KMC YAWAPIGA GEITA GOLD 2-1 PALE PALE NYANKUMBU


TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
Mabao ya KMC leo yamefungwa na Waziri Junior dakika ya tisa na Juma Shemvuni dakika ya 40, wakati bao pekee la Geita Gold limefungwa na Tariq Seif dakika ya 38.
KMC inafikisha pointi saba, Geita Gold inabaki na pointi nne baada ya wote kucheza mechi nne.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA