WAARABU WANNE WATANGULIZA MGUU MMOJA MMOJA QATAR 2022
TIMU za Kaskazini mwa Afrika zimepata matokeo mazuri dhidi ya timu za ukanda wa Jangwa la Sahara katika mechi za kwanza za raundi ya mwisho kufuzu Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini Qatar.
Uwanja wa Kimataifa Cairo Jijini Cairo, wenyeji Misri wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Senegal, bao la kujifunga la beki wa Nancy ya Ufaransa, Saliou Ciss dakika ya nne.
Uwanja wa Douala Jijini Douala, wenyeji, Cameroon wamechapwa 1-0 na Algeria, bao pekee la mshambuliaji wa Sporting Lisbon ye Ureno, Islam Slimani dakika ya 40,
Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako, wenyeji, Mali wamechapwa 1-0 na Tunisia, bao la kujifunga la beki wa Standard Liège ya Ubelgiji, Moussa Sissako dakika ya 36.
Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa, wenyeji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wamelazimishwa sare ya 1-1 na Morocco.
Mshambuliaji sa Brentford ya England, Yoane Wissa alianza kuifungia DRC dakika ya 12, kabla ya mshambuliaji wa Gent ya Ubelgiji, Tarik Tissoudali kuisawazishia Morocco dakika ya 76.
Mechi iliyokutanisha wapinzani wa Afrika Magharibi watupu baina ya wenyeji, Ghana na jirani zao Nigeria ililazimishwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Baba Yara Jijini Kumasi.
Mechi za marudiano zitachezwa Jumanne na washindi wa jumla watano watajikatia tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini place in Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18, mwaka huu.
Comments
Post a Comment