KAGERE ALIVYOMUAGA SERGE WAWA JANA SIMBA


MSHAMBULIAJI Mnyarwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere (kushoto) akiwa amekumbatina na beki Serges Pascal Wawa Sfondo baada ya mechi ya kumuaga Muivory Coast huyo jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kufuatia kuitumikia Simba tangu mwaka 2017.
Wawa mwenye umri wa miaka 36 sasa, mzaliwa wa Bingerville, Ivory Coast aliagwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu jana Simba ikishinda 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kutua Simba mwaka 2017 akitokea El-Merreikh ya Sudan ambako alikuwa anacheza kwa mara ya pili.
Haswa kisoka aliibukia ASEC Mimosas mwaka 2003 ambako alicheza hadi 2010 alipokwenda El-Merreikh alikocheza hadi 2014 akahamia Azam FC ya Dar es Salaam.
Mwaka 2016 alirejea Al-Merrikh kwa msimun mmoja, kabla ya kurejea Tanzania na kujiunga na Simba SC.
Katika kipindi hicho cha miaka mitano, Wawa ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu akiwa na Simba,   2017–18, 2018–19, 2019–20 na 2020–21, Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mawili, 2019–20 na 2020–2021, Ngao za Jamii nne 2017, 2018, 2019 na 2020 na Kombe la Mapinduzi mara tatu, 2011, 2015 na 2022.
Lakini pia amewezesha Simba kufika Robo Fainali ya Ligi Mabingwa mara mbili, 2018–19 na 2020–21 pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.





Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA