LIVERPOOL YAIPIGA SPURS 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA ENGLAND
TIMU ya Liverpool imefufua matumaini ya ubingwa baada ya ushindi wa 3-1 jana dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Tottenham Hotspur, London.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Mbrazil Roberto Firmino dakika ya 45, beki wa England, Trent Alexander-Arnold dakika ya 47 na winga Msenegal, Sadio Mane dakika ya 65, wakati la Spurs lilifungwa na kiungo Mdenmark, Pierre-Emile Hojbjerg dakika ya 49.
Liverpool inafikisha pointi 37 mechi ya 20 nafasi ya nne, inazidiwa pointi nne na Mn City yenye mechi moja mkononi, Tottenham inabaki nafasi ya sita pointi 33 mechi 19 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Comments
Post a Comment