Posts

Showing posts from February, 2021

SIMBA NA KAGERA SUGAR DAR, YANGA SC KUIFUATA TANZANIA PRISONS SUMBAWANGA 16 BORA KOMBE LA TFF

Image
 SIMBA SC itamenyana na Kagera Sugar hapa Dar es Salaam  na Yanga SC itaifuata Tanzania Prisons huko Sumbawanga mkoani Rukwa katika Hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

LEWANDOWSKI APIGA MBILI BAYERN MUNICH YASHINDA 5-1

Image
MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski jana amefunga mabao mawili, Bayern Munich ikiibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya FC Cologne katika mchezo wa Bundesliga Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich – na sasa wanaongoza kwa ponti mbili zaidi ya RB Leipzig (52-50) baada ya mechi 23 kwa wote. Mpoland huyo akifikisha mabao 28 – huku mabao mengine ya Bavarian yakifungwa na Serge Gnabry aliyetokea benchi mawili pia na lingine Eric Maxim Choupo-Moting na la kufutia machozi la Cologne lilifungwa na Ellyes Skhiri  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MANCHESTER CITY YAICHAPA WEST HAM UNITED 2-1 ETIHAD

Image
TIMU ya Manchester City imezidi kujisogeza jirani na ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya West Ham United jana Uwanja wa Etihad, hivyo kuongoza ligi hiyo kwa pointi 13 zaidi ya Manchester United wanaofuatia. Ushindi huo wa 20 mfululizo kwa kikosi cha Pep Guardiola kwenye mashindano yote ulitokana na mabao ya Ruben Dias dakika ya 30 na John Stones dakika ya 68, huku bao pekee la West Ham likifungwa na Michail Antonio dakika ya 43   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MESSI, DEMBELE WAFUNGA BARCELONA YASHINDA 2-0 LA LIGA

Image
TIMU ya Barcelona jana imeshindia 2-0 ugenini dhidi ya Sevilla katika mchezo wa La Liga, mabao ya Ousmane Dembele dakika ya 29 na Lionel Messi dakika ya 85 Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan, hivyo kupanda nafasi ya pili, ikiizidi pointi moja Real Madrid (53-52), ambayo kesho inacheza na Real Sociedad   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

PRINCE DUBE MPUMELELO AFUNGA BAO PEKEE AZAM FC YAICHAPA MBUNI 1-0 NA KUTINGA 16 BORA KOMBE LA TFF

Image
BAO pekee la mshambuliaji Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbuni FC katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.Azam FC sasa itamenyana na Polisi Tanzania iliyoitoa Kwamndolwa FC.

YANGA SC YAICHAPA KEN GOLD 1-0 KWA MBINDE NA KUSONGA MBELE MICHUANO YA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

Image
BAO la penalti la Mrundi, Fiston Abdul Razak limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Azam Sports Federation Cup jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Yanga SC inasonga mbele Hatua ya 16 Bora na itakutana na mshindi kati ya Sahare All Stars na Tanzania Prisons zinazomenyana kesho.

MOROCCO YAAGA AFCON U20, NI UGANDA NA TUNISIA NUSU FAINALI

Image
TIMU ya Morocco imtupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) baada ya kufungwa kwa penalti 4-1 na Tunisia kufuatia sare ya 0-0 jana Uwanja wa Olimpiki de Nouakchott Jijini Nouakchott. Nayo Gambia ilikamilisha idadi ya timu za Nusu Fainali baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), mabao ya Wally Fofana dakika ya tano,  Momodou Bojang dakika ya 49 na Alieu Barry dakika ya 90 na ushei. Mechi za Nusu Fainali zitachezwa Jumatatu, Ghana na Gambia na Uganda na Tunisia hapo hapo Uwanja wa Olimpiki wa Nouakchott. Ghana iliitoa Cameroon kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 na Uganda iliita Burkina Faso kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0.

SIMBA SC 3-0 AFRICAN LYON (KOMBE LA TFF)

Image
 

SIMBA SC YAENDELEA KUNG'ARA, YAWATANDIKA ACRICAN LYON 3-0 NA KUSONGA MBELE AZAM SPORTS FEDERATION CUP

Image
SIMBA SC imetinga Hatua ya 16 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya African Lyo leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na Ibrahim Ajibu mawili dakika ya 10 na 44 na Mzimbabwe Perfect Chikwende dakika ya 63.

KIM POULSEN AITA WACHEZAJI 43 KIKOSI CHA AWALI TAIFA STARS WAKIWEMO KELVIN YONDAN NA CHILUNDA

Image
KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Paulsen ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 43 kwa maandalizi ya mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nyumbani na ugenini dhidi ya Equatorial Guinea. Kikosi hicho kitacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Kenya kabla ya kuwavaa Equatorial Guinea kuwania tiketi ya AFCON.

AUBAMEYANG APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA BENFICA 3-2 RUROPA LEAGUE

Image
TIMU ya Arsenal imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora UEFA Europa League baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Benfica jana Uwanja wa Georgios KaraiskákiJijini Piraeus. Arsenal inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza. Mabao ya Arsenal yalifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang mawili dakika ya 21 na 87 na Kieran Tierney dakika ya 67, wakati ya Benfica yamefungwa na Diogo Gonçalves dakika ya 43 na Rafa Silva dakika ya 61. 

NAMUNGO FC YAKAMILISHA BIASHARA VIZURI NA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA BAADA YA KUWATOA WAANGOLA

Image
TIMU ya Namungo FC ya Ruangwa mkaoni Lindi imefanikiwa kwenda Hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kufungwa 3-1 na Primiero do Agosto ya Angola jioni ya leo Uwanja ww Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Namungo FC inakwenda Hatua ya 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 7-5 baada ya kushinda 6-2 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam pia. Namungo inaingia Kundi D ambako itakuwa na Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids FC ya Misri na Nkana FC ya Zambia.

MAN CITY WAICHAPA BORUSSIA MONCHENGLADBACH 2-1

Image
TIMU ya Manchester City imetanguliza mguu mmoja Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach, mabao ya Bernardo Silva na Gabriel Jesus Uwanja wa Puskas Arena Jijini Budapest, Hungary   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

BABA MZAZI WA ALISSON BECKER AFARIKI DUNIA AKIOGELEA KWENYE BWAWA BRAZIL

Image
Alisson Becker (lkushoto) akiwa na baba yake, Jose (kulia) amefariki dunia baada ya kuzama kwenye bwawa ziwani nchini Brazil   PICHA ZAIDI GONGA HAPA BABA wa makipa Alisson wa Liverpool na Muriel wa Fluminense, Jose Agostinho Becker amekutwa amekufa akiwa ana umri wa miaka 57. Alikuwa anaogelea jirani na nyumbani kwake kwenye bwawa huko Lavras do Sul, kilomita 320 kutoka Porto Alegre, kusini mwa Brazil kabla ya maji kumshinda na kuzama kisha kupotea tangu Jumatano. Iliripotiwa amepotea tangu Jumatano Saa 11 jioni kwa saa za huko kabla ya mwili wake kupatikana Saa 7:50 Alhamisi usiku. Jose Agostinho Becker naye pia alikuwa kipa wa timu ya ridhaa ya ndiye alichangiua mno hata wanaye, Alisson na Muriel kuwa makipa bora.

SERENGETI BOYS YAPANGWA KUNDI MOJA NA ALGERIA, NIGERIA NA KONGO FAINALI ZA AFCON U17 MOROCCO JULAI MWAKA HUU

Image
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imepangwa Kundi B pamoja na Algeria, Kongo na Nigeria katika Fainali za AFCON U17 nchini Morocco Julai mwaka huu.

GIROUD APIGA BONGE LA BAO CHELSEA YAILAZA ATLETICO MADRID 1-0

Image
MSHAMBULIAJI Mfaransa, Olivier Giroud jana amefunga bao zuri la tik tak dakika ya 68 akiiwezesha Chelsea kushinda 1-0 dhidi ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa kwanza wa Hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Taifa wa Bucharest nchini Romania   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MSUVA ACHEZA KIPINDI KIMOJA WYDAD CASABLANCA YASHINDA 1-0 UGENINI LIGI YA MABINGWA

Image
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amecheza kipindi kimoja tu, timu yake Wydad Athletic Club, maarufu Wydad Casablanca ikiibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, Petro Atletico Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda nchini Angola. Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga ya nyumbani, Tanzania alimpisha Mohammed Ounajem mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kuipigania Wydad kwa dakika 45. Na shujaa wa mchezo akawa Ayoub El Kaabi aliyefunga bao pekee kwenye mchezo huo wa Kundi C dakika ya 71 akimalizia pasi ya Muaid Ellafi. Ushindi huo unaifanya Wydad ipate pointi tatu za kwanza katika mchezo wake wa kwanza na sasa inashika nafasi ya pili nyuma ya Horoya ya Guinea yenye pointi za mechi mbili . Kaizer Chiefs iliyocheza mechi moja tu ikitoa sare ya 0-0 na Hoyora ina pointi moja, wakati Petro de Luanda inashika mkia baada ya kufungwa mechi zote mbili za kwanza.

SIMBA SC 1-0 AL AHLY (LIGI YA MABINGWA AFRIKA)

Image
 

SIMBA SC YAITWANGA AL AHLY YA MISRI 1-0 NA KUPANDA KILELENI KUNDI A LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA wa Tanzania, Simba Sports Club wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 31, kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kwa shuti la umbali wa mita 20 baada ya kuwahadaa viungo wa Ahly  Aliou Dieng, raia wa Mali na Mmisri Akram Tawfik kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama. Kwa ushindi huo, Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili kufuatia ushindi wa ugenini wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya AS Vita mjini Kinshasa Febaruari 12. Baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, E l Merreikh leo Uwanja wa Al-Hilal Jijini Omdurman, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inakaa nafasi ya pili ikilingana pointi na Al Ahly. Mechi ijayo S

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA EDGAR FONGO, MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA

Image

AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA BILA KUFUNGANA NA TANZANIA PRISONS MECHI YA LIGI KUU CHAMAZI

Image
  AZAM FC wamelazimshwa sare ya 0-0 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

NGORONGORO HEROES YATUPWA NJE FAINALI ZA AFCON U20 BAADA YA KUCHAPWA 3-0 NA MOROCCO MAURITANIA

Image
TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, AFCON U20 baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi C jana Uwanja wa Olimpiki wa Nouakchott nchini Mauritania. Mabao ya Morocco yalifungwa na viungo El Mehdi Moubarik dakika ya nne kwa penalti, Mohammed Amine Essahel dakika ya nane na mshambuliaji Ayoub Mouloua dakika ya 13. Tanzania inamaliza na pointi moja nyuma ya Ghana iliyomaliza na pointi nne sawa na Gambia waliomaliza nafasi ya pili, wakati Morocco imeongoza kwa pointi zake saba. Ghana imefuzu Robo Fainali za AFCON U20 kama mshindi wa tatu bora zaidi ya washindi wa tatu wa makundi A na B. RATIBA YA ROBO FAINALI AFCON U20 Alhamisi Februari 25, 2021 Saa1:00 usiku Cameroon U20   -  Ghana U20 Saa 4:00 usiku Burkina Faso U20   -  Uganda U20 Ijumaa Februari 26, 2021 Saa 1:00 usiku Morocco U20   -  Tunisia U20 Saa 4:00 usiku Jamhuri ya Afrika ya Kati. U20   -  G

NAMUNGO FC YAPANGWA KUNDI MOJA RAJA CASABLANCA, PYRAMIDS YA MISRI NA NKANA FC KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
TIMU ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi itapangwa Kundi D itafuzu hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), katika Kundi hilo Namungo itakuwa na Raja Club Athletic ya Morocco, Pyramids FC ya Misri na Nkana FC ya Zambia. MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA KUNDI A Enyimba FC  ES Sétif  Orlando Pirates  Ahli Benghazi  KUNDI B  RS Berkane  JS Kabylie  Cotonsport  NAPSA Stars  KUNDI C  Etoile Sahel  CS Sfaxien  Salitas FC  ASC Jaraaf  KUNDI D   Raja Club Athletic  Pyramids FC  Nkana FC  Namungo SC/Primeiro Agosto

MAN UNITED YAJIWEKA SAWA NAFASI YA PILI ENGLAND BAADA YA KUICHAPA NEWCASTLE 3-1

Image
TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Old Trafford. Mabao ya Manchester Unted yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 30, Daniel  James dakika ya 57 na Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya 75, wakati la Newcastle United limefungwa na Allan Saint-Maximin dakika ya 36. Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 49 na kurejea nafasi ya pili,ikiizidi wastani wa mabao tu Leicester City, wote wakiwa nyuma ya Manchester City inayoontoza kwa pointi 10 zaidi baada ya kwote ucheza mechi 25   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MECHI YA CR BELOUIZDAD YA ALGERIA NA MAMELODI SUNDOWNS YA AFRKA KUSINI LIGI YA MABINGWA KUCHEZWA DAR

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika limeridhia mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya CR Belouizdad ya Algeria ichezwe Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Februari 28, mwaka huu.