Posts

Showing posts from October, 2019

SIMBA SC WAHAMISHIA HASIRA ZOTE KWA MBEYA CITY BAADA YA KUPIGWA NA MWADUI

Image
Kocha Mkuu wa Simba SC, Mbelgiji Patrick Aussems akielekea kwenye gari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutoka Mwanza walipounganisha usafiri wa anga wakitokea Shinyanga kwa usafari wa basi ambako Jumatano walifungwa 1-0 na Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara    Wachezaji Ibrahim Ajibu (kushoto) na Haruna Shamte (kulia) baada ya kuwasili Dar es Salaam kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City Jumapili Uwanja wa Uhuru Miraj Athumani 'Madenge' mbele akifuatiwa na kipa Beno Kakolanya  Kiungo Francis Kahata baada ya kuwasili Dar es Salaam tayari kwa mchezo na Mbeya City Jumapili

YANGA SC YAWAFUATA PYRAMIDS FC KIKAMILIFU KUJARIBU KUPINDUA MEZA CAIRO JUMAPILI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KIKOSI cha Yanga SC kimeondoka leo jioni mjini Dar es Salaam kwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano, mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Pyramids FC Jumapili wiki hii Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo. Yanga SC inatakiwa kushinda 2-0 ugenini au kushinda kwa tofauti ya bao moja kuanzia 3-2 kwenye mchezo huo utakaoanza Saa 4:00 usiku, kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Huo ulikuwa mwendelezo wa rekodi ya Yanga kutoshinda nyumbani mechi za michuano ya Afrika kuanzia Ligi ya Mabingwa ambako ushindi wa ugenini wa 1-0 uliwavusha Raundi ya pili baada ye sare ya 1-1 nyumbani na Township Rollers kabla ya kwenda kutolewa na Zesco United kufuatia kufungwa 2-1 Ndola ikitoka kutoka sare ya 1-1 Dar es Salaam. Na pamoja na kuuhamishia Mwanza mchezo wake na Pyramids FC kwa imani ya kupata ushindi, lakini mambo yalikuwa magum

MBAO FC CHUPUCHUPU KUPIGWA TENA KIRUMBA, YACHOMOA KWA PENALTI DAKIKA YA MWISHO

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM BAO la penalti dakika ya 90 na ushei limeinusuru Mbao FC kuchapwa tena nyumbani, baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Tanzania Prisons ilitangulia kwa bao la Samsom  Mbangula dakika ya 16 akimalizia krosi ya beki Salum Kimenya. Refa Abel William kutoka Arusha aliyekuwa anasaidiwa na Josephat Pombe wa Shinyanga na Nestory Lvagala wa Tabora akawapa penalti Mbao FC dakika ya 90 na ushei na mshambuliaji Waziri Junior akawasawazishia wenyeji. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo imechezwa mjini Mwanza pia na Alliance FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Mbeya City Uwanja wa Nyamagan. Lakini Alliance ililazimika kucheza pungufu kuanzia dakika ya 72 kufuatia mchezaji wake, John Mwanda kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Iddi Gamba.

SAMATTA AFUNGA BAO MUHIMU KRC GENK YATOKA NYUMA NA KUPATA SARE YA 2-2 NYUMBANI

Image
Na Mwandishi Wetu, GENK MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga bao la kwanza la kusawazisha, timu yake, KRC Genk ikitoka nyuma kwa 2-0 na kipata sare ya 2-2 na wageni, Royal Antwerp FC katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk. Samatta alifunga bao hilo dakika ya 69 akimalizia pasi ya kiungo Mbelgiji, Bryan Heynen kabla ya kiungo Mnorway, Sander Berge kuisawazishia Genk dakika ya 90 na ushei. Na hiyo ilifuatia Royal Antwerp FC kutangulia kwa mabao ya mshambuliaji Mcameroon, Didier Lamkel Ze dakika ya nane akimalizia pasi ya beki Muangola, Aurelio Buta na mshambuliaji Mreno, Ivo Rodrigues dakika ya 47 akimalizia pasi ya kiungo Mbelgiji, Alexis De Sart. Kwa sare hiyo, Genk inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 12 wakiwa wanazidiwa pointi moja na Antwerp inayolingana na Sporting Charleroi na AA Gent. Club Brugge inaendelea kuongoza Ligi Daraja la A Ubelgiji kwa pointi zake 30 za mechi 12, ikifuatiwa na Sta

RONALDO AFUNGIA DAKIKA YA MWISHO JUVE YAICHAPA GENOA 2-1

Image
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Juventus kwa penalti dakika ya 90 na ushei baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Antonio Sanabria kwenye boksi katika ushindi wa 2-1 dhidi ya 2-1 kwenye mchezo wa Serie A usiku wa jana Uwanja wa Allianz mjini Torino. Juventus walitangulia kwa bao la Leonardo Bonucci dakika ya 36, kabla ya Christian Kouame kuisawazishia Genoa dakika ya 40   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

RODRYGO AFUNGA REAL MADRID YAICHAPA LEGANES 5-0 LA LIGA

Image
Kinda Mbrazil, Rodrygo Silva de Goes aliyeoandishwa kutoka timu B akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya saba katika ushindi 5-0 dhidi ya Leganes kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabéu. Mabao mengine ya Real yalifungwa na T. Kroos dakika ya nane, Nahodha Sergio Ramos kwa penalti dakika ya 24, mkongwe Karim Benzema kwa penalti pia dakika ya 69 na Luka Jovic dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo kikosi cha kocha Zinadine Zidane kinafikisha pointi 21 katika mchezo wa 10, sasa kikizidiwa pointi moja na vinara, Barcelona amabo pia ni mabingwa watetezi   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

RASHFORD AIPELEKA MANCHESTER UNITED ROBO FAINALI CARABAO

Image
Marcus Rashford akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la ushindi Manchester United dakika ya 73 ikiwalaza wenyeji, Chelsea 2-1 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge mjini London. Rashford pia ndiye aliyefunga bao la kwanza la Man United dakika ya 25 kwa penalti, baada ya Daniel James kuchezewa rafu na Marcos Alonso, lakini Michy Batshuayi akaisawazishia Chelsea dakika ya 61   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

LIVERPOOL YAING'OA ARSENAL KWA MATUTA CARABAO BAADA YA SARE YA 5-5

Image
Curtis Jones akipongezwa na wenzake baada ya kufunga penalti ya ushindi Liverpool ikiichapa Arsenal kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 5-5 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao usiku wa jana Uwanja wa Anfield. Mabao ya Liverpool yalifungwa na Shkodran Mustafi aliyejifunga dakika ya sita, James Milner kwa penalti dakika ya 43, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 58 na Divock Origi dakika ya 62 na 90 na ushei, wakati ya Arsenal yalifungwa na Lucas Torreira dakika ya 19, Gabriel Martinelli dakika ya 26 na 36, Ainsley Maitland-Niles dakika ya 54 na Joe Willock dakika ya 70. Penalti za Liverpool zilifungwa na Milner, Adam Lallana, Rhian Brewster, Origi na Curtis Jones, wakati za Arsenal zilifungwa na Héctor Bellerin, Mattéo Guendouzi, Martinelli na Maitland-Niles huku , Dani Ceballos pekeea akikosa   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SIMBA SC YAPUNGUZWA KAZI SHINYANGA, YACHAPWA 1-0 NA MWADUI FC KAMBARAGE

Image

AZAM FC MAZOEZINI KUJIANDAA NA MCHEZO UJAO WA LIGI KUU DHIDI YA KAGERA SUGAR CHAMAZI

Image
Mshambuliaji Mrundi wa Azam FC, Suleiman Ndikumana akiwa mazoezini jana kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Jumatatu ijayo hapo hapo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam   Kiungo wa Azam FC, Frank Domayo akiwa mazoezini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Jumatatu ijayo Mshambuliaji wa Azam FC, Frank Domayo akiwa mazoezini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Jumatatu ijayo  Beki Mganda wa Azam FC, Nico Wadada akiwa mazoezini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Jumatatu ijayo

MESSI APIGA MBILI BARCELONA YAICHAPA REAL VALLADOLID 5-1

Image
Lionel Messi akishangilia baada ya kufunga mabao mawili dakika za 34 na 75 katika ushindi wa 5-1 wa Barcelona dhidi ya Real Valladolid usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Mabao mengine ya Barca yalifungwa na Clement Lenglet dakika ya pili, Arturo Vidal dakika ya 29 na Luis Suarez dakika ya 77, wakati la Real lilifungwa na Kiko Olivas dakika ya 15   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

AGUERO APIGA MBILI MANCHESTER CITY YAICHAPA SOUTHAMPTON 3-1

Image
Sergio Aguero na Nicolas Otamendi (kulia) wakipongezana baada ya wote kufunga katika ushindi wa 3-1 wa Manchester City dhidi ya Southampton kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi England usiku wa jana Uwanja wa Etihad. Aguero aliyefikisha mechi 350 Manchester City jana, alifunga mabao yake dakika ya 38 na 56 baada ya Otamendi kufunga la kwanza dakika ya 20 kabla ya Jack Stephens kuifungia Southampton la kufutia machozi dakika ya 75  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

AISHI KUDAKA MECHI YA 100 LEO TANGU ASAJILIWE SIMBA JUNI 2017

Image
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM LIGI Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi saba kuchezwa kwenye viwanja tofauti, ingawa macho na masikio ya wengi yataelekezwa Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga. Huko, mabingwa watetezi na timu bora kwa sasa nchini, Simba SC watakuwa wanamenyana na wenyeji, Mwadui FC kuanzia Saa 10:00 jioni. Na hapana shaka, kocha Mbelgiji Patrick Aussems ataendelea kumuamini mlinda mlango wake namba moja, Aishi Salum Manula kuwa kumuanzisha.  Aishi Manula anatarawa kusimama kwenye lango la Simba kwa mara ya 100 leo Na kama ataanzishwa leo, Aishi atakuwa anasimama kwenye lango la Simba kwa mara ya 100 tangu asajiliwa kutoka timu iliyomuibua na kumkuza kisoka, Azam FC Juni mwaka 2017. Hapana shaka mechi 100 ndani ya miaka miwili ni kielelezo tosha cha namna Aishi, ambaye pia ni kipa bora wa Ligi Kuu mara tatu mfululizo anavyotumika Simba SC akiwa chachu ya mafanikio ya timu katika misimu hii miwili. Mbele na nyuma, kushoto na kulia ni A

AISHI MANULA ALIVYOPATA MAPOKEZI MAZURI SIMBA SC ILIPOWASILI SHINYANGA KUIVAA MWADUI FC KESHO

Image
Mashabiki wa Simba SC wakimpiga picha kwa furaha kipa Aishi Manula baada ya kikosi cha timu hiyo kuwasili Shinyanga jana kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mwadui FC kesho Uwanja wa Kambarage

EBITOKE AFURAHISHWA NA MAHUSIANO MAZURI YA KIMTANDAO BAINA YA TANZANIA NA CHINA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MSANII wa vichekesho hapa nchini Anastazia Exavery maarufu kwa jina la 'Ebitoke', amekoshwa na mahusiano mazuri ya kimtandao baina ya Tanzania na China. Ebitoke ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa pande hizo mbili Tanzania na China na yeye akiwa mmoja wa wageni wenye ushuhuda wa mitandao ya kijamii. Msanii huyo alisema, anaimani muunganiko huu wa nchi zote mbili utakuwa ni tija kubwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.  "Mitandao ya kijamii ni kitu kikubwa sana kwani Mimi ni shahidi mkubwa sana katika hilo, kwani nimepata umaarufu mkubwa kupitia mitandao hiyo ya kijamii mpaka sasa nina wafuasi zaidi ya mil 2 naenda mil 3,"amesema. Mkutano huo ulioandaliwa na startimes umekuwa na manufaa makubwa kwa washiriki kwani wengi wao walikiri mitandao hiyo ya jamii ni moja ya sehemu za kumuinua mtu kwa namna moja ama nyingine. Nae Zhau Hui kutoka China alisema, wao wamefarijika sana na kufurahi kuendeleza muung

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA INNOCENT HAULE

Image

MBEYA CITY YAZINDUKA NA KUICHAPA MBAO FC 2-1 KIRUMBA, ALLIANCE 1-1 PRISONS NYAMAGANA

Image
Na Asha Said, MWANZA TIMU ya Mbeya City imezinduka na kupata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Martin Saanya wa Morogoro aliyesaidiwa na Sunday Kamba Abdulaziz Ally wote wa Arusha, Mbao FC ilipata pigo dakika ya kwanza tu baada ya kuanza kipindi cha pili, kufuatia mchezaji wake, Babilas Chitembe kumchezea rafu Baraka Ngusa kwenye boski. Rafu hiyo ilisababisha na penalti iliyowapa bao la kuongoza Mbeya City, lililofungwa na nyota wake, Peter Mapunda dakika ya 48. Mshambuliaji Said Khamis Junior akapoteza nafasi ya kuisawazishia Mbao FC baada ya mkwaju wake wa penalti kuokolewa na kipa Haroun Mandanda dakika ya 88 kufuatia Datus Peter kuchezewa rafu na beki wa Mbeya City, Hassan Mwasapili. Mshambuliaji Emmanuel Charles Lukinda akaisawazishia Mbao FC dakika ya 90 na wakati mashabiki wa timu hiyo hawajamaliza kushangilia, Peter Mapunda akaifungia Mbeya City bao la ushindi kwa shuti la mpi

YANGA SC 1-2 PYRAMIDS FC (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)

Image

REFA AKATAA BAO LA ARSENAL YATOA SARE 2-2 NA CRYSTAL PALACE

Image
Beki Mgiriki wa Arsenal, Sokratis Papastathopoulos akilalamika baada ya kukataliwa bao lake dakika za mwishoni kufuatia refa Martin Atkinson kutazama marudio ya picha za video (VAR) wakitoa sare ya 2-2 na Crystal Palace kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Papastathopoulos dakika ya saba na beki mwingine, Mbrazil David Luiz dakika ya tisa, wakati ya Crystal Palace yamefungwa na Luka Milivojevic kwa penalti dakika ya 32 na Jordan Ayew dakika ya 52   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MAN UNITED WAKOSA PENALTI MBILI, WASHINDA 3-1 UGENINI

Image
Wachezaji wa Manchester United wakipongezana kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Norwich City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Carrow Road, mabao ya Scott McTominay dakika ya 21, Marcus Rashford dakika ya 30 na Anthony Martial dakika ya 73 dhidi ya moja la Onel Hernandez dakika ya 88. Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kingeondoka na ushindi mkubwa zaidi kama si Rashford na Martial kukosa penalti 29 na 44   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

LIVERPOOL YAICHAPA SPURS 2-1 ANFIELD, SASA YAIZIDI POINTI SITA MAN CITY

Image
Mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah akimrukia Nahodha wake, kiungo Jordan Henderson kushangilia naye baada ya wote kufunga katika ushindi wa 2-1 wa Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield.  Henderson alifunga la kwanza dakika ya 52 na Sakah la pili kwa penalti dakika ya 75, wakati bao pekee la Spurs limefungwa na Harry Kane sekunde ya 40 na kwa ushindi huo Liverpool imefikisha pointi 28 katika mchezo wa 10 sasa ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Manchester City   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SIMBA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, AZAM FC YAPIGWA 1-0 NA RUVU MLANDIZI

Image
Na Mwandishi Wetu, ARUSHA SIMBA SC imeendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Miraj Athumani ‘Madenge’ au Sheva dakika ya 39 akimalizia pasi ya kiungo Muzamil Yassin. Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems inafikisha pointi 18 katika mchezo wa sita ikiendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100. Hali ni mbaya kwa Singida United ambayo leo imepoteza mechi ya tano kati ya nane, nyingine tatu zote ikitoa droo, hivyo kuendelea kushika mkia.  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC bao pekee la Moses Shaaban dakika ya 68 akimalizia pasi ya Abdurahman Mussa dakika ya 27. Nayo Biashara United ikaichapa 1-0 Namungo FC, bao pekee la Juma Mpakala dakika ya 72 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. Coastal Union wakaib

YANGA SC YACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AFRIKA, YACHAPWA 2-1 NA PYRAMIDS FC MWANZA

Image
Na Mwandishi Wetu, MWANZA YANGA SC imejiweka kwenye mazingira magumu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania nafasi hiyo jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Yanga sasa wanaendeleza rekodi yao ya kutoshinda mechi za nyumbani za michuano ya Afrika kuanzia Ligi ya Mabingwa ambako ushindi wa ugenini wa 1-0 uliwavusha Raundi ya pili baada ye sare ya 1-1 nyumbani na Township Rollers kabla ya kwenda kutolewa na Zesco United kufuatia kufungwa 2-1 Ndola ikitoka kutoka sare ya 1-1 Dar es Salaam. Na pamoja na kuuhamishia Mwanza mchezo wake wa kwanza mchujo wa kuwania hatua ya makundi, Yanga SC leo imeshindwa kugeuza matokeo, zaidi yamekuwa mabaya kabisa baada ya kufungwa kutoka sare za Dar es Salaam.  Sasa Yanga SC watatakiwa kwenda kujaribu kushinda ugenini kwenye mchezo wa marudiano Novemba 3, mwaka huu Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 mjini Cairo kwa mechi zao za nyumbani. Katika mchezo wa l