YANGA KUANZIA DJIBOUTI, SIMBA NAMIBIA AU ZAMBIA, AZAM...
DROO ya Raundi za awali za michuano ya klabu imepangwa makao ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Jijini Cairo nchini Misri na mabingwa wa Tanzania, Yanga wataanza na Asas ya Djibouti.
Wakifanikiwa kuitoa timu hiyo ya Djibouti, Yanga SC watakutana na mshindi wa jumla kati ya kati ya Otoho ya Kongo Brazzaville na El Mereikh ya Sudan kuwania tiketi ya makundi.
Simba SC itaanzia Raundi ya Pili ya mchujo moja kwa moja kuwania kuingia hatua ya makundi kwa kumenyana na mshindi kati ya African Stars ya Namibia na Power Dynamos ya Zambia ambayo watacheza nayo kwenye Simba Day.
Kwa upande wao mabingwa wa Zanzibar, KMKM watamenyana na St George ya Ethiopia, mtihani ambao ikiuvuka itakutana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.
Katika Kombe la Shirikisho, Singida Big Stars wataanza na JKU ya Zanzibar, huku Azam FC wakimenyana na Bahir Dar ya Ethiopia.
Azam FC ikifuzu itamenyana na Club Africain ya Tunisia, wakati Singida Fountain Gate ikipita itakutana na Future ya Misri.
Comments
Post a Comment