LUC EYMAEL AFUKUZWA KAZI YANGA SC KWA KUWATOLEA ‘MANENO MACHAFU’ MASHABIKI
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mbelgiji, Luc Eymael amefukuzwa kazi Yanga SC baada ya miezi saba tu kazini kutokana na kutoa kauli zilizotafsiriwa kama za kibaguzi dhidi ya mashabiki.
Taarifa ya Yanga kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba kutokana na kauli hizo za kibaguzi uongozi umeamua kumfuta kazi Eymael kuanzia leo (Julai 27, 2020) na kuhakikisha anaondoka nchini haraka iwezekanavyo.
“Uongozi wa klabu ya Yanga umesikitishwa na kauli zisizo za kiungwana na za kibaguzi zilizotolewa na Kocha wake Luc Eymael na kusambaa katika mitandao ya kijamii,”imesema taarifa ya Yanga na kuongeza;.
“Baadhi ya kauli hizo za Kocha Luc Eymael amesikika akitoa kauli za kuwashutumu Mashabiki kwamba hawana elimu, watu kwenye nchi hii ni wapumbavu, mashabiki hawajui mpira kazi yao ni kupiga kelele kama nyani na bata, Viongozi wa Klabu ni sifuri na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania lipo kwa ajili ya Simba tu,”.
Aidha, Uongozi wa Yanga umewaomba radhi viongozi wa nchi, Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Viongozi wa Klabu ya Simba, wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga, pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na kauli za kuudhi na kudhalilisha zilizotolewa na kocha huyo.
“Klabu ya Yanga inathamini na kuamini katika misingi ya nidhamu na utu, na inapingana na aina yoyote ya Ubaguzi,”imeongeza taarifa hiyo iliyosainiwa na kaimu Katibu Mkuu wa klabu, Wakili Simon Patrick.
Eymael anaondoka Yanga SC baada ya kuiongoza timu katika mechi 32 tangu ajiunge nayo Januari ikishinda 16, sare 11 na kufungwa tano.
Anaondolewa siku moja baada ya kuisaidia Yanga SC kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli FC jana Uwanja wa Samora mjini Iringa, bao pekee, David Molinga Ndama ‘Falcao’ dakika ya 38 .
Kwa ushindi huo, Yanga SC imefikisha pointi 72 na kumaliza ikizidiwa pointi 16 na mabingwa, Simba SC na wakiwazidi pointi mbili Azam FC waliomaliza nafasi ya tatu.
REKODI YA LUC EYMAEL YANGA SC
1 Yanga SC 0-3 Kagera Sugar (Ligi Kuu Uhuru)
2 Yanga SC 0-1 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
3 Yanga SC 3-1 Singida United (Ligi Kuu Singida)
4 Yanga SC 2-0 Tanzania Prisons (Kombe la TFF Taifa)
5 Yanga SC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Taifa)
6 Yanga SC 2-1 Lipuli FC (Ligi Kuu Taifa)
7 Yanga SC 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Taifa)
8 Yanga SC 1-1 Mbeya Cty (Ligi Kuu Taifa)
9 Yanga SC 0-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Taifa)
10 Yanga SC 1-1 Polisi Tanzania (Ligi Kuu Moshi)
11 Yanga SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Tanga)
12 Yanga SC 1-0 Gwambina FC (Kombe la TFF Taifa)
13 Yanga SC 2-0 Alliance FC (Ligi Kuu Taifa)
14 Yanga SC 2-0 Mbao FC (Ligi Kuu Taifa)
15 Yanga SC 1-0 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
16 Yanga SC 0-1 KMC (Ligi Kuu Taifa)
17 Yanga SC 1-1 Namungo FC (Ligi Kuu Ruangwa)
18 Yanga SC 3-1 Transit Camp (Alikuwa kwao, kirafiki Dar)
19 Yanga SC 0-3 KMC (Alikuwa kwao, kirafiki Uhuru)
20 Yanga SC 1-0 Mwadui FC (Ligi Kuu Kambarage)
21 Yanga SC 1-1 JKT Tanzania (Ligi Kuu Dodoma)
22 Yanga SC 0-0 Azam FC (Ligi Kuu Tafia)
23 Yanga SC 2-2 Namungo FC (Ligi Kuu Taifa)
24 Yanga SC 3-2 Namungo FC (Ligi Kuu Taifa)
25 Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Kombe la TFF Taifa)
26 Yanga SC 0-0 Biashara United (Ligi Kuu Musoma)
27 Yanga SC 1-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Kaitaba)
28 Yanga SC 1-4 Simba SC (Kombe la TFF Taifa)
29 Yanga SC 3-1 Singida United (Ligi Kuu Taifa)
30 Yanga SC 1-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Taifa)
31 Yanga SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Taifa)
32 Yanga SC 1-0 Lipuli FC (Ligi Kuu Samora)

Comments
Post a Comment