SIMBA SC YAMREJESHA RASMI ‘MTU MBAYA’ LUIS MIQUISSONE



KLABU ya Simba imemrejesha kiungo wake mshambuliaji wa Kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone ambaye amevunja mkataba na Al Ahly ya Misri baada ya miaka miwili tangu ajiunge nayo.
Miquissone alijiunga na Simba SC Januari mwaka 2020 akitokea UD Songo ya kwao, Msumbiji ambako alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kabla ya Agosti mwaka 2021 kununuliwa na Al Ahly akisaini mkatab wa miaka minne.
Baada ya kutua Al Ahly, Miquissone hakufanikiwa kuendeleza makali yake aliyokuwa nayo Simba na kufika Septemba 2, mwaka jana akatolewa kwa mkopo Abha ya Saudi Arabia.
Akiwa Abha mambo hayakumuendea vizuri Miquissone, kwani katika kipindi chote cha msimu amecheza mechi nne na hajafanikiwa kufunga hata bao moja na kwa sasa anahusishwa na taarifa za kurejea Simba SC.
Luis Jose Miquissone anakamilisha idadi ya wachezaji tisa wapya Simba katika dirisha hili, kati yao watani wa kigeni wakiwemo Wacameroon wawili, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotton Sport ya kwao na kiungo mshambuliaji, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
Wageni wengine waliosajiliwa Simba ni kiungo Mkongo Fabrice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan, winga wa kushoto na Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast.
Na wazawa wanne ni beku wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ kutoka Mtibwa Sugar, beki wa katí, Hussein Kazi kutoka klabu ya Geita Gold, kiungo Abdallah Hamisi Riziki kutoka Orapa United FC ya Botswana na mshambuliaji wa zamani wa Azam FC Shaaban Iddi Chilunda.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA