Posts

Showing posts from December, 2020

WABUNGE WA ZAMANI NA WA SASA WAGONGANA KUWANIA UENYEKITI WA KLABU YA SIMBA SC FEBRUARI 7

Image
WABUNGE wa sasa na wa zamani wamejitokeza kuwania nafasi ya Uenyekiti wa klabu ya Simba SC Februari 7, mwakani.   Hao ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Chemba, Juma Suleiman Nkamia, Mbunge wa zamani wa Kilwa, Murtaza Ally Manungu na Mbunge wa sasa, Rashid Abdallah Shangazi wa jimbo la Mlalo, Lushoto mkoani Tanga. Pamoja na hao wagombea wengine hadi sasa ni Bittony Innocent Mkwakisu na Khamis Omar Mtika.

YANGA SC CHUPUCHUPU KUZAMA KWA PRISONS, WASAWAZISHA MWISHONI SARE 1-1 SUMBAWAGA

Image
VINARA, Yanga SC wameendeleza rekodi ya kupoteza mechi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu baada ya leo kulazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tisa zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi. Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Tanzania Prisons wakawashitua Yanga SC kwa bao la Jumanne Elfadhili dakika sita tu ndani ya kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri ya Nurdin Chona. Pilikapilika za Yanga zikafanikiwa kuzaa matunda dakika 12 kabla ya filimbi ya mwisho, mkombozi akiwa na mchezaji mpya kutoka Burundi, Said Ntibanzokiza. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania bao pekee la Ismail Aziz dakika ya 88 Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Pamoja na ushindi huo, Azam FC inayofu

REAL MADRID YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA ELCHE KATIKA LA LIGA

Image
REAL Madrid imelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Elche katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Manuel Martinez Valero usiku wa jana. Luka Modric alianza kuifungia Real Madrid dakika ya 20, lakini Fidel Chaves akaisawazishia Elche kwa penalti dakika ya 52 baada ya Dani Carvajal kumvuta jezi Antonio Barragan.  Matokeo hayo yanaifanya Real Madrid ifikishe pointi 33 baada ya kucheza mechi 16 na wanabaki nafasi ya pili, wakizidiwa pointi mbili na mahasimu wao, Atletico Madrid ambao pia wana mechi mbili mkononi   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SIMBA SC 4-0 IHEFU SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE NYINGINE ENGLAND, 0-0 NA NEWCASTLE UNITED

Image
Liverpool imelazimishwa sare ya bila kufungana na Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa St. James' Park. Sare hiyo inaifanya Liverpool ifikishe pointi 33 baada ya kucheza mechi 16 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya mahasimu wao, Manchester United ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

KAGERE APIGA MBILI, TSHABALALA NA MUGALU MOJA KILA MMOJA SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 4-0 DAR

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbila ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa Ihefu SC 4-0 jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck inafikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 15, ingawa inabaki nafasi ya pili mbele ya vinara, Yanga SC wenye pointi 43 za mechi 17. Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Nassor Mwinchui wa Pwani aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Geoffrey Msakila wa Geita hadi mapumziko SImba SC walikuwa mbele kwa mabao 3-0. Leo biashara ilifunguliwa na beki wa kulia, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dakika ya tisa akimalizia kazi nzuri ya beki wa kulia, Shomari Kapombe, wote wazawa. Mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu misimu miwili mfululizo iliyopita akaifungia Simba SC mabao mawili dakika ya 15 akimalizia pasi ya winga Luis Miqussion kutoka Msumbiji na daki

BARCELONA WALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA EIBAR LA LIGA

Image
Ousmane Dembele akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la kusawazisha Barcelona dakika ya 67 katika sare ya 1-1 na Eibar iliyotangulia kwa bao la Kike dakika ya 57 usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

MAN UNITED YAICHAPA WOLVES 1-0 BAO LA RASHFORD DAKIKA YA MWISHO

Image
Marcus Rashford akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Manchester United dakika ya 90 na ushei ikiwalaza Wolverhampton Wanderers 1-0 usiku wa jana Uwanja wa Venue Old Trafford. Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 30 na kurejea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 15   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

LACAZETTE AFUNGA BAO PEKEE ARSENAL YAILAZA BRGHTON 1-0 THE AMEX

Image
Alexandre Lacazette akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Arsenal dakika ya 66, kiasi cha sekunde 21 baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Martinelli katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion Uwanja wa Amex   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA DEO LUCAS KATIKA SPORTS AM

Image

METACHA MNATA ATEMWA, JUMA KASEJA AITWA PAMOJA NA AISHI MANULA NA DANIEL MGORE TAIFA STARS YA CHAN

Image
KIPA namba wa Yanga SC, Metacha Boniphace Mnata hajaorodheshwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoanza maandalizi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) .  

WAZIRI BASHUNGWA AKUTANA NA MAGWIJI WA SOKA NA KUAHIDI KUENDELEZA HESHIMA YA MICHEZO NCHINI

Image
Na Shamimu Nyaki –WHUSM, DAR ES SALAAM WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha heshima ya michezo hapa nchini inarejea. Bashungwa ameyasema hayo jana Jijini Dar  es  Salaam ambapo alifanya kikao na makocha pamoja na wanamichezo wa zamani na ameeleza kuwa  Serikali imeanza kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Michezo. "Lengo la kikao hiki ni kupokea mawazo kutoka kwenu namna bora ya kuendesha michezo ili tupate mafanikio kama ambayo tulipata hapo zamani wakati nyie mkilitumikia taifa letu katika soka" alisema,  Waziri Bashungwa. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa akisalimiana na mmoja wa mchezaji wa zamani baada ya kikao na Wachezajia pamoja na Makocha wa zamani kuhusu maendelo ya michezo nchini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (katikati), Naibu Waziri Abdallah Ulega wakiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji pamoja na Makocha wa z

SIMON MSUVA AENDELEA KUNG'ARA WYDAD CASABLANCA, AFUNGA BAO BAO PEKEE YASHINDA 1-0 MOROCCO

Image
HABARI njema zaidi ni kwamba – Simon Msuva si tu mchezaji pale Wydad bali ni ‘Supa Staa’ baada ya vitu alivyofanya muda mfupi tu wa kuwa na timu hiyoaliyojiunga nayo mwezi huu kutoka Difaa El jadida ya Morocco pia. Mwishoni Jumamosi alifunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Maghreb Fès, hilo likiwa bao la pili tangu ajiunge na timu hiyo – baada ya kufunga pia katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Hassania Agadir Desemba 19. Kwa matokeo hayo, Wydad Casablanca imefikisha pointi 12 ikizidiwa moja na Raja wanaoongoza Botola Pro baada ya wote kucheza mechi tano. 

TFF YASEMA SINGIDA UNITED INAWADAI SH MILIONI 1 TU ZAWADI YA USHINDI WA PILI KOMBE LA TFF 2019

Image
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema klabu ya Lipuli FC ya Iringa inadai Sh Milioni 1 tu katika zawadi yake ya ushindi wa pili Kombe la Shirikisho Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup msimu uliopita      

SIMBA SC YAMSIMAMISHA JONAS MKUDE KWA MUDA USOJULIKANA KUTOKANA NA UTOVU WA NIDHAMU

Image
KLABU ya Simba SC imemsimamisha kwa muda usiojulikana kiungo wake Jonas Mkude kutokana na utovu wa nidhamu. Taarifa iliyotolewa na mtendaji mkuu wa klabu hiyo kwa vyombo vya habari imesema Mkude amesimamishwa ili kupisha kusikilizwa kwa tuhuma zinazomkabili mchezaji huyo bila kutaja ni tuhuma zipi huku swala lake likipelekwa katika kamati ya nidhamu ya timu hiyo. Taarifa hiyo imesema klabu hiyo haitaweza kuvumilia kwa namna yoyote vitendo vya utovu wa nidhamu na kudai nidhamu ndo uti wa mgongo wa mafanikio ya klabu hiyo. Vitendo alivyovifanya Jonas Mkude itakuwa ni pigo kwa klabu hiyo ya Msimbazi inayokabiliwa na mchezo muhimu wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Platinum ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa mwanzoni mwa mwezi ujao jijini Dar Es Salaam.

SIMBA SC 5-0 MAJI MAJI (KOMBE LA TFF)

Image
 

BEKI MKONGWE NCHINI KELVIN YONDAN ALIYEACHWA NA VIGOGO, YANGA SC ASAJILIWA NA POLISI TANZANIA

Image
Na Clement Shari, ARUSHA KLABU ya soka ya Polisi Tanzania yenye maskani yake mjini Moshi mkoani Kilimanjaro imetangaza kumsajili beki wa zamani wa klabu ya Yanga Kelvin Patrick Yondan katika dirisha hili dogo ambalo kwa sasa lipo wazi. Msemaji wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro kwa njia ya ujumbe wa Sauti alioutuma kwa wanahabari amesema mchezaji huyo amepewa mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Polisi Tz. Lukwaro amesema tayari mchezaji huyo amekwishakutua mjini Moshi kuanza majukumu kwenye timu yake mpya Mara baada ya kukaa nje ya dimba kwa nusu msimu. Wiki iliyopita zilikuwepo tetesi za mchezaji huyo kusajiliwa na Polisi lakini uongozi wa timu hiyo haukuwa tayari kuweka mambo hadharani. Lukwaro amesema klabu ya Polisi italitumia dirisha hili dogo kukiimarisha kikosi chake bila ya kutaja ni wachezaji gani wanaotaraji kuwasajili na nafasi zao za uwanjani.  Mpaka sasa klabu ya Polisi Tz ipo katika nafasi ya 6 ikiwa na alama 23 Mara baada ya kucheza michezo 17 ya Mzunguko wa kwanza

LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA WEST BROM ANFIELD

Image
BAO la dakika ya 89 la la Sam Johnstone liliwasaidia wageni, West Bromwich Albion kupata sare ya 1-1na wenyeji na mabingwa watetezi, Liverpool waliotangulia kwa bao la Sadio Mane dakika ya 12 Uwanja wa Anfield. Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 32 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya Everton baada ya wote kucheza mechi 15   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SIMBA SC YAIFUMUA MAJI MAJI YA SONGEA 5-0 NA KUSONGA MBELE AZAM SPORTS FEDERATION CUP

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wamesonga mbele michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Maji Maji ya Songea usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.  Mabao ya Simba SC katika mchezo wa leo yamefungwa na beki mzawa Gardiel Michael dakika ya tatu, mshambuliaji Mkongo Chris Mugalu dakika ya sita, beki Mzanzibari Ibrahim Ame dakika ya 60, mshambuliaji Mrwanda Meddie Kagere dakika ya 78 na kiungo kutoka Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 90. Mechi nyingine za leo, Mtibwa Sugar iliilaza 1-0 Geita Gold, bao pekee la Ismail Mhesa dakika ya 67 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Beno Kakolanya, David Kameta, Gardiel Michael, Ibrahim Ame, Kennedy juma, Said Ndemla/Shomari Kapombe dk66, Miraj Athumani ‘Madenge’, Rally Bwalya/Luis Miquissone dk66, Ibrahim Ajibu, Chris Mugalu/Meddie Kagere dk65 na Francis Kahata. Maji Maji; Mputi Jaffar, Juma Abdallah

MABONDIA WA TANZANIA WAADHIBU WAGENI KWA VIPIGO TOFAUTI DAR

Image
MABONDIA nyota wa Tanzania jana waliwashinda wapinzani wao kutoka nchi tofauti kwa staili mbalimbali katika ukumbi wa Next Door Arena – Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ akiwa kivutio zaidi baada ya kumshinda Symon Tcheta wa Malawi kwa KO raundi ya kwanza. Mfaume Mfaume alishinda kwa pointi dhidi ya Chikondi Makawa wa Malawi sawa Ismail Galiatano aliyemshinda Israel Kamwamba wa Malawi pia, wakati Tonny Rashid alimpiga Hassan Milanzi wa Zimbabwe kwa KO raundi ya pili, Selemani Kidunda akamchapa Limbani Masamba wa Malawi pia kwa KO raundi ya pili. Mpinzani wa Twaha Kiduku, Guy Tshimanga Tshitundu kutoka Kongo hakutokea, wakati Juma Choki akamchaka Issa Nampepeche kwa TKO raundi ya tatu katika pambano la watoto wa nyumbani.

MANCHESTER CITY WAITANDIKA NEWCASTLE UNITED 2-0 ETIHAD

Image
MABAO ya Ilkay Gundogan dakika ya 14 na Ferran Torres dakika ya 55 jana yaliipa Manchester City ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad. Kwa ushindi huo, kikosi cha Pep Guardiola kinafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 14 na kusogea nafasi ya tano, sasa wakizidiwa pointi moja na mahasimu wao wa Jiji, Manchester United wanaoshika nafasi ya nne   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

ARSENAL WAZINDUKA ENGLAND NA KUITANDIKA CHELSEA 3-0 EMIRATES

Image
MABAO ya Alexandre Lacazette kwa penalti baada ya Reece James kuchezewa rafu na Kieran Tierney dakika ya 34, Granit Xhaka dakika ya 44 na Bukayo Saka dakika ya 56 jana yaliipa Arsenal ushindi wa 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates. Ushindi huo wa kwanza kwa The Gunners kwenye mechi ya mashindano ya nyumbani tangu Novemba 1, unampa ahueni kocha Mikel Arteta sasa akifikisha pointi 17 baada ya mechi 15 na sasa wanashika nafasi ya 14, wakati Chelsea ya kocha Frank Lampard inabaki na pointi zake 25 baada ya mechi 15 katika nafasi ya saba   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

YANGA SC WASHEREHEKEA KRISIMASI KWA KUWAFARIJI YATIMA NA WAGONJWA WA HOSPITALI YA MBOZI

Image
VIGOGO wa soka Tanzania, Yanga SC jana katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi walitoa zawadi katika kituo cha kulelea watoto yatima na hospitali ya Mbozi mkoani Songwe.  Yanga imeweka kambi Mbeya baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu SC kujiandaa na mchezo wao ujao dhidi ya Tanzania Prisons Sumbawanga mkoani Rukwa