Posts

Showing posts from December, 2023

AUGUSTINE OKRAH NI MCHEZAJI MPYAWA YANGA SC

Image
KLABU ya Yanga imemtambulisha winga Mghana, Augustine Okrah (30) kama mchezaji wake mpya, miezi sita tu tangu aachane na watani wao, Simba SC. Okrah aliyetambulishwa usiku wa jana wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar anakuwa mchezaji mpya wa pili dirisha hili dogo baada ya kiungo Mzanzibari, Shekhan Khamis.

AZAM FC YASAJILI KIPA WA TIMU YA TAIFA YA SUDAN KWA MKOPO

Image
KLABU ya Azam FC imemsajili kipa wa Kimataifa wa Sudan, Mohamed Mustafa kwa mkopo wa miezi sita kutoka El Merreikh ya kwao, Omdurman. Mohamed Mustafa (27) ambaye pia anadakia timu ya taifa ya Sudan, anajiunga na Azam FC kutoka  Al-Ahli ya Atbara alipokuwa anacheza kwa mkopo pia tangu mwaka 2018. Mustafa alijiunga na Merreikh Omdurman mwaka 2014 akitokea Merreikh Al-Fasher aliyoanza kuidakia mwaka 2011, kabla ya mwaka 2017 kupelekwa kwa mkopo Al-Merrikh SC ya Nyala na baadaye Al-Ahli Atbara. Huyo anakuwa kipa wa tatu wa kigeni kwenye kikosi cha Azam FC baada ya Mcomoro, Ali Ahamada (32) na Mghana Iddrisu Abdulai (26). Baada ya kuumia mnfululizo kwa makipa hao wa kigeni mapema Desemba, Azam FC ikawa inamtumia kipa wa tatu, Zuberi Foba Masoud (21) kwenye mechi zake ambaye alifanya vizuri.

KIPRE JUNIOR MCHEZAJI BORA, BRUNO KOCHA BORA LIGI KUU DESEMBA

Image
WINGA wa Azam FC, Zenón Kipre Emmanuel Junior amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Desemba 2023 akiwashinda Prince Dube Mpumelelo anayecheza naye timu moja na Mburkinabe, Stephane Aziz Ki wa Yanga. Pamoja naye, Kocha wa timu hiyo, Mfaransa Bruno Ferry ameshinda Tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi huo dhidi ya Muargentina Miguel Gamondi wa Yanga na Ahmad Ally wa Tanzania Prisons.

AZAM FC YAWACHAPA CHIPUKIZI 1-0 NA KUONGOZA KUNDI A MAPINDUZI

Image
BAO pekee la mshambuliaji Msenegal, Alassane Diao dakika ya 12 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Chipukizi United katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. Ushindi huo unaifanya Azam FC iongoze kundi hilo kwa pointi zake nne sasa ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Mlandege na Vital’O ya Burundi zenye pointi mbili kila moja, wakati Chipukizi United sasa inashika mkia kwa pointi yake moja.

MAN CITY YAWACHAPA VIBONDE SHEFFIELD UNITED 2-0 ETIHAD

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mabao ya Manchester City yamefungwa na Rodri dakika ya 14 na Julian Alvarez dakika ya 61 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 40 na kusogea nafasi ya tatu, wakiizidi tu wastani wa mabao Arsenal baada ya wote kucheza mechi 19, wakati Sheffield United inabaki na pointi zake tisa mkiani baada ya kucheza mechi 20 kwenye Ligi ya timu 20.

CHELSEA YAICHAPA LUTON TOWN 3-2 PALE PALE KENILWORTH

Image
TIMU ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Luton Town katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Kenilworth Road mjini Luton, Bedfordshire. Chelsea iliuanza vizuri mchezo kwa mabao mfululizo yaliyofungwa na Cole Palmer mawili dakika ya 12 na 70 na Noni Madueke dakika ya 37, kabla ya Luton Town kupata mabao yake kupitia kwa Ross Barkley dakika ya 80 na Elijah Adebayo dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya 10, wakati Luton Town inabaki na pointi zake 15 za mechi 19 nafasi ya 18 kwenye ligi ya timu 20.

MABINGWA MLANDEGE SARE TENA, 1-1 NA VITAL’O KOMBE LA MAPINDUZI

Image
MABINGWA watetezi, Mlandege FC wamekamilisha mechi mbili za Kundi A bila ushindi baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Vital’O ya Burundi leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. Mlandege walitangulia kwa bao la kiungo Optatus Yustin Lupekenya dakika ya 45 baada ya kazi nzuri ya Mcolombia, Diego Fernando, lakini mshambuliaji Kessy Jordan Nimbona akaisawazishia Vital’O dakika ya 64. Timu zote sasa zina pointi mbili bada ya kutoa sare katika mechi zao za kwanza pia, Mlandege na Azam FC na Vital’O na Chipukizi United. Mechi nyingine ya Kundi A itafuatia Saa 2:15 kati ya Azam FC na Chipukizi United hapo hapo New Amaan Complex.

SINGIDA YAANZA NA MOTO KOMBE LA MAPINDUZI, YAUA 4-1

Image
TIMU ya Singida Fountain Gate jana imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, JKU katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa New Amani Complex, Zanzibar. Mabao ya Singida Fountain Gate yalifungwa na washambuliaji, Mkenya Elvis Rupia mawili dakika ya 16 na 48, Mnyarwanda Meddie Kagere dakika ya 80 na Mkongo Francy Kazadi dakika ya 86, wakati la JKU limefungwa na Saleh Masoud Abdallah dakika ya 61 kwa penalti. Mchezo uliotangulia jana wa Kundi C, KVZ iliichapa Jamhuri 2-0, mabao ya Akram Mhina dakika ya nane na 53.

SHABIKI WA SIMBA SC, MAN UNITED ATAJIRIKA NA MILIONI 173 ZA M-BET

Image
SHABIKI wa   klabu   ya  Simba  na   timu   ya  Manchester United  ya  England  Seif   Babu   amefunga  droo   ya   Perfect12  ya   kampuni   ya   M-Bet   kibabe   baada  ya   kushinda   Sh  173,056,020  kwa   kubashiri   matokeo   ya  mechi  12  za   ligi   mbalimbai   duniani   kwa usahihi . Babu   ambaye   ni   mkazi   wa  Iringa,  alisema   kuwa haikuwa   kazi   rahisi   kubashiri   matokeo   hayo   pamoja   na uk weli   kuwa   kuna   baadhi   ya   timu   zimekuwa   zikipata matoeko   tofauti ,  tena   ya   kushangaza . Mshindi   huyo   alifunguliwa   akaunti   na   kuweka   fedha hizo   kwenye   benki   ya  CRDB  ambao   inashikiana   na   M-Bet.  Alisema   kuwa   michezo   min gi   ya   Ligi   za   mpira   wa miguu   imekuwa   na   matokeo   ambayo    huwezi   kutarajia na   kupata   changamoto   kubwa   wakati   wa   kukamilisha mkeka  wake. “ Nimebashiri   kwa   miezi   kadhaa   na   nimekuwa   nikaribia kushinda ,  unapokosa   unatakiwa   usikate   tamaa ,  hivyo nilipopig