Posts

Showing posts from December, 2022

MAN CITY YAAMBULIA SARE 1-1 KWA EVERTON

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Everton Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland alianza kuifungia Man City dakika ya 24 hilo likiwa bao lake la 27 la msimu, kabla ya Demarai Gray kuisawazishia Everton dakika ya 64. Kwa matokeo hayo, Man City inafikisha pointi 36, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi saba na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 16. Kwa upande wao, Everton wanabaki na pointi zao 15 za mechi 17 nafasi ya 16.

AZAM FC YAMALIZA MWAKA NA USHINDI WA 6-1 DHIDI YA MBEYA CITY

Image
WENYEJI, Azam FC wamefunga mwaka kwa kishindo baada ya kuwatandika Mbeya City mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ mawili dakika ya 22 na 54, Mzimbabwe Prince Dube dakika ya 51, Mkenya Kenneth Muguna dakika ya 56, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 71 na Cleophace Mkandala dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 40, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi nne na Simba na 10 na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 19. Kwa Mbeya City ambayo bao lake pekee la limefungwa na Richardson Ng’ondya dakika ya 78 inabaki na pointi zake 21 za mechi 19 nafasi ya 10.

MTIBWA SUGAR 0-1 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

YANGA YAMALIZA MWAKA KWA USHINDI WA 1-0 MANUNGU

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wameuga mwaka 2022 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 26. Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 50 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya watani, Simba baada ya wote kucheza mechi 19. Kwa upande wao, Mtibwa Sugar baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 24 za mechi 19 nafasi ya nane.

BODI YAFANYA MAREKEBISHO RATIBA LIGI KUU KUPISHA MAPINDUZI CUP

Image
BODI ya Ligi imefanya marekebisho maalum ya ratiba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza mapema mwakani visiwani Zanzibar.

LIVERPOOL YAICHAPA LEICESTER CITY 2-1 ANFIELD

Image
TIMU ya Liverpool imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester City usiku wa Ijumaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield. Liverpool ilinufaika na makosa ya beki wa kati wa Leicester, Wout Faes aliyejifunga mabao yote mawili dakika za 38 na 45 baada ya kiungo Kiernan Dewsbury-Hall kutangulia kuwafungia wageni dakika ya nne. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 16, ingawa inabaki nafasi ya sita wakati Leicester City inabaki na pointi zake 17 za mechi 17 nafasi ya 13.

BOCCO NA NTIBANZOKIZA WAPIGA HAT TRICK SIMBA YAITANDIKA PRISONS 7-1

Image
WENYEJI, Simba SC wamefunga mwaka vizuri baada ya ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mshambuliaji na Nahodha, John Bocco amefunga mabao matatu dakika za 12, 46 na 62 wakati akichezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya, kiungo Mrundi Saido Ntibanzokiza pia amefunga mabao matatu dakika za 60, 63 na lingine limewekwa nyavuni na Shomari Kapombe dakika ya 88. Ni ushindi unaoifanya Simba ifikishe pointi 44 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga SC. Kwa Tanzania Prisons ambayo bao lake limefungwa na Jeremiah Juma dakika ya 29 baada ya kichapo kikali cha leo inabaki na pointi zake 21 za mechi 19 nafasi ya 11.

SINGIDA STARS YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 LITI

Image
WENYEJI, Singida Big Stars wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Mabao ya Singida Big Stars yote yamefungwa na nyota wake wa Kibrazil, Biemes Camo dakika ya 30 na Bruno Gomes kwa penalti dakika ya 80, wakati la Geita Gold limefungwa na Haruna Shamte kwa penalti pia dakika ya 45 na ushei. Kwa matokeo hayo, Singida Big Stars inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC ambao pia wana mechi moja mkononi. Kwa upande wao Geita Gold baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 24 za mechi 19 nafasi ya saba.

AZAM FC YAWATEMA SALULA NA CHILUNDA

Image
KLABU ya Azam FC imetangaza kuachana na wachezaji wake wawili, kipa Ahmed Ali Suleiman ‘Salula’ na mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda. Hao wanaungana na kiungo Ibrahim Hajib Migomba aliyekuwa wa kwanza kutemwa dirisha hili dogo na tayari amejiunga na Singida Big Stars.

10BET TANZANIA YATAJA WASHINDI WA PROMOSHENI YA KOMBE LA DUNIA

Image
KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya 10bet imetangaza wazawadia washindi mbalimbali 50 wa promosheni ya kombe la dunia (WC Bonanza Promotion). Michuano ya kombe la dunia ilifanyika nchini Qatar na timu ya Argentina chini ya nahodha wao, Lionel Messi ilitwaa ubingwa. Meneja Masoko wa kampuni10bet Tanzania George Abdulrahman alisema kuwa kati ya washindi hao 50, washindi 10 walizawadiwa simu janja (smartphones) ambapo washindi wengine 20 walizawadiwa jezi za timu za mataifa mbalimbali yaliyoshiriki katika michuano hiyo na washindi 30 walizawadiwa fedha taslimu. Washindi hao wamefanikiwa kushinda zawadi mbalimbali baada ya kufanikiwa kupata pointi nyingi kati ya maelfu ya mashabiki wa soka waliokuwa wakibashiri matokeo mbalimbali wakati wa michuano hiyo na tayari washindi hao  wamekwisha chukua zawadi zao.  “Tunajisikia fahari kubwa kuwazawadia wmashabiki wa soka walioshiriki kwa kubashiri kupitia michezo  yetu mbalimbali,” alisema Mlay. Mlay pia aliwaomba mashabiki wa soka wenye

MFALME WA SOKA DUNIANI PELE AFARIKI DUNIA

Image
MFALME wa soka duniani, Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’ amefariki dunia jana akiwa ana umri wa miaka 82 baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu. Anasifiwa kwa kufunga mabao 1,281 katika rekodi ya dunia katika mechi 1,363 katika kipindi cha miaka 21 ya maisha yake, yakiwemo mabao 77 katika mechi 92 za nchi yake. Mchezaji pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, akinyakua taji hilo mnamo 1958, 1962 na 1970, Pele alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne wa Fifa mnamo 2000. Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na kibofu katika miaka ya hivi karibuni. Pele alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo wake mnamo Septemba 2021 katika Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo, baada ya uvimbe huo kugunduliwa katika vipimo vya kawaida. Alirejeshwa hospitalini mwishoni mwa Novemba 2022. Binti yake Kely Nascimento amewafahamisha mashabiki kuhusu hali ya babake kwa taarifa za mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kutoka hospitalini. Siku ya Alhamisi alichapis

MAN CITY YAWACHAPA LEEDS UNITED 3-1 ELLAND ROAD

Image
TIMU ya Manchester City jana imewatandika wenyeji, Leeds United mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Elland Road Jijini Leeds, West Yorkshire. Mabao ya Man City yamefungwa na Rodri dakika ya 45 na Erling Haaland mawili dakika ya 51 na 64, wakati la Leeds limefungwa na Pascal Struijk dakika ya 73. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 35, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 15, wakati Leeds United inabaki na pointi zake 15 za mechi 15 nafasi ya 15.

YANGA SC YATUMA BARUA AZAM FC KUWATAKA AKAMINKO NA KIPRE

Image
KLABU ya Yanga SC imewasilisha barua kuomba kumsajili kiungo Mghana, James Akaminko na winga Muivory Coast Kipre Junior wote wa Azam FC.

CHELSEA YAICHAPA BOURNEMOUTH 2-0 DARAJANI

Image
WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Mabao ya The Blues katika mchezo huo yamefungwa na Kai Havertz dakika ya 16 na Mason Mount dakika ya 24 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 24 katika mchezo wa 15 na kusogea nafasi ya nane, wakati AFC Bournemouth inabaki na pointi zake 16 za mechi 16 nafasi ya 14.

TAFSIRI ZA KISHERIA NA SABABU ZA FEISAL KUVUNJA MKATABA YANGA...

Image
Na Oscar Oscar, Dar es Salaam TATIZO kubwa la nchi yetu, kila anayejua Lugha ya Kiingereza anadhani anaweza Kutafsiri Document ya Kisheria.  My dear brothers and sisters, Sheria ina Tafsiri tofauti kabisa na Kiingereza tunachoombea Maji ya kunywa! Feisal anaweza kuvunja Mkataba wake na Yanga wakati wowote lakini ni lazima kuwe na extraordinary circumstances (i.e kacheza chini ya 10% ya mechi zote za Yanga, kama hajalipwa Mshahara kwa miezi miwili mfululizo, kama kuna makubaliano yoyote na Klabu ambayo hayajatekelezwa yenye uwezo wa kuathiri performance yake uwanjani). Ili kifungu alichotumia Feisal kuvunja Mkataba kiwe halali ni lazima mambo hayo hapo juu yote au Moja liwe halijatekelezwa. Kuna chochote Yanga hawajampa? Jibu ni hapana. Kapewa kila kitu. Kinachotusumbua watanzania wengi ni Mentality za Ki-Socialism na Uswahili! Aziz KI akilipwa 20M, na wewe unataka kupewa hiyo hiyo. Bernard Morrison akipewa Gari, na wewe unataka upewe wakati si sehemu ya makubaliano kwenye mkataba

SIMBA SC YAICHAPA KMC 3-1 UWANJA WA CCM KIRUMBA

Image
VIGOGO, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji na Nahodha John Bocco dakika ya 16, winga Mghana Augustine Okrah dakika ya 55 na beki Mkongo, Henock Inonga Baka 'Varane' dakika ya 73, wakati la KMC limefungwa na Sadallah Lipangile dakika ya 52. Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 41, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi sita na mabingwa watetezi, mahasimu wao, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 18. Kwa upande wao KMC baada ya matokeo ya leo wanabaki na pointi zao 22 za mechi 18 pia katika nafasi ya tisa.  

KAGERA SUGAR YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA GEITA GOLD KAITABA

Image
WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya 2-2 na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mabao ya Kagera Sugar leo yamefungwa na Deus Bukenya dakika ya 32 na Anuary Jabir dakika ya 53, wakati ya Geita Gold yamefungwa na Geoffrey Manyasa dakika ya 41 na Daniel Lyanga dakika ya 88. Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi 24 katika mchezo wa 18, Kagera Sugar ikienda nafasi ya sita na Geita Gold nafasi ya saba.

INONGA AONGEZA MKATABA SIMBA SC HADI MWAKA 2025

Image
BEKI Hennock Inonga Baka ‘Varane’ ameongeza mkataba wa kuitumikia klabu ya Simba hadi mwaka 2025.

WAWILI TU WAPITISHWA KUWANIA UENYEKITI SIMBA SC

Image
WAKILI Moses Stewart Kaluwa amepitishwa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa klabu ya Simba dhidi ya Mwenyekiti wa sasa, Mbunge Ally Murtaza Manungu katika uchaguzi wa mapema mwakani.

IHEFU SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 3-1 MBARALI

Image
WENYEJI, Ihefu SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali mkoani Mbeya. Mabao ya Ihefu SC leo yamefungwa na wachezaji wa zamani wa Azam FC, kiungo Joseph Mahundi dakika ya 60 na 88 na mshambuliaji Obrey Chirwa dakika ya 74, wakati la Mtibwa Sugar limefungwa na Ismail Mhesa dakika ya 52. Kwa ushindi huo, Ihefu SC wanafikisha pointi 17 katika mchezo wa 18 na kusogea nafasi ya 13, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 24 za mechi 18 nafasi ya sita.

SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA NI MOTO

Image
SAKATA la kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum Abdallah na Yanga limechukua sura mpya kufuatia mchezaji huyo kuomba kuondoka na kulipa gharama za mkataba wake. Taarifa ya Yanga leo imesema; “Klabu  inathibitisha kupokea barua kutoka kwa mchezaji tarehe 23 Disemba 2022 inayoeleza kuvunja Mkataba wake baina yake na Klabu. Klabu ya Yanga imemuandikia na kumjibu Feisal na miongoni mwa majibu ni kama ifuatavyo; Hakuna misingi ya kikanuni wala kisheria kulingana na mkataba wake ambazo zinampa haki mchezaji kusitisha mkataba wake na Klabu kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa sasa Kanuni na Taratibu za FIFA ziko wazi na zimeelezea taratibu zote juu ya Jambo la aina hii. Kwamba, Mkataba baina ya mchezaji na Klabu hauwezi kuvunjwa na upande mmoja tu bila kujadiliana na upande wa pili wakati msimu wa ligi ukiwa unaendelea. Kwamba, kwa mazingira hayo, barua ya mchezaji ina dhana potofu na haina misingi ya kisheria ya kuvunja mkataba baina ya klabu na mchezaji Na kwa mantiki h

SIMBA QUEENS 1-1 YANGA PRINCESS (LIGI YA WANAWAKE TZ BARA)

Image
 

SIMBA QUEENS NA YANGA PRINCESS ZAGAWANA POINTI KWA SARE YA 1-1

Image
TIMU za Simba Queens na Yanga Princess zimegawana pointi katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Bao la Simba katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji wake Mkenya, Vivian Aquino likiwa la kusawazisha baada ya Mnigeria, Chioma Wogu kuanza kuifungia Yanga Princess. Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi nne baada ya kucheza mechi tatu, zikiwa zimefungwa moja moja na kushinda moja moja mbali na sare ya jana.

KAGERA SUGAR 1-1 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC YATOA SARE NA KAGERA SUGAR 1-1 KAITABA

Image
WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ni Kagera Sugar ya kocha Mecky Mexime iliyotangulia kwa bao la Deus Bukenya dakika ya 15, kabla ya beki Mkongo, Henock Inonga Baka kuisawazishia Simba dakika ya 38. Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar wanafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya sita, wakati Simba inayofikisha pointi 38 inabaki nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 17. Ni mabingwa watetezi, Yanga SC wanaoendelea kuongoza Ligi Kuu baada ya raundi 17, wakiwa na pointi zao 44, wakati Azam FC yenye pointi 37 ni ya tatu.

GEITA GOLD YATOA SARE 1-1 NA AZAM FC NYANKUMBU

Image
WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Ni wageni, Azam FC waliotangulia kwa bao la mshambuliaji wake Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 15, kabla ya kiungo Offen Francis Chikola kuisawazishia Geita Gold kwa penalti dakika ya 69. Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya sita, wakati Azam FC sasa ina pointi 37, baada ya wote kucheza mechi 17, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa mabao na Simba SC ambayo ina mechi moja mkononi.

PRISONS YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 SOKOINE

Image
WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Zabona Khamis dakika ya tatu na Samson Mbangula dakika ya 78 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 18 katika mchezo wa 17 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 11. Kwa upande wao, Dodoma Jiji wanateremkia nafasi ya 12 wakizidiwa tu wastani wa mabao na Prisons baada ya wote kucheza mechi 17.

KABURU, MANGUNGU WAITWA KWENYE USAILI UCHAGUZI SIMBA SC

Image
MWENYEKITI wa sasa wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu pamoja na Makamu Mwenyekiti wa zamani, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ni miongoni mwa wagombea walioitwa kwenye usaili kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa klabu mapema mwakani.

YANGA SC 3-0 COASTAL UNION (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

MAYELE APIGA MBILI YANGA YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 DAR

Image
MSHAMBULIAJI Mkongo, Fiston Kalala Mayele amefunga mabao mawili kuiwezesha Yanga SC kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mayele alifunga mabao yake dakika ya 29 na 47 hivyo kufikisha mabao 13 jumla kwenye ligi msimu huu na kuendelea kuongoza kwa mabao matatu ya Mzambia wa Simba, Moses Phiri. Aliyekamilisha ushindi wa Yanga leo ni kiungo Mzanzibari, Fiesal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 66 na sasa mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 44 katika mchezo wa 17 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi saba zaidi ya watani, Simba SC wenye mechi moja mkononi. Hali si nzuri kwa Coastal Union, kwani baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 15 za mechi 17 nafasi ya 13.

RUVU SHOOTING NA MTIBWA SUGAR ZATOKA 0-0 UHURU

Image
TIMU za Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting zimegawana pointi baada ya sare ya bila kufungana leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Kwa sare hiyo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 17, ingawa inabaki nafasi ya 15, wakati Mtibwa Sugar inafikisha pointi 24 katika mcchezo wa 17 japokuwa inabaki nafasi ya tano.

AZAM FC YAACHANA RASMI NA IBRAHIM AJIBU

Image
KLABU ya Azam FC imetangaza kuachana na kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu Migomba iliyemsajili Desemba mwaka jana kutoka Simba SC.

HATIMAYE DK MSOLLA AMKABIDHI OFISI INJINIA HERSI YANGA

Image
HATIMAYE Rais wa Yanga SC, Mhandisi Hersi Ally Said leo amekabidhiwa rasmi ofisi na Uongozi uliopita chini ya Mwenyekiti Dk. Mshindo Msolla baada ya zoezi la ukaguzi wa hesabu za Klabu kukamilika.

GEITA GOLD 0-5 SIMBA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
 

DODOMA JIJI YAWAPIGA MBEYA CITY 2-1 PALE PALE SOKOINE

Image
TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Dodoma Jiji FC leo yamefungwa na Christian Ziggah dakika ya 17 na Zidane Sereri dakika ya 70, wakati la Mbeya City limefungwa na Eliud Ambokile dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 16 na kusogea nafasi ya 11, wakati Mbeya City wanabaki na pointi zao 20 za mechi 16 nafasi ya nane.

SINGIDA STARS YAICHAPA PRISONS 2-1 PALE PALE SOKOINE

Image
TIMU ya Singida Big Stars imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Singida Big Stars yamefungwa na Bruno Gomes dakika ya tano na Meddie Kagere dakika ya 57, wakati la Tanzania Prisons limefungwa Jumanne Elfadhil kwa penalti dakika ya 79. Kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 30 katika mchezo wa 16, ingawa wanabaki nafasi ya nne wakizidiwa pointi nne na vigogo, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.

MTIBWA SUGAR YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA NAMUNGO MANUNGU

Image
WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. Omary Suleiman alianza kuifungia Mtibwa Sugar dakika ya 78, kabla ya Peteme Counou kuisawazishia Namungo FC dakika ya 90 na ushei. Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 16 ikisogea nafasi ya tano, wakati Namungo inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 16 nafasi ya tisa.

SIMBA, YANGA NA AZAM ZATENGANISHWA KOMBE LA MAPINDUZI

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wamepangwa Kundi C pamoja na Mlandege na KVZ katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari 1 hadi 13, mwakani. Kwa upande wao, mabingwa wa Bara, Yanga SC wao wapo Kundi B pamoja na Singida Big Stars na wenyeji, KMKM ambao pia ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar. Kundi A linaundwa na Azam FC ya Dar es Salaam, wenyeji, Malindi SC na Jamhuri FC ya Pemba, wakati Kundi D kuna Namungo ya Lindi, Aigle Noir ya Burundi na Chipukizi ya Pemba. RATIBA KOMBE LA MAPINDUZI Januari 1, 2023 Mlandege v KVS Saa 10:15 Malindi SC v Jamhuri Saa 2:15 Januari 2, 2023 Namungo v Chipukizi Saa 10:15 Singida BS v KMKM Saa 2:15 Januari 3,2023 Azam FC v Malindi SC Saa 10:15 Simba SC v Mlandege Saa 2:15 Januari 4, 2023 Chipukizi v Aigle Noir Saa 10:15 Yanga SC v KMKM Saa 2:15 Januari 5, 2023 Jamhuri v Azam FC Saa 10:15 KVZ v Simba SC Saa 2:15 Januari 6, 2023 Namungo v Aigle Noir Saa 10:15 Yanga SC v Singida BS Saa 2:15 Januari 8, 2023 NUSU FA

BEN POL AJA KAZI MPYA HATARI INAITWA NYUMBANI

Image
MSANII nguli wa Muziki hapa nchini Behnam Paul maarufu kama Ben Pol ameachia kibao kipya kinachofahamika kama Nyumbani. Katika wimbo wa Nyumbani Ben Pol ambaye asili yake ni Dodoma ameeleza raha na uzuri wa kurejea Nyumbani huku akisifia maadili mazuri, mtindo wa maisha, vyakula n.k katika jamii zetu za kitanzania. “Kwangu mimi Nyumbani ni zaidi ya sehemu tu, Nyumbani ni mahali popote ambapo unahisi upendo na amani, unajihisi kupata sapoti, unasikilizwa, unaeleweka, unapokelewa katika hali zote bila kujali mafanikio yanayoonekana kwa macho. Nawakaribisha wadau wote wa Muziki wa Tanzania kufurahia wimbo huu ambao sasa unapatikana katika mitandao yote tukiendelea kujivunia tulikotoka, kujivunia utanzania wetu, u-Afrika wetu, utu wetu” - Ben Pol. Video ya Nyumbani imefanyika katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani chini ya utayarishaji wa kampuni ya Redshot.

