MBAO FC CHUPUCHUPU KUPIGWA TENA KIRUMBA, YACHOMOA KWA PENALTI DAKIKA YA MWISHO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BAO la penalti dakika ya 90 na ushei limeinusuru Mbao FC kuchapwa tena nyumbani, baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Tanzania Prisons ilitangulia kwa bao la Samsom  Mbangula dakika ya 16 akimalizia krosi ya beki Salum Kimenya.
Refa Abel William kutoka Arusha aliyekuwa anasaidiwa na Josephat Pombe wa Shinyanga na Nestory Lvagala wa Tabora akawapa penalti Mbao FC dakika ya 90 na ushei na mshambuliaji Waziri Junior akawasawazishia wenyeji.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo imechezwa mjini Mwanza pia na Alliance FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Mbeya City Uwanja wa Nyamagan.
Lakini Alliance ililazimika kucheza pungufu kuanzia dakika ya 72 kufuatia mchezaji wake, John Mwanda kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Iddi Gamba.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA