LIVERPOOL YAICHAPA BOURNEMOUTH 4-0 NA KUJIWEKA SAWA KILELENI ENGLAND
TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vitality mjiki Bournemouth, Dorset.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Darwin Nunez mawili dakika ya 49 na 90 na ushei na Diogo Jota dakika ya 70 na 79.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 48 katika mchezo wa 21 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wana mchezo mmoja mkononi.
Kwa upande wao, Bournemouth wanabaki na pointi zao 25 za mechi 20 nafasi ya 12.
Comments
Post a Comment