Posts

Showing posts from March, 2021

PAULINE GEKUL NAIBU WAZIRI MPYA WA MICHEZO, ULEGA AREJESHWA MIFUGO NA UVUVI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samiah Suluhu Hassan amemteua Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Abdallah Ulega ambaye amerejeshwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa Naibu Waziri. Awali, Pauline aliyezaliwa Septemba 25, mwaka 1978 ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini tangu mwaka 2015 – mpaka sasa alikuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi tangu mwaka jana.

MWANAYANGA NA MMILIKI WA SINGIDA UNITED, DK MWIGULU NCHEMBA ACHUKUA NAFASI YA DK MPANGO WIZARA YA FEDHA

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samiah Suluhu Hassan amemteua Dk Mwigulu Lameck Nchemba, Mlezi wa klabu ya Singida United kuwa Waziri wa Fedha, nafasi iliyoachwa wazi na Dk Philip Isdori Mpango aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais.  Awali, Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi na mpenzi wa klabu ya Yanga alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria baada ya pia kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi.

AFRIKA MASHARIKI WATAZAMAJI FAINALI ZA AFCON 2022 CAMEROON

Image
NCHI zote za Afrika, Tanzania, Kenya na Uganda zitakuwa watazamaji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika kati ya Januari na Februari mwakani nchini Cameroon. Kutokana wa CECAFA (Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati) ni Sudan na Ethiopia pekee zimefuzu, wakati Comoro imeandika historia kwa kufuzu kwa mara ya kwanza. Timu nyingine zilizofuzu ni wenyeji, Cameroon, mabingwa watetezi, Algeria, Senegal, Mali, Tunisia, Burkina Faso, Guinea, Gabon, Gambia, Misri, Ghana, Equatorial Guinea, Zimbabwe, Ivory Coast, Morocco, Nigeria, Malawi, Mauritania, Guinea-Bissau na Cape Verde.

RONALDO NA JOTA WAFUNGA URENO YAICHAPA LUXEMBOURG 3-1

Image
URENO imeichapa Luxembourg 3-1 katika mchezo wa A kufuzu Kombe la Dunia jana Uwanja wa Josy Barthel, Luxembourg. Mabao ya Ureno yalifungwa na Diogo Jota dakika ya 45, Cristiano Ronaldo dakika ya 50 na Joao Palhinha dakika ya 80, wakati la Luxembourg lilifungwa na Gerson Rodrigues dakika ya 30. Kwa ushindi huo, Ureno inafikisha pointi saba, sawa na Serbia, baada ya wote kucheza mechi tatu, wakati Luxembourg inabaki na pointi zake tatu katika nafasiya tatu, ikifuatiwa na Jamhuri ya Ireland na Azerbaijan hazina pointi   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

UBELGIJI YAICHAPA BELARUS 8-0 KUFUZU KOMBE LA DUNIA

Image
LICHA ya kuwapumzisha nyota wake kama Kevin De Bruyne, Romelu Lukaku na Dries Mertens, lakini Ubelgiji jana iliwachapa Belarus 8-0 katika mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia Uwanja wa King Power at Den Dreef, Heverlee. Mabao ya Ubelgiji yalifungwa na Michy Batshuayi moja, Hans Vanaken, Leandro Trossard kila mmoja mawili, Jeremy Doku, Denis Praet na Christian Benteke moja kila mmoja. Kwa ushindi huo wanafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi ya Jamhuri ya Czech inayofuatia, wakati Belarus inabaki na pointi zake tatu sawa na Wales, huku Estonia ambayo haina pointi inashika mkia   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

TANZANIA YAJIWEKA PAZURI KUFUZU AFCON YA SOKA LA UFKWENI BAADA YA KUIPIGA BURUNDI 8-3

Image
TANZANIA jana imeichapa Burundi 8-3 katika mcheza wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa soka la Ufukweni (AFCON - Beach Soccer) mwakani, 2022 uliofanyika Ufukwe wa Coco, Dar es Salaa. Baaaa ya mchezo huo wa jana, timu hizo zitarudiana Aprili 3 na mshindi wa jumla atasonga mbele.

ALIYELISIFIA BAO LA MORRISON BUNGENI ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan amewasilisha jina la Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa nchi. Mpango alijipatia umaarufu mkubwa kwa wapenzi wa michezo baada ya kusifia bao la Mghana Bernard Morrison aliloifungia Yanga katika ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wa jadi, Simba Machi 18 mwaka jana Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Dk Mpango alilisifu bao hilo wakati hotuba ya kufungia Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2020-2021 Bungeni Jijini Dodoma Juni mwaka jana. Dk Mpango alikumbushia bao hilo siku huyo, huku akiwapiga kijembe kimtindo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndungai na Naibu wake, Dk Tulia Ackson wakati akimwagia sifa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Dk John Magufuli. "Mheshimiwa Spika, mwisho,  japo si kwa umuhimu Rais wetu ni mkakamavu na mpezni wa maendeleo ya michezo nchini," alisema Dk Mpango na kuongeza kwenye kufungia hotuba yake kwa

MKENYA RAZACK SIWA ASAINI MKATABA WA KUWA KOCHA WA MAKIPA WA KLABU YA YANGA

Image
KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga SC, Hajji Mfikirwa akiwa ameshika nakala za mkataba pamoja na Razak Siwa (kulia) baada ya Mkenya huyo kuajiriwa kama kocha wa makipa wa klabu hiyo leo Dar es Salaam

MBAPPE AKOSA PENALTI, LAKINI UFARANSA YASHINDA 2-0 UGENINI

Image
PAMOJA na mshambuliaji wake nyota, Kylian Mbappe kukosa penalti dakika ya 75, lakini Ufaransa jana iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Kazakhstan mabao ya Ousmane Dembele dakika ya 19 na Sergiy Maliy aliyejifunga dakika ya 44 katika mchezo wa Kundi D kufuzu Fainali za Kombe la Dunia Uwanja wa Astana Arena mjini Nur-Sultan. Mabingwa wa dunia, Ufaransa wanafikisha pointi wanafikisha pointi nne baada ya mechi mbili na kuendelea kuongoza kundi kwa pointi mbili zaidi ya Finland na Ukraine, wakati Bosnia-Herzegovina ina pointi moja na Kazakhstan haina kitu   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

UJERUMANI YAICHAPA ROMANIA 1-0 KUFUZU KOMBE LA DUNIA

Image
BAO pekee la Serge Gnabry dakika ya 16 jana liliipa Ujerumani ushindi wa 1-0 dhidi ya Romania Uwanja wa Taifa wa Bucuresti katika mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia kwa bara la Ulaya. Ujerumani inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili za awali na kuendelea kuongoza Kundi kwa wastani tu dhidi ya Armenia inayofuatia, zikifuatiwa na Macedonia Kaskazini Romania zenye pointi tatu kila moja, wakati Iceland na Liechtenstein hazina pointi   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

TANZANIA 1-0 LIBYA (KUFUZU AFCON DAR)

Image
 

TAIFA STARS YAKAMILISHA MECHI ZAKE ZA KUFUZU AFCON KWA KUICHAPA LIBYA 1-0 BAO PEKEE LA MSUVA

Image
TANZANIA imekamilisha mechi zake za Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Libya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Wydad Club Athletic ya Morocco, Simon Happygod Msuva aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 45. Pamoja na ushindi huo, Taifa Stars haijafuzu AFCON kufuatia kuzidiwa kete na Tunisia na Equatorial Guinea zilizoshika nafasi mbili za kwanza na kukata tiketi ya Cameroon mwakani. Tanzania inamaliza nafasi ya tatu kwa pointi zake saba, nyuma ya Equatorial Guinea yenye pointi tisa, Tunisia pointi 16, wakati Libya yenye pointi tatu imeshika mkia. x

EQUTORIAL GUINEA 1-0 TANZANIA (KUFUZU AFCON)

Image
 

WACHEZAJI WA AZAM FC WANAVYOENDELEA KUJIFUA KUJIWEKA SAWA KUIVAA MTIBWA SUGAR APRILI 6 CHAMAZI

Image
Abdalllah Kheri (kushoto) akimdhibiti beki mwenzake, Mzimbabwe Bruce Kangwa katika mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mechi yao ijayo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Aprili 6 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam 

TAIFA STARS YATUPWA NJE AFCON YA CAMEROON MWAKANI BAADA YA KUPIGWA 1-0 NA EQUATORIAL GUINEA MJINI MALABO

Image
TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Equatorial Guinea jana Uwanja wa Nuevo do Malabo. Katika mchezo huo wa Kundi D kuwania tiketi ya AFCON ya mwakani Cameroon, bao pekee la Equatorial Guinea lilifungwa na Nahodha wake, Emilio Nsue Lopez dakika ya 90. Sasa Equatorial Guinea inafikisha pointi tisa na kuendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Tunisia zote zikifuzu AFCON ya mwakani.  Tanzania inabaki nafasi ya tatu na itamenyana na Libya wiki ijayo Dar es Salaam kukamilisha ratiba.

UFARANSA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA UKRAINE KUFUZU KOMBE LA DUNIA

Image
UFARANSA imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ukraine katika mchezo wa kwanza wa Kundi D kufuzu Kombe la Dunia kwa Ulaya jana Uwanja wa Stade de France Jijini Paris. Mshambuliaji wa Barcelona, Antoine Griezmann alianza kuwafungia mabingwa hao wa dunia dakika ya 19, kabla ya beki wa PSG, Presnel Kimpembe kujifunga dakika ya 57 kuwapatia bao la kusawazisha Ukraine. Kwa matokeo hayo, Ufaransa timu hizo zinaungana na Bosnia-Herzegovina na Finland kuanza na pointi moja baada ya nao kutoka sare ya 2-2 jana Uwanja wa Helsingin Jijini Helsinki, wakati Kazakhstan ambayo haijacheza haina pointi   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

BOSI WA SIMBA SC, MO DEWJI ALIVYOMUAGA ALIYEKUWA RAIS WA TANZANIA DK JOHN POMBE MAGUFULI

Image
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mohamed 'Mo' Dewji akiuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, mwaka huu juzi uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam

TAIFA STARS KATIKA MAZOEZI YA MWISHO NAIROBI KABLA YA KUWAFUATA EQUATORIAL GUINEA MECHI YA KUFUZU AFCON MALABO

Image
WACHEZAJI wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakifanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Chuo cha Utalii, Nairobi, Kenya, kabla ya kusafiri kwenda Malabo kumenyana na wenyeji, Equatorial Guinea Machi 25 katika mchezo wa Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon 

ARSENAL YATOKA NYUMA 3-0 KUPATA SARE YA 3-3 NA WEST HAM

Image
TIMU ya Arsenal jana imetoka nyuma kwa mabao matatu na kupata sare ya 3-3 na West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa London. West Ham walitangulia kwa mabao ya Jesse Lingard dakika ya 15, Jarrod Bowen dakika ya 17 na Tomas Soucek dakika ya 32. Mabao ya Arsenal yalifungwa na Soucek dakika ya 38 na Craig Dawson dakika ya 61 wote wakijifunga na Alexandre Lacazette dakika ya 82

LEICESTER CITY YAIKONG'OTA MAN UNITED 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND

Image
TIMU ya Leicester City imetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester United Uwanja wa King Power, Leicestershire. Mabao ya Leicester yalifungwa na Kelechi Iheanacho dakika ya 24 na 78 na Youri Tielemans dakika ya 52, wakati la Man United lilifungwa na Mason Greenwood dakika ya 38. Sasa Laicester City itakutana na Southampton katika Nusu Fainali wakati Chelsea iliyoitoa Sheffield United itakutana na Manchester City iliyoitoa Everton Aprili 17.

BOSI MKUBWA WA AZAM FC AUNGANA NA WATANZANIA WENGINE KUMUAGA ALIYEKUWA RAIS WA TANZANIA DK JOHN MAGUFULI

Image
Mtendaji Mkuu wa Bakhresa Group, Abubakar Bakhresa (katikati), wamiliki wa Azam FC akiwa na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Hussein Sufiani Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, mwaka huu

WACHEZAJI WA YANGA SC WALIVYOUAGA MWILI WA ALIYEKUWA RAIS WA TANZANIA, DK JOHN POMBE MAGUFULI

Image
  KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Abdul Razak Fiston akiwoangoza wachezaji wenzake na Maafisa mbalimbali kwenda kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, mwaka huu leo uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla kiwoangoza wachezaji wenzake na Maafisa mbalimbali kwenda kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli