Posts

Showing posts from January, 2024

MANCHESTER CITY YAICHAPA BURNLEY 3-1 ETIHAD

Image
WENYEJI, Manchester City usiku wa jana wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mabao ya Manchester City yamefungwa na Julian Álvarez mawili, dakika ya 16 na 22 na Rodri dakika ya 46, wakati la Burnley limefungwa na A. Al Dakhil dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 21 na kurejea nafasi ya pili, nyuma ya Liverpool inayoongoza kwa pointi zake 51 za mechi 22, wakati Arsenal yenye pointi 46 za mechi 22 ni ya tatu. Kwa upande wao Burnley baada ya kichapo cha jana inabaki na pointi zake 12 za mechi 22 nafasi ya 19 kwenye Ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.

DUBE NA DIAO WAFUNGA AZAM FC YAICHAPA KVZ 3-1 CHAMAZI

Image
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KVZ katika mchezo wa kirafiki jioni ya Jumatano Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na washambuliaji, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo na Wasenegal,, Msenegal Alassane Diao na beki Cheikh Sidibe.

SIMBA SC YAIRARUA TEMBO 4-0 NA KUSONGA MBELE ASFC

Image
TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federatión Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tembo ya Tabora leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Luis Miquissone wa Msumbiji dakika ya 11, Mrundi Saido Ntibanzokiza dakika ya 31 na washambuliaji wapya, Saleh Karabaka dakika ya 81 na Mgambia, Pa Omar Jobe dakika ya 83.

ARSENAL YAICHAPA NOTTINGHAM FOREST 2-1 THE CITY GROUND

Image
TIMU ya Arsenal jana imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England  Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire. Mabao ya Arsenal yalifungwa na Gabriel Jesus dakika ya 65 na Bukayo Saka dakika ya 72, wakati bao pekee la Nottingham Forest lilifungwa na Taiwo Awoniyi dakika ya 89. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 22 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Liverpool ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati mabingwa watetezi, Manchester City wana pointi 43 za mechi 20 nafasi ya tatu. Nottingham Forest baada ya adhabu hiyo wanabaki na pointi zao 20 za mechi 22 nafasi ya 16.

BAFANA BAFANA YAITUPA NJE MOROCCO, MALI YAING’OA BURKINA FASO

Image
TIMU ya Afrika Kusini imefanikiwa kutinga Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Morocco usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro nchini Ivory Coast. Mabao ya Bafana Bafana yalifungwa na Evidence Makgopa dakika ya 57 na Teboho Mokoena dakika ya 90 na ushei. Haikuwa siku kabisa kwa Simba wa Atlasi, kwani mbali na Achraf Hakimi kugongesha kwenye nguzo mkwaju wa penalti dakika ya 83 uliotolewa na Refa Mahmood Ismail wa Sudan baada ya Teboho Mokoena kuunawa mpira, lakini Sofyan Amrabat alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Mokoena dakika ya 90 na ushei. Bafana Bafana itakutana na Cape Verde Jumamosi ya Februari 3 Uwanja wa Charles Konan Banny mjini Yamoussoukro katika Robo Fainali. Katika mchezo uliotangulia wa Hatua ya 16 Bora jana, Mali iliitupa nje Burkina kwa kuichapa mabao 2-1 Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo. Mabao ya Mali yalifungwa na Edmond Tabsoba aliyejifunga dakika ya tatu na Las

MZIZE APIGA TATU YANGA YASHINDA 5-1 ASFC

Image
KIKOSI cha Yanga leo kimefanikiwa kutinga Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federatión Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya Hausung ya Njombe Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo, Jonás Mkude dakika ya 20, winga Mahalatse ‘Skudu’ Makudubela dakika ya 25 na mshambuliaji Clement Mzize, matatu dakika za 27,33 na 57, wakati bao pekee la Hausung limefungwa na Tonny Jailos dakika ya 70. Mechi nyingine za Azam Sports Federatión Cup leo Mtibwa Sugar imeichapa Nyakagwe mabao 3-0 Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro na Kagera Sugar imeilaza Dar City 4-0 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Raundi ya Pili ya ASFC itakamilishwa kesho kwa mchezo kati ya Simba SC na Tembo FC ya Tabora Uwanja wa Azam Complex.

IVORY COAST YAIVUA SENAGAL UBINGWA KWA MATUTA

Image
TIMU ya Senegal imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa kwa penalti 5-4 na wenyeji, Ivory Coast katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro mjini Yamoussoukro. Mshambuliaji wa Al Shabab, Mouhamadou Habibou Diallo alianza kuifungia Senegal dakika ya nne tu akimalizia krosi ya mkongwe, Sadio Mané wa Al Nassr kabla ya Franck Kessié wa Al Ahli, zote za Saudí Arabia kuisawazishia Ivory Coast kwa penalti dakika ya 86. Sasa Ivory Coast itakutana na Cape Verde katika Robi Fainali ambayo iliitoa Mauritania kwa kuichapa 1-0 katika mchezo uliotangulia jana, bao pekee la  Ryan Mendes kwa penalti dakika ya 88 Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan.

DRC YAITOA MISRI KWA MATUTA, KUKUTANA NA GUINEA ROBO FAINALI

Image
TIMU ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Misri usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro nchini Ivory Coast. DRC walitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Young Boys ya Uswisi Meschack Elia Lina dakika ya 37, kabla ya mshambuliaji wa Nantes ya Ufaransa, Mostafa Mohamed kuisawazishia Misri kwa penalti dakika ya 45. Pamoja na Misri kumaliza pungufu kufuatia mchezaji wake Hamdi Mohamed kutolewa kwa nyekundu katika dakika za nyongeza kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, lakini ilifanikiwa kumaliza dakika 120 na kwenda kwenye mikwaju ya penalti. Sasa DRC itakutana na Guinea ambayo mapema jana iliitoa Equatorial Guinea kwa kuichapa 1-0, bao pekee la mshambuliaji wa Le Havre ya Ufaransa, Mohamed Lamine Bayo dakika ya 90 Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan.

MAN UNITED YAICHAPA NEWPORT COUNTRY 4-2 NA KUSONGA MBELE FA

Image
TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Raundi ya Tano ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Newport County leo Uwanja wa Rodney Parade mjini Newport, Casnewydd. Mabao ya Manchester United yamefungwa na Nahodha, Bruno Fernandes dakika ya saba, Kobbie Mainoo dakika ya 13, Antony dos Santos dakika ya 68 na Ramsus Hojlund dakika ya 90. Kwa upande wao, Newport County inayoshiriki League Two (Daraja la Tatu) England mabao yao yamefungwa na Bryn Morris dakika ya 36 na Will Evans dakika ya 47.

LIVERPOOL YASHINDA 5-2 NA KUSONGA MBELE KOMBE LA FA ENGLAND

Image
TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Norwich City katika mchezo wa Raundi ya Nne Kombe la FA England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool. Mabao ya Liverpool yamefungwa na  Curtis Jones dakika ya 16, Darwin Nunez dakika ya 28, Diogo Jota dakika ya 53, Virgil van Dijk dakika ya 63 na Ryan Gravenberch dakika ya 90. Kwa upande wao Norwich City mabao yao yamefungwa na Ben Gibson dakika ya 22 na  Borja Sainz dakika ya 69 safari yao ikiishia Raundi ya Nne.

NIGERIA YAITUPA NJE CAMEROON BAADA YA KUICHAPA 2-0 ABIDJAN

Image
WINGA wa Atalanta ya Italia, Ademola Lookman usiku wa kuamkia leo amefunga mabao yote kuiwezesha Nigeria kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Cameroon katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan nchini Ivory Coast. Lookman alifunga bao la kwanza dakika ya 36, akimalizia kazi nzuri ya Mwanasoka Bora wa Afrika ambaye anacheza naye Serie A,Victor Osimhen mshambuliaji wa Napoli na bao la pili akafunga dakika ya 90 kwa msaada wa beki wa Fulham ya England, Calvin Bassey. Mapema dakika ya tisa, Lookman alimsetia vizuri beki wa West Bromwich Albion ya England, Oluwasemilogo 'Semi' Ajayi akafunga, lakini bao likakataliwa kwa msaada wa Msaada wa Marudio ya Picha za Video (VAR). Katika mchezo uliotangulia jana wa Hatua ya 16 Bora AFCON, Angola iliwatupa nje jirani zao Namibia kwa kuwachapa 3-0, mshambuliaji wa Al-Wakrah ya Qatar, Jacinto Muondo 'Gelson' Dala akifunga mawili dakika ya 38 na 42, kabla ya ms

MAN CITY YASONGA MBELE KOMBE LA FA, CHELSEA YABANWA DARAJANI

Image
BAO la beki Mholanzi, Nathan Benjamin Aké dakika ya 88 liliipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur katika mchezo wa Raundi ya Nne Kombe la FA England usiku wa jana Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London. Wakati Man City inakwenda Raundi ya Tano, mchezo mwingine wa Raundi ya Nne Kombe la FA jana, wenyeji Chelsea ililazimishwa sare ya 0-0 na Aston Villa Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, hivyo timu hizo zitarudiana.

TANZANIA NA IVORY COAST ZATAKA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA MICHEZO

Image
WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast, Adjé Silas na kujadili juu ya kusaini makubaliano maalum ya ushirikiano (MOU) katika sekta ya michezo baina ya nchi hizo ili kuibua na kukuza vipaji. Waziri Ndumbaro ameipongeza nchi hiyo kwa maandalizi mazuri ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yanayoendelea kwa kujenga miundombinu mizuri ikiwemo viwanja na barabara Amesema Tanzania inajifunza kwa Ivory Coast kwa kuwa itakua mwenyeji wa michuano hiyo kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027 Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Tanzania, Ally Mayai na viongozi wengine wa Wizara ya Michezo wa Ivory Coast. PICHA: MKUTANO WA MAWAZIRI WA MICHEZO TANZANIA NA IVORY COAST 

SIMON MSUVA AJIUNGA NA AL- NAJMA YA SAUDI ARABIA

Image
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva amejiunga na klabu ya Al-Najma yenye maskani Mji wa Unaizah inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia. Msuva anajiunga na Al Najma kufuatia kuachana na JS Kabylie aliyojiunga nayo Agosti mwaka jana akitokea nyingine ya Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia, Al-Qadsiah aliyoichezea kuanzia mwaka 2022. Awali Msuva aliibukia akademi ya Azam FC mwaka 2010, kabla ya kuhamia Moro United 2011 na baadaye vigogo wa soka nchini, Yanga ambako alicheza hadi mwaka 2017 alikwenda Morocco. Klabu yake ya kwanza ilikuwa Difaâ El Jadida aliyocheza hadi mwaka 2020 alipohamia Wydad Athletic alikodumu hadi mwaka 2022 akahamia Saudí Arabia. Anarejea Saudi Arabia baada ya kuichezea Tanzania katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo imetolewa Raundi ya kwanza tu baada ya kushika mkia katika Kundi F ikiambulia pointi mbili sawa na Zambia, wakiziacha Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zikisonga mbele. Lakini M

LIVERPOOL YATINGA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND

Image
TIMU ya Liverpool FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Fulham jana Uwanja wa Craven Cottage Jijini London. Mshambuliaji Mcolombia, Luis Díaz alianza kuifungia Liverpool dakika ya 11, kabla ya beki Mfaransa, Issa Diop kuisawazishia Fulham dakika ya 76. Liverpool inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia ushindi wa nyumbani wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Januari 10 Uwanja wa Anfield. Na sasa Liverpool itamenyana na Jumapili ya Februari 25 kuanzia Saa 1:30 usiku Uwanja wa Wembley Stadium Jijini London.

TAIFA STARS NA ZAMBIA ZATOLEWA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa bastará imetupwa nje Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika licha ya sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa mwisho wa Kundi F usiku wa jana Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo nchini Ivory Coast. Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi F, Morocco iliichapa Zambia 1-0, bao pekee la kiungo wa Galatasaray ya Uturuki, Hakim Ziyech dakika ya 37 Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro. Morocco inamaliza na pointi saba kileleni ikifuatiwa na DRC yenye pointi tatu na zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora, wakati Zambia iliyomaliza na pointi tatu nafasi ya tatu sasa na Tanzania zinaaga mashindano hayo. Mechi za mwisho za Kundi E jana zote zilimalizika kwa sare ya bila mabao,Afrika Kusini na Tunisia Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly na Namibia dhidi ya Mali Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro. Mali imeongoza Kundi E kwa pointi zake tano, ikifuatiwa na Afrika Kusini yenye pointi nne na zote zimefuzu Hatua ya 16 Bora, h

BURKINA FASO NA CAMEROON ZASONGA MBELE, ALGERIA WATOLEWA

Image
TIMU ya Burkina Faso imefuzu Hatua ya Mtoano Fainali za Kombe la  Mataifa ya Afrika licha ya kuchapwa mabao 2-0 na Angola usiku wa jana katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro mjini Yamoussoukro, Ivory Coast. Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki alicheza kwa dakika 89, kabla ya kumpisha Boureima Hassane Bandé wa HJK Helsinki ya Finland, mabao ya Angola yakifungwa na Mabululu dakika ya 36 na Zine dakika ya 90 na ushei. Mechi nyingine ya Kundi D jana, bao pekee la beki wa Al Hudod ya Iraq, Mohamed Dellahi Yali dakika ya 37 liliipa Mauritania ushindi wa 1-0 dhidi ya Algeria Uwanja wa de Bouaké mjini Bouaké, Ivory Coast. Angola imemaliza kileleni na pointi zake saba, ikifuatiwa na Burkina Faso pointi nne, wakati Mauritania nafasi ya tatu pointi tatu na Algeria iliyoambulia pointi mbili imeshika mkia. Katika mechi za Kundi C zilizotangulia jana, mabingwa watetezi, Senegal walikamilisha mechi zao zote za makundi kwa ushindi baada ya k

NIGERIA NA MISRI ZASONGA MBELE, IVORY COAST NA GHANA OUT AFCON

Image
NIGERIA imefanikiwa kwenda Hatua ya Mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Guinea-Bissau katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan, Ivory Coast. Bao pekee la Súper Eagle alijifunga beki wa ya Ligue2 Ufaransa, Opa Sanganté dakika ya 36.  Mechi nyingine ya Kundi A wenyeji Ivory Coast walitupwa nje baada ya kutandikwa mabao 4-0 na Equatorial Guinea Uwanja wa  Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidja.  Mabao ya Equatorial Guinea yalifungwa na nyota wanaocheza timu za madaraja ya chini Hispania, mshambuliaji Emilio Nsue wa Intercity mawili dakika ya 42 na 75, viungo, Pablo Ganet wa Alcoyano dakika ya 73 na Jannick Buyla wa SD Logroñés dakika ya 88. Kwa matokeo hayo, Equatorial Guinea inamaliza kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake saba, ikiizidi wastani wa mabao tu Nigeria na zote zinasonga mbele, wakati Ivory Coast imemaliza nafasi ya tatu pointi tatu, huku Guinea-Bissau ambao hawana hata

LIVERPOOL YAICHAPA BOURNEMOUTH 4-0 NA KUJIWEKA SAWA KILELENI ENGLAND

Image
TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vitality mjiki Bournemouth, Dorset. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Darwin Nunez mawili dakika ya 49 na 90 na ushei na Diogo Jota dakika ya 70 na 79. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 48 katika mchezo wa 21 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wana mchezo mmoja mkononi. Kwa upande wao, Bournemouth wanabaki na pointi zao 25 za mechi 20 nafasi ya 12.

MSUVA AFUNGA STARS YADROO NA ZAMBIA WACHACHE

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Zambia katika mchezo wa Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) leo Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro nchini Ivory Coast. Taifa Stars iliuanza vyema mchezo huo na Kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 11 tu kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simon Happygod Msuva aliyemalizia pasi ya Nahodha na mshambuliaji wa PAOK ya Ugiriki, Mbwana Ally Samatta. Zambia ikapata pigo dakika ya kiungo wake, Roderick Kabwe anayechezea Sekhukhune United ya Afrika Kusini kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 44 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano. Bado Chipolopolo wakamudu kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wa Leicester City, Patson Daka dakika ya 88 akimalizia kwa kichwa kona ya kiungo wa Simba ya Tanzania, Clatous Chama. Mechi nyingine ya Kundi F leo, Morocco pia ilitoa sare ya kufungana bao 1-1 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hapo hapo Uwanja wa Laurent P

PAMBA FC YAPIGA HONI LIGI KUU, YACHAPA STAND 4-1 NYAMAGANA

Image
WENYEJI, Pamba FC jana waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mwana Stand United katika mchezo wa Ligi ya NBC Champonship Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Mabao ya Pamba FC yalifungwa na Mudathir Said, Hassan Mwasapili, Haruna Chanongo na Lazaro Mlingwa, wakati bao pekee la Stand United lilifungwa na Lucas Sesana.  Mechi nyingine za jana za Ligi ya NBC Championship, Mbuni FC iliichapa Pan Africans mabao 3-1 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijjini Arusha na Mbeya City ikawatandika Mbeya Kwanza 4-2 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Ligi ya NBC Championship itaendelea leo kwa michezo mingine mitatu; TMA na Cosmopolitan Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, COPCO na Biashara United Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Ken Gold na Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Msimamo wa NBC Championship ni Pamba FC kileleni pointi 40 mechi 18, ikifuatiwa na Ken Gold pointi 39 mechi 17.   

MALI YAITOA MAURITANIA AFCON, BURKINA FASO SARE NA ALGERIA 2-2

Image
TIMU ya taifa ya Angola jana imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu Hatua ya Mtoano Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mauritania katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa La Paix mjini Bouaké, Ivory Coast.  Mabao ya Angola yalifungwa na washambuliaji Gelson Dala wa Al Wakrah ya Qatar mawili dakika ya 30 na 50 na Deivi Miguel Vieira 'Gilberto' wa  Petro de Luanda ya kwao dakika ya 53, wakati ya Mauritania yalifungwa na washambuliaji pia,  Sidi Amar wa  Nouadhibou ya kwao na  Aboubakary Koita wa  Sint-Truiden ya Ubelgiji. Mechi nyingine ya Kundi D jana,  Algeria ilitoka sare ya 2-2 Burkina Faso hapo hapo Uwanja wa La Paix mjini Bouaké. Mabao ya Burkina Faso yalfungwa na washambuliaji Mohamed Konaté wa  Akhmat Grozny ya Urusi dakika ya 45 na  Bertrand Traoré wa Aston Villa dakika ya 71 kwa penalti, wakati ya Algeria yalifungwa na mshambuliaji wa Al Sadd ya Qatar,Baghdad Bounedjah yote dakika ya 51 na 90 na ushei. Kwa matokeo hayo, Angola

ARSENAL YAICHAPA CRYSTAL PALACE 5-0 EMIRATES

Image
WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi  Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Magalhães dakika ya 11, kipa Dean Henderson aliyejifunga dakika ya 37, Leandro Trossard dakika ya 59 na Gabriel Martinelli mawili dakika ya 90+4 na 90+5. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya tatu, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake 21 za mechi 21 nafasi ya 14.

SENEGAL NA CAPE VERDE ZASONGA MBELE AFCON, CAMEROON HALI MBAYA

Image
MABINGWA watetezi, Senegal jana wamefanikiwa kwenda Hatua ya Mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cameroon katika mchezo wa Kundi C Uwanja Charles Konan Banny mjini Yamoussoukro, Ivory Coast. Mabao ya Simba wa Teranga yalifungwa na washambuliaji Ismaïla Sarr wa Marseille ya Ufaransa dakika ya 16, na nyota wanaocheza Saudi Arabia, Mouhamadou Habibou Diallo wa Al Shabab dakika ya 71 na Nahodha Sadio Mané wa Al Nassr dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Simba wa Teranga lilifungwa na wa Jean-Charles Victor Castelletto Nantes ya Ufaransa dakika ya 83. Mechi nyingine ya Kundi C, Guinea iliichapa Gambia 1-0, bao pekee la kiungo wa Atromitos ya Ugiriki, Aguibou Camara dakika ya 69 hapo hapo Uwanja Charles Konan Banny. Senegal ipo kileleni mwa Kund C kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Guinea yenye pointi nne, Cameroon pointi moja na Gambia ambayo haina pointi inashika mkia. Sasa Cameroon italazimika kuifunga Gambia mabao ya kutosh

TFF YAMSIMAMISHA KAZI AMROUCHE, CAF YAMFUNGIA

Image
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemsimamisha kazi Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mualgeria Adel Amrouche na kumteua mzalendo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuwa Kaimu Kocha Mkuu. Hatua ya TFF inafuatia Shirikisho la Soka Afrika kumfungia mechi nane Amrouche baada ya kutoa kauli zisizo za kiungwana dhidi ya Morocco kuelekea mchezo wa kwanza wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Jumatano wiki hii. Amrouche aliituhumu Morocco kuwa inajipangia muda wa kucheza mechi zake na marefa wa kuchezesha pia akilenga kuaminisha ni kwa sababu hiyo wanafanya vizuri. Simba wa Atlasi, Morocco wailifunga Tanzania, Taifa Stars 3-0 kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa Kundi F Jumatano Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro nchini Ivory Coast.  Mabao ya Simba wa Atlasi yalifungwa na beki wa Al-Shabab ya Saudí Arabia, Romain Ghanem Paul Saïss dakika ya 30, kiungo wa Marseille ya Ufaransa, Azzedine Ounahi na mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri dakika ya 80. Taifa Stars ilimaliza pungufu

TANZANIA YAJIFUNZA KWA IVORY COAST MAANDALIZI YA AFCON

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro ametembelea Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San Pedro, Ivory Coast ili kuona ambavyo nchi hiyo imefanya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu. Waziri Dk. Ndumbaro amefanya hivyo ili kujifunza namna ambavyo Ivory Coast wamefanikiwa naye ajifunze kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za mwaka 2027 ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa kushirikiana na Kenya na Uganda. Dk. Ndumbaro amesema aina ya uwanja aliouona unafaa pia katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo amesema Serikali mbali na kuendelea kujenga viwanja vya michezo Dodoma na Arusha inaendelea kukaribisha wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo katika ujenzi wa miundombinu ya michezo katika mikoa mingine.  Katika ziara hiyo, Dk. Ndumbaro aliambatana na Kaimu Balozi wa Kituo cha Abuja anayehudumia pia nchi ya Ivory Coast, Judika Nagunwa, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Ally Mayay na Maafisa wengine wa Wizara. PICHA: WAZIRI DK NDUM

SALAH AUMIA, MISRI YADROO NA GHANA, NIGERIA YAIZIMA IVORY COAST

Image
WAKATI Nigeria imeweka hai matumaini ya kwenda Hatua ya Mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu zinazoendelea nchini Ivory Coast, Ghana imejiweka njia panda. Nigeria ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ivory Coast katika mchezo wa Kundi A jana Uwanja Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan bao la mkwaju wa penalti la beki wa PAOK ya Ugiriki, William Paul Troost-Ekong dakika ya 56. Mechi nyingine ya Kundi A jana, Equatorial Guinea ilishinda 4-2 dhidi ya Guinea-Bissau hapo hapo Uwanja Olympique Alassane Ouattara. Sasa Equatorial Guinea wanaongoza Kundi A kwa wastani wa mabao dhidi ya Nigeria wote wakiwa na pointi nne, Ivory Coast pointi tatu nafasi ya tatu na Guinea-Bissau inashika mkia haina pointi. Mchezo pekee wa Kundi B jana ulimalizika kwa sare ya 2-2 baina ya Misri na Ghana Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan. Mabao ya Ghana yalifungwa na winga Mohammed Kudus wa West Ham United ya England yote dakika ya 45 na 71, wakati ya Misri yalifun

TAIFA STARS PUNGUFU YACHAPWA 3-0 NA MOROCCO AFCON

Image
TANZANIA imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi F usiku huu Uwanja wa Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro, Ivory Coast.  Mabao ya Simba wa Atlasi yamefungwa na beki wa Al-Shabab ya Saudí Arabia, Romain Ghanem Paul Saïss dakika ya 30, kiungo wa Marseille ya Ufaransa, Azzedine Ounahi na mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri dakika ya 80. Taifa Stars ilimaliza pungufu baada ya kiungo wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine Novatus Dismas Miroshi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

YANGA SC YAAJIRI MAAFISA WANNE WAPYA

Image
KLABU ya Yanga imeajiri Maafisa wanne wapya katika Idara tofauti kuziba nafasi za walioondoka na kuongeza nguvu ya utendaji katika maeneo mengine. Hao ni pamoja na Maafisa wawili wa Idara ya Wanachama na Mashabiki, Khamis Jecha na Jimmy Kindoki, Afisa Idara ya Habari na Mawasiliano, Willy Shemoka na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko, Ibrahim Samuel.

SIMBA SC YASAJILI BEKI WA TANZANIA PRISONS

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha beki Edwin Charles Balua (22) kuwa mchezaji wake mpya wa sita dirisha hili dogo kutoka Tanzania Prisons ya Mbeya. Wengine ni viungo wawili, Msenegal Babacar Sarr (26) kutoka US Monastir ya Tunisia na winga, Ladaki Juma Chasambi (19) kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro. Wapo pia washambuliaji, Muivory Coast Freddy Michael Kouablan (25) kutoka Green Eagles ya Zambia ambako alikuwa anaongoza kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo, Mgambia, Pa Omar Jobe (25) kutoka Zhenis ya Kazakhstani na Saleh Karabaka Kikuya (23) kutoka JKU ya Zanzíbar. Katika dirisha hili dogo Simba SC pia imeachana na washambuliaji wake wawili wa kigeni, Mkongo Jean Othos Baleke na Mzambia, Moses Phiri, hivyo kufanya jumla ya wachezaji sita iliyowaondoa dirisha hili dogo. Wengine ni wazawa viungo Jimson Stephen Mwanuke (24), Nassor Yahaya Kapama (27) na washambuliaji Shaaban Iddi Chilunda (25) na Mohamed Mussa Saleh (22).

NYOTA WA YANGA, DIARA NA AZIZ KI WAANZA NA SHANGWE AFCON

Image
NYOTA wa Yanga, kipa Djigui Diarra na kiungo Stephane Aziz Ki jana walianza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Ivory Coast baada ya timu zao kushinda mechi za kwanza za makundi yake. Aziz Ki alicheza kwa dakika 86 kabla ya kumpisha mshambuliaji wa  Amiens SC  ya Ligue2 Ufaransa, Boureima Hassane Bandé Burkina Faso ikishinda 1-0 dhidi ya Mauritania katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Bouake. Bao pekee la Burkina Faso lilfungwa kwa mkwaju wa penalti na mshambuliaji wa Aston Villa ya England, Bertrand Isidore Traoré dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya timu dakika 90 za kawaida za mchezo. Kwa upande wake, kipa Diarra alikuwa langoni mwanzo hadi mwisho wa mchezo wa Kundi E, akiiongoza Mali kushinda 2-0 dhidi ya Afrika Kusini Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo. Mabao ya Mali yalifungwa na beki wa  Real Sociedad ya Hispania,  Hamari Traoré dakika ya 60 na mshambuliaji wa  Auxerre , Lassine Fanta Mady Sinayoko dakika ya 66. Mapema dakika ya 19 msham

SIMBA SC YAWATEMA NA BALEKE NA PHIRI PIA

Image
KLABU ya Simba imeachana na washambuliaji wake wawili wa kigeni, Mkongo Jean Othos Baleke na Mzambia, Moses Phiri, hivyo kufanya jumla ya wachezaji sita iliyowaondoa dirisha hili dogo. Wengine ni wazawa viungo Jimson Stephen Mwanuke (24), Nassor Yahaya Kapama (27) na washambuliaji Shaaban Iddi Chilunda (25) na Mohamed Mussa Saleh (22). Ikumbukwe Simba imesajili wachezaji watano wapya dirisha hili dogo wakiwemo viungo wawili, Msenegal Babacar Sarr (26) kutoka US Monastir ya Tunisia na winga, Ladaki Juma Chasambi (19) kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro. Wengine wote ni washambuliaji, Muivory Coast Freddy Michael Kouablan (25) kutoka Green Eagles ya Zambia ambako alikuwa anaongoza kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo, Mgambia, Pa Omar Jobe (25) kutoka Zhenis ya Kazakhstani na Saleh Karabaka Kikuya (23) kutoka JKU ya Zanzíbar.

WAZIRI DK NDUMBARO AZUNGUMZA NA WACHEZAJI KABLA STARS KUIVAA MOROCCO KESHO

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo maalumu na kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kilichoweka kambi katika Jiji la San Pedro nchini Ivory Coast kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mashindano ya AFCON 2023 dhidi ya Morocco. Mhe. Ndumbaro amezungumza na wachezaji hao mara baada ya kushuhudia mazoezi na utayari wa kikosi hicho kuelekea mchezo wao na Timu ya Taifa ya Morocco utakaopigwa jijini humo Januari 17, 2024. Baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa muda wa takribani saa mbili, Waziri Dkt. Damas Ndumbaro amesema ameridhishwa na maandalizi ya kikosi hicho, Ari na morali ya wachezaji na benchi la ufundi ambayo inatoa picha nzuri ya kufanya vizuri katika kundi F la michuano hiyo. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Bw. Wallace Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) ambaye pia ni Mkuu wa msafara wa timu Bw. Suleiman Mahamoud Jabir. PICHA: KIKAO CHA WACHEZAJI NA WAZIRI DK NDU

SIMBA SC YAWAACHA WANNE KWA MIPIGO WAMO CHILUNDA NA MWANUKE

Image
KLABU ya Simba imeachana na wachezaji wake wanne, viungo Jimson Stephen Mwanuke (24), Nassor Yahaya Kapama (27) na washambuliaji Shaaban Iddi Chilunda (25) na Mohamed Mussa Saleh (22). Ikumbukwe Simba imesajili watano wapya dirisha hili dogo wakiwemo viungo wawili, Msenegal Babacar Sarr (26) kutoka US Monastir ya Tunisia na winga, Ladaki Juma Chasambi (19) kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro. Wengine wote ni washambuliaji, Muivory Coast Freddy Michael Kouablan (25) kutoka Green Eagles ya Zambia ambako alikuwa anaongoza kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo, Mgambia, Pa Omar Jobe (25) kutoka Zhenis ya Kazakhstani na Saleh Karabaka Kikuya (23) kutoka JKU ya Zanzíbar.

YANGA SC YAACHANA NA WINGA 'MTAALAMU' JESUS MOLOKO

Image
KLABU ya Yanga imeachana na winga, Jesus Ducapel Moloko baada ya misimu miwili na nusu tangu ajiunge nayo Agosti mwaka 2021 akitokea AS Vita ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

MABINTI 25 WAITWA SERENGETI GIRLS YA KUIVAA ZAMBIA KOMBE LA DUNIA

Image
KOCHA Bakari Nyundo Shime ameteua wachezaji 25 kuunda timu ya taifa ya wasichana kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Zambia kufuzu Kombe la Dunia.

CAPE VERDE YAIDUWAZA GHANA, NIGERIA NA MISRI ZASAWAZISHA KUPATA SARE

Image
  BAO la dakika ya 90 na ushei la winga wa Ankaragücü ya Uturuki, Garry Mendes Rodrigues liliiwezesha Cape Verde kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ghana katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika jana Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan.  Cape Verde ilitangulia kwa bao la dakika ya 17 la kiungo waSan Jose Earthquakes ya California, Marekani Jamiro Gregory Monteiro Alvarenga, kabla ya Alexander Djiku kuisawazishia Ghana dakika ya 56. Mechi nyingine ya Kundi B jana, Misri ilitoa sare ya 2-2 na Msumbiji hapo hapo Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny, mabao ya Mamba yakifungwa na mawinga, Witiness Chimoio João Quembo 'Witi'  wa Nacional ya Ureno na Clésio Palmirim David Baúque wa Gabala ya Azerbaijani.  Sasa Cape Verde inaongoza Kundi B kwa pointi zake tatu, ikifuatiwa na Misri na Msumbiji zenye pointi moja kila moja, wakati Ghana inaanzia nyuma ya timu zote hizo. Mapema jana ulipigwa mchezo wa Kundi A Nigeria ikilazimisha sare ya 1-1 na Equatorial Guinea, 

MLANDEGE MABINGWA TENA KOMBE LA MAPINDUZI, MNYAMA CHALI ZENJI

Image
WENYEJI, Mlandege SC imefanikiwa kutetea ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba ya Dar es Salaam usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji mpya, Joseph Akandwanaho kutoka Mbarara City ya kwao, Uganda aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 54.

CHELSEA YAICHAPA FULHAM 1-0 STAMFORD BRIDGE

Image
  WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham bao pekee la Cole Palmer kwa penalti dakika ya 45 na ushei katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya nane, wakati Fulham inabaki na pointi zake 24 za mechi 21 pia nafasi ya 13.

NGUSHI APELEKWA KWA MKOPO COASTAL UNION HADI MWISHO WA MSIMU

Image
KLABU ya Yanga imempeleka mshambuliaji wake, Crispin Ngushi Mhagama Coastal Union ya Tanga kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu. Taarifa ya Yanga leo imesema; "Mchezaji wetu anajiunga na Coastal Union kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu,". Ngushi alijiunga na Yanga dirisha dogo la Januari 8, mwaka 2022 kutoka Mbeya Kwanza ameshindwa kuwavutia makocha wa timu hiyo kwa kipindi hicho cha miaka miwilia kuanzia Mtunisia Nasreedin Nabi na hata sasa Muargentina, Miguel Gamondi.

DIARRA NA MALI WALIVYOWASILI IVORY COAST KWA AJILI YA AFCON

Image
KIPA wa Yanga SC, Djigui Diarra akiteremka kwenye Ndege baada ya kuwasili na timu yake ya taifa, Mali mjini Korhogo nchini Ivory Coast kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kuanza kesho nchini humo. Mali itaanza na Afrika Kusini Januari 16 katika mchezo wa Kundi E, kabla ya kumenyana na Tunisia Januari 20 Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly na kumaliza na kumalizia na Namibia Uwanja wa Laurent Pokou. PICHA: DIARRA NA MALI WALIVYOWASILI IVORY COAST KWA AJILI YA AFCON

MSUVA NA SAMATTA WANAVYOJIPANGA KUIPIGANIA TAIFA STARS AFCON

Image
NYOTA wa timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva (kushoto) na Nahodha, Mbwana Samatta wakifanya mazoezi ya viungo Gym Jijini San Pedro nchini Ivory Coast kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Morocco Januari 17. Wapinzani wengine wa Taifa Stars Kundi F ni Zambia watakaocheza nao Januari 21 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watakaomenyana nao Januari 24. PICHA: TAIFA STARS WAKIJIFUA GYM IVORY COAST KUJIANDAA KUIVAA MOROCCO AFCON 

LIVERPOOL YAICHAPA FULHAM 2-1 CARABAO CUP ANFIELD

Image
TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup usiku wa jana Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool. Mabao ya Liverpool yalifungwa na Curtis Jones dakika ya 68 na Cody Gakpo dakika ya 71 kufuatia Willian kuanza kuifungia Fulham dakika ya 19. Timu hizo zitarudiana Januari 24 Uwanja wa Craven Cottage Jijini London na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Chelsea na Middlesbrough katika Fainali. Mechi ya kwanza Middlesbrough ilishinda 1-0 juzi Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough na timu hizo zitarudiana Januari 23 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.

SIMBA SC YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI KWA MATUTA

Image
TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada y ushindi wa penalti 3-2 dhidi ya Singida Fountain Gate leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. Singida Fountain Gate ilitangulia kwa bao la mshambuliaji Mkenya Elvis Rupia dakika ya 11, kabla ya kiungo Mkongo Fabrica Luamba Ngoma kuisawazishia Simba SC dakika ya 90 na ushei. Na kwenye mikwaju ya penalti kipa wa Simba SC, Ali Salim aliyeokoa penalti za mabeki Gardiel Michael, Hamad Waziri na mshambuliaji Mnyarwanda Meddie Kagere kuipa Simba tiketi ya Fainali Kombe la Mapinduzi. Waliofunga penalti za Simba ni viungo Luis Jose Miquissone, raia wa Msumbiji, Israel Patrick Mwenda na Moses Phiri, wakati ya Shomari Kapombe iliokolewa na ya Mrundi, Saido Ntibanzokiza ikagonga mwamba wa juu na kwenda nje. Ni viungo, Mkenya Duke Abuya na mzawa, Deus Kaseke pekee waliofunga upande wa Singida Fountain Gate.

TAIFA STARS IKIJIWEKA NA MECHI YA UFUNGUZI AFCON DHIDI YA MOROCCO

Image
NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta akiwa mazoezini Jijini San Pedro nchini Ivory Coast kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Morocco Januari 17. Wapinzani wengine wa Taifa Stars Kundi F ni Zambia watakaocheza nao Januari 21 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watakaomenyana nao Januari 24. PICHA: TAIFA MAZOEZINI IVORY COAST KUJIANDAA NA AFCON

CHELSEA YACHAPWA 1-0 NA MIDDLESBROUGH KOMBE LA LIGI ENGLAND

Image
WENYEJI, Middlesbrough wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea usiku wa jana katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Hayden Hackney dakika ya 37 na sasa timu hizo zitarudiana Januari 23 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London na mshindi wa jumla atakwenda Fainali ya michuano hiyo. Nusu Fainali nyingine ya Carabao Cup ni leo kati ya Liverpool na Fulham Uwanja wa Anfield kabla ya timu hizo kurudiana Januari 24 Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.

MLANDEGE YATINGA FAINALI KWA MATUTA KOMBE LA MAPINDUZI

Image
MABINGWA watetezi, Mlandege SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 New Amaan Complex, Zanzíbar. Shujaa wa Mlandege leo kwa mara nyingine amekuwa kipa wake Othman Hassan aliyeokoa penalti mbili za wachezaji wa APR, Sharaf Shiboub na Ramadhan Niyibizi, huku za Eric Ndayishimiye na Soulei Sanda pekee zikimpita. Waliofunga penalti za Mlandege ni Mjamaica Malik Zidan, Emanuel Pius, Said Mussa Said na Mganda Arafat Galiwango, huku mkwaju wa Yussuf Suleiman Hajji ‘Jusa’ ukiokolewa na kipa Pierre Ishimwe wa APR. Sasa Mlandege itasubiri kukutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya Simba SC na Singida Fountain Gate hapo hapo New Amaan Complex.

MAN UNITED YASONGA MBELE KOMBE LA FA ENGLAND

Image
TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Raundi ya Nne ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Wigan Athletic jana Uwanja wa DW mjini Wigan. Mabao ya Manchester United yamefungwa na Diogo Dalot dakika ya 22 na Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya 74 na kwa ushindi huo kikosi cha Kocha Mholanzi, Erik ten Hag kitakutana na mshindi kati ya Newport County na Eastleigh.