Posts

Showing posts from July, 2020

KUNGO WA KAGERA SUGAR, ZAWADI PETER MAUYA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA YANGA

Image
Kiungo Zawadi Peter Mauya (katikati) akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC, Wakili Peter Simon (kulia) na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Wana Jangwani hao akitokea Kagera Sugar ya Bukoba 

ERASTO NYONI AMKABIDHI JEZI MPYA DOGO ALIYEANDIKA JINA LAKE KWENYE FULANA CHAKAVU

Image
Beki wa Simba SC, Erasto Edward Nyoni akimkabidhi zawadi ya jezi na bukta shabiki wake  kijana mdogo, Jumanne Ulimwengu ambaye wiki kadhaa zilizopita alionyeshwa Azam TV akiwa na fulana iliyoandikwa jina la mchezaji huyo anayemudu kucheza nafasi za kiungo pia. Baada ya kumkabidhi jezi, mtoto Jumanne amemuomba Nyoni kumnunulia baiskeli ili aitumie wakati wa kwenda shule na Nyoni ameahidi kumnunulia baiskeli hiyo

AKINA MSUVA WALAZIMISHWA SARE YA PILI MFULULIZO YA BILA KUFUNGANA LIGI KUU YA MOROCCO

Image
Na Mwandishi Wetu, MAZGHAN KUINGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana kwa mara nyingine alishindwa kuisaidia timu yake, Difaa Hassan El-Jadidi kuondoka na pointi zote tatu baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan, Casabablanca.  Sare hiyo inafuatia sare nyingine ya 0-0 na Raja Casabablanca hapo hapo Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Morocco baada ya kurejea kufuatia kusimama tangu Machi kutokana na  mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona. Na Msuva (p i cha n i  kul i a) , mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam alicheza mechi zote hizo mbili kwa ustadi mkubwa kama kawaida yake – lakini tu bahati haikuwa yake kuweza kufunga. Na baada ya sare hizo mbili mfululizo, Difaa Hassan El-Jadidi inafikisha pointi 27 kufuatia kucheza mechi 20 za Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro na kupanda kwa nafasi moja hadi ya nane, sasa ikiizidi pointi tatu Youssoufia Berrechid

AWESU AWESU ALIYEKUWA ANATAKIWA NA YANGA ASAINI MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA AZAM FC

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KLABU ya Azam FC imekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wa Kagera Sugar, Awesu Awesu, kwa mkataba wa miaka miwili. Awesu ambaye alikuwa anawaniwa pia na vigogo, Yanga SC, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Azam FC kwenye dirisha kubwa la usajili kwa ajili ya msimu ujao, ukiwa ni usajili huru baada ya kumaliza mkataba wake Kagera Sugar. Kiungo huyo ambaye aliwahi kulelewa kwenye kituo cha Azam Academy kwa miaka miwili 2014-2015, amesaini mkataba huo leo Alhamisi jioni mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'. Rasta huyo amekuwa na kiwango kizuri kwa misimu miwili mfululizo akiwa na Singida United na msimu huu Kagera Sugar, katika mashindano yote msimu huu akiwa amefunga jumla ya mabao saba. Imemchukua safari ya miaka mitano kwa Awesu kurejea tena Azam FC, baada ya kuondoka Azam Academy mwaka 2015, akijiunga na Madini ya Arusha, kabla ya kutua Mwadui kisha Singida United na msimu uliopita Kagera Sugar.

MAREFA WATANO KUCHEZESHA FAINALI YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP SUMBAWANGA JUMAPILI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kwa pamoja na Bodi ya Ligi wametaja marefa watakaochezesha Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) Jumapili Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. Hao ni Abubakar Mturo wa Mtwara, Abdallah Mwinyimkuu wa Singida, Ahmed Arajiga wa Mara, Ramadhani Kayoko wa Dar es Salaam na wasaidizi wao Abdulaziz Ally wa Arusha na Hamdani Said wa Mtwara.   Wote hao watakuwa chini ya mkufunzi Israel Mujuni Nkongo, Mtathmini wa Mechi Soud Abdi wa Arusha na Kamisaa Omar Gindi wa Kigoma. Tayari kikosi cha Namungo FC kipo Sumbawanga tangu jana kwa ajili ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Lindi kutwaa taji hilo, wakati Simba SC wao siku mbili hizi nao watasafiri kwenda Sumbawanga. Azam Sports Federation Cup (ASFC) ni michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania ambayo bingwa wake hushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Lakini kwa mwaka huu Namungo imejihakikishia kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani

IHEFU YABISHA HODI LIGI KUU BAADA YA KUIPIGA MBAO FC 2-0, MBEYA CITY YAJIWEKA NJIA PANDA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya Ihefu FC imebisha hodi Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mabo FC ya Mwanza katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania Uwanja wa Highland Estae, Mbalizi mkoani Mbeya. Mabao ya Ihefu yamefungwa na Steven Mwaijala kwa penalti dakika ya nne na Mridi Tangai dakika ya 4 na sasa watahitaji kuulinda ushindi wao kwenye mchezo wa marudiano Jumapili Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ili kupanda Ligi Kuu. Mbeya Cty walitangulia kwa bao la Suleiman Ibrahim dakika ya 41, kabla ya wenyeji, Geita Gold kusawazisha dakika ya 68 kwa bao la kujifunga la Rehani Kibingu. Nayo Mbeya Cty imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Geita Gold Uwanja wa sekondari ya Nyankungu katika mchezo mwingine wa mchezo (Play-Offs) leo. Mbeya City watahitaji kushinda nyumbani Jumapili Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kwenye mchezo wa marudiano ili kubaki Ligi Kuu. Mbeya City na Mbao FC zilimaliza nafasi ya 15 na 16 katika Ligi Kuu, hivyo kul

BENJAMIN WILLIAM MKAPA NAJUA UMEENDA, ILA ACHA NISEME!

Image
Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM Dunia ni mahali ambapo tunaletwa ili tuishi.Maisha yetu yananzia kwa wazazi wetu na walezi wetu na kisha tunahamia kwenye jamaa na jamii zetu. Huko ndipo hukutana na mengi hukutana na wengine na ndipo urafiki na uadui pia hupatikana,ndipo tunaifahamu Dunia kwa uzuri na ubaya wake. Nilikukuta huku kwa jamii nilikuona na kujifunza mengi kupitia kwako nilipata majibu ya maswali yangu hata kabla ya kukuuliza kwani kila ulilosema juu ya maisha na wanadamu lilikuwa linajibu moja ya maswali yangu ya muda mrefu. Kuna wakati sio tu pesa na mali zinaweza kukufanya upate amani ya akili,mwili na roho bali hata maneno yenye busara na tumaini yanaweza kukupeleka mbali katika tumaini na tulizo la moyo. Leo umeondoka nikiwa bado kijana lakini wewe katika umri wako wa uzee umri ambao hata kibiblia ni zawadi pia kwa maana umeenda katika ile ziada ni jambo la bahati na jema ila bado hainifanyi nisiumie na kuhuzunika juu yako baba. Yapo mengi ulisema na kuyaandik

CLATOUS CHAMA NA FEISAL SALUM WA YANGA SC WASHINDA TUZO YA MACHEZAJI BORA WA MSIMU SPORTPESA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM VIUNGO, Mzambia Clatous Chama wa Simba SC na Feisal Salum wa Yanga SC wameshinda tuzo za Machezaji Bora wa Msimu wa klabu zao baada ya zoezi la upigaji kura kwa mashabiki lililoendeshwa na kampuni hiyo. Taarifa ya SportsPesa kupitia ukurasa wake wa Instagram leo imesema;  “Hongereni sana Clatous Chama kuwa SportPesa Mchezaji Bora wa Msimu kutoka Simba na Fei Toto kuwa SportPesa Mchezaji Bora wa msimu kutoka Yanga. Kura nyingi ndio ziliamua ushindi huu kwa pande zote mbili.  Lakini taarifa hiyo haikusema wawili hao watapewa zawadi gani kwa ushindi wao huo zaidi ya kumaliza kwa kusema; “Hii ni Zawadi toka kwa Mdhamini Mkuu wa Vilabu vyote viwili,”. Wakati Chama ameisaidia Simba SC kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mzanzibari Feisal Salum ameiwezesha Yanga SC kumaliza katika nafasi ya pili.

RAIS DK. MAGUFULI AUBADILI JINA UWANJA WA TAIFA, SASA KUITWA UWANJA WA MKAPA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli ameubadili jina Uwanja wa Taifa na sasa utakuwa unajulikana kama Uwanja wa Mkapa ili kumuenzi Rais mstaafu wa Serikali ya awamu ya tatu nchini, marehemu Dk. Benjamin William Mkapa. Mkapa aliyefariki dunia Julai 24 Jijini Dar es Salaam ndiye aliyefanikisha ujenzi wa Uwanja huo wa kisasa wa michezo nchini. Akizungumza wakati wa zoezi la kuuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mkapa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo, Rais Dk. Magufuli amesema kwamba Watanzania hawatamsahau Rais huyo mstaafu wa awamu ya tatu kwa kuwaachia Uwanja huo. Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli ameubadili jina Uwanja wa Taifa na sasa utakuwa unajulikana kama Uwanja wa Mkapa aliyefariki dunia Julai 24 Jijini Dar es Salaam  “Najua Watanzania hawatamsahau Mzee Mkapa kwa kuwajengea Uwanja mkubwa wa michezo tunaouona mbele yetu. Kwa sasa wengi wanataka Uwanja ule uitwe Uwanja wa Mkapa au Mkapa

LUC EYMAEL AFUKUZWA KAZI YANGA SC KWA KUWATOLEA ‘MANENO MACHAFU’ MASHABIKI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA Mbelgiji, Luc Eymael amefukuzwa kazi Yanga SC baada ya miezi saba tu kazini kutokana na kutoa kauli zilizotafsiriwa kama za kibaguzi dhidi ya mashabiki. Taarifa ya Yanga kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba kutokana na kauli hizo za kibaguzi uongozi umeamua kumfuta kazi Eymael kuanzia leo (Julai 27, 2020) na kuhakikisha anaondoka nchini haraka iwezekanavyo. “Uongozi wa klabu ya Yanga umesikitishwa na kauli zisizo za kiungwana na za kibaguzi zilizotolewa na Kocha wake Luc Eymael na kusambaa katika mitandao ya kijamii,”imesema taarifa ya Yanga na kuongeza;. “Baadhi ya kauli hizo za Kocha Luc Eymael amesikika akitoa kauli za kuwashutumu Mashabiki kwamba hawana elimu, watu kwenye nchi hii ni wapumbavu, mashabiki hawajui mpira kazi yao ni kupiga kelele kama nyani na bata, Viongozi wa Klabu ni sifuri na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania lipo kwa ajili ya Simba tu,”. Aidha, Uongozi wa Yanga umewaomba radhi viongozi wa nchi, Uongozi wa Shirik

JUVENTUS MABINGWA SERIE A KWA MARA YA TISA MFULULIZO

Image
Cristiano Ronaldo (wa pili kushoto) akipongezwa na makocha baada ya mechi dhidi ya Sampdoria, ambayo Juventus walishinda 2-0 usiku wa jana Uwanja wa Allianz Jijin0 Torino na kutwaa taji la Serie A kwa mara pili mfululizo tangu Mreno huyo ajiunge na timu hiyo na la tisa mfululizo kwao. Mabao ya Juventus yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 45 na ushei na  Federico Bernardeschi dakika ya 67 na kwa ushindi huo, Juventus inafikisha pointi 83 kuelekea mechi mbili za mwisho ikiizidi pointi saba Inter Milan inayoafuatia   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

VARDY AWAPIKU AUBAMEYANG, INGS KIATU CHA DHAHABU ENGLAND

Image
Mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy ameshnda tuzo ya Katu cha Dhahabu cha Ligi Kuu ya England baada ya kumaliza msimu na mabao 23, mbele ya Pierre-Emerick Aubameyang, Danny Ings waliomaliza na mabao 22 kila mmoja, Raheem Sterling wa Manchester City 20, Mohamed Salah wa Liverpool 19, Harry Kane wa Tottenham Hotspur 18, Sadio Mane wa Liverpool 18, Raúl Jiménez wa Wolverhampton Wanderers, Anthony Martial na Marcus Rashford wa Manchester United 17 kila mmoja  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

LIVERPOOL YAMALIZA NA USHINDI WA 3-1 DHIDI YA NEWCASTLE UNITED

Image
Mshambuliaji Msenegal, Sadio Mane akishangilia baada ya kuifungia Liverpool bao la tatu dakika ya 89 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa St. James' Park. Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na beki Mholanzi Virgil van Dijk dakika ya 38 na mshambuliaji Mbelgiji Divock Origi dakika ya 59 na kwa ushindi huo mabingwa hao wanamaliza na pointi 99 wakiwazidi pointi 18 Manchester City waliomaliza nafasi ya pili   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MAN CITY YAISINDIKIZA NORWICH CITY CHAMPIONSHIP NA 5-0

Image
Kevin de Bruyne akishangilia na David Silva (kushoto) baada ya kuifungia Manchester City mabao mawili dakika ya 45 na 90 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Norwich City ambao tayari wameshuka daraja kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad. Mabao mengine ya Manchester City yamefungwa na Gabriel Jesus dakika ya 11, Raheem Sterling dakika ya 79 na Riyad Mahrez dakika ya 83 na kwa ushindi huo, timu ya Pep Guardiola inamaliza na pointi 81 katika nafasi ya pili, ikizidiwa pointi 18 na mabingwa, Liverpool   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

ARSENAL YAISHUSHA DARAJA WATFORD BAADA YA KUICHAPA 3-2

Image
Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia Arsenal  mabao mawili   dakika ya tano kwa penalti kufuatia Craig Dawson kumuangusha Alexandre Lacazette na dakika ya 33 akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la pili, Kieran Tierney dakika ya 24 katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Watford kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates. Mabao ya Watford yamefungwa na  Troy Deeney  dakika ya  43  na Danny Welbeck  dakika ya 66 na matokeo hayo wanashuka daraja baada ya kumaliza na pointi 34 katika nafasi ya 19 wakiungana na AFC Bournemouth na  Norwich City kuteremka. Arsenal inamaliza nafasi ya nane na pointi zake 56, ikizidiwa tatu na zote,  Tottenham Hotspur iliyomaliza ya sita na  Wolverhampton ya saba   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

CHELSEA YAFUZU LIGI YA MABNGWA BAADA YA KUICHAPA WOLVERHAMPTON 2-0

Image
Kinda wa England, Mason Mount akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Chelsea kabla ya Olivier Giroud kufunga la pili, yote katika dakika za nyongeza kipindi cha kwanza The Blues wakiichapa 2-0 Wolverhampton Wanderers kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijin London. Chelsea inafikisha pointi 66 na kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Manchester Cty iliyomaliza nafasi ya tatu   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

LIPULI FC 0-1 YANGA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

MAN UNTED YAIPIGA LEICESTER CITY 2-0 KING POWER NA KUFUZU LIGI YA MABINGWA

Image
Wachezaji wa Manchester United wakipongezana baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Leicester City leo kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power, mabao ya Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya 71 na Jesse Lingard dakika ya 90 hivyo kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msmu ujao.  Kwa ushindi huo, Manchester United imefikisha pointi 66 na kumaliza nafas ya tatu ikiwazidi wastani wa mabao tu Chelsea na ikizidiwa pointi 15 na mahasimu wao wa Jiji, Manchester City waliomaliza nafasi ya pili nyuma ya mabingwa, Liverpool wenye pointi 99, wakati Leicester City inabaki na pointi zake 62, hivyo kumaliza nafasi ya tano, nyuma ya Chelsea yenye pointi 66   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SAMATTA AINUSURU ASTON VILLA KUSHUKA DARAJA BAADA YA SARE YA 1-1 NA WEST HAM UNITED

Image
Na Mwandishi Wetu, LONDON MSHAMBULIAJI wa kimatiafa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amekuwa sehemu ya kikosi cha Aston Villa kilichoinusuru timu hiyo kushuka daraja baada ya sare ya 1-1 na wenyeji, West Ham United Uwanja wa London. Samatta alicheza kwa dakika 68 mchezo huo wa Ligi Kuu ya England kabla ya kumpisha chipukizi wa England, Keinan Davis wakati huo timu hizo hazijafungana. Nyota wa England, Jack Grealish alianza kuifungia Aston Villa dakika ya 84 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake, Mscotland John McGinn bao lililodhaniwa litakuwa la ushindi. Mbwana Samatta amekuwa sehemu ya kikosi cha Aston Villa kilichoinusuru timu yao kushuka daraja leo   PICHA ZAIDI GONGA HAPA Lakini mshambuliaji wa kimataifa wa Ukraine Andriy Yarmolenko akaisawazishia West Ham United dakika ya 85 akimalizia pasi ya kiungo wa England, Declan Rice.   Kwa matokeo hayo, Aston Villa inakamilisha msimu wa Ligi Kuu ya England na pointi 35, ikizizidi pointi moja moja AFC Bournemouth na Watford zilizoungan

YANGA SC YAICHAPA LIPULI FC 1-0 SAMORA NA KUMALIZA KATIKA NAFASI YA PILI LIGI KUU TZ BARA7

Image
Na Mwandishi Wetu, IRINGA VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli FC jioni ya leo Uwanja wa Samora mjini Iringa. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji David Molinga Ndama ‘Falcao’ dakika ya 38 na kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 72, ikizidiwa pointi 16 na mabingwa, Simba SC na wakiwazidi pointi mbili Azam FC waliomaliza nafasi ya tatu.  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Nassor Mwinchui wa Pwani aliyesaidiwa na Charles Simon wa Dodoma na Anold Bugado wa Tanga, Molinga aliyesajiliwa Agosti mwaka jana kutoka kwao, Kongo alifunga bao hilo akimalizia pasi ya mkongwe, Mrisho Khalfan Ngassa kutoka upande wa kulia. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Simba SC imeshinda 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Mabao ya Simba SC yamefungwa yote leo yamefungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco dakika ya pili na

KAPTENI BOCCO APIGA ZOTE MBILI SIMBA SC YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 UWANJA WA USHIRIKA

Image
Na Mwandishi Wetu, MOSHI MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wamemaliza kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi katika mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Saanya wa Morogoro aliyesaidiwa na Makame Mdogo na Joseph Pombe wa Shinyanga, mabao ya Simba SC yamefungwa yote leo yamefungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco dakika ya pili na 45 na ushei, wakati la Polisi limefungwa na Marcel Kaheza dakika ya 30. Kwa matokeo hayo, Simba SC iliyobeba taji la Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu na mara ya 21 jumla, inamaliza na pointi 88, ikifuatiwa na watani wao wa jadi, Yanga SC waliomaliza na pointi 72, wakati Azam FC imemaliza na pointi 70 nafasi ya tatu. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Yanga SC wameshinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli FC bao pekee la David Molinga dakika ya 38 Uwanja wa Samora mjini Iringa. Tanzania Prisons imelazimishwa sare ya 2-2 na Azam FC Uwanja wa Sokoine mjini Mb

ALLIANCE FC, NDANDA SC, LIPULI FC ZAUNGANA NA SINGIDA UNITED KUSHUKA DARAJA LIGI KUU

Image
Na Mwandishi Wetu, MWANZA TIMU za Alliance FC ya Mwanza, Ndanda SC ya Mtwara na Lipuli FC ya Iringa zimeungana na Singida United kushuka daraja baada ya mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo. Alliance FC imeshuka licha ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.  Mabao ya Alliance FC yamefungwa na Martin Kiggi dakika ya kwanza, Israel Patrick dakika ya 25 na Juma Nyangi dakika ya 65, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Bigirimana Blaise dakika ya nane na Frank Mkumbo dakika ya 61. Ndanda SC yenyewe imechapwa 2-0 na Mbao FC, mabao ya Jordan John dakika ya 66 na Waziri Junior dakika ya 18 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, wakati Lipuli imechapwa 1-0 na Yanga SC, bao pekee la David Molinga dakika ya 38 Uwanja wa Samora mjini Iringa. Alliance FC ya Mwanza imeungana na  Ndanda SC ya Mtwara, Lipuli FC ya Iringa na  Singida United kushuka daraja   Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Simba SC imeshinda 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika

PSG WATWAA KOMBE LA UFARANSA BAADA YA KUIPIGA AS SAINT-ETIENNE 1-0

Image
Wachezaji wa Paris Saint-Germain wakishangilia na Kombe la Ufaransa baada ya kukabidhiwa usiku wa jana kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Saint-Etienne bao pekee la Neymar da Silva Santos Junior dakika ya 14 katika mchezo wa fainali Uwanja wa Stade de France Jijini Paris   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

RAIS MKAPA ALIYEWAPA WATANZANIA ZAWADI YA UWANJA WA KISASA WA MICHEZO AFARIKI DUNIA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM RAIS mstaafu wa Serikali ya awamu ya tatu nchini, Benjamin William Mkapa aliyefanikisha ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa michezo Tanzania (Uwanja wa Taifa) uliopo Dar es Salaam amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Taarifa ya kifo cha Mzee Mkapa imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli usiku wa kuamkia leo kupitia Televisheni ya Taifa, TBC. Rais Magufuli amesema kwamba kiongozi huyo wa zamani wa taifa amefariki katika hospitali moja jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu. “Mzee Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya tatu amefariki. Amefariki kwenye hospitali mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa. Niwaombe watanzania tulipokee hili. Taifa limepata msiba mkubwa. Tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele ya haki," amesema Rais Magufuli. Katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Twitter rais Magufuli amemuomboleza Mkapa na kusema atamkumbuka "kwa ma