Posts

Showing posts from January, 2021

SIMBA SC WATWAA KOMBE LA KWANZA 2021 BAADA YA KUTOA SARE YA 0-0 NA TP MAZEMBE YA DRC LEO DAR

Image
WENYEJI, Simba SC wametwaa taji la Simba Super Cup licha ya kulazimishwa sare ya 0-0 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo Simba SC inamaliza na pointi nne kufuatia ushindi wa 4-1 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Al Hilal ya Sudan Jumatano hapo hapo kwa Mkapa. Hilal ya Sudan imemaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tatu baada ya kuichapa Mazembe 2-1 Ijumaa. Kiungo kutoka Msumbiji, Luis Miquissone aliteuliwa Mchezaji Bora wa Mechi ya leo na kupewa Sh 500,000. Kiungo Mzambia, Larry Bwalya aliteuliwa Mchezaji Bora wa Mashindano, wakati Mfungaji Bora ni winga Mghana, Bernard Morrison aliyepachika mabao mawili na Kipa Bora Beno Kakolanya wote waliapata Sh. Milioni 2 kila mmoja. 

CAMEROON NA MALI ZATINGA NUSU FAINALI CHAN, KONGO ZOTE NJE

Image
WENYEJI Cameroon wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana Uwanja wa Omnisport Jijini Douala. Mabao ya Cameroon jana yalifungwa na Yannick N'Djeng dakika ya 29 na Felix Oukine Tcheoude dakika ya 41, wakati la DRC lilifungwa na Makabi Lilepo dakika ya 2. Nayo Mali ilifanikiwa kwenda Nusu Fainali baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Kongo katika mchezo mwingine wa Robo Fainali jana Uwanja wa Omnisport Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde. Fainali za CHAN zinatarajiwa kuendelea leo Morocco ikimenyana na Zambia Saa 1:00 usiku na Guinea na Rwanda Saa 4:00. Mshindi kati ya Morocco na Zambia atakutana na Mali katika na mshindi kati ya Guinea na Rwanda atamenyana na Cameroon katika Nusu Fainali Jumatano, wakati Fainali itafuatia Jumapili baada ya mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Jumamosi.

ARSENAL YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA MAN UNITED EMIRATES

Image
WENYEJI, Arsenal wamelazimishwa sare ya 0-0 Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Emirates, London  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

MAN CITY YAICHAPA SHEFFIELD 1-0 NA KUZIDI KUPAA KILELENI ENGLAND

Image
BAO pekee la Gabriel Jesus dakika ya tisa akimalizia pasi ya Ferran Torres, jana liliipa ushindi wa 1-0 Manchester City dhidi ya Sheffield United FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 20, sasa wakiongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya mahasimu wao wa Jiji, Manchester United waliotoa sare ya 0-0 na Arsenal jana Uwanja wa Emirates katika mechi yao ya 21   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

MO DEWJI: DHAMIRA YETU NI KUTWAA TENA UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA NA MATAJI YOTE NCHINI

Image
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mohammed 'Mo' Dewji amesema kwamba dhamira yao ni kutetea tena ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara pamoja na kutwaa tena Ngao ya Jamii "Napenda Kuwait aarti fun kwamba sisi katika uongozi wa Simba tumejizatiti na kuweka mikakati ya kuhakikisha tunachukua tena Ubingwa wa Ligi, kuchukua Kombe la FA, na kufika mbali kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika,"amesema na kuongeza; "Pia tunaendelea na mikakati ya kuhakikisha kwamba Klabu yetu inajenga chapa na sifa bora Afrika na kote duniani. Sehemu ya mkakati huo ni haya mashindano tuliyoandaa ya Simba Super Cup, ambayo hadi sasa yamefanikiwa na yamepokelewa vizuri kote Afrika. Nia yetu ni kwamba mashindano haya ya Simba Super Cup tuyafanye kila mwaka,".  "Tayari tumeanza maandalizi ya mashindano haya kwa msimu ujao ambapo tutaongeza idadi ya timu kubwa za Afrika. Nia yetu pia ni kwamba mashindano haya yajiendeshe yenyewe kibiashara. Vyanzo vya fedha za ku
Image
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Fiston Abdul Razak akiwa mazoezini na timu yake mpya, Yanga SC siku moja baada ya kujiunga nayo rasmi jana kufuatia kusaini mkataba wa miezi sita.

SIMBA SC KUMENYANA NA DODOMA JIJI FEBRUARI 2 JAMHURI KABLA YA KUWAVAA AZAM FC FEBRUARI 7 DAR VIPORO VYA LIGI KUU

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC watamenyana na Dodoma FC Februari 2 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kabla ya kuwavaa Azam FC Februari 7, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mechi zao mbili za viporo za Ligi Kui ya Tanzania Bara.

PRINCE DUBE MPUMELELO APIGA MBILI AZAM FC YAICHAPA KMC 3-1 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI

Image
AZAM FC imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube mawili na kiungo mzawa, Mudathir Yahya moja, wakati la KMC limefungwa na Lusajo Mwaikenda kwa penalti.

CAS YAMREJESHA AHMAD MADARAKANI KWA MUDA KAMA RAIS WA CAF

Image
MAHAKAMA ya usuluhishi wa michezo, CAS, imemrudisha kwa muda madarakani Ahmad Ahmad kama Rais wa Shirikisho la soka la Afrika, CAF. Novemba 19 mwaka jana, kamati ya maadili ya Shirikisho la soka duniani, FIFA, ilimfungia Ahmad kujihusisha na soka kwa miaka 5, baada ya kumkuta na hatia ya kukiuka kanuni za maadili za uongozi wa soka. Kifungo hiki kilikuwa na maana kwamba Ahmad hawezi tena kutetea nafasi yake katika uchaguzi mkuu wa CAF utakaofanyika Machi 12. Lakini alikata rufaa CAS na kuomba adhabu yake iondolewe kwanza hadi rufaa yake itakaposikilizwa. Ahmad alitaka afunguliwe ili apate muda wa kuchukua fomu ya kugombea katika uchaguzi mkuu wa CAF. CAS imepanga kuisikiliza rufaa yake Machi 2 mwaka huu, lakini kwa maagizo kwamba adhabu yake iondolewe na arudi madarakani hadi hukumu ya rufaa itakapotoka. Hii sasa itampa fursa Ahmad kuchukua fomu yake na kugombea. Katika kipindi ambacho hakuwa madarakani, majukumu yake yalikaimiwa na makamu wake, Constant Omari, ambaye ni raia

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA CHARLES BONIFACE MKWASA

Image
 

IBRAH CLASS ATWAA TAJI LA WBF BAADA YA KUMDUNDA MMALAWI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM BONDIA Ibrahim Mgendera ‘Ibrah Class’ amefanikiwa kutwaa taji la WBF Intercontinental uzito wa  Super Light baada ya kumshinda Dennis Mwale wa Malawi kwa poonti za majaji wote katika pambano la raundi la 12 usiku wa jana ukumbi wa Next Door Arena, Masaki Jijini Dar es Salaam. Class jana ameshinda pambano la 26 tangu aanze ngumi za kulipwa Juni 26 mwaka 2010, kati ya hayo 11 ameshinda kwa KO, wakati mengine sita amepigwa, matatu kwa TKO.  Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa alikuwepo ukumbini jana na akamvisha Ibrah Class taji hilo jipya ambalo linafanya awe na mikanda minne jumla, mengine WPBF, GBC na AAC (All Africans Champion).  Class amepigwa na Mtanzania mwenzake mmoja tu, Said Zungu Julai 26, mwaka 2010 ukumbi wa Swai Garden Pub Jijini Dar es Salaam katika pambano lake la kwanza kabisa na baada ya hapo, wengine waliomshinda ni wageni tu na tena wakiwa nyumbani kwao. Watanzania wengine wawili waling’a

MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC, FISTON ABDUL RAZAK ALIVYOWASILI LEO DAR BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MIEZI SITA

Image
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Fiston Abdul Razak baada ya kuwasili Dar es Salaam leo kujiunga na klabu ya Yanga kufuatia kusaini mkataba wa miezi sita. Huyo ni mchezaji mpya wa tatu tu kusajili Yanga SC dirisha dogo baada ya Mrundi mwenzake, Said Ntibanzokiza na beki mzawa. Dickson Job kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.

AL HILAL YAZINDUKA NA KUICHAPA TP MAZEMBE 2-1 DAR MICHUANO YA SIMBA SUPER CUP

Image
TIMU ya Al Hilal ya Sudan imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa michuano maalum ya Simba Super Cup leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Al Hilal iliyochapwa 4-1 na wenyeji, Simba SC katika mchezo wa kwanza juzi, yamefungwa na Bonganga Vinny dakika ya 30 na Mohamed Musa dakika ya 90 baada ya TP Mazembe kutangulia kwa bao la Moustapha Kouyate dakika ya 12. Michuano hiyo itakamilishwa Jumapili kwa mchezo kati ya wenyeji, Simba SC na TP Mazembe.

MBWANA SAMATTA NA MCHEZAJI MWENZAKE MPYA, OZIL WAKIJIANDAA NA MECHI YA LIGI KESHO UTURUKI

Image
MSHAMBULIji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta (kushoto) akiwa na mchezaji mwenzake mpya Fenerbahce, kiungo Mjerumani, Mesut Ozil (katikati) kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki kesho dhidi ya Rizespor kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Ulker Fenerbahçe Sukru Saracoglu Sports Complex Jijini Ä°stanbul 

CARLOS CARLINHOS ANAVYOREJEA YANGA SC KAMA MPYA KUONGEZA NGUVU LALA SALAMA LIGI KUU

Image
KIUNGO Muangola, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo, maarufu Carlinhos akiwa mazoezini na timu yake, Yanga SC kwenye kambi yao, Avic Centre, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kuwa nje kwa maumivu tangu Novemba Carlinhos nyuma kabisa kulia akiwa  Yanga SC kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara

NYOTA WAWILI CHIPUKIZI WA TANZANIA WAENDA NCHINI TUNISIA KUJIUNGA NA KLABU YA LIGI KUU

Image
WINGA wa Namungo FC, Abeid Athumani na mshambuliaji wa Azam FC, Paul Peter aliyekuwa anacheza kwa mkopo KMC FC wameondoka jana usiku kwenda Tunisia kujiunga na klabu ya Union Sportive de Tataouine inayoshiriki Ligi kuu nchini humo.

LIVERPOOL YAIPIGA SPURS 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA ENGLAND

Image
TIMU ya Liverpool imefufua matumaini ya ubingwa baada ya ushindi wa 3-1 jana dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Tottenham Hotspur, London. Mabao ya Liverpool yalifungwa na Mbrazil Roberto Firmino dakika ya 45, beki wa England, Trent Alexander-Arnold dakika ya 47 na winga Msenegal, Sadio Mane dakika ya 65, wakati la Spurs lilifungwa na kiungo Mdenmark, Pierre-Emile Hojbjerg dakika ya 49.  Liverpool inafikisha pointi 37 mechi ya 20 nafasi ya nne, inazidiwa pointi nne na Mn City yenye mechi moja mkononi, Tottenham inabaki nafasi ya sita pointi 33 mechi 19   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SIMBA SC 4-1 AL HILAL (SIMBA SUPER CUP)

Image
 

MANCHESTER UNITED YACHAPWA 2-1 NA SHEFFIELD UNITED NYUMBANI

Image
MANCHESTER United jana wamepoteza nafasi ya kurejea kileleni katika Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Sheffield United Uwanja wa Old Trafford. Beki Kean Bryan alianza kuwafungia Sheffield dakika ya 23, kabla ya Nahodha wa Manchester United, Harry Maguire kuisawazishia timu yake dakika ya 64 na mtokea benchi, Oliver Burke akawafungia wageni bao la ushindi dakika 10 baadaye. Manchester United inabaki nafasi ya pili na pointi zake 40 baada ya kucheza mechi 20, ikizidiwa pointi moja na mahasimu wao wa Jiji, Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi 

TAIFA STARS YATOLEWA CHAN BAADA YA SARE YA 2-2 NA GUINEA JIJINI DOUALA

Image
TANZANIA imetupwa nje ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya sare ya 2-2 na Guinea usiku wa Jumatano katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Uwanja wa Reunification Jijini Douala nchini Cameroon. Mabao ya Tanzania yamefungwa na kiungo wa Mtibww Sugar, Baraka Majogoro dakika ya 23 na beki wa Namungo FC, Edward Charles Manyama dakika ya 67, wakati ya Guinea yamefungwa na Barry Yacouba kwa penalti dakika ya tano baada ya mlinzi Carlos Protas kuunawa mpira na la pili Victor Kantabadouno dakika ya 82. Taifa Stars iliyo chini ya kocha Mrundi, Etienne Ndayiragije inamaliza na pointi nne nyuma ya Guinea na Zambia zilizofungana kwa pointi tano kila moja. Baada ya sare ya 0-0 na Zambia katika mchezo wa mwisho Jumatano Uwanja wa Limbe, Namibia inamaliza na pointi moja na kuungana na Tanzania kurejea nyumbani. Sasa Zambia itamenyana na mabingwa watetezi, Morocco na Guinea na Rwanda Jumapili, wakati Robo Fainali nyingine ni Jumamosi Mali na Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya

TFF YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA KUKUZA MIUNDOMBINU YA SOKA NA CHUO CHA UHASIBU MKOANI ARUSHA

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Eliamani Sedokeya wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa maendeleo ya kukuza miundombinu na mpira wa miguu huku wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, kwenye hafla ya utiaji saini iliyofanyika Jumatano ukumbi wa IAA, Arusha. Rais wa TFF Wallace Karia na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Profesa Eliamani Sedokeya wakitia saini makubaliano ya ushirikiano wa maendeleo ya kukuza miundombinu na mpira wa miguu huku wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa, kwenye hafla ya utiaji saini iliyofanyika IAA, Arusha

AFISA HABARI WA YANGA SC, HASSAN BUMBULI AFUNGIWA MIAKA MITATU KUJIBUSISHA NA SOKA NDANI NA NJE YA NCHI

Image
AFISA Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amefungiwa kujishughulisha na soka ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mi tatu kwa tuhuma za kutotii uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

RAIS WA TFF, WALLACE KARIA APITISHWA KUGOMBEA UJUMBE WA BARAZA LA FIFA

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amepitishwa kugombea Ujumbe wa Baraza la Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

YANGA SC YAMTAMBULISHA RASMI NIZAR KHALFAN SAMBAMBA NA KOCHA MPYA WA MAZOEZI YA VIUNGO

Image
KLABU ya Yanga imemtambulisha Edem Mortotsi kuwa kocha wake mpya wa mazoezi ya viungo. Pia imemtambulisha rasmi mchezaji wake wa zamani, Nizar Khalfan kuwa Kocha mpya Msaidizi