AZAM FC YAITANDIKA MALIMAO 9-0 KOMBE LA TFF CHAMAZI
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kusonga mbele Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 9-0 dhidi ya Malimao FC ya Katavi jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC katika mchezo huo yamefungwa na Sospeter Bajana, Shaaban Iddi Chilunda, Keneth Muguna, Kipre Junior, Abdul Suleiman ‘Sopu’ mawili, Yahya Zayd, Cyprian Kachwele na David Chilawanga.
Comments
Post a Comment