NI AL AHLY NA KAIZER CHIEFS FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

MABINGWA watetezi, Al Ahly wamefanikiwa kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Esperance ya Tunisia usiku huu Uwanja wa WE Al-Ahly Jijiji Cairo nchini Misri.
Mabao ya Ahly yamefungwa na Ali MaĆ¢loul kwa penalti dakika ya 38, Mohamed Sherif dakika ya 56 na Hussein El Shahat dakika ya 60 na kwa matokeo hayo wanaenda fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza Jumamosi iliyopita Tunisia. 
Al Ahly sasa itakutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Wydad Athletic baada ya sare ya 0-0 leo Johannesburg kufuatia ushindi wa 1-0 Jumamosi iliyopita Morocco.




Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA

NI YANGA BINGWA KOMBE LA MUUNGANO 2025