UFARANSA YAIFUATA ARGENTINA FAINALI KOMBE LA DUNIA

Image
MABINGWA watetezi, Ufaransa wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Morocco jana Uwanja wa Al Bayt mjini Al Khor nchini Qatar. Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Theo Hernández dakika ya tano tu ya mchezo huo na Randal Kolo Muani dakika ya 79 na kuzima ndoto za Morocco kuweka rekodi mbili kwa mpigo. Sasa Ufaransa itakutana na Argentina katika Fainali tamu mno Jumapili Uwanja wa Lusail Iconic mjini Lusail. Nayo Morocco iliyoweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia itamenyana na Croatia Jumamosi Uwanja wa Khalifa International mjiji Al Rayyan kuwania nafasi ya tatu.

ARGENTINA YATINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA

Image
TIMU ya Taifa ya Argentina imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Croatia jana Uwanja wa Lusail Iconic Stadium Jijini Lusail nchini Qatar. Mabao ya Argentina yamefungwa na Nahodha Lionel Messi kwa penalti dakika ya 34 na Julian Álvarez mawili dakika ya 39 na 69 baada ya kazi nzuri ya Nahuel Molina na sasa watasubiri kukutana na mshindi kati ya Mabingwa watetezi, Ufaransa na Morocco zinazomenyana leo.

TIMU 32 ZILIZOSALIA MICHUANO YA AZAM FEDERATION CUP

Image
HIZI ndizo timu zilizofuzu Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).

SIMBA SC YAPANGWA NA RAJA, HOROYA NA VIPERS YA UGANDA

Image
TIMU ya Simba SC ya Tanzania imepangwa Kundi C pamoja na Raja Casablanca ya Morocco, Horoya ya Guinea na Vipers ya Uganda katika Hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kundi A kuna mabingwa watetezi, Wydad Athletic ya Morocco, Petro Atletico ya Angola, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Kundi B kuna Al Ahly ya Misri, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, El Hilal ya Sudan na Cotón Sport ya Cameroon, wakati Kundi D zipo Esperance ya Tunisia, Zamalek ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria na El Merreikh ya Sudan.

YANGA SC 8-0 KURUGENZI (ASFC)

Image
 

YANGA PRINCESS YAMPIGA CHINI EDNA, YAMCHUKUA KOCHA WA SIMBA QUEENS

Image
KLABU ya Yanga Princess imemtambulisha aliyekuwa Kocha wa Simba Queens, Sebastian Nkoma kuanza kuinoa timu hiyo akichukua nafasi ya Edna Lema aliyeondolewa.

SIMBA SC 8-0 EAGLE FC (ASFC)

Image
 

BARBARA ATANGAZA KUNG'ATUKA SIMBA SC JANAURI 2023

Image
MTENDAJI Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez jana ametangaza kujiuzulu wadhifa huo ifikapo januari mwakani, ikiwa ni miaka miwili tu tangu apewe wadhifa huo Novemba mwaka 2022.

MOROCCO YAWEKA REKODI KOMBE LA DUNIA, YATINGA NUSU FAINALI

Image
TIMU ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ureno leo Uwanja wa Al Thumama Jijini Doha. Bao pekee la Simba wa Atlasi katika mchezo huo limefungwa na Youssef En-Nesyri dakika ya 42 na sasa Morocco ambayo inakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia itakutana na mshindi kati ya Ufaransa na England.

AZAM FC YAITANDIKA MALIMAO 9-0 KOMBE LA TFF CHAMAZI

Image
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kusonga mbele Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 9-0 dhidi ya Malimao FC ya Katavi jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC katika mchezo huo yamefungwa na Sospeter Bajana, Shaaban Iddi Chilunda, Keneth Muguna, Kipre Junior, Abdul Suleiman ‘Sopu’ mawili, Yahya Zayd, Cyprian Kachwele na David Chilawanga.