Posts

Showing posts from May, 2024

AZAM YATINGA FAINALI KIBABE KOMBE LA TFF, YAITWANGA COASTAL 3-0

Image
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inatambulishwa kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na viungo washambuliaji, Abdul Hamisi Suleiman 'Sopu' (23) mawili dakika ya 42 kwa penalti na 79 na lingine Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' (26) dakika ya 68. Sasa Azam FC itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili ya CRDB Bank Federation Cup baina ya mabingwa watetezi, Yanga na Ihefu SC zitakazomenyana kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. 

DODOMA JIJI 0-1 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA YAICHAPA DODOMA JIJI FC 1-0 JAMHURI

Image
VIGOGO, Simba SC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Muivory Coast Freddy Michael Koublan dakika ya saba akimalizia kazi nzuri ya winga Edwin Barua. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 60, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 27. Kwa upande wao Dodoma Jiji FC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 27 nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16, ambazo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja.

YANGA SC WALIVYOWASILI ARUSHA KUIVAA IHEFU JUMAPILI

Image
KIKOSI cha Yanga kimewasili salama Jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Ihefu SC keshokutwa kuanzia Saa 9:30 Alasiri Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini humo. Mshindi wa mechi za michuano hiyo ambayo sasa inatambulishwa kama CRDB Bank Federation Cup atakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya Azam FC na Coastal Union zinazomenyana kesho Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. GONGA KUTAZAMA PICHA YANGA ILIVYOWASILI ARUSHA 

MAHODHA WA ZAMANI TAIFA STARS JELLAH MTAGWA AFARIKI DUNIA

Image
BEKİ na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Jellah Mtagwa (70) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Muhimbili Mloganzila alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Mtagwa aliyekuwa beki hodari wa kati enzi zake - amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kiharusi tangu mwaka 2004 kufuatia kuanguka akiwa anatembea katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Mtagwa alikuwa Nahodha wa Taifa Stars kwa miaka 10 mfululizo kuanzia mwaka 1973 akimrithi beki wa kati pia, Omar Zimbwe hadi 1983 alipomuachia Charles Boniface Mkwasa mlinzi pia na kiungo. Aliiongoza Taifa Stars kufuzu Fainali za Kwanza za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria na mwaka 1982 sura yake iliwekwa kwenye stempu kutokakana na umaarufu wakati huo. Ilikuwa wakati wa mechi za Kufuzu Kombe la Dunia mwaka 1982 nchini Hispania ambazo Taifa Stars ilitolewa na Nigeria katika Raundi ya Pili baada ya kuitoa, Kenya katika Raundi ya kwanza ya mchujo huo. Jellah alizaliwa mwaka 1953 Morogoro mjini akapata elimu

AZİZ Kİ ATANGAZA JEZI YA UBINGWA WA 30 YANGA

Image
KIUNGO was Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki ametumika kwenye kampeni maalum ya klabu yake, Yanga SC kutangaza jezi za ubingwa wa 30 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. GONGA KUTAZAMA VIDEO AZİZ KI AKITANGAZA JEZI YA UBINGWA WA 30

SIMBA SC WAWASILI MAKAO MAKUU YA NCHI KUIVAA DODOMA JIJI

Image
KIKOSI cha Simba SC kimewasili salama Jijini Dodoma mapema leo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, kesho Uwanja wa Jamhuri. Simba SC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 57 za mechi 26 nyuma ya Azam FC yenye pointi 60 za mechi 27, wakati Dodoma Jiji ina pointi 30 za mechi 26 nafasi ya 11. Na wote wapo nyuma ya mabingwa tayari, kwa mara ya tatu mfululizo, Yanga SC yenye pointi 71 za mechi 27. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

MAN UNITED YAICHAPA NEWCASTLE 3-2 OLD TRAFFORD

Image
WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Mabao ya Mancheater United yamefungwa na washambuliaji, chipukizi wa umri wa miaka 19, Muingereza mwenye asılı ya Ghana, Kobbie Boateng Mainoo dakika ya 31, Muivory Coast Amad Diallo Traoré mwenye umri wa miaka 21 dakika ya 57 na Mdenmark Rasmus Winther Højlund dakika ya 84. Kwa upande wao Newcastle United mabao yao yamefungwa na washambuliaji Muingereza Anthony Michael Gordon (23) dakika ya 49 na bwana mdogo wa umri wa miaka 19, Lewis Kieran Hall dakika ya 90. Kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 57, ingawa inabaki nafasi nane ilizidiwa tu wastani wa mabao na Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 37.

TAIFA STARS YACHAPWA 2-1 NA SUDAN KIRAFIKI SAUDI ARABIA

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania imefungwa bao 1-0 na Sudan katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa King Fahd Sport City mjini Ta'if, Saudi Arabia. Katika mchezo huo, kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ amemtumia kinda wa umri wa miaka 17, Jabir Seif Mpanda (pichani) wa akademi ya Getafe ya Hispania, huo ukiwa mchezo wake wa kwanza Taifa Stars na alikuwa mchezaji mdogo zaidi zaidi ya wote uwanjani leo.

CHILAMBO ASAINI MKATABA MPYA AZAM FC HADI 2026

Image
BEKI wa kulia, Nathaniel Raphael Chilambo (24) amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Azam FC hadi mwaka 2026.

MTIBWA SUGAR 1-3 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

DURAN APIGA MBILI ASTON VILLA YATOA SARE 3-3 NA LIVERPOOL

Image
WENYEJI, Aston Villa usiku wa jana wametoa sare ya kufungana mabao 3-3 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham. Mabao ya Aston Villa yalifungwa na kiungo Mbelgiji, Youri Marion Tielemans dakika ya 12 na mshambuliaji Mcolombia, Jhon Jader Duran mawili dakika ya 85 na 88. Mabao ya Liverpool yalifungwa na kipa Muargentina, Emiliano Martínez aliyejifunga dakika ya pili, winga Mholanzi Cody Mathes Gakpo dakika ya 23 na beki Muingerea mwenye asili ya Ghana, Jarell Amorin Quansah dakika ya 48. Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 79, ingawa inabaki nafasi ya tatu, wakati Aston Villa inafikisha pointi 78 nayo inabaki nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 37.

YANGA SC MABINGWA TENA LIGI KUU YA NBC TZ BARA

Image
RASMI, Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo na mara ya 30 jumla baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mtibwa Sugar walitangulia kwa bao la Charles Ilamfya dakika ya 32, kabla ya Yanga kutoka nyuma kwa mabao ya Mzambia Kennedy Musonda dakka ya 62, Nasry Kyombo aliyejifunga dakika ya 66 na Clement Mzize dakika ya 81. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 71 katika mchezo wa 27 ambazo hakuna timu nyingine katika Ligi Kuu inayoweza kuzifikisha, hivyo kujihakikishia taji la ubingwa msimu huu, 2023-2024. Hali inazidi kuwa mbaya kwa Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo ikibaki na pointi zake 20 za mechi 27 mkiani kabisa mwa Ligi Kuu. Sehemu pekee ya Mtibwa Sugar kujinusuru kutoshuka Daraja ni kwenye mchujo, Play-Offs kama itashinda mechi zake zote tatu zilizobaki dhidi ya Namungo nyumbani na Ihefu na Mashujaa ugenini na kumaliza nafasi ya 14 au ya 13. Na hiy

TABORA UNITED YAICHAPA MASHUJAA 1-0 UWANJA WA MWINYI

Image
BAO pekee la Eric Okutu dakika ya 70 jana liliipa Tabora United ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Kwa ushindi huo, Tabora United inafikisha pointi 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14, wakizidiwa wastani wa mabao na Mashujaa FC baada ya wote kucheza mechi 27. Wapo mbele ya Geita Gold yenye pointi 24 nafasi ya 15 na Mtibwa Sugar pointi 20 nafasi ya mwisho, ya 16 baada ya wote kucheza mechi 26. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu zitashuka daraja na mbili nyingine, ya 13 na 14 zitamenyana baina yao nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kusalia Ligi Kuu.

NICOLAS JACKSON AIPIGIA LA USHINDI CHELSEA YAICHAPA NOTTINGHAM 3-2

Image
  TIMU ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire. Mabao ya Chelsea yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Ukraine, Mykhailo Mudryk (23) dakika ya nane, washambuliaji Muingereza mwenye asili ya Jamaica, Raheem Shaquille Sterling (29) dakika ya 80 na Msenegal mzaliwa wa Gambia, Nicolas Jackson dakika ya 82. Kwa upande wao  Nottingham Forest mabao yao yamefungwa na beki Muivory Coast, mzaliwa wa Ufaransa, Willy-Arnaud Zobo Boly (33) dakika ya 16 na winga mwenye asili ya Ghana, Callum James Hudson-Odoi (23) dakika ya 74. Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya saba, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake 29 za mechi 37 nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.

MAN CITY YAITANDIKA FULHAM 4-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND

Image
MABINGWA watetezu, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London. Mabao ya Man City yamefungwa na beki Mcroatia, Josko Gvardiol (22) mawili dakika ya 13 na 71, huku mengine yakifungwa na kiungo Muingereza, Philip Walter Foden (23) dakika ya 71 na mshambuliaji Muargentina, Julian Alvarez (24) kwa penalti dakika ya 90'+6. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 85 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England ikiizidi pointi mbili Arsenal baada ya wote kucheza mechi 36, wakati Fulham inabaki na pointi zake 44 za mechi 37 nafasi ya 14.

COASTAL UNION YAICHAPA SINGIDA FG 2-0 MKWAKWANI

Image
WENYEJI, Coastal Union wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Mabao ya Coastal Union yamefungwa na mshambuliaji Crispin Ngushi Mhagama (25) dakika ya 26 na kiungo Greyson Gerard Gwalala (30) dakika ya 46. Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi zake 29 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 26.

MASAWE APIGA ZOTE MBILI NAMUNGO FC YAILAZA GEITA GOLD 2-0 RUANGWA

Image
WENYEJI, Namungo FC wameibukana ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Namungo FC yamefungwa na kiungo mkwenye anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, Jacob Raymond Masawe (31) dakika ya 43 na 45'+4. Kwa ushindi huo, Namungo FC wanafikisha pointi 30 na kusogea nafasi ya saba, wakizizidi tu wastani wa mabao JKT Tanzania na Kagera Sugar baada ya wote kucheza mechi 26. Hali ni mbaya kwa Geita Gold baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao24 za mechi 26 nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja. Nyingine mbili, ya 13 na 14 mwisho wa msimu zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu. 

TASWA KUWAFUNDA WAANDISHI CHIPUKIZI NCHINI

Image
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatarajiwa kuendesha mafunzo kwa waandishi wa Habari wanaochipukia katika nchi mbalimbali nchini.

WASHINDI WA PROMOSHENI YA TWENZETU DUBAİ NA PARIMATCH WAPATIKANA

Image
Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya Parimatch, Eric Gelard (kushoto) akikabidhi ticket kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Twenzetu Dubai, Daniel Kasanga.  WASHINDI promosheni ya Twenzetu Dubai na Parimatch wapatikana, kupaa Jumatatu kwenda Dubai Dar es Salaam. Washindi wawili wa promosheni ya Twenzetu Dubai na Parimatch inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch wamepatikana na watasafiri Dubai Jumatatu ijayo. Washindi hao ni Daniel Kasanga, mkazi wa Ruvuma na Mohamed Salim mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Parimatch, Ismail Mohamed. Ismail alisema kuwa Kasanga ni mshindi wa droo ya wiki ya kwanza na Salim ameshinda droo ya wiki ya pili kupitia mchezo Aviator ndani ya Casino. Alisema kuwa safari hiyo itagharimiwa na kampuni yao ikiwa pamoja na usafiri, visa, malazi kwenye hoteli ya kifahari na gharama za kutembelea maeneo mbalimbali ya kitalii na kihistoria wakiwa Dubai. “Kasanga na Salim wameshinda tiketi ya

IHEFU YAAMBULIA SULUHU KWA JKT TANZANIA UWANJA WA LITI

Image
WENYEJI, Ihefu SC wamelazimishwa sare ya bila mabao na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida. Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi 29 katika nafasi ya 10 na JKT Tanzania inafikisha pointi 32 nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 26.  

MAKAMU RAIS WA YANGA, ARAFAT MKURUGENZI MPYA BENKI YA PBZ

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Rais Yanga SC, Arafat Ally Haji kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA GEORGE MASATU KUHUSU PAMBA KUREJEA LIGI KUU

Image
 

MTIBWA SUGAR YAZINDUKA, YAICHAPA TABORA UNITED 3-0 MANUNGU

Image
WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Jimson Mwanuke dakika ya 15, Charles Ilamfya dakika ya 55 na Nickson Mosha dakika ya 79. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 20, ingawa inaendelea kushika mkia, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 23 nafasi ya 15 katika ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 26.

MUDATHIR ATOKEA BENCHI KUIPA YANGA USHINDI DHIDI YA KAGERA SUGAR

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wamepata ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Mudathir Yahya Abbas dakika ya 83 akimalizia pası ya kiungo mwenzake, Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso. Mudathir alifunga bao hilo dakika 10 tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua na kwa ushindi huo Yanga inafikisha pointi 68 katika mchezo wa 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 57 za mechi 25 na Simba SC pointi 53 za mechi 24. Kwa upande wao Kagera Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 26 pia nafasi ya saba.

MASHUJAA YAICHAPA KMC 3-0 LAKE TANGANYIKA

Image
TIMU ya Mashujaa FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na Jeremanus Josephat dakika ya 12, Hassan Cheda dakika ya 22 na Relliants Lusajo dakika ya 60. Kwa ushindi huo, Mashujaa FC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 13, wakati KMC inabaki na pointi zake 33 za mechi 26 pia nafasi ya tano katika ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja. Nyingine mbili, ya 13 na 14 mwisho wa msimu zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

TABORA UNITED YAFUNGIWA KUSAJILI KWA NYINGINE TENA NA TENA

Image
KLABU ya Tabora United imefungiwa kufanya usajili wa mchezaji mpya hadi hapo itakapomlipa madai yake mchezaji wake Mkongo, Makuntima Kisombe Gulyan.

BORUSSIA DORTMUND YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA, PSG NA MBAPPE OUT

Image
TIMU ya Borussia Dortmund imefanikiwa kuingia Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Paris Saint-Germain ya akina Kylian Mbappé usiku huu Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris nchini Ufaransa. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki mkongwe wa umri wa miaka 35, Mats Julian Hummels dakika ya 50 akimalizia kazi nzuri ya Mjerumani mwenzake, kiungo Julian Brandt. Kwa matokeo hayo Borussia Dortmund wanakwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-0 kufuatia kushinda 1-0 pia kwenye mechi ya kwanza nyumbani Mei 1 bao pekee la kiungo Mjerumani, Niclas Fullkrug Uwanja wa Signal Iduna Park Jijini Dortmund. Sasa Borussia Dortmund watakutana na mshindi wa jumla kati ya Bayern Munich ya Ujerumani pia na Real Madrid ya Hispania ambazo zitarudiana kesho Jijini Madrid baada ya sare ya 2-2 kwenye mechi ya kwanza Jijini Munich wiki iliyopita. Fainali ya UEFA Champions League msimu huu itapigwa Uwanja wa Wembley Jijini London Jumamosi ya Juni 1 mwaka huu

GUEDE AWA MCHEZAJI BORA YANGA MWEZI APRILI

Image
MSHAMBULIAJI Muivory Coast, Joseph Gnadou Guede ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Yanga kwa mwezi Aprili mwaka huu. Guede ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwaangusha kipa wa Mali, Djigui Diarra na kiungo mzawa, Jonás Mkude alioingia nao Fainali na kwa ushindi huo atapatiwa kitita en cha Sh. Milioni 3 kutoka kwa wadhamini, kampuni ya NIC Insurance.

ALLY SALIM KUONGOZA TAIFA STARS MECHI ZA KIRAFIKI SUDAN

Image
KOCHA Hemed Suleiman ‘Morocco’ ameteua kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya taifa ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoondoka kesho kwenda Sudan kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki. 

SIMBA SC YAICHAPA TABORA UNITED 2-0 CHAMAZI

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na kiungo wa Mali, Sadio Kanoute dakika ya 19 na mshambuliaji Edwin Balua dakika ya 77. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 53 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya tatu  nyuma ya Azam FC yenye pointi 57 na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 65 baada ya wote kucheza mechi 25. Kwa upande wao Tabora United wanabaki na pointi zao 23 za mechi 25 sasa katika nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja. Nyingine mbili, ya 13 na 14 mwisho wa msimu zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

SERIKALI YAMTEUA ABUBAKAR BAKHRESA KAMATI YA MAANDALIZI YA CHAN NA AFCON

Image
WIZARA ya Utamaduni Sanaa na Michezo imeunda Kamati ya Maandalizi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa kushirikiana na Uganda na Kenya. Katika Kamati hiyo itakayokuwa chini ya Mwenyekiti, Leodegar Chilla Tenga mmoja wa Wajumbe ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Bakhresa Group Limited, Abubakar Said Salim Bakhresa kuwa Mjumbe.

AZAM FC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MANUNGU

Image
TIMU ya Azam FC imeichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya yamefungwa na kiungo mzawa, Feisal Salum dakika ya 20 na winga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 65 na kwa ushindi huo Azam FC inafikisha pointi 57, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nane na mabingwa watetezi, Yanga baada ya timu zote kucheza mechi 25. Hali inazidi kuwa mbaya kwa Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo ikibaki na pointi zake 17 baada ya kucheza mechi 25 pia na inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16. Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

IHEFU SC YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 SINGIDA MABAO YA WAKENYA

Image
TIMU ya Ihefu SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Mabao yote ya Ihefu leo yamefungwa na Wakenya, mshambuliaji Elvis Baranga Rupia dakika ya 35 na kiungo Duke Ooga Abuya dakika ya 90’+3. Kwa ushindi huo, Ihefu SC inafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya 11, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 27 na kushukia nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 25 sasa.

LIVERPOOL YAICHAPA TOTTENHAM 4-2 ANFIELD

Image
WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Tottenham Hotspur usiku wa Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool. Mabao ya Liverpool yamefungwa na mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah dakika ya 16, beki Mscotland,  Andrew Robertson dakika ya 45, mshambuliaji Mholanzi, Cody Gakpo dakika ya 50 na kiungo Muingereza, Harvey Elliott dakika ya 59. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 78 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 82 za mechi 35 na  vinara, Arsenal wenye pointi 83 za mechi 36, wakati Tottenham Hotspur inabaki na pointi zake 60 za mechi 35 nafasi ya tano.

CHELSEA YA MOTO KABISA WEST HAM YAFA TANO MTUNGI

Image
WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na Waingereza viungo Cole Palmer dakika ya 15, Conor Gallagher dakika ya 30, washambuliaji Chukwunonso Madueke dakika ya 36 na Msenegal Nicolas Jackson dakika ya 48 na 80. Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 35 na kusogea nafasi ya saba, wakati West Ham United inabaki na pointi zake 49 za mechi 36 sasa nafasi ya tisa.

GUEDE AWEKA BAO PEKEE YANGA YAIKANDA MASHUJAA 1-0 KIGOMA

Image
MABINGWA watetezi, Young Africans wamezidi kulikaribia taji la tatu mfululizo la Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na la 30 jumla baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Shukrani kwa mfungaji wa bao hilo pekee mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Gnadou Guede dakika ya 41 akimalizia pasi ya kiungo mzawa, Mudathir Yahya Abbas baada ya kazi nzuri ya kiungo mshambuliaji Mburkinabe, Stephane Aziz Ki. Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 65 katika mchezo wa 25 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 11 zaidi ya Azam FC inayofuatia ingawa ina mechi moja mkononi na kesho inacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Kwa upande wao Mashujaa FC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 23 za mechi 25 sasa nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16. Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati

AZIZ KI MCHEZAJI BORA, GAMONDI KOCHA BORA LIGI KUU APRILI

Image
KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki wa Yanga ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Aprili, huku Muargentina Miguel Ángel Gamondi wa timu hiyo pia akishinda Tuzo ya Kocha Bora mwezi huo. Wakati Aziz Ki amewashinda mchezaji mwenzake wa Yanga, Joseph Gnadou Guede alioingia nao Fainali - Gamondi amewashinda Mfaransa Bruno Ferry wa Azam FC na mzawa, Malale Hamsini wa JKT Tanzania alioingia nao Fainali pia.

JKT TANZANIA YAICHAPA GEITA GOLD 2-0 MBWENI

Image
WENYEJI, JKT Tanzania wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam. Mabao ya JKT Tanzania inayofundishwa na Kocha Malale Hamsini yamefungwa na Najim Magulu dakika ya 45’+3 na Daniel Lyanga dakika ya 56. Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 25 na kusogea nafasi ya nane, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 24 za mechi 25 pia nafasi ya 13.

SIMBA SC 2-0 MTIBWA SUGAR (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF KWA KISHINDO

Image
TIMU ya Azam FC imekamilisha idadi ya timu nne za Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayotambulishwa kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Namungo FC usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na viungo, Muivory Coast Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon dakika ya 10, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 15, Feisal Salum Abdallah dakika ya 19 na Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 52, wakati bao pekee la Namungo FC limefungwa na kiungo pia, Ayoub Semtawa dakika ya 45 na ushei. Azam FC sasa itamenyana na Coastal Unión katika Nusu Fainali ambayo juzi iliitoa Geita Gold kwa kuichapa bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Nusu Fainali nyingine ni baina ya mabingwa watetezi, Yanga dhidi ya Ihefu ambayo iliitoa Mashujaa FC kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0 juzi pia Uwanja wa LITI mjini Singida.

SIMBA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 CHAMAZI KOUBLAN AMEWEKA

Image
WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dares Salaam. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na mshambuliaji, Muivory Freddy Michael Koublan dakika ya 35 na kiungo mzawa, Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 64. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 23, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 54 na Yanga 62 baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 17 za mechi 24 nafasi ya mwisho, ya 16.

RONWEN WILLIAMS AJITIA KITANZI MAMELODI HADI 2028

Image
KLABU ya Mamelodi Sundowns is imetangaza kumuongeza mkataba wa miaka minne kipa wake mzawa, Ronwen Williams ambao utamfanya adumu Chloorkop angalau mwaka 2028. Mkataba huo unatoa fursa kwa Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ aliyejiunga na Mamelodi Sundowns mwaka 2022 kuongeza mwaka mmoja zaidi. Ronwen Williams amekuwa na msimu mzuri aliiwezesha Mamelodi kutwaa mataji ya Ligi Kuu ya DStv, African Football League (AFL) na kufuzu kwenye michuano ijayo ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA. Alifanya vizuri pia kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) akishinda Tuzo ya Kipa Bora wa michuano hiyo baada ya kuiwezesha Bafana Bafana kumaliza nafasi ya tatu.