Posts

Showing posts from July, 2023

TABORA UNITED YAMSAJILI KIPA WA ENYIMBA YA NIGERIA

Image
KLABU ya Tabora United iliyopanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kama Kitayosce imemsajili kipa John Noble Barinyima (30) kutoka Enyimba International ya kwao, Nigeria.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA HAMZA MANENO, KIUNGO WA ZAMANI WA SIMBA

Image
 

MSHAMBULIAJI MPYA YANGA AANZIA KUJIFUA GYM KIGAMBONI

Image
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga SC, Hafiz Konkoni akiwa mazoezini kwenye kambi ya timu hiyo, Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya baada ya kusajiliwa mwishoni mwa wiki kutoka Bechem United ya kwao, Ghana. PICHA: HAFIZ KONKONI AKIJIFUA GYM

SIMBA SC YASHINDA 4-1 MECHI YA KIRAFIKI KAMBINI UTURUKI

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya timu ya Batman Petrolspor katika mchezo wa kirafiki kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu mjini Ankara nchini Uturuki. Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Soğuksu Spor Kompleksi, mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mcameroon, Willy Essomba Onana, kiungo Mrundi Saido Ntibanzokiza, beki Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na mshambuliaji na Nahodha John Raphael Bocco. Huo ulikuwa mchezo wa nne kwa Simba katika kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Uturuki, baada ya Alhamisi kucheza mechi mbili na Turan FK ya Turkmenistan na kushinda 2-0 kabla ya kufungwa 1-0, wakati mechi nyingine walitoa sare ya 1-1 na Zira FK ya  Azerbaijan Julai 24. Batman Petrolspor ni timu inayoshiriki Lig 3 ambayo ni ngazi ya nne katika mfumo wa ligi za Uturuki, baada ya Süper Lig, Lig 1 na Lig 2 na mafanikio yake makubwa kihistoria ni kucheza Lig 2 pekee.

YANGA YASAJILI MSHAMBULIAJI MPYA KUTOKA GHANA

Image
KLABU ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji Hafiz Wontah Konkoni (23) kutoka Bechem United ya kwao, Ghana kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao. Huyo anakuwa mchezaji mpya wa nane baada ya mabeki Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate, Gift Freddy kutoka SC Villa ya Uganda, Kouassi Attohoula Yao, viungo, Peodoh Pacôme Zouzoua wote kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Wengine ni viungo Jonás Mkude kutoka Simba SC, Mahlatse Skudu Makudubela kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini na Maxi Mpia Nzengeli kutoka AS Maniema Union ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). VIDEO: UTAMBULISHO WA HAFIZ WONTAH KONKONI YANGA SC

YANGA YASHINDA 10-0 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI LEO

Image
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya timu ya Magereza katika nchezo wa kirafiki kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu huko Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Kennedy Musonda na Clement Mzize kila mmoja matatu, Pacôme Zouzoua, Skudu Mahlatsi Makudubela, Stephane Aziz Ki na Maxi Mpia Nzengeli. Huo ni mchezo wa pili tu wa kujipima kwa Yanga baada ya Julai 22 kuibuka na ushindi wa 1-0, bao la Musonda dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.

YANGA YAMUUZA BANGALA KWA AZAM FC, ASAINI MIAKA MIWILI

Image
KIUNGO wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Yanick Litombo Bangala amejiunga na klabu ya Azam FC kutoka Yanga, zote za Dar es Salaam. Taarifa ya Azam FC leo imesema; “Tumefikia makubaliano na klabu ya Yanga ya kumnunua, mchezaji kiraka, Bangala na amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufuzu vipimo vya afya,”.

AZAM FC MABINGWA TENA LIGI YA VIJANA U17

Image
TIMU ya Azam FC jana imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa mara ya pili mfululizo. Hiyo ni kufuatia sare tasa ya wapinzani wao wa karibu, Yanga SC dhidi ya Mbeya Kwanza jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam baada ya Azam FC kushinda 4-0 dhidi ya African Sports, katika mchezo uliotangulia. Azam FC iliingia kwenye mchezo huo ikiwa mbele kwa pointi tatu dhidi ya Yanga na baada ya matokeo ya jana sasa inaongoza kwa pointi tano kuendelea mechi moja moja za mwisho.

PAMBANO LA NGUMI LA KIMATAIFA LIVE TV 3 KESHO

Image
MABONDIA pambano la Bongo Fighting Championship (BFC) wakamilisha zoezi la Kupima uzito na Afya zao huku bondia wakike nchini Tanzania afunguka mazito mara baada ya kukutana Uso kwa uso na Mpinzani wake Homakoma.  Zoez hilo la kupima uzito limefanyika mapema leo Julai 28,2023 katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam na mabondia mbalimbali kujitokeza kwa zoezi hilo la uthibitisho wa awali kabla ya kupanda ulingoni ambapo Muasisi wa pambano hilo  Scott Farrel amepima uzito kuelekea pambano la kirafiki dhidi ya mpinzani wake  Marcus Warry,Abdul ubaya dhidi ya Ivan Maguma wakati Musa dragon dhidi ya Amos kutoka Kenya wakati  Ajemi amani dhidi Khamis msondo, Huku pambano la Muhaythai pambano kuu ni Emmanuel shija dhidi ya Yusuph Fundi a.k.a Jet Lee. Aidha,Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema wamejipanga kurusha maudhui yote yatakayojiri katika pambano hilo ambapo ameongeza kuwa mengi mazuri yanakuja mwezi septemba huku akihaidi kuwa Kampuni haitaacha

SINGIDA BIG STARS NA AS VITA AGOSTI 2 LITI

Image
TIMU ya Singida Fountain Gate itacheza mchezo wa kirafiki na As Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Agosti 2, mwaka huu Uwanja wa Liti, Singida katika tamasha la Singida Big Day.

EDWARD CHARLES MANYAMA BAADA YA MATIBABU TUNISIA

Image
BEKI wa kushoto wa Azam FC, Edward Charles Manyama akiwa amefungwa kinga mkononi baada ya kuumia juzi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Club Tunisien nchini iTunisia ambako klabu yake imeweka kambi ya kujiandaa na msimu. PICHA: EDWARD MANYAMA BAADA YA MATIBABU TUNISIA

YANGA SC WANAVYOENDELEA KUJIFUA KWENYE KAMBI YAO KIGAMBONI

Image
KIKOSI cha Yanga SC kinaendelea na mazoezi kwenye kambi yake ya Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya. PICHA: WACHEZAJI YANGA MAZOEZINI KIGAMBONI VIDEO: WACHEZAJI YANGA MAZOEZINI KIGAMBONI

KLABU YA WEST ARMENIA YASAJILI WACHEZAJI WAWILI WA TANZANIA

Image
KLABU ya West Armenia FC ya is an Armenia imesajili wachezaji wawili wa Tanzania kiungo Erick Edson Mwijage kutoka Kagera Sugar na mshambuliaji Yusuph Athumani Shaaban kutoka Yanga SC. Klabu ya mjini Yerevan inajipanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Armenia na sasa inaimarisha kikosi chake kwa kusajili nyota wapya kutoka nchi tofauti.

SIMBA SC YACHAPWA 1-0 NA TURAN FK LEO UTURUKI

Image
KLABU ya Simba imepoteza mechi ya Kwanza katika kambi yake ya kujiandaa na msimu mjini Ankara nchini Uturuki baada ya kuchapwa 1-0 na Turan FK ya Turkmenistan, bao la dakika ya nne la Roderik Miller jioni ya leo. Huo ulikuwa mchezo wa marudiano baina ya timu hizo baada ya mchana wa leo Simba kushinda 2-0, mabao ya Kibu Dennis na Nahodha, John Raphael Bocco. Kwa ujumla Simba imekwishacheza mechi nne kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Uturuki baada ya sare ya 1-1 na Zira FK ya  Azerbaijan Julai 24. Turkmenistan ni nchi inayopatikana Asia ya Kati ikiwa imepakana na Kazakhstan upande wa Kaskazini Magharibi na Uzbekistan kwa Kaskazini Mashariki, ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 138 kwenye renki za FIFA ikiwa chini ya Tanzania ambayo ipo nafasi ya 123.

SIMBA YAICHAPA 2-0 TIMU YA TURKMENISTAN MECHI YA KIRAFIKI LEO

Image
MABAO ya Kibu Dennis na Nahodha, John Raphael Bocco yameipa Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Turan FK ya Turkmenistan katika mchezo wa kirafiki leo mjini Ankara nchini Uturuki. Huo ulikuwa nchezo wa pili wa kirafiki katika kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Uturuki baada ya sare ya 1-1 na Zira FK ya  Azerbaijan Julai 24 na baadaye Saa 12:00 jioni timu hizo zitarudiana hapo hapo Ankara. Turkmenistan ni nchi inayopatikana Asia ya Kati ikiwa imepakana na Kazakhstan upande wa Kaskazini Magharibi na Uzbekistan kwa Kaskazini Mashariki, ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 138 kwenye renki za FIFA ikiwa chini ya Tanzania ambayo ipo nafasi ya 123.

AZAM FC YACHAPWA 3-1 NA STADE TUNISIEN MECHI YA KIRAFIKI LEO TUNISIA

Image
TIMU ya Azam FC imechapwa mabao 3-1 na Stade Tunisian katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Pac Hedi Enneifer mjini Bardo nchini Tunisia. Bao pekee la Azam FC iliyoweka kambi mjini Sousse nchini Tunisia kujiandaa na msimu mpya limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 53. Huo ni mchezo wa pili Azam FC wanafungwa kati ya minne waliyocheza baada ya awali kufungwa 3-0 na Esperance huku wao wakishinda mechi mbili, 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan na 2-1 dhidi ya wenyeji wengine, US Monastir.

WIZARA YA MICHEZO YAKUTANA NA MARAIS WA NCHI WANACHAMA CECAFA DAR

Image
KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amekutana na Marais wa Mashirikisho ya Mpira wa Miguu ya nchi wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambapo amewaomba kuiunga mkono Tanzania, Kenya na Uganda ambazo  zinaomba kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa  Miguu Afrika (CAF) 2027. Marais walioshiriki kikao hicho ni Wales Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambaye ni Rais wa CECAFA sasa,  Augustino Maduot, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Sudan Kusini, Paulos Andromariam, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Eritrea, Isayas Jiral, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ethiopia, Doris Petra Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya pamoja na watendaji wakuu wa CECAFA Bw. Mossi Yusuf Meneja wa Mashindano CECAFA na Auka Gocheo Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA. Kikao hicho  kimefanyika kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Tanzania na Burundi ambayo imechezwa Julai 25, 2023 k

TANZANIA YAANZA VYEMA MICHUANO YA MABINTI CECAFA U18 CHAMAZI

Image
WENYEJI, Tanzania wameanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa mabinti chini ya umri wa miaka 18 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya  Burundi leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mechi nyingine ya leo, Uganda wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ethiopia hapo hapo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

HABIB KONDO KOCHA MPYA WA NTIBWA SUGAR

Image
KLABU ya Mtibwa Sugar imemtambulisha Habib Kondo kuwa kocha wake mpya kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

YANGA KUANZIA DJIBOUTI, SIMBA NAMIBIA AU ZAMBIA, AZAM...

Image
DROO ya Raundi za awali za michuano ya klabu imepangwa makao ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Jijini Cairo nchini Misri na mabingwa wa Tanzania, Yanga wataanza na Asas ya Djibouti. Wakifanikiwa kuitoa timu hiyo ya Djibouti, Yanga SC watakutana na mshindi wa jumla kati ya kati ya Otoho ya Kongo Brazzaville na El Mereikh ya Sudan kuwania tiketi ya makundi. Simba SC itaanzia Raundi ya Pili ya mchujo moja kwa moja kuwania kuingia hatua ya makundi kwa kumenyana na mshindi kati ya African Stars ya Namibia na Power Dynamos ya Zambia ambayo watacheza nayo kwenye Simba Day. Kwa upande wao mabingwa wa Zanzibar, KMKM watamenyana na St George ya Ethiopia, mtihani ambao ikiuvuka itakutana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri. Katika Kombe la Shirikisho, Singida Big Stars wataanza na JKU ya Zanzibar, huku Azam FC wakimenyana na Bahir Dar ya Ethiopia. Azam FC ikifuzu itamenyana na Club Africain ya Tunisia, wakati Singida Fountain Gate ikipita itakutana na Future ya Misri.

SIMBA SC KUMENYANA NA POWER DYNAMOS KWENYE SIMBA DAY

Image
KLABU ya Simba itamenyana na Power Dynamos FC ya Zambia katika tamasha la Simba Day Agosti 6 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

CEDRIC KAZE NDIYE KOCHA MPYA MKUU NAMUNGO FC

Image
KLABU ya Namungo FC imemtambulisha Mrundi, Cedric Kaze kuwa kocha wake Mkuu kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Kaze anajiunga na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi baada ya kufanya kasi Yanga kwa awamu mbili, kwanza kama Kocha Mkuu na baadaye Kocha Msaidizi hadi msimu uliopita.

SIMBA SC YAMUUZA SAKHO TIMU YA LIGUE 2 UFARANSA

Image
KLABU ya Simba SC imefikia makubaliano na klabu ya  Union Sportive Quevillaise-Rouen Métropole  ya nchini Ufaransa kumnunua mchezaji wake, Msenegal Pape Ousmane Pape Ousmane Sakho. Winga huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Simba SC Agosti mwaka 2021 akitokea Teungueth FC ya kwao, Senegal na baada ya misimu miwili mizuri anaondoka Msimbazi. Union Sportive Quevillaise-Rouen Métropole, inayofahamika zaidi kama US Quevilly-Rouen, ama US Quevilly, au QRM ni timu inayoshiriki Ligi ya pili kwa ukubwa nchini Ufaransa, Ligue 2.

KIPA MPYA WA SIMBA MBRAZIL JEFFERSON LUIS AANZA MAZOEZI UTURUKI

Image
KIPA mpya wa Simba, Mbrazil Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior akidaka mpira kwa ustadi kwenye mazoezi ya timu hiyo kufuatia kuripoti kambini mjini Ankara nchini Uturuki kwenye kambi ya timu hiyo kujiandaa na msimu. PICHA: JEFFERSON LUIS MAZOEZINI SIMBA SC UTURUKI 

KAIZER CHIEFS WAMTEMBELEA RAIS MWINYI IKULU ZANZÍBAR

Image
KIKOSI cha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambacho kipo nchini kwa mwaliko wa klabu ya Yanga leo kimemtembelea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi Ikulu visiwani humo. PICHA: ZIARA YA KAIZER CHIEFS ZANZIBAR 

SIMBA SC YAMTAMBULISHA KIPA MPYA KUTOKA BRAZIL

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha mlinda mlango Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior kutoka Resende ya kwao, Brazil kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao. Jefferson Luis Szerban de Oliveira Junior anakwenda kuwa kipa wa nne kwenye kikosi cha Simba baada ya Aishi Manula, Ally Salum na Ally Ferouz. Kwa ujumla anakuwa mchezaji mpya wa 10 mpya kwenye kikosi cha Simba wakiwemo Wacameroon wawili, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotton Sport ya kwao na kiungo mshambuliaji, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda. Wengine wapya Simba ni kiungo Mkongo Fabrice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan, mawinga José Luis Miquissone kutoka Al Ahly ya Misri na Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast. Kuna wazawa wanne ambao beki wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ kutoka Mtibwa Sugar, beki wa katí, Hussein Kazi kutoka klabu ya Geita Gold, kiungo Abdallah Hamisi Riziki kutoka Orapa United FC ya Botswana na mshambuliaji wa zamani wa Azam FC Shaab

AZAM FC YAICHAPA MONASTIR 2-1 MECHI YA KIRAFIKI TUNISIA

Image
KLABU ya Azam FC kesho imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, US Monastir katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini Monastir nchini Tunisia. Mabao ya Azam FC iliyoweka kambi mjini Sousse nchini Tunisia kujiandaa na msimu yamefungwa na viungo Mghana, James Akaminko dakika ya 13 na Mguinea Djibril Sillah dakika ya 39 baada ya Monastir kusawazisha. Huo ni mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Azam FC kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mjini Sousse nchini Tunisia baada ya awali kushinda 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan Julai 14 na kufungwa 3-0 na wenyeji, Esperance Julai 19.

YANGA YAICHAPA KAIZER CHIEFS 1-0 DAR BAO PEKEE LA MUSONDA

Image
BAO pekee la mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda dakika ya 45 na ushei limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. VÍDEO: BAO PEKEE LA KENNEDY MUSONDA DHIDI YA KAIZER CHIEFS 

MAYELE, BANGALA NA DJUMA SHABANI KWAHERI YANGA SC

Image
NYOTA watatu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), beki Djuma Shabani, kiungo Yanick Bangala na Fiston Kalala Mayele historia yao imefungwa Yanga baada ya misimu miwili. Wachezaji hao na beki Mmali, Mamadou Doumbia hawajatambulishwa kama sehemu ya kikosi cha Yanga cha msimu mpya kwenye Siku ya Mwananchi jioni hii klabu hiyo ikimenyana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mayele anahusishwa na kuhamia Pyramids ya Misri, wakati Djuma Shabani na Bangala wanaweza kurejea klabu za kwao, TP Mazembe ya Lubumbashi na AS Vita ya Kinshasa. Hiki ndio kikosi kizima kipya cha Yanga msimu wa 2023-2024

SIMBA SC YAMREJESHA RASMI ‘MTU MBAYA’ LUIS MIQUISSONE

Image
KLABU ya Simba imemrejesha kiungo wake mshambuliaji wa Kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone ambaye amevunja mkataba na Al Ahly ya Misri baada ya miaka miwili tangu ajiunge nayo. Miquissone alijiunga na Simba SC Januari mwaka 2020 akitokea UD Songo ya kwao, Msumbiji ambako alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kabla ya Agosti mwaka 2021 kununuliwa na Al Ahly akisaini mkatab wa miaka minne. Baada ya kutua Al Ahly, Miquissone hakufanikiwa kuendeleza makali yake aliyokuwa nayo Simba na kufika Septemba 2, mwaka jana akatolewa kwa mkopo Abha ya Saudi Arabia. Akiwa Abha mambo hayakumuendea vizuri Miquissone, kwani katika kipindi chote cha msimu amecheza mechi nne na hajafanikiwa kufunga hata bao moja na kwa sasa anahusishwa na taarifa za kurejea Simba SC. Luis Jose Miquissone anakamilisha idadi ya wachezaji tisa wapya Simba katika dirisha hili, kati yao watani wa kigeni wakiwemo Wacameroon wawili, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotto

MOROCCO KOCHA MPYA GEITA GOLD, TIMU KUJIFUA RWANDA

Image
KLABU ya Geita Gold imemuajiri Mzanzibari, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kuwa kocha wake mpya Mkuu akichukua nafasi ya Freddy Félix Minziro aliyehamia Tanzania Prisons ya Mbeya. Katika hatua nyingine, Geita Gold wametoka programu yao ya maandalizi ya msimu mpya ambayo yanahusisha ziara ya mechi za kirafiki nchini Rwanda.

AZAM FC KUCHEZA NA US MONASTIR KESHO TUNISIA

Image
KLABU ya Azam FC kesho itamenyana na wenyeji, US Monastir katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini n Monastir nchini Tunisia kuanzia Saa 3:00 usiku kwa saa za nyumbani, Tanzania. Huo utakuwa mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Azam FC kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mjini Sousse nchini Tunisia baada ya awali kushinda 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan Julai 14 na kufungwa 3-0 na wenyeji, Esperance Julai 19.

MISS TANZANIA 2023 KUONDOKA NA BENZ NA SH MILIONI 10 LEO MASAKI

Image
WAREMBO 20 wabaki vinywa wazi mara baada ya kutangazwa rasmi zawadi ya Miss Tanzania   gari aina ya Mercedes benz yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 za Kitanzania pamoja na pesa taslim  Milioni 10 kwa atakaeibuka Mshindi Usiku wa Leo  katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.  Akizungumza na Wanahabari wakati wa kutambulisha zawadi hiyo. Jijini Dar es salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa, amesema kuwa Fainali ya Miss Tanzania  itapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa warembo wenyewe huku akisisitiza kuwa Fainali hiyo itakuwa ya kitofauti kutokana na kupangika kwa matukio ya kiburudani zaidi. "Nilipata nafasi ya kupita kambini kushuhudia mazoezi ya Fainali ya Miss Tanzania kutoka kwa washiriki wenyewe Kiukweli kuna hatari watu wanajifua namna ya kutembea jukwaani (catwalk) zaidi ya Mrembo Halima Kopwe (Miss Tanzania 2021) lipieni ving'amuzi mshuhudie burudani hiyo kupitia chaneli ya  St bongo ndani ya Startimes. " Malisa amewas

KOCHA MPYA YANGA AAHIDI SOKA YA KUVUTIA DHIDI YA KAIZER CHIEFS KESHO

Image
KOCHA mpya wa Yanga SC, Muargentina Miguel Angel Gamondi ameahidi mchezo wa kuvutia kesho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Akizungumza leo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Gamondi amesema kwamba watajaribu kucheza vizuri ili kuwapa furaha mashabiki. "Tunatarajia kuwa na malengo makubwa zaidi kwa sababu hii ni klabu kubwa yenye mashabiki wengi wenye nguvu na ushawishi kutaka klabu hii iendelee kufanya vizuri zaidi hasa kwenye mashindano ya kimataifa," amesema Gamondi. Gamondi kwa upande wa timu bado wapo kwenye maandalizi na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs watautumia kama sehemu ya maandalizi yao kuelekea msimu mpya.   "Kesho ni siku kubwa kwa mashabiki wa Yanga pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherehekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania klabu hii kubwa yenye

KAIZER CHIEFS WAWASILI DAR TAYARI KUIKABILI YANGA KESHO MKAPA

Image
KIKOSI cha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kimewasili Alfajiri ya leo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao, Yanga SC kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi kesho jioni Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. VÍDEO: KAIZER CHIEFS WAKIWASILI DAR LEO

AZAM FC WANAVYOJIFUA KWENYE KAMBI YAO YA KUJIANDAA NA MSIMU TUNISIA

Image
MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC, Msenegal Alassane Diao akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo Alhamisi mjini Sousse nchini Tunisia katika kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya. PICHA: WACHEZAJI WA AZAM FC MAZOEZINI TUNISIA 

YAMGA SC WANAVYOJIANDAA KUIKABILI KAIZER CHIEFS JUMAMOSI DAR

Image
KIUNGO wa Kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho akiwa kwenye mazoezi ya Yanga leo Uwanja wa Avic Town, eneo la Somangira, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya. Yanga inatarajiwa kuuzindua msimu wake mpya kwa kumenyana na vigogo wa Afrika Kusini, Kaizer Chiefs Jumamosi Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. PICHA: WACHEZAJI WA YANGA SC MAZOEZINI LEO KIGAMBONI 

AZAM FC YAACHIA JEZI MPYA ZA 2023-2024 KITU BAGAMOYO SUGAR

Image
HATIMAYE Azam FC imeonyesha jezi zake tatu za msimu mpya zenye mvuto wa kiwango cha juu, zikiwa na nembo ya bidhaa mpya ya Bakhresa Group Limited, Bagamoyo Sugar.

KOPUNOVIC ALIYEWAHI KUINOA SIMBA SC ATUA TABORA UNITED

Image
ALIYEWAHI kuwa kocha wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic amejiunga na klabu ya Tabora United ya Tabora iliyopanda Ligi Kuu ya NBC kama Kitayosce FC. Goran Kopunovic (56) ni kocha mwenye uzoefu aliyeanzia kwenye kucheza kama mshambuliaji nyumbani kwao, Serbia kabla ya kuja Afrika ambako amefundisha timu za Polisi ya Rwanda katí ya 2010 na 2013 na Simba SC ya Dar es Salaam mwaka 2015. Baada ya hapo alirejea kwao, Serbia kabla ya kwenda Hungary kufundisha timu ya BFC Siófok katí ya 2015 na 2017 na Salavan ya Urusi hadi mwaka jana na sasa anarejea Tanzania kwa awamu ya pili.

AZAM FC YACHAPWA 3-0 NA ESPERANCE MECHI YA KIRAFIKI LEO TUNISIA

Image
TIMU ya Azam FC imechapwa Mabao 3-0 na wenyeji, Esperance katika mchezo wa kirafiki leo kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Tunisia. Mechi ya kwanza ya kujipima nguvu Ijumaa iliyopita, Azam FC iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan Jijini Tunis.

MEYA WA KIZILCAHAMAM ATEMBELEA MAZOEZI YA SIMBA UTURUKI

Image
MEYA Süleyman Acar wa Manispaa ya Kızılcahamam, jimbo Ankara ambako Simba SC imeweka kambi, leo ametembelea mazoezi ya jioni ya timu hiyo na kukutana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi, kabla ya kukabidhiwa zawadi na Nahodha John Bocco.  VÍDEO: MEYA WA KIZILCAHAMAM ALIPOTEMBELEA MAZOEZI YA SIMBA LEO UTURUKI 

KOCHA MPYA YANGA AJITOKEZA KWENYE KUCHANGIA DAMU MLOGANZILA

Image
RAIS wa Yanga SC, Hersi Ally Said (kushoto) na Kocha Mkuu, Muargentina Miguel Angel Gamondi wamewatembelea wapenzi wa klabu hiyo waliojitokeza kuchangia damu katika hospitali ya Mloganzila Jijini Dar es Salaam kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi Jumamosi. PICHA: WANAYANGA WALIOJITOKEZA KUCHANGIA DAMU