Posts

Showing posts from October, 2021

SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA COASTAL

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Timu zote zilimaliza pungufu baada ya mchezaji mmoja kila upande kutolewa kwa kadi nyekundu, wakianza Coastal kumpoteza Benedictor Jacob Mwamlangwa dakika ya 29, kabla ya Simba kumpoteza beki wake Mkongo, Hennock Inonga Baka dakika ya 90. SIimba SC inafikisha pointi nane na Coastal imetimiza pointi tatu katika mchezo wa nne kila timu.

SPORTSPESA ILIVYOBADILI TASWIRA YANGA SC

Image
NDANI ya miaka minne tu, kampuni maarufu zaidi nchini ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa ndio inayoshikilia rekodi ya kuwa kampuni iliyoweka fedha nyingi zaidi za udhamini katika klabu kongwe zaidi nchini ya Yanga na ndio mabingwa wa kihistoria. Yanga ndio klabu kongwe na ambayo imechukua makombe mengi zaidi ya Ligi Kuu Bara ikifuatiwa na watani wake wa jadi  Simba ambao walitokea ubavuni mwa klabu hiyo kongwe zaidi.  Sifa namba moja ya mashabiki wa Yanga ni wale walio na mapenzi ya dhati na klabu yao katika vipindi vyote kwa maana ya raha na shida na wamekuwa wakionyesha mapenzi ya kiwango cha juu sana kuhakikisha Yanga inafanya vema kwa kuiunga mkono. Mashabiki wa Yanga, wengi wanatambua mchango mkubwa wa  SportPesa  licha ya kwamba Yanga haijawa na vipindi vizuri sana lakini tayari mambo yameanza kubadilika. Wakati SportPesa inatimiza miaka minne ya kuzaliwa hapa nchini, tayari udhamini wake wa miaka minne wa kumwaga kitita cha zaidi ya Sh bilioni moja kwa kila mwaka, ndio u

DK MSOLLA AENGULIWA UCHAGUZI BODI SABABU YA VYETI

Image
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Dk Mshindo Mbette Msolla ameenguliwa kwenye uchaguzi wa Bodi ya Ligi Tanzania kwa kile kilichoelezwa hajakidhi vigezo kanuni ya 9 (7) ya vigezo vya kanuni za uchaguzi za TFF toleo la 2021. Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Msolla Msolla ameenguliwa kwa kutowasilisha nakala halisi za vyeti vya Taaluma, wakati Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu hakuhudhuria usaili. Mwenyekiti wa sasa Bodi, Steven Jarvis Mnguto wa Coastal Union ndio mgombea pekee aliyeitishwa kwenye nafasi hiyo kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu mkoani Kigoma, huku Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ pekee akipitishwa kugombea nafasi ya Makamu.

YANGA SC 2-0 AZAM FC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
 

MAN UNITED YAZINDUKA, YASHINDA 3-0

Image
TIMU ya Manchester United imezinduka na kuichapa Tottenham Hotspur mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa  Tottenham Hotspur Jijini London. Mabao ya Manchester United leo yamefungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 36, Edinson Cavani dakika ya 64 na Marcus Rashford dakika ya 86. Kwa ushindi huo, Manchester United imefikisha pointi 17, mbili zaidi ya Tottenham baada ya timu zote kucheza mechi 10.

YANGA YAIKUNG'UTA AZAM FC 1-0

Image
MABAO ya washambuliaji Wakongo, Fiston Kalala Mayele na Jesus Ducapel Moloko yameipa Yanga SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mayele alifunga bao la kwanza dakika ya 36 akimalizia kazi nzuri ya beki mzawa, Kibwana Shomari na Moloko akafunga dakika ya 73 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi nne na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya Dodoma Jiji FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi. Azam FC yenyewe baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake nne za mechi nne sasa.

CHELSEA YAICHAPA NEWCASTLE 3-0 ST JAMES

Image
TIMU ya Chelsea imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya England baada ya kuwachapa wenyeji, Newcastle United mabao 3-0 leo Uwanja wa St. James' Park . Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na beki wa kimataifa wa England, Reece James mawili dakika ya 65 na 77 na kiungo Mtaliano mzaliwa wa Brazil, Jorge Luiz Frello Filho ‘Jorginho’ dakika ya 81. Kwa ushindi huo, The Blues inafikisha pointi 25 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 10, wakati Newcastle inabaki na pointi nne za mechi 10 pia katika nafasi ya 19.

ARSENAL YAICHAPA LEICESTER 2-0 KING POWER

Image
MABAO ya Gabriel Magalhães dakika ya tano na  Emile Smith Rowe dakika ya 18 yameipa Arsenal ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa King Power. Arsenal inafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya tano, ikiizidi pointi tatu Leicester baada ya wote kucheza mechi 10.

CRYSTAL PALACE YAICHAPA MAN CITY 2-0 ETIHAD

Image
MABAO ya Wilfried Zaha ya sita na Conor Gallagher dakika ya 88 yameipa Crystal Palace ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja Etihad. Pamoja na ushindi huo, kikosi cha kocha Patrick Vieira kilimaliza pungufu baada ya Aymeric Laporte kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 na ushei. Kwa kipigo hicho kwenye mechi ya 200 kazini kocha Pep Guardiola sasa anazidiwa pointi tano na vinara Chelsea baada ya wote kucheza mechi 10. Crystal Palace yenyewe inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 10.

LIVERPOOL YADUWAZWA NYUMBANI NA BRIGHTON

Image
WENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya 2-2 na Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield. Liverpool ilitangulia kwa mabao ya Jordan Henderson dakika ya nne na Sadio Mane dakika ya 24, kabla ya Brighton kuzinduka kwa mabao ya Enock Mwepu dakika ya 41 na Leandro Trossard dakika ya 65. Kwa sare hiyo ya nyumbani, kikosi cha Jurgen Klopp kinafikisha pointi 22, kikizidiwa pointi tatu na Chelsea inayoongoza baada ya wote kucheza mechi 10. Brighton yenyewe baada ya sare ya leo inafikisha pointi 16 kufuatia kucheza mechi 10 pia kikisogea nafasi ya sita.

TANZANITE YAANZA VYEMA CECAFA U20

Image
TANZANIA imeanza vyema michuano ya wasichana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Women’s 20 baada ya kuichapa Eritrea 1-0 jioni ya leo Uwanja wa FTC Njeru nchini Uganda.    Bao pekee la Tanzanite jioni ya leo limefungwa na Clara Luvanga dakika ya 90 na timu hiyo itashuka tena dimbani Jumatatu kumenyana na Burudani kabla ya kuivaa Ethiopia Jumatano, Uganda Jumamosi ijayo na kukamilisha mechi zake kwa kucheza na Djibouti Novemba 9.

DODOMA JIJI YAICHAPA MTIBWA 1-0 UHURU

Image
TIMU ya Mtibwa Sugar imeendelea kufanya vibaya katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo pia kuchapwa 1-0 na Dodoma Jiji FC bao pekee la Seif Abdallah Karihe dakika ya 61 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 10 baada ya mechi tano na kupanda kileleni, ikiizidi pointi moja Yanga ambayo hata hivyo ina mechi mbili mkononi, wakati Mtibwa Sugar wanabaki na pointi mbili katika mechi tano pia.

MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA AFARIKI DUNIA

Image
MCHEZAJI wa zamani wa Simba SC, Akilimali Yahya, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi ya Oktoba 30, 2021 katika Hospital ya Maweni, Kigoma. Winga huyo aliyecheza Simba SC kuanzia mwaka 2003 hadi 2008 anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo nyumbani kwao Ujiji Kigoma. Baada ya kucheza Simba SC kati ya 2003 na 2008, Akilimali aliyezaliwa Desemba 5, mwaka 1986 alikwenda Mtibwa Sugar ambako alicheza hadi 2010 alipohamia JKT Tanzania alikocheza kwa msimu mmoja akahamia  Coastal Union ya Tanga kabla ya kustaafu soka ya ushindani. Mungu ampumzishe kwa amani. Amin. GONGA HAPA KUTAZAMA VIDEO

KAGERA SUGAR YAICHAPA KMC 1-0 UHURU

Image
BAO la Meshack Abraham dakika ya 16 limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, KMC jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Ushindi huo unaifanya Kagera Sugar ifikishe pointi nane baada ya mechi tano na kupanda nafasi ya tatu nyuma ya Polisi Tanzania na Yanga zenye pointi tisa kila moja, wakati KMC inabaki na pointi mbili baada ya mechi tano pia. Mechi nyingine ya Ligi Kuu, Mbeya Kwanza imelazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Kiungo mkongwe Ramadhani Suleiman Chombo ‘Redondo’ alianza kuifungia Biashara United dakika ya 13, kabla ya mshambuliaji Hamisi Kanduru kuisawazishia Mbeya Kwanza dakika ya 81. Wakati Mbeya Kwanza inafikisha pointi sita, Biashara United imetimiza pointi tano katika mechi nne wote.

SUNDAY MANARA ATEULIWA KAMATI YA UFUNDI YANGA

Image
UONGOZI wa klabu ya Yanga umewateua wachezaji wake wa zamani, Ally Mayai Tembele na Sunday Ramadhani Manara kuunda Kamati ya Ufundi ya klabu hiyo.

ASIYEVAA NEMBO YA NBC ANASHUSHWA DARAJA

Image
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imesema klabu ambayo haitavaa jezi yenye nembo ya Mdhamini, NBC kuanzia sasa itatozwa faini ya Sh. Milioni 3 kila mchezo na inaweza kuchukuliwa hatua kali ziadi ikiwemo kushushwa Daraja au kufungiwa.

LIVERPOOL YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA LIGI

Image
TIMU ya Liverpool imetinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi England baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Preston North End usiku huu Uwanja wa Deepdale mjini Preston. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Takumi Minamino dakika ya 62 akimalizia pasi ya Neco Williams na Divock Origi dakika ya 84.

WEST HAM YAITOA MAN CITY KWA MATUTA

Image
WENYEJI, West Ham United wametinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi England baada ya kuitoa Manchester City kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa London Jijiji London. Waliofunga penalti za West Ham ni Mark Noble, Jarrod Bowen, Craig Dawson, Aaron Cresswell na Said Benrahma, wakati za Man City zilifungwa na João Cancelo, Gabriel Jesus na Jack Grealish baada ya Phil Foden kikosi ya kwanza. Mara ya mwisho Manchester City  kutolewa kwenye Carabao Cup ilikuwa ilikuwa Oktoba 26, 2016 walipofungwa na mahasimu wao, Man United.

SIMBA SC YAPOZA MACHUNGU YA GALAXY

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wamefuta machozi ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Lakini haukuwa ushindi mwepesi, kwani wenyeji hao walilazimika kusubiri hadi dakika ya 89 kupata bao hilo pekee tena kwa mkwaju wa penalti wa kiungo Mzambia, Rally Bwalya. Simba SC inafikisha pointi saba baada ya mechi tatu, kufuatia kutoa sare mechi ya kwanza na Biashara United mjini Musoma mkaoni Mara kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Dodom Jiji FC mjini Dodoma. Polisi Tanzania ya Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya mwanzo mzuri wakishinda mechi tatu mfululizo leo wamepoteza mechi ya kwanza. Ikumbukwe Simba ilifungwa 3-1 na Jwaneng Galaxy ya Botswana Jumapili katika mchezo wa kuwania kuingia Hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa na kutolewa kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mechi ya kwanza Gaborone.

TFF YASEMA HAIHUSIKI KUFUKUZWA KWA GOMES

Image
  SHIRIKISHO la SOKA Tanzania (TFF), limesema halihusiki na kufukuzwa kwa kocha yeyote wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kama inavyopotoshwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa ya TFF imesema kwamba klabu zote za Ligi Kuu zilikamilisha taratibu za kusajili maafisa wake wa benchi la Ufundi na walipitishwa wote kwa mujibu wa taratibu. Taarifa ya TFF inafuatia madai kwamba Simba SC imewafukuza makocha wake wa kigeni kwa sababu walizuiwa na shirikisho hilo kufanya kazi nchini kwa sababu hawana sifa. Simba ilitangaza kuachana na Kocha wake, Didier Gomes Da Rosa siku mbili baada ya timu kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kuchapwa 3-1 nyumbani na Hwaneng Galaxy Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Pamoja na Gomes, wameondolewa pia kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov na ko cha wa viungo, Mtunisia Adel Zrane – wanabaki Mnyarwanda Hitimana Thierry na Suleiman Matola.