Posts

Showing posts from June, 2021

MESSI BADO BAO MOJA TU AMFIKIE MAREHEMU MARADONA ARGENTINA

Image
NYOTA wa Barcelona, Lionel Messia juzi amefunga mabao mawili kuiwezesha Argentina kuichapa Bolivia 4-1 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Copa America huko Brazil na kubakiuza bao moja kumfikia gwiji wa Argentina, Diego Maradona. Messi mwenye umri wa miaka 34 sasa, amefikisha mabao 31 katika mechi 148, wakati marehemu Maradona alifunga 32 katika mechi 87, zikiwemo za ushindi wa Kombe la Dunia 1986, wakati Messi bado hajashinda taji na timu yake hiyo ya taifa. Messi pia ameweka rekodi ya mchezaji aliyeichezea mechi nyingi zaidi timu ya taifa ya Argentina, akimpiku beki mstaafu, Javier Mascherano.

KARIA KUGOMBEA URAIS WA TFF BILA MPINZANI BAADA YA WAGOMBEA WENGINE WOTE WAWILI KUENGULIWA KWENYE USAILI

Image
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace John Karia atatetea nafasi yake bila upinzani katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 7 Jijini Tanga. Hiyo ni baada ya wapinzani wake wote wawili waliobaki kuenguliwa katika usaili uliofanyika Juni 25. mwaka huu Dar es Salaam.

ENGLAND YAICHAPA UJERUMANI 2-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI EURO 2020

Image
ENGLAND imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Ujerumani leo Uwanja wa Wembley Jijini London. Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo, Raheem Sterling dakika ya 75 akimalizia pasi ya Luke Shaw na Harry Kane dakika ya 86 akimalizia pasi ya Jack Grealish na sasa Three Lions itakutana na mshindi kati ya Sweden na Ukraine.

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA SABRI RAMADHANI 'CHINA'

Image
 

MBAPPE AKOSA PENALTI YA MWISHO UFARANSA YATUPWA NJE EURO 2020

Image
USWISI imetinga Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya kufungana mabao 3-3 ndani ya dakika 120 usiku huu Uwanja wa Taifa wa Bucharest nchini Romania. Mabao ya Uswis yamefungwa na Haris Seferović dakika ya 15 na 81 na Mario Gavranović dakika ya 90, wakati ya Ufaransa yamefungwa na Karim Benzema dakika ya 57 na 59 na Paul Pogba dakika ya 75. Na katika mikwaju ya penati Mario Gavranović, Fabian Schär, Manuel Akanji, Ruben Martínez na Admir Mehmedi waliifungia Uswisi, wakati Pogba, Olivier Giroud, Marcus Thuram na Presnel Kimpembe walifunga za Ufaransa, kabla ya Kylian Mbappé kukosa ya mwisho iliyopanguliwa na kipa Yann Sommer. Kwa matokeo hayo, Uswisi itakutana na Hispania katika Robo Fainali Ijumaa.

TFF YASEMA MASHABIKI WAPYA 13782 NDIO WATAKAOUZIWA TIKETI KWA AJILI YA PAMBANO LA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI

Image
 SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema tiketi 13782 mpya ndizo zitauzwa kwa ajili ya mchezo wa watani wa jadi Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Hiyo ni kwa sababu sehemu nyingine imetengwa kwa ajili ya mashabiki waliokata tiketi kwa ajili ya mchezo ulioahirishwa Mei 8.

HISPANIA YATINGA ROBO FAINALI EURO 2020 BAADA YA KUIPIGA CROATIA 5-3

Image
HISPANIA imekata tiketi ya Robo Fainali Euro 2020 baada ya ushindi wa 5-3 dhidi ya Croatia leo Uwanja wa Parken Jijini Copenhagen katika mchezo uliodumu kwa dakika 120. Mabao ya Hispania yamefungwa na Pablo Sarabia dakika ya 38, Azpilicueta dakika ya 57, Ferran Torres dakika ya 76, Alvaro Morata dakika ya 100 na Mikel Oyarzabal dakika ya 103, wakati ya Croatia yamefungwa na Pedri Lopez aliyejifunga dakika ya 20, Mislav Oršić dakika ya 85 na Mario Pašalić dakika ya 90 na ushei.

BRAZIL YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA MAKUNDI KWA SARE COPA AMERICA

Image
WENYEJI, Brazil wamekamilisha mechi zao za Kundi B Copa America kwa sare ya 1-1 na Ecuador usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Olímpico Pedro Ludovico Teixeira huko Goiânia, Goiás. Wenyeji walitangulia kwa bao la Éder Militão dakika ya 37 akimalizia pasi ya Éverton, kabla ya Ángel Mena kuisawazishia Ecuador dakika ya 53 akimalizia pasi ya Enner Valencia. Mechi nyingine ya kundi hilo jana, Peru Venezuela 1-0, bao pekee la André Carrillo Uwanja wa Taifa wa Brasília. Brazil imemaliza kileleni mwa Kundi B kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Peru pointi saba, Colombia nne, Ecuador tatu na zote zimetinga Robo Fainali, wakati Venezuela iliyoshika mkia kwa pointi zake mbili imeaga mashindano.

NI RAJA NA JS KABYLIE FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA JULAI 10 BENIN

Image
TIMU ya Raja Athletic imeingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Pyramids FC ya Misri kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 0-0. Baada ya sare nyingine ya 0-0 usiku wa jana Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca kufuatia sare ya wiki iliyopita ya 0-0 pia Jijiji Cairo, Raja wakakata tiketi yao ya fainali kwa matuta na sasa watakutana na JS Kabylie ya Algeria Julai 10A nchini Benin. Kabylie yenyewe imeitoa Cotonsport de Garoua ya Cameroon kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya ushindi wa 3-0 usiku wa jana Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers kufuatia ushindi wa 2-1 wiki iliyopita ugenini.

UBELGIJI YAITUPA NJE URENO NA RONALDO WAO EURO 2020

Image
UBELGIJI wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Ureno usiku huu Uwanja wa Olímpico Jijini Sevilla nchini Hispania. Pongezi kwa mfungaji ww bao hilo pekee, kiungo Thorgan Hazard dakika ya 42 akimalizia pasi ya mchezaji mwenzake wa Borussia Dortmund, beki Thomas Meunier. Sasa Ubelgiji watakutana na Italia Ijumaa baada ya kumfungisha virago Cristiano Ronaldo na wenzake katika Hatua ya 16 Bora tu.

CZECH YAITUPA NJE UHOLANZI EURO 2020, KUKUTANA NA DENMARK ROBO FAINALI

Image
JAMHURI ya Czech imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Uholanzi leo Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest nchini Hungary. Mabao ya Czech yamefungwa na Tomas Holes dakika ya 68 na Patrik Schick dakika ya 80 na kwa ushindi huo itakutana na mshindi kati ya Denmark Jumamosi.

SIMBA SC 1-0 AZAM FC (KOMBE LA TFF)

Image
 

WANACHAMA WA YANGA WAPITISHA MABADILIKO YA KATIBA KUELEKEA MFUMO MPYA WA UENDESHAJI KLABU YAO

Image
WANACHAMA wa klabu ya Yanga kwa kauli moja leo wamepitisha Mabadiliko ya Katiba yatakayowawezesha kufanya marekebisho ya mfumo wa uendeshaji. Wanachama hao wameunga mkono mabadiliko hayo katika Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa DYCC, Chang’ombe Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi. Katika mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya ambaye pia ni mwanachama wa klabu hiyo, alimsifu Mwenyekiti, Dk. Mshindo Mbette Msolla kuiongoza vyema klabu hiyo. Mzee Kikwete pia akaitilia ubani klabu kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya watani Jumamosi kwa kusema; "Yanga ni timu yangu, naipenda sana, inapofungwa naumia inaposhinda nafurahi sana na naamini Jumamosi ijayo tutashinda,". Aidha, Dk Msolla, kocha wa zamani wa timu ya taifa na klabu mbalimbali alitangaza Baraza jipya la Wadhamini wa klabu ambalo litaundwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, U

ITALIA NAYO YATINGA ROBO FAINALI EURO 2020 BAADA YA DAKIKA 120

Image
ITALIA imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Austria katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 usiku huu Uwanja wa Jijini London. Baada ya dakika 90 ngumu, Federico Chiesa aliifungia bao la kwanza Italia dakika ya 95, kabla ya Matteo Pessina kufunga la pili dakika ya 105 na Sasa Kalajdzic akaifungia la kufutia machozi Austria dakika ya 114.

NI AL AHLY NA KAIZER CHIEFS FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
MABINGWA watetezi, Al Ahly wamefanikiwa kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Esperance ya Tunisia usiku huu Uwanja wa WE Al-Ahly Jijiji Cairo nchini Misri. Mabao ya Ahly yamefungwa na Ali Maâloul kwa penalti dakika ya 38, Mohamed Sherif dakika ya 56 na Hussein El Shahat dakika ya 60 na kwa matokeo hayo wanaenda fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza Jumamosi iliyopita Tunisia.  Al Ahly sasa itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Wydad Athletic baada ya sare ya 0-0 leo Johannesburg kufuatia ushindi wa 1-0 Jumamosi iliyopita Morocco.

SIMON MSUVA ACHEZA KIPINDI KIMOJA WYDAD YALAZIMISHWA SARE NA KAIZER CHIEFS JOHANNESBURG NA KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva amecheza kipindi kimoja leo timu yake, Wydad Athletic ya Morocco ikilazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Kaizer Chiefs katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa FNB Jijiji Johannesburg, Afrika Kusini. Msuva alimpisha kiungo Mlibya, Muaid Ellafi  kipindi cha pili na kwa sare hiyo, Kaizer Chiefs wanakwenda Fainali kufuatia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jijini Casablanca nchini Morocco Jumamosi iliyopita.

DENMARK YAISHINDILIA WALES 4-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI EURO 2020

Image
DENMARK wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Wales leo Uwanja wa Johan Cruijff Arena Jijini Amsterdam nchini Uholanzi. Mabao ya Denmark yamefungwa na Kasper Dolberg dakika ya 27 na 48, Joakim Mæhle dakika ya 88 na   Martin Braithwaite dakika ya 90 na ushei na sasa itakutana na mshindi  kati ya Uholanzi na Jamhuri ya Czech.

SIMBA SC YAICHAPA AZAM FC 1-0 NA KUITUPA NJE ASFC, KUKUTANA NA YANGA SC KATIKA FAINALI JULAI 25 KIGOMA

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wamefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo, kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone dakika ya 90 na ushei akimalizia mpira wa adhabu alioanzishiwa na winga Mghana, Bernard Morrison baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa nje kidogo ya boksi upande wa kulia. Sasa Simba SC watakutana na watani wao wa jadi, Yanga SC katika fainali Julai 25 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma kuwania taji la tatu mfululizo la Azam Sports Federation Cup (ASFC). Ikumbukwe jana Yanga SC iliitoa Biashara United ya Mara kwa kuichapa 1-0 pia, bao pekee la mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

YANGA SC 1-0 BIASHARA UNITED (KOMBE LA TFF TABORA)

Image
 

CHIPUKIZI MWENYE KIPAJI MTANZANIA, KELVIN JOHN AJIUNGA NA TIMU YA ZAMANI YA SAMATTA, GENK HADI MWAKA 2024

Image
 MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Kelvin John Pius mwenye umri wa miaka 18 amejiunga  klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji baada ya kusaini utakaomalizika mwaka 2024. Taarifa rasmi ya Genk leo imemshukuru mchezaji wake wa zamani, Mtanzania pia, Mbwana Ally Samatta kwa kuwasaidia kuinasa saini ya kinda huyo mwenye kipaji kutoka akademi ya Brook House Collage ya England aliyojiunga nayo mwaka 2019 baada ya kung'ara kwenye Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17. Samatta, Nahodha wa Taifa Stars mwenye umri wa miaka 28 sasa, alipita Genk kwa miaka minne kuanzia 2016 kabla ya kwenda Aston Villa ya England mwaka 2020 ambayo baada ya miezi kadhaa ilimtoa kwa mkopo Fenerbahce ya Uturuki.

YANGA SC YATINGA FAINALI ASFC BAADA YA KUICHAPA BIASHARA UNITED 1-0 BAO PEKEE LA YACOUBA SOGNE TABORA

Image
 VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Sogne aliyefunga bao hilo dakika ya 22 akimalizia pasi ya kiungo Mzanzibar, Feisal Salum Abdallah. Yanga sasa watakutana na mshindi kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na Azam FC zinazomenyana kesho katika Nusu Fainali nyingine Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.

RUVU SHOOTING YALAZIMISHWA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA POLISI TANZANIA LEO UWANJA WA MABATINI MECHI YA LIGI KUU

Image
RUVU Shooting imelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. David Ulomi alianza kuifungia Ruvu Shooting dakika ya 34, kabla ya Tariq Seif kuisawazishia Polisi Tanzania dakika ya 58. Kwa ushindi huo, Polisi Tanzania imefikisha pointi 42 baada ya kucheza mechi 32 na kusogea nafasi ya saba, wakati Ruvu Shooting inayofikisha pointi 38 za mechi 32 pia inasonga nafasi ya 10.

KAMATI YA MAADILI YA TFF YAMFUTIA ADHABU YA KUMFUNGIA MWAKALEBELA MIAKA MITANO KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

Image
 KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfutia adhabu ya kufungiwa miaka mitano kutojisjighulisha na soka pamoja na faini ya Sh. Milioni 7 aliyopewa na Aprili 2, mwaka huu na Kamati hiyo. Mwakalebela alitozwa faini ya Sh Milioni 5 baada ya kutiwa hatiani kwa kutoa maneno ya uchochezi kwa nia ya kuchochea mashabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga dhidi ya vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu nchini. Uamuzi huo ulitolewa na Kamati ya Maadili ya TFF kwa kuzingatia kifungu cha 73(4) cha kanuni za maadili za TFF toleo la 2013. Mwakalebela alilalamikiwa kuwa Februari 19 mwaka huu aliitisha mkutano na Waandishi wa Habari na kudai kuwa TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tazania Bara (TPLB) na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi hiyo zinaihujumu Yanga, madai ambayo alishindwa kuthibitisha mbele ya kamati. Katika shtaka la pili, Mwakalebela alilalamikiwa kwa kutoa taarifa za uongo Oktoba 1, 2020 baada ya kuitisha mkutano na kudai kuwa anao mkataba kati ya mchezaji Bernard Morri

BRAZIL YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUICHAPA COLOMBIA 2-1

Image
WENYEJI, Brazil wamefuzu Robo Fainali ya Copa America baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Colombia katika mchezo wa Kundi B usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Nilton Santos Jijini Rio de Janeiro. Mabao ya Brazil yamefungwa na Roberto Firmino dakika ya 78 akimalizia pasi ya Renan Lodi na Casemiro dakika ya 90 na ushei akimalizoa pasi ya Neymar, wakati la Colombia limefungwa na Luis Díaz dakika ya 10 akimalizia pasi ya J. Cuadrado. Brazil inafikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu ma kuendelea kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Colombia yenye pointi nne za mechi nne, Peru pointi nne pia, Ecuador na Venezuela pointi mbili kila timu baada ya kucheza mechi tatu wote pia.

URENO YAFUZU KWA MLANGO WA ‘UANI’ 16 BORA YA EURO 2020,

Image
TIMU za Ufaransa, Ujerumani na Ureno zimefuzu Hatua ya 16 Bora baada ya mechi zao za mwisho za Kundi F leo. Ureno imamaliza kwa sare ya 2-2 na Ufaransa leo Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest, Hungary. Mabao ya Ureno yote yamefungwa  na Cristiano Ronaldo na yote kwa penalti dakika ya 30 na 60, wakati ya Ufaransa yamefungwa na 45'+2 K. Benzema yote, la kwanza kwa penalti pia dakika ya 45 na ushei na la pili dakika ya 47 akimalizia pasi ya Paul Pogba. Nayo Ujerumani imelizimishwa sare ya 2-2 na Hungary Uwanja wa Venue Allianz Arena Jijini Munich. Mabao ya Ujerumani yamefungwa na Kai Havertz 66' na Leon Goretzka dakika ya 84, wakati ya Hungary yamefungwa na Ádám Szalai dakika ya 11 na András Schäfer dakika ya 68. Ufaransa inamaliza kileleni na pointi zake tano, ikifuatiwa na Ujerumani pointi nne na zote zinafuzu 16 Bora, wakati Ureno iliyomaliza na pointi nne pia inafuzu kama Mshindi wa tatu Bora huku safari ya Hungary ikiishia hapa. Timu nyingine zilizofuzu 16 Bora ni Wa

HISPANIA NA SWEDEN ZATINGA 16 BORA EURO 2020, LEWANDOWSKI NJE

Image
HISPANIA imefuzu Hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Slovakia katika mchezo wa Kundi E wa Euro 2020 leo Uwanja wa Olímpico Jijini Sevilla. Mabao ya Hispania yamefungwa na Martin Dúbravka aliyejifunga dakika ya 30, Aymeric Laporte dakika ya 45, Pablo Sarabia dakika ya 56, Ferran Torres dakika ya 67 na Juraj Kucka aliyejifunga dakika ya 71. Mechi nyingine ya kundi hilo, Sweden imeichapa Poland 3-2 Uwanja wa Saint-Petersburg Jijini St. Petersburg, Urusi. Mabao ya Sweden yamefungwa na Emil Forsberg mawili dakika ya pili na 59 na Viktor Claesson dakika ya 90 na ushei, wakati ya Poland yote yamefungwa na Robert Lewandowski dakika ya 61 na 84. Sweden inamaliza kileleni na pointi zake saba, ikifuatiwa na Hispania pointi tano na zote zinafuzu 16 Bora ya michuano hiyo, wakati Slovakia iliyomaliza na pointi tatu na Poland pointi moja zote zinaaga.