MO DEWJI: DHAMIRA YETU NI KUTWAA TENA UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA NA MATAJI YOTE NCHINI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mohammed 'Mo' Dewji amesema kwamba dhamira yao ni kutetea tena ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara pamoja na kutwaa tena Ngao ya Jamii
"Napenda Kuwait aarti fun kwamba sisi katika uongozi wa Simba tumejizatiti na kuweka mikakati ya kuhakikisha tunachukua tena Ubingwa wa Ligi, kuchukua Kombe la FA, na kufika mbali kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika,"amesema na kuongeza;
"Pia tunaendelea na mikakati ya kuhakikisha kwamba Klabu yetu inajenga chapa na sifa bora Afrika na kote duniani. Sehemu ya mkakati huo ni haya mashindano tuliyoandaa ya Simba Super Cup, ambayo hadi sasa yamefanikiwa na yamepokelewa vizuri kote Afrika. Nia yetu ni kwamba mashindano haya ya Simba Super Cup tuyafanye kila mwaka,". 

"Tayari tumeanza maandalizi ya mashindano haya kwa msimu ujao ambapo tutaongeza idadi ya timu kubwa za Afrika. Nia yetu pia ni kwamba mashindano haya yajiendeshe yenyewe kibiashara. Vyanzo vya fedha za kugharamia mashindano haya ni:- wadhamini, malipo ya utangazaji, viingilio na mchango wangu binafsi,". 
"Wito wangu maalum kwenu ni kwamba, ili mashindano yajayo yawe bora zaidi, nawaomba tuje uwanjani, tujaze uwanja kwenye mechi za haya mashindano,". 
"Tukija kwa wingi tutakuwa tumefanikiwa mambo manne:- tumechangia klabu yetu kimapato, tumeyapa mashindano haya hadhi na heshima stahili, tumevutia timu nyingine kubwa Afrika ziombe kuja kushiriki, na tumewapa wachezaji wetu moyo na hamasa,". 
"Kwa hiyo, nawaomba shime tuje uwanjani kwa wingi kwenye mechi yetu na TP Mazembe siku ya Jumapili, tarehe 31.01.2021. Pamoja na kwamba tunaweza kuitazama mechi kwenye luninga lakini mapato yatakuja Simba, na tutaweza kufanya mambo makubwa zaidi,  kama tutakuja mpirani. Tuonyeshe mapenzi na uzalendo kwa Klabu yetu kwa kuja kwenye mechi,". 
"Hii pia itatupa moyo sisi viongozi kuendelea kubuni na kutekeleza mambo makubwa na mazuri zaidi. Shime, tukutane kwa Mkapa Jumapili saa kumi alasiri. Tuma huu ujumbe kwa mwana-Simba mwenzako," amesema.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA