MAN CITY YASONGA MBELE KOMBE LA FA, CHELSEA YABANWA DARAJANI
BAO la beki Mholanzi, Nathan Benjamin Aké dakika ya 88 liliipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur katika mchezo wa Raundi ya Nne Kombe la FA England usiku wa jana Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
Wakati Man City inakwenda Raundi ya Tano, mchezo mwingine wa Raundi ya Nne Kombe la FA jana, wenyeji Chelsea ililazimishwa sare ya 0-0 na Aston Villa Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, hivyo timu hizo zitarudiana.
Comments
Post a Comment