DIOP WA SENEGAL ALIYEWATUNGUA WAFARANSA 2002 AFARIKI DUNIA

KIUNGO wa zamani wa Senegal, Papa Bouba Diop amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 42 baada ya kuugua kwa muda mrefu kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo jana.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Senegal, Victor Ciss amethibitisha kifo cha mchezaji huyo na Rais wa Senegal, Macky Sall amesema kupitia akaunti yake ya Twitterjana kwamba; "Ni msiba mkubwa kwa nchi,".
]]alijipatia umaarufu mkubwa baada ya kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Ufaransa kwenye mchezo wa ufunguzi wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002.


Kikosi cha Senegal mwaka huo kilifanikiwa kufika hatua Robo Fainali ya michuano hiyo kabla ya kutolewa na Uturuki.
Diop pia alikuwemo kwenye kikosi cha Simba wa Teranga kilichofungwa na Cameroon kwa mikwaju ya penalti mwaka 2002 katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Alitwaa Kombe la FA England akiwa na Portsmouth mwaka 2008, wakati pia aling'ara akiwa na klabu za Lens ya Ufaransa, Fulham, West Ham United na Birmingham City za England pia.




Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA