kwa sababu kwenye ajenda yetu, ajenda za Mkutano Mkuu mojawapo inakuwa ni uchaguzi," amesema Karia. Aidha, Karia amesema kwamba katika kikao cha Kamati ya Utendaji wamepokea taarifa ya utekelezaji na kuzungumzia miradi ya ujenzi wa vituo vya Kigamboni Jijini Dar es Salaam na Mnyanjani, Tanga. "Lakini pia tumekuwa na kupokea taarifa kutoka Kamati yetu ya Sheria kwenye marekebisho ya baadhi

SIMBA SC WAZAWADIWA SH MILIONI 50 KWA KUFIKA HATUA YA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
 MDHAMINI mkuu wa Simba  kampuni ya Sportpesa leo imeikabidhi klabu hiyo zawadi ya Sh. Milioni 50 kama zawadi kwa kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba SC ilitinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuongoza Kundi A mbele ya mabingwa watetezi. Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na El Merreikh ya Sudan. Lakini safari yake katika michuano hiyo ilifikia tamati mbele ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao 4-3, ikifungwa 4-0 Johannesburg na kushinda 3-0 Dar es Salaam.

TFF YASEMA KLABU ITAKAYOKUWA INADAIWA NA MCHEZAJI HAITASHIRIKI LIGI KUU MSIMU UJAO

Image
 SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema klabu ambayo itakuwa inadaiwa na mchezaji haitaruhusiwa kushiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.

MMOJA TU APITISHWA KUGOMBEA UENYEKITI WA CHAMA CHA WANASOKA TANZANIA UTAKAOFANYIKA MWEZI UJAO NCHINI

Image
 MWENYEKITI wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA) Mussa Mohamed Kisoki pekee amepitishwa kugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao.

SIMBA SC 3-0 DODOMA JIJI FC (KOMBE LA TFF)

Image
 

TANZANIA YATUPWA NJE FAINALI ZA SOKA LA UFUKWENI AFRIKA BAADA YA KUCHAPWA 3-1 NA SENEGAL JIJINI DAKAR

Image
 TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Soka la Ufukweni Afrika baada ya kuchapwa 3-1 na wenyeji, Senegal katika mchezo wa Kundi A jana fukwe za Bahari ya Atlantic Jijini Dakar. Hiyo ni baada ya timu hiyo kufungwa pia 4-3 na jirani zao, Uganda katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo na sasa itamenyana na Misri kesho kuwania nafasi ya tano. Sasa Senegal itakutana Morocco kesho katika Nusu Fainali na Uganda itamenyana na Msumbiji wakati fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu zitafanyika Jumamosi.

VILLARREAL WAISHINDA MAN UNITED KWA MATUTA NA KUTWAA TAJI LA EUROPA LEAGUE

Image
TIMU ya Villarreal ya Hispania imefanikiwa kutwaa taji la UEFA Europa League  baada ya ushindi wa penalti 11-10 dhidi ya Manchester United ya England kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Energa Jijini Gdańsk, Poland. Gerard Moreno alianza kuifungia Villarreal dakika ya 29 akimalizia pasi ya Dani Parejo, kabla ya  Edinson Cavani kuisawazishia Man United dakika ya 55 akimalizia pasi ya Scott McTominay. Waliofunga penalti za Villarreal ni Gerard Moreno, Dani Raba, Paco Alcácer, Alberto Moreno, Dani Parejo, Moi Gómez, Fred, Francis Coquelin, Mario Gaspar, Paul Torres na kipa Gerónimo Rulli. Na Man United zilifungwa na Juan Mata, Alex Telles, Bruno Fernandes, Marcus Rashford, Edinson Cavani, Albiol, Daniel James, Luke Shaw, Axel Tuanzebe na Victor Lindelof, wakati David de Gea alikosa mkwaju wake ukipanguliwa na kipa mwenzake, Rulli.  GONGA KUSOMA ZAIDI