Posts

Showing posts from February, 2024

NI LIVERPOOL NA MAN UNITED ROBO FAINALI FA ENGLAND

Image
VIGOGO, Chelsea, Manchester United, Manchester City na Liverpool wamefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali Kombe la FA England. Manchester City juzi waliwatandika wenyeji, Luton Town mabao 6-2 Uwanja wa Kenilworth Road mjini Luton, Bedfordshire, mshambuliaji Mnorway, Erling Braut Haaland akifunga mabao matano dakika ya tatu, 18, 40, 56 na 58. Bao lingine la Manchester City lilifungwa na kiungo Mcroatia, Mateo Kovačić, huku mabao yote ya Luton Town yakifungwa na kiungo Muingereza, Jordan Charles Clark dakika ya 45 na 52.  Jana Chelsea ikaichapa Leeds United 3-1 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Mabao ya Chelsea yalifungwa na mshambuliaji Msenegal, Nicolas Jackson dakika ya 15, winga wa Ukraine, Mykhailo Mudryk dakika ya 37 na kiungo Muingereza, Conor John Gallagher, wakati ya Leeds United yalifungwa na mshambuliaji Mspaniola, Mateo Joseph dakika ya nane na 59. Nayo Manchester United ikaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest bao pekee la Casemiro dakik

SIMBA SC 6-0 TRA (KOMBE LA TFF)

Image
 

PRISONS YAKWEA TANO BORA LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA TABORA UNITED 2-1

Image
TIMU ya Tanzania Prisons jana iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Tanzania Prisons yalifungwa na Zabona Mayombya dakika ya 21 na Samson Mbangula dakika ya 88, huku bao pekee la Tabora United likifungwa na Erick Okutu dakika ya 17. Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya tano, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 18 nayo inabaki nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 18.

IHEFU SC YABANWA NYUMBANI, YATOA SARE NA MSHUJAA 1-1

Image
WENYEJI, Ihefu SC jana wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja LITI mjini Singida. Mshambuliaji Mkenya, Elvis Rupia alianza kuifungia Ihefu SC dakika ya 11, kabla ya Omary Omary kuisawazishia Mashujaa dakika ya 73. Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi 20, japokuwa inabaki nafasi ya 11 na Mashujaa inatimiza pointi 15, ingawa inabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 18. 

SIMBA SC YAIFUMUA TRA 6-0 AZAM FEDERATION CUP

Image
TIMU ya Simba SC imefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 6-0 dhidi ya TRA ya Kilimanjaro leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba yamefungwa na Ladack Chasambi dakika ya 13, Freddy Michael Kouablan dakika 51, Sadio Kanoute dakika ya 39, 53 na 54 na Pa Omary Jobe dakika ya 71.

GEITA GOLD YATOKA SULUHU NA KAGERA SUGAR NYANKUMBU

Image
WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya bila mabao na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa sekondari ya Nyankumbu mjini Geita. Kwa suluhu hiyo, Geita Gold inafikisha pointi 17 katika nafasi ya 14 na Kagera Sugar inafikisha pointi 22, ingawa inabaki nafasi ya saba baada ya timu zote kucheza mechi 18.

MTIBWA SUGAR MAMBO MAGUMU, YABANWA MANUNGU

Image
WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya bila mabao na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi tisa, ingawa inaendelea kushika mkia kwenye ligi, wakati Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 20 na inabaki nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 17.

JKT TANZANIA NA KMC HAKUNA MBABE, 0-0 MBWENI

Image
WENYEJI, JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam. Kiungo Najim Magulu alianza kuifungia JKT Tanzania dakika ya nane, kabla ya mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda kuisawazishia KMC dakika ya 40. Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 18, ingawa inabaki nafasi ya 12, wakati KMC imetimiza pointi 24 katika mchezo wa 18 nayo inabaki nafasi ya tano.