AZAM FC YAMSAJILI MKONGWE WA BURUNDI, NDIKUMANA ALIYEWAHI KUCHEZA SIMBA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Burundi, Suleiman Ndikumana, kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Nyota huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam pia, amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', mmoja wa maofisa wa timu hiyo, Abubakar Mapwisa na wakala wa mchezaji huyo, Milner James.
Ndikumana aliyekuwa akichezea Al Adalah ya Saudi Arabia, ni mmoja wa washambuliaji wazoefu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na ametua Azam FC baada ya kupendekezwa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' (kulia), akimkabidhi jezi ya klabu hiyo mshambuliaji mpya, Suleiman Ndikumana 

Hii ni timu ya pili kuwahi kucheza nchini Tanzania, nyingine ikiwa ni Simba aliyochezea 2006, pia akiwa na uzoefu barani Ulaya, akipita Molde ya Norway na FK Tirana ya Albania.
Huo ni usajili wa tatu kwa Azam FC, kwa ajili ya msimu ujao baada ya awali kulamilisha usajili wa wachezaji wengine wawili, winga Idd Seleman 'Nado' na kiungo mshambuliaji, Emmanuel Mvuyekure.
Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo kwenye maandalizi makali kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame, inayotarajia kuanza kutimua vumbi Julai 7 nchini Rwanda, ikiwa kama bingwa mtetezi wa michuano hiyo.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA