Posts

Showing posts from November, 2020

AZAM FC YATANGULIA KIPINDI CHA KWANZA, BIASHARA UNITED WACHOMOA KIPINDI CHA PILI, 1-1

Image
AZAM FC imetoa sare ya 1-1 na wenyeji, Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume Musoma mkoani Mara. Ayoub Lyanga alianza kuifungia Azam FC dakika ya 20, lakini Timothy Omwenga akaisawazishia Biashara United dakika ya 59. Azam FC iliyokuwa inacheza mechi ya kwanza baada ya kumfukuza kocha wake Mromania, Aristica Cioaba, inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 13 na kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikizidiwa pointi tano na vinara, Yanga SC. Biashara United yenyewe inafikisha pointi 19 baada ya mechi 13 pia na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya saba, ikiizidi KMC pointi moja, ambayo hata hivyo ina mechi mbili mkononi. 

NGORONGORO HEROES YAICHAPA SUDAN KUSINI 1-0, KUMENYANA NA UGANDA FAINALI CECAFA U-20

Image
TANZANIA imefanikiwa kwenda Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini jioni ya leo Uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu mkoani Arusha. Pongezi kwa mfungaji wa bao pekee la Tanzania Kassim Haruna dakika ya 56 na sasa Ngorongoro Heroes itamenyana na Uganda katika fainali iliyoitoa Kenya. Katika Nusu Fainali ya kwanza, The Kobs waliichapa Kenya 3-1 hapo hapo Uwanja wa Black Rhino Academy na watamenyana na Tanzania Jumatano.

DIOP WA SENEGAL ALIYEWATUNGUA WAFARANSA 2002 AFARIKI DUNIA

Image
KIUNGO wa zamani wa Senegal, Papa Bouba Diop amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 42 baada ya kuugua kwa muda mrefu kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo jana. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Senegal, Victor Ciss amethibitisha kifo cha mchezaji huyo na Rais wa Senegal, Macky Sall amesema kupitia akaunti yake ya Twitterjana kwamba; "Ni msiba mkubwa kwa nchi,". ]]alijipatia umaarufu mkubwa baada ya kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Ufaransa kwenye mchezo wa ufunguzi wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002. Kikosi cha Senegal mwaka huo kilifanikiwa kufika hatua Robo Fainali ya michuano hiyo kabla ya kutolewa na Uturuki. Diop pia alikuwemo kwenye kikosi cha Simba wa Teranga kilichofungwa na Cameroon kwa mikwaju ya penalti mwaka 2002 katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Alitwaa Kombe la FA England akiwa na Portsmouth mwaka 2008, wakati pia aling'ara akiwa na klabu za Lens ya Ufaransa, Fulham, West Ham United

CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA TOTTENHAM STAMFORD BRIDGE

Image
Vita ya Wafaransa; Tanguy Ndombele wa Tottenham Hotspur akimtoka kiungo mwenzake Mfaransa, N'Golo Kante wa Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Stamford Bridge, London timu zao zikitoka sare ya bila kufungana  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

ARSENAL WAPIGWA MECHI YA TANO MSIMU HUU, WACHAPWA 2-1 NA WOLVES

Image
TIMU ya Arsenal jana imechapwa mabao 2-1 na Wolverhampton Wanderers kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates, London. Mabao ya Wolves yalifungwa na Pedro Neto dakika ya 27 na Daniel Podence dakika ya 42, wakati la Wolves lilifungwa na Gabriel Magalhaes dakika ya 30 hicho kikiwa kipigo cha tano kwa Washika Bunduki wa London katika mechi 10 walizocheza msimu huu kwenye ligi  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

MSHAMBULIAJI TEGEMEO WA AZAM FC, PRINCE DUBE MPUMELELO ALIVYOKWENDA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

Image
  Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube Mpumelelo, akiwa safarini kuelekea nchini Afrika Kusini jana alfajiri, kufanyiwa matibabu ya mkono wake wa kushoto alioumia kwenye mechi ya Ligi Kuu yaTanzania Bara dhidi ya Yanga Novemba 25. Mzimbabwe huyo atafanyiwa matibabu katika hospitali ya Vincent Pallotti Jijini Cape Town, ambako wachezaji wote wa Azam FC wamekuwa wakitibiwa hapo kwa ufanisi mkubwa.

SIMBA SC YAWAZIMA WANIGERIA KWAO, YAWACHAPA PLATEAU UNITED 1-0 MFUNGAJI CHAMA JOS

Image
Na Mwandishi Wetu, JOS SIMBA SC imetanguliza mguu mmoja mbele Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Plateau United jioni ya leo Uwanja wa Kimataifa wa Jos International, Jijini Jos nchini Nigeria Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mzambia Clatous Chota Chama dakija ya 53 akimalizia kazi nzuri ya winga kutoka Msumbiji, Luis Jose Miquissone. Sasa mabingwa wa Tanzania watakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Wakifanikiwa kuitoa Plateau United, SImba SC watakutana na mshindi kati ya Costa do Sol ya Msumbiji na Platinum FC ya Zimbabwe kuwania kuingia Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi. Mechi ya kwanza jana, Platinum FC walishinda 2-1 ugenini Uwanja wa Taifa wa Zimpeto Jijini Maputo, Msumbiji na timu hizo zitarudiana Desemba 5 Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare, Zimbabwe.  Kikosi cha Plateau United kilikuwa; Adamu Abubakar, Ibrahim Babawo, Denni

CAVANI ATOKEA BENCHI NA KUIFUNGIA MABAO MAWILI MAN UNITED IKITOKA NYUMA NA KUSHINDA 3-2

Image
Edinson Cavani akishangilia baada ya kutokea benchi na kufunga mabao mawili ndani ya dakika 15 za mwisho, Manchester United ikitoka nyuma kwa 2-0 na kushinda 3-2 dhidi ya wenyeji, Southampton kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. Mary's. Cavani aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mason Greenwood alifunga mabao yake dakika za 74 na 90 na ushei baada ya Bruno Fernandes kufunga la kwanza dakika ya 59 kufuatia Southampton kutangulia kwa mabao ya Jan Bednarek dakika ya 23 na James Ward-Prowse dakika ya 33   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MESSI AMUENZI MARADONA BAADA YA KUFUNGA BAO LA NNE BARCELONA IKISHINDA 4-0 LA LIGA

Image
Lionel Messi akionyesha ishara ya kumuenzi Diego Maradona aliyefariki dunia Jumatano kwao, Argentina baada ya kuifungia Barcelona bao la nne dakika ya 73 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Osasuna kwenye mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Nou Camp. Mabao mengine ya Barcelona yamefungwa na Martin Braithwaite dakika ya 29, Antoine Griezmann dakika ya 42 na Philippe Coutinho dakika ya 57 na kwa ushindi huo, Barca inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi tisa na sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa La Liga ikixidiwa pointi tisa na vinara, Real Sociedad   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

POLISI TZ YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA COASTAL UNION MOSHI, PRISONS YAICHAPA MWADUI FC 2-0 SUMBAWANGA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Coastal Union ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar e Salaam. Tariq Seif Kiakala alianza kuifungia Polisi Tanzania dakika ya 50, kabla ya Raizin Hafidh kuisawazishia Coastal Union dakika ya 75.  Polisi Tanzania inafikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 13, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa pointi tatu na zote, Ruvu Shooting na Simba SC zinazofuatana nafasi ya tatu na ya nne, wakati Coastal Union inafikisha pointi 16 baada ya mechi 13 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11. Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting ya Pwani imelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Ruvu Shooting imefikisha pointi 23 baada ya mechi 13 pia na kuendelea kukamata nafasi ya nne, nyuma ya Simba SC yenye pointi 23 za mechi 11. Katika mchezo uliotangulia mchana, Tanzania Prisons iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa N

MLANDEGE YACHAPWA 5-0 NA CS SFAXIEN YA TUNISIA PALE PALE ZANZIBAR LIGI YA MABINGWA

Image
Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR TIMU ya Mlandege FC ya Zanzibar imeanza vibaya michuano ya Afrika, baada ya kuchapwa 5-0 na CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezi wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa jana uwanja wa Amaan, Zanzibar. Baada ya kipigo hicho, sasa Mlandege itatakiwa kwenda kushinda kuanzia 6-0 kwenye mchezo wa marudiano Tunisia ili kusonga mbele Ligi ya Mabingwa. Mshambuliaji Mnigriaa Eduwo Kingsley alifunga bao la kwanza dakika ya 30, kabla ya Watunisia, beki Hani Amamou kufunga la pili dakika ya 41 na mshambuliaji Firas Chaouat kufunga matatu mfululizo dakika ya 56, 78 na 84. Juzi, Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Kombe la Shirikisho, KVZ walichapwa 1-0 na Alamal Atbara, bao pekee la Captain Basheer dakika ya 12, Uwanja wa Al-Hilal mjini Omdurman, Sudan. Tanzania Bara, Namungo FC wao walianza vyema Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Al Rabita ya Sudan Kusini usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji Dar es Salaam. Mabao ya Namu

HAZARD AUMIA, REAL MADRID YACHAPWA 2-1 NYUMBANI NA ALAVES

Image
Eden Hazard akiwa chini baada ya kuumia kabla ya kutolewa nafasi yake ikichukuliwa na  Rodrygo dakika ya 28  katika mchezo wa La Liga Real Madrid ikichapwa 2-1 na Deportivo Alavés kwenye mchezo wa La Liga jana Uwanja Alfredo Di Stéfano. Mabao ya Deportivo Alavés yalifungwa na Lucas Pérez kwa penalti dakika ua tano na Joselu dakika ya 49, baada ya Casemiro kuifungia la kufutia machozi Reakl Madrid dakika ya 86   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MIKE TYSON AREJEA ULINGONI NA KUMSHUGHULIKIA ROY JONES JR

Image
Mike Tyson (kushoto) akimsukumia konde Roy Jones Jr katika pambano la raundi nane la kukumbushia enzi zao asubuhi ya leo ukumbi wa Staples Center Jijini Los Angeles ambalo majaji walitoa maamuzi ni droo. Pamoja na hayo, mashabiki waliwakosoa majaji, wakidai Mike Tyson aliyekuwa anapigana baada ya miaka 15 ameshinda. Baada ya pambano hilo na Jones Jr mwenye umri wa miaka 51, Tyson mwenye miaka 54 amesema ataendelea kupigana 'mapambano ya kirafiki' kama hayo   PICHA ZADI GONGA HAPA

YANGA SC 1-0 JKT TANZANIA (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
 

NAMUNGO FC WAANZA VYEMA MICHUANO YA AFRIKA, YAWATANDIKA WASUDAN KUSINI 3-0 CHAMAZI

Image
 TIMU ya Namungo FC imeanza vyema Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Al Rabita ya Sudan Kusini usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji Dar es Salaam. Mabao ya Namungo FC katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Awali yamefungwa ma Mghana Steven Sey dakika ya 20 na 39 na Shiza Kichuya dakika ya 64 na timu hizo zitarudiana wiki ijayo Sudan Kusini. x

MAHREZ APIGA HAT TRICK MAN CITY YAICHAPA BURNLEY 5-0 ETIHAD

Image
Nyota wa Algeria, Riyad Mahrez akishangilia baada ya kuifungia mabao matatu Manchester City dakika za sita 22 na 69 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad, mabao mengine yakifungwa na Benjamin Mendy dakika ya 41 na Ferran Torres dakika ya 66   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

VAR YAKATAA MABAO YA SALAH, MANE LIVERPOOL YATOA SARE 1-1 NA BRIGHTON

Image
Kiungo Pascal Gross akiifungia Brighton & Hove Albion bao la kusawazisha kwa penalti dakika ya 90 na ushei katika sare ya 1-1 na Liverpool iliyotangulia kwa bao la Diogo Jota dakika ya 60 Uwanja wa The Amex jana.  Katika mchezo huo, Neal Maupay wa Brighton alikosa penalti dakika ya 20 ambayo ilienda juu ya lango, wakati Mohamed Salah na Sadio Mane wote walifunga mabao yaliyokataliwa kwa msaada wa VAR   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

KASEKE TENA, YANGA SC YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 NA KUJINAFASI KILELENI LIGI KUU TZ BARA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM YANGA SC imejiweka sawa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Yanga SC inayofundishwa na kocha Mrundi, Cedric Kaze inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 13 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya Azam FC wanaofuatia, ingawa wana mechi moja mkononi. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abel William wa Arusha, aliyesaidiwa na Sunday Komba wa Kilimanjaro na Hamdan Said wa Mtwara, bao pekee la Yanga SC limefungwa na kiungo Desu Kaseke dakika ya 33 akimalizia pasi ya Mburkinabe Yacouba Sogne. Huu ni ushindi wa pili mfululizo ukitokana na bao la Kaseke kwa pasi yule yule Yacouba baada ya ushindi wa 1-0 pia dhidi ya Azam FC katikati ya wiki, kufuatia sare tatu mfululizo 0-0 na Gwambina, 1-1 na Simba SC na 1-1 na Namungo FC. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Dodoma Jiji FC imeichapa Ihefu SC 3-0, mabao

SIMBA SC WAKIJIFUA MJINI JOS KABLA YA KUWAVAA PLATEAU UNITED KESHO KATIKA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
Beki wa Simba SC, Josh Onyango akiwa mazoezini leo mjini Jos, Nigeria wakijiandaa na mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Plateau United kesho   Na hapa ni wachezaji wa Simba SC wakipata chakula kuelekea mchezo dhidi ya wenyeji, Plateau United kesho  

KIKOSI CHA AZAM FC KILIVYOWASILI MUSOMA LEO TAYARI KUWAVAA BIASHARA UNITED JUMATATU KARUME

Image
  Kipa wa Azam FC, David Mapigano  kisu baada ya kikosi cha Azam FC kuwasili mjini Musoma mkoani= Mara leo mchana tayari kwa mchezo wake wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Biashara United Jumatatu Uwanja wa Karume mjini humo.

CAF YARUHUSU MASHABIKI ASILIMIA 50 KUINGIA MECHI ZA MICHUANO YA AFRIKA ZA KLABU ZA TANZANIA

Image
  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeridhia asilimia 50 ya mashabiki kuingia uwanjani kushuhudia michezo ya Raundi ya Awali michuano ya Afrika, itakayozihusisha Namungo FC leo na Simba SC wiki ijayo.

IBRAHIM CLASS AMSHINDA KWA POINTI MZAMBIA NA KUTETEA TAJI

Image
Refa akimuinua mkono Bondia Mtanzania, Ibrahim Class baada ya kumshinda kwa pointi, Mzambia Mzambia, Simon Ngoma kwenye pambano la Raundi 10 ukumbi wa PTA, Saba Saba na kufanikiwa kutetea mkanda wake wa GBC uzito wa Feather Ibrahim Class akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumshinda kwa pointi, Mzambia Mzambia, Simon Ngoma  Ibrahim Class akivalishwa mkanda wake baada ya ushindi wa jana ukumbi wa PTA, Saba Saba

AL AHLY YAIPIGA ZAMALEK 2-1 NA KUTWAA TAJI LA TISA LIGI YA MABINGWA

Image
TIMU ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa taji la tisa la rekodi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya mahasimu wao wa nyumbani, Zamalek Uwanja wa KImataifawa Cairo, Misri usiku wa jana. Shujaa wa Al Ahly jana alikuwa ni Mohamed Madgy Afsha aliyefunga bao zuri la ushindi zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika. Fainali hiyo ya mahasimu wa Cairo, ambayo inakuwa ya kwanza kukutanisha timu za nchi moja kwenye historia ya michuano hiyo, ilikaribia kumalizika kwa sare kabla ya Magdy kuwakabidhi Mashetani Wekundu taji. Amr Al Sulaya alianza kuifungia Al Ahly dakika ya tano, kabla ya Mahmoud Abdel Razek Fadlallah 'Shikabala' kuisawazishia Zamalek dakika ya 31.  Kwa Kocha Pitso Mosimane aliyejiunga na Ahly kiasi cha miezi mitatu iliyopita, hilo linakuwa taji lake la pili la Ligi ya Mabingwa, akiifunga timu ile ile baada ya awali kutwaa Kombe hilo mwaka 2016 alipokuwa Mamelodi Sundowns ya kwao, Afrika Kusini. Ahly pia imeendeleza rekodi ya kutofungwa na timu za nyum

KIKAO CHA MCHAKATO WA MABADILIKO YA MFUMO WA UENDESHAJI NDANI YA YANGA SC CHAFANA LEO

Image
  Wajumbe katika picha ya pamoja baada ya kikao cha kupitia ripoti ya mapendekezo ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga yanayofanyika katika makao makuu ya La Liga mjini Madrid nchini Hispania. Kikao hicho kimehudhuriwa na; Mhandisi Hersi Said kutoka Yanga, Marco De Santis Meneja Miradi wa LaLiga Afrika, Juan Botella Meneja wa LaLiga Africa na Alvaro Paya Mwanamsafara wa LaLiga Tanzania na Rwanda,