Posts

Showing posts from June, 2022

COASTAL UNION WAWASILI ARUSHA KUIVAA YANGA

Image
MSHAMBULIAJI tegemeo wa Coastal Union, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ akiteremka kwenye basi baada ya kuwasili Arusha kuelekea Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Yanga Jumamosi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

MTIBWA NA PRISONS JUMAPILI SOKOINE, JUMATANO MANUNGU

Image
MECHI za mchujo wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons zutachezwa Jumapili na Jumatano, Julai 6. Mechi ya kwanza itachezwa Jumapili Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Tanzania Prisons wakiwa wenyeji na marudiano na Jumatano Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro Mtibwa wakiwa wenyeji. Timu itakayoshinda itabaki Ligi Kuu na itakayofungwa itakwenda kumenyana na JKT Tanzania kutoka Championship na mshindi ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao. Mechi dhidi ya JKT Tanzania zimepngwa kucheza Julai 9 Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na marudiano Julai 13 Sokoine au Manungu.

YUSSUF BAKHRESA AMEAMUA, ASHUSHA MUIVORY COAST MWINGINE AZAM

Image
KLABU ya Azam FC imetambulisha mchezaji mwingine kutoka Ivory Coast, naye pia kiungo mshambuliaji, Tape Edinho aliyesaini mkataba wa miaka mitatu. Azam FC imemnunua Edinho tumemnunua kutoka ES Bafing ya kwao, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025. Usajili wa nyota huyo mwenye uwezo mkubwa umekamilishwa na Mkurugenzi timu, Yusuf Bakhresa akishirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'. Mkali huyo amechaguliwa kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1) msimu huu, kutokana na ubora wake wa kuhenyesha wachezaji wa timu pinzani. Msimu uliomalizika, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matano na kuchangia pasi tisa zilizozaa mabao. Anakuwa Muivory Coast wa pili kutambulishwa leo baada ya  Kipre Junior Zunon kutokea Sol FC ya kwao pia ambaye naye amesaini mkataba wa miaka mitatu.

MRENO NDIYE KOCHA MPYA AL AHLY

Image
KLABU ya Al Ahly ya Misri imemtambulisha Mreno,  José Ricardo Soares Ribeiro  kuwa kocha wake mpya Mkuu akichukua nafasi ya Muafrika Kusini, Pitso Mosimane aliyefukuzwa mwezi huu. Soares , ambaye ni winga wa zamani wa Kimataifa wa Ureno, anajiunga na mabingwa hao wa kihistoria Afrika akitokea klabu ya  Gil Vicente FC ya kwao, Ureno. Mosimane aliondolewa kazini baada ya Ahly kufungwa na Wydad Casablanca katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

YUSSUF BAKHRESA ASHUSHA KIFAA CHA IVORY COAST AZAM

Image
KLABU ya Azam FC imemsajili kiungo mshambuliaji, Kipre Junior Zunon kutokea Sol FC ya kwao, Ivory Coast kwa mkataba wa miaka mitatu, zoezi ambalo limefanikishwa na Mkurugenzi wa klabu hiyo, Yussuf Bakhresa akishirikiana na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

ARAJIGA KUCHEZESHA FAINALI YA ASFC JUMAMOSI ARUSHA

Image
REFA Ahmed Arajiga wa Manyara ndiye atakayechezesha Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya Coastal Union ya Tanga na Yanga ya Dar es Salaam Jumamosi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

UCHAGUZI WA MATAWI YANGA WASOGEZWA MBELE TENA

Image
KAMATI ya Uchaguzi ya Yanga imesogeza mbele muda chaguzi za matawi ya klabu hiyo hadi Julai 4 kuelekea uchaguzi Mkuu wa mabingwa hao Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

MBEYA KWANZA 0-0 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC YAMALIZA LIGI KWA SARE SONGEA

Image
MABINGWA, Yanga SC wamemaliza Ligi Kuu ya Tanzania Bara vizuri kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Bao pekee la Yanga limefungwa na winga Dennis Nkane na kwa matokeo hayo wanamaliza na pointi 74, wakiwazidi pointi 13 mabingwa wa misimu minne iliyopita, Simba SC.

GEORGE MPOLE MFUNGAJI BORA LIGI KUU

Image
MSHAMBULIAJI Mzawa, George Mpole Mwaigomole ndiye mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kufunga bao la 17 leo, Geita Gold ikilazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Mpole amempiku mshambuliaji Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele aliyemaliza na mabao 16 baada ya leo kushindwa kufunga kwa mara ya pili mfululizo timu yake ikiibuka na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar. Msimu wa Ligi Kuu 2021-2022 umehitimishwa leo, timu za Mbeya Kwanza na Biashara United zikishuka daraja, huku Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons zikienda katika mechi za mbili za mchujo baina yao nyumbani na ugenini kuwania kubaki Ligi Kuu. Timu itakayoshinda itabaki Ligi Kuu na itakayofungwa itakwenda kumenyana na JKT Tanzania kutoka Championship na mshindi ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.

MBOMBO APIGA HATI-TRICK AZAM YAFUZU KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Biashara United leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Ilikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo aliyefunga mabao matatu, huku bao lingine likifungwa na Never Tigere.

NOVATUS DISMAS AJIUNGA NA SV WEREGEM YA UBELGIJI

Image
KIUNGO chipukizi Mtanzania, Novatus Dismas Miroshi amejiunga na klabu ya SV Zulte Waregem ya Ligi Kuu ya Ubelgiji. Miroshi amesaini mkataba wa kujiunga na SV Zulte Waregem jana, akitokea Beitar Tel Aviv Bat Yam alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka Maccabi Tel Aviv, zote za Israel. Kisoka, Miroshi aliibukia akademi ya Azam FC, kabla ya kutolewa kwa mkopo Biashara United akapate uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ambako msimu wake wa kwanza tu alipata nafasi ya kwenda Israel.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA DOUGLAS MUHANI

Image
 

KOCHA MKUU MPYA WA SIMBA NI MSERBIA ZORAN

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha rasmi Mserbia, Zoran Manojlovic kuwa kocha wake mpya Mkuu, akichukua nafasi ya Mspaniola, Pablo Franco Martin aliyefukuzwa mapema mwezi huu. “Kwa furaha kubwa tunapenda kumtangaza kocha wa makombe, Zoran Manojlovic kuwa Kocha Mkuu wa timu yetu,” imesema taarifa ya Simba SC leo. WASIFU WA ZORAN MANOJLOVIC Kuzaliwa  21 July 1962  (age 59) [1] KLABU ALIZOFUNDISHA Klabu ya sasa  Simba  (Kocha Mkuu) KLABU ZA AWALI  Mwaka  Timu 2017–2019 Primeiro de Agosto  (Angola) 2019–2020 Wydad AC  (Morocco $ 2020–2021 Al-Hilal  (Sudán) 2021 CR Belouizdad  (Algeria) 2021 Al-Tai  (Saudi Arabia) 2022– Simba  SC (Tanzania)

BILIONEA GHALIB ALIPOFIKISHIWA MATAJI YA YANGA

Image
MFADHILI na Mdhamini wa Yanga SC, Ghalib Said Mohamed (GSM) akiwa na Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Ngao ya Jamii wakati wa sherehe za ubingwa juzi Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU MGENI RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI

Image
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye Tamasha la kwanza la kihistoria la Utamaduni  kitaifa  Julai 2, 2022  Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliyoyatoa kwenye Tamasha la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro la kutaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa tamasha kubwa la kitaifa la utamaduni litakaloshirikisha mikoa yote ya Tanzania ili kutangaza hazina ya utamaduni wa makabila ya Tanzania Duniani. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amefafanua kuwa tamasha hilo litaambatana na matembezi maalum ya kitamaduni (Utamaduni Carnival) katika jiji la Dar es Salaam ambayo yameandaliwa njia  maalum za kupita ikiwemo daraja la juu la Mfugale, Kijazi, Tanzanite na daraja la mwalimu Nyerere. Amesema,  tamasha hilo litatoa fursa kwa  makabila yote  nchini kuonesha  tamaduni zao kupitia  ngoma na v

KOCHA MSAUZI WA MAKIPA SIMBA ATIMKIA ORLANDO

Image
KOCHA wa makipa wa klabu ya Simba SC, Tyron Damons ameagwa rasmi na imeelezwa anakwenda kujiunga na klabu ya Orlando Pirates ya kwao,  Afrika Kusini. “Klabu ya Simba inamtakia kila la heri Kocha wa magoli kuondoka klabuni kwetu mwishoni mwa msimu huu,” “Tyron amepata kazi kunako klabu ya Orlando Pirates ya nchini kwao Afrika Kusini na tayari amewasilisha ombi la kutaka kuondoka klabuni kwetu na kujiunga na miamba hiyo ya Afrika Kusini,” imesema taarifa ya Simba SC. Aidha, taarifa hiyo imeongeza kwamba tayari mchakato wa kutafuta mrithi wa Tyron umeanza na dhamira ni kumpata kocha mpya wa makipa kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya. 

KASSIM DEWJI AFICHUA KINACHOITAFUTA SIMBA SC

Image
 

WACHEZAJI AZAM FC WAPANDISHA BENDERA YAO MLIMA KILIMANJARO

Image
KIKOSI cha Azam FC juzi kilipanda Mlima Kilimanjaro na kupandisha bendera yake kwenye kilele cha Mlima huo ikiwa ni ishara ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii wa nchi, kupitia ziara yake ya Royal Tour.

RAIS WA FIFA AIPONGEZA YANGA KWA UBINGWA WA 28

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, ambao unakuwa ni wa 28 na wa rekodi kwao kihistoria.

WAZIRI MCHENGERWA AFICHUA SIRI YA UBINGWA YANGA

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa kombe la katika ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu huu. Mchengerwa  ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuchukua Ubingwa huo huku akipongeza mshikamano na furaha za mashabiki, ambazo wamezionyesha  wakati wa kukabidhiwa kombe hilo na mapokezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. " Kwa aina ya shangwe za ubingwa zilizofanyika jana na leo ni sawa na zile za mataifa yaliyoendelea ya Ulaya. Hakika mpira wa miguu ni mchezo mkubwa na pendwa duniani ambao huwaunganisha watu pamoja na kuleta amani, mshikamano, furaha na umoja baina ya wananchi" Ameongeza kuwa watanzania zaidi ya 90% ni wapenzi wa mchezo wa soka na amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inaboresha miundombinu ya michezo na kuleta usawa katika michezo hasa mpira wa miguu ili  kila mtanzania aweze kupata furaha. "Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais S

MAPOKEZI HADI SHEREHE ZA UBINGWA ZILIVYOFANA YANAG

Image
JIJI la Dar es Salaam jana lilikuwa ni kijani na njano, wakati wa mapokezi ya mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu, Yanga pale JNIA wakitokea Mbeya ambako juzi walikabidhiwa Kombe lao na msafara ulikwenda makao makuu ya klabu, Jangwani kupitia Msimbazi, kwenye klabu ya mahasimu wao, Simba na baadaye sherehe kwa mfadhili wao, GSM pale Samora kabla ya kumalizia Kidimbwi. 

TANZANIA PRISONS 1-0 SIMBA SC

Image
 

TANZANIA PRISONS YAICHAPA SIMBA 1-0 SOKOINE

Image
WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya vigogo, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Nahodha wake, Benjamin Asukile dakika ya 54 na kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 29 za mechi 29 na kusogea nafasi ya 14. Kwa upande wao, Simba wanabaki na pointi zake 60 nafasi ya pili nyuma ya mabingwa tayari, Yanga wenye pointi 71 baada ya wote kucheza mechi 29.

KICHUYA APIGA HAT TRICK NAMUNGO YAICHAPA MTIBWA 4-2 MANUNGU

Image
KIUNGO mshambuliaji, Shiza Ramadhani Kichuya ameifungia mabao matatu Namungo FC ikitoka nyuma na kuichapa timu yake ya zamani, Mtibwa Sugar 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Kichuya amefunga mabao hayo dakika za 24, 51 na 66 huku bao lingine la Namungo likifungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 73, wakati ya Mtibwa yamefungwa na Nzigamasabo Steve kwa penalti dakika ya sita na George Makang’a dakika ya 10. Namungo FC inafikisha pointi 40 baada ya ushindi huo na kusogea nafasi ya tano, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 31 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 29.

AZAM PUNGUFU YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 JAMHURI

TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. 

YANGA SC WAKABIDHIWA KOMBE LAO SOKOINE

Image
WACHEZAJI wa Yanga SC wakifuaria na Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia kukabidhiwa jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya baada ya mchezo dhidi ya wenyeji, Mbeya City uliomalizika kwa sare ya 1-1. 

YANGA SC YAENDELEZA REKOD YA KUTOPOTEZA MECHI LIGI KUU

Image
MABINGWA, Yanga wameendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.   Mshambuliaji Mkongo, Heritier Makambo alianza kuifungia Yanga dakika ya 40, kabla ya kiungo Mganda, Joseph Ssemunju kuisawazishia Mbeya City kwa penalti dakika ya 50 kufuatia Nahodha, Bakari Mwamnyeto kuunawa mpira kwenye boksi. Yanga wanafikisha mechi 29 bila kupoteza mechi, wakiwa tayari mabingwa kwa pointi zao 71, nyuma yao wakiwa mabingwa wa misimu minne iliyopita, Simba SC wenye pointi 60 za mechi 28 na kesho watamenyana na Tanzania Prisons hapo hapo Sokoine, Mbeya. Kwa Mbeya City, sare hiyo inawafanya wafikishe pointi 39 baada ya mechi 29 katika nafasi ya tisa. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union bao pekee la beki David Luhende dakika ya 15 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Nayo imeichapa Polisi Ta

KMKM WALIVYOTWAA UBINGWA WA ZANZIBAR

Image
 

SIMBA SC 2-0 MTIBWA SUGAR (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

TANZANIA YAPEWA MALAWI KUFUZU FAINALI ZA BEACH SOCCER

Image
TANZANIA itamenyana na Malawi katika kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Soka ya Ufukweni baadaye mwaka huu nchini Msumbiji. Tanzania itaanzia ugenini kati ya Julai 22 na 24, kabla ya timu hizo kurudiana Dar es Salaam kati ya Agosti 5 na 7.

SERENGETI GIRLS YAPANGWA NA CANADA, JAPANA NA UFARANSA

Image
TANZANIA imepangwa Kundi D pamoja na Canada, Japan na Ufaransa katika Fainali za Kombe la Dunia la Wanawake chini ya umri wa miaka 17 zinazotarajiwa kuanza Oktoba 11 hadi 30, mwaka huu nchini India. Wenyeji, India wamewekwa Kundi A kama ilivyo ada pamoja na Marekani, Morocco na Brazil, wakati Kundi B linaundwa na Ujerumani, Nigeria, Chile na New Zealand. Mabingwa watetezi, Hispania walioshinda taji lao la kwanza mwaka 2018 nchini Uruguay wamepangwa Kundi C pamoja na Colombia, Mexico na China. Serengeti Girls ilifuzu baada ya kuitoa Cameroon kwa jumla ya mabao 5-1, ikishinda 4-1 Jijini Yaoundé, kabla ya kushinda 1-0 Zanzibar.

FIFA YAIFUNGIA GEITA GOLD KUSAJILI WACHEZAJI WAPYA

Image
KLABU ya Geita Gold imefungiwa kusajili wa mchezaji mpya hadi hapo itakapomalizana na aliyekuwa kocha wake, Ettiene Ndayiragijje iliyemfukuza baada ya mechi kadhaa mwanzoni mwa msimu.

KAGERE ALIVYOMUAGA SERGE WAWA JANA SIMBA

Image
MSHAMBULIAJI Mnyarwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere (kushoto) akiwa amekumbatina na beki Serges Pascal Wawa Sfondo baada ya mechi ya kumuaga Muivory Coast huyo jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kufuatia kuitumikia Simba tangu mwaka 2017. Wawa mwenye umri wa miaka 36 sasa, mzaliwa wa Bingerville, Ivory Coast aliagwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu jana Simba ikishinda 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kutua Simba mwaka 2017 akitokea El-Merreikh ya Sudan ambako alikuwa anacheza kwa mara ya pili. Haswa kisoka aliibukia ASEC Mimosas mwaka 2003 ambako alicheza hadi 2010 alipokwenda El-Merreikh alikocheza hadi 2014 akahamia Azam FC ya Dar es Salaam. Mwaka 2016 alirejea Al-Merrikh kwa msimun mmoja, kabla ya kurejea Tanzania na kujiunga na Simba SC. Katika kipindi hicho cha miaka mitano, Wawa ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu akiwa na Simba,   2017–18, 2018–19, 2019–20 na 2020–21, Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ma

YANGA WAWASILI MBEYA KUBEBA MWALI WAO JUMAMOSI

Image
KIKOSI cha Yanga kimewasili Jijini Mbeya kuelekea mchezo wa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbeya City Jumamosi Uwanja wa Sokoine. Tayari Bodi ya Ligi imesema Yanga watakabidhiwa Kombe lao baada ya mchezo huo, kabla ya mapema siku inayofuata, yaani Jumapili kurejea Dar es Salaam na kupokewa na umati wa mashabiki na wapenzi wa timu hiyo huku wachezaji wakibebwa kwenye basi maalum la wazi  na kulitembeza Kombe hadi makao makuu ya klabu, Jangwani.

SIMBA YA MATOLA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI

Image
VIGOGO, Simba SC wamewaaga mashabiki wao kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wa mwisho nyumbani msimu huu. Nyota kutoka Senegal, Pape Ousmane Sakho alianza kuifungia Simba dakika ya 16 akimalizia pasi ya Kibu Dennis, kabla ya kumsetia kiungo mwenzake, Mmalawi, Peter Banda kufunga bao la pili dakika ya 43. Huo ni mchezo wa tatu mfululizo Simba inashinda chini ya kocha wa muda Suleiman Matola baada ya kufukuzwa Mspaniola, Pablo Franco Martin, ikitoka kushinda 3-1 dhidi ya 3-0 dhidi ya Mbeya City na 3-1 dhidi ya KMC, zote Uwanja wa Mkapa. Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 60, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi 10 na mabingwa tayari, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 28 kuelekea mechi mbili kukamilisha msimu. Mtibwa Sugar wenyewe baada ya kuchapwa leo wanabaki na pointi zao 31 za mechi 28 pia nafasi ya 12 katika Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili z

YANGA SC 2-0 POLISI TANZANIA (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

FIFA YAISHUSHIA ‘KITU KIZITO’ BIASHARA UNITED

Image
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) imeifungia klabu ya Biashara United ya Mara kufanya Usajili wa wachezaji wapya kwa madirisha mawili.

AZAM FC YAICHAPA PRISONS 1-0 NA KUREJEA TATU BORA

Image
WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa Jumatano Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Bao pekee la Azam FC limefungwa na mshambuliaji wake Mkongo. Idris Mbombo dakika ya 21 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 43 na kupanda nafasi ya tatu, wakiizidi pointi Geita Gold baada ya wote kucheza mechi 28. Hali inazidi kuwa mbaya kwa Tanzania Prisons baada ya kichapo hicho wanabaki pointi zao 26 katika nafasi ya 14 katika Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitateremka moja kwa moja. Ikumbukwe timu zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao katika mechi mbili za nyumbani na ugenini na timu itakayoshinda ndiyo itabaki Ligi Kuu, wakati itakayofungwa itacheza na JKT Tanzania ya Championship na mshindi atacheza tena Ligi Kuu msimu ujao.

YANGA SC YAICHAPA POLISI 2-0 NA KUZIDI KUUSTAWISHA UBINGWA

Image
VIGOGO, Yanga SC wamezidi kuustawisha ubingwa wao baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 12 na Chico Ushindi Wakubanza dakika ya 17 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 70 katika mchezo wa 28, sasa wakiwazidi pointi 13 washindi wa pili tayari, Simba SC ambao wamecheza mechi 28. Polisi Tanzania inabaki na pointi zake 36 za mechi 28 sasa nafasi ya saba. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji KMC wameitandika Mbeya Kwanza mabao 4-1 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

DIRISHA LA USAJILI BARA KUFUNGULIWA JULAI MOSI

Image
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetoa taarifa rasmi leo kwamba dirisha la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa kimashindano nchini litafunguliwa Julai 1, mwaka huu